Showing posts with label SIRI ILIYOPO KATIKA USOMAJI WA VITABU. Show all posts
Showing posts with label SIRI ILIYOPO KATIKA USOMAJI WA VITABU. Show all posts

Wednesday, May 8, 2019


Mtu anakwambia "HII FURSA HAIKUHITAJI KUFANYA KAZI KWA BIDII. WEWE UKISHAJIUNGA, MAMBO MENGINE YOTE TUTAKUFANYIA SISI." Hapo Umeliwa.
VIJANA Wengi sana wa kitanzania HATUPENDI KUFANYA KAZI KWA BIDII NDIO MAANA HUWA TUNAKAMATIKA KIRAHISI SANA.

Na hiyo ni sababu kubwa sana ya BIASHARA YA KUBETI KUSHIKA SANA KASI NCHINI MWETU. Kila Siku unasikia namna mpya ya Kubeti.

#Zaidi ya Yote: Ikiwa Unataka Elimu kama hizi za biashara na Fursa, JIPATIE KITABU CHA "MBINU 16 ZA KUONGEZA MAUZO KWENYE BIASHARA YAKO" kwa Gharama nafuu kabisa. Njoo WhatsApp kwa kubofya hii LINK ili kupata Kitabu: https://wa.me/255764793105.

Tuesday, May 7, 2019


(I) Itakusaidia katika KUCHAGUA VYEMA Aina ya Vitabu Vitakavyokusaidia katika KUNOA UWEZO ULIYOMO NDANI YAKO-Kipaji, Karama, Kipaji, na Huduma.

VITABU VIPO VINGI SANA Tanzania na duniani kote, lakini SIO VYOTE VIKUFAAVYO, kama vile ambavyo Mwanamke mmoja Hawezi Akamfaa kila Mwanaume kuwa nae katika Ndoa hata kama Kaumbika kwa Namna Nzuri na ya Kupendeza sana – kwa sababu “Uzuri wa Sura Hautafsiri Usafi wa Moyo” –Lamax.

Kwa hiyo jambo la kwanza kabisa kabla ya kuanza USOMAJI WA VITABU NI "KUJITAMBUA."
Usijeukawekeza Nguvu zako nyingi kwenye Kusoma Vitabu vya Ufugaji wa Samaki na Wakati unatakiwa kuwa Mchezaji wa Mpira wa Miguu.

Kumbuka: USIPOJUA UNATAKIWA KUFANYA NINI KWENYE HAYA MAISHA YA HAPA DUNIANI, BASI UNAWEZA UKAPATA TAABU SANA KWENYE ENEO LA USOMAJI WA VITABU.

#Zaidi ya hapo JIPATIE KITABU CHA "NAMNA YA KUSOMA KITABU - How to Read A book" cha LACKSON TUNGARAZA kwa Mfumo wa PDF Leo ili UNUFAIKE zaidi. Unapitwa na mambo mazuri Mengi sana kwa Kutokujua Usomaji mzuri wa Vitabu.


Mawasiliano ya kupata Kitabu: 0764793105, au https://wa.me/255764793105 Kwa WhatsApp.
USHINDWE MWENYEWE.


Monday, May 6, 2019


Kitabu cha Kwanza: "MBINU 16 ZA KUONGEZA MAUZO KWENYE BIASHARA YAKO.".



- Ndani ya Kitabu hiki Utapata Mbinu 16 za uhakika za Kukusaidia katika Kuongeza Mauzo (SALES) kwenye Biashara Yako yo yote Ile uifanyayo Mtandaoni au nje ya Mitandao. Ni zaidi ya mwaka tangu kilipozinduliwa rasmi, na kimekwisha Kuwasaidia Watu Wengi Kibiashara.

Wewe Unasubiri nini Kukua KIFEDHA wakati huu ambao Watu wanasema ya kwamba VYUMA VIMEKAZA (Hali ya Kiuchumi ni Ngumu, na hakuna Faida kwenye Biashara)?? KITABU HIKI NI MKOMBOZI WAKO. JIPATIE NAKALA YAKO LEO KWA "SOFT COPY" (pdf) po pote pale Ulipo Duniani. Ni Tsh 10,000/= tu.

- Bofya hii LINK kuwasiliana nasi moja kwa moja kwa WhatsApp: https://wa.me/255764793105.


Kitabu cha Pili: "NAMNA YA KUSOMA KITABU - How to Read A book.".


- Ndani ya hiki Kitabu utakutana na mambo mazuri sana ya Kukusaidia kupata hamu ya Kusoma Vitabu kwa ufasaha na kuweza Kuishi Ndoto Yako.

- Ndani yake utayapata "MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZA USOMAJI WA VITABU, NAMNA YA KUSOMA KITABU, SHUHUDA NA MASHAURI YA WASOMAJI MAARUFU WA VITABU, pamoja na MASWALI KUMI YA MUHIMU."
.
- Unaanzaje Kukosa hiki Kitabu?? AMUA LEO KUWA WA TOFAUTI, Mr. Lamax aliwahi kusema ya kwamba; "Usomaji wa Vitabu Sio Kipaji, ni TABIA Inayotengenezwa na Mtu Mwenyewe Kila Siku."

-Bofya hii LINK kuwasiliana nasi moja kwa moja WhatsApp: https://wa.me/255764793105. Utakipata kwa Tsh. 5000/= tu katika Mfumo wa "SOFT COPY  (pdf)."


MWANDISHI WA VITABU VYOTE ni LACKSON TUNGARAZA. Unaweza Kumjua zaidi kwa Undani na Yote ayafanyayo kwa KUBOFYA hii LINK: https://lacksontungaraza.blogspot.com/2019/03/lackson-tungaraza-ni-nani-haswa.html?m=1.


KARIBU SANA LEO.
- Kwa Mawasiliano ya Kawaida: +255 (0) 764 793 105.

Saturday, March 16, 2019

Nakumbuka Wakati nilipokuwa Field ya mwaka wa pili St. John's University of Tanzania  (SJUT) iliyopo Jijini Dodoma, ndiyo Wakati nilipopata wazo  (idea) la Kuandika Kitabu ambacho kitawasaidia Vijana wenzangu Wengi Juu ya Changamoto za Ujanani ambazo zimesheheni Kila Upande kuanzia kwenye familia, Jamii, na Mitandaoni.

Hakikuwa Kitabu changu cha kwanza Kuandika, Ila kwa namna kilivyougusa moyo Wangu niliona Kiwe cha kwanza kutoka halafu ndipo Vitabu vingine vitafuata.

Kilichonisukuma zaidi Kuandika hicho kitabu ni aina ya maisha ambayo niliyapitia katika Ujana Wangu kabla na baada ya kuamua kurudi kwa Mungu. Na pia aina ya maisha ambayo vijana wa Sasa Wameamua kuyaishi bila Kujua ya kwamba Wanapanda mbegu ya kuwaharibu Wao na Kizazi chao.

Wakati naandika hicho Kitabu Nilikuwa naishi kwa Kijana niliyekutana naye huko huko maeneo ya SJUT, na pia alikuwa ni mwanafunzi wa hapo Chuoni. Nadhani Ulikuwa ni mpango wa Mungu kuniruhusu niishi katika Yale Mazingira yaliyopelekea niandike Kitabu. Lakini haikuwa rahisi kihivyo kwa Sababu mwanzoni nilikuwa najilaumu Kuishi katika Yale Mazingira, na pia nilikuwa namwomba sana Mungu awaondoe Machoni pangu Wale Vijana Watukutu waliyokuwa wanakuja na Stori zisizofaa pale nilipokuwa naishi kwa wakati huo.

Asubuhi moja wakati namwomba Mungu ili awazuie Vijana waharibifu kuja pale nilipokuwa naishi, ndani Yangu nikaja WAZO Jipya ambalo Sikulitegemea Kabisa. Niliambiwa hivi, "TATIZO HALIKIMBIWI, TATIZO LINATATULIWA. HAYA YANAYOFANYWA HAPA NA HAWA VIJANA YANAFANYWA PIA NA VIJANA WENGINE WALIYO MBALI NAWE." Baada ya kupata hilo wazo, nikaacha kwanza Kuomba na kuanza kulitafakari. Katika Kutafakari Kwangu, nikaona ni vyema niandike kile ambacho kitawasaidia Vijana Wote  [Wakati huo Nilikuwa Sina wazo la Maandishi hayo kuja kuwa kitabu]. Kwa hiyo nikaondoka na kwenda kuketi mahali kulipokuwa na Kompyuta Yangu ili nianze Kuandika Yaliyomo Moyoni mwangu. Nikaanza kwa kuangalia Changamoto kubwa 5 zinazowasumbua vijana wengi sana. Nikapata hizi hapa:

(1). Peer pressure - Makundi Rika.
(2). Kutaka UMAARUFU.
(3). Kutaka Mafanikio ya haraka.
(4). Tamaa.
(5). Kiburi.

Baada ya Kuandika zote na kuzielezea kwa Kina, nikaona haitakuwa vyema kwa kuziongelea tu bila kuwa na Suluhisho. Hapo nikapata sehemu ya Pili Iitwayo "NAMNA YA KUZIVUKA CHANGAMOTO."


Kisha nikapata tena wazo la kuwaelezea VIJANA ni kwa namna gani wataweza kufikia Hatma zao za Kimaisha  (Destiny), kwa Sababu nilijua Watakuwa na Maswali Mengi mioyoni mwao juu ya namna ya Kuishi baada ya kuzivuka zile Changamoto kubwa za Ujanani. Kwa hiyo nikapata sehemu ya Tatu Iitwayo "IFIKIE HATMA YAKO" (Reach & Fulfill your own Destiny). Kwa Uongozi wa Mungu nikaandika hatua ambazo Kila Mtu anapaswa kuzifuata kama Ana nia ya dhati ya kufikia Ile Mipango ambayo MUNGU anayo kwa ajili Yake.

Sasa Nilipokuwa nataka kuhitimisha, nikapata tena wazo la Kuwasaidia MABINTI kwenye eneo la MAHUSIANO Yao na Mungu, Yao na Wao Wenyewe (Self Relationship), na Yale ya Kimapenzi. Kwa nini nilitakiwa kufanya hivyo? Kwa Sababu niliona namna ambavyo mabinti wengi walikuwa wanadanganywa na vijana wa Mtaa Ule wa SJUT, UDOM, na kwingineko. Na pia niliona ya kwamba Mwanamke akijitambua Vizuri ataifanya pia na Jamii Yake Yote kuwa Imara. Na hapo nikapata sehemu ya Nne Iitwayo "KWAKO BINTI YANGU MPENDWA [Uzuri na Urembo Usiopitwa wa Wakati].

Mwishoni kabisa nikapata Shida ya JINA LA KITABU. Nikaomba USHAURI wa Watu mbali mbali, lakini napo nikaona kama vile Sijaridhika. Baadae ndipo nikapata Jina la "SITARUDI NYUMA TENA." Ambalo nililiona liko poa sana, kwa nini? Kwa Sababu LIMEKAA KWENYE MFUMO WA "KIAPO" ya kwamba MTU aliyekwisha kufahamu anayopaswa kufanya katika Maisha Yake HUPASWI KABISA KURUDI TENA NYUMA kwenye maisha yake ya Awali ambayo hayampeleki ambako Mungu anamtaka awepo.
JOSEPH MSEMBE AKIJISOMEA KITABU


Taratibu za Mwisho zikafuata hadi nikakitoa hicho KITABU changu cha kwanza cha Hard Copy  (Nakala Ngumu) mwezi Oktoba, 2017.

Kwa hayo Yote niliyoyaandika hapo Juu Utakuwa Umejua yaliyokuwa yamejificha NYUMA YA PAZIA hadi hicho Kitabu kuwa Jinsi Unavyokiona Leo. NAKUKARIBISHA SANA KUPATA NAKALA YAKO MOJA YA KITABU HICHO CHA "SITARUDI NYUMA TENA" ILI NAWE "ULE KIAPO" CHA KIMAISHA KWA MAENDELEO YAKO BINAFSI, FAMILIA YAKO, NA JAMII YOTE INAYOKUZUNGUKA. Gharama ya Kitabu ni Tsh. 5000/= tu.

Mawasiliano! 0764793105
@LACKSONTUNGARAZA
AMUA LEO KUWA WA TOFAUTI.

Tuesday, March 5, 2019


Mwanzoni Uliamini ya kwamba KWA KUJIAJIRI ndipo UTAPATA UHURU WA KIFEDHA na KIUCHUMI. Ukakataa KUAJIRIWA kwa Sababu ya kasoro Yake ya KUWEKEWA UKOMO WA FEDHA UNAYOINGIZA (Income) kutoka kwa MWAJIRI wako.


LAKINI LEO!

Huamini tena kama Ulikuwa Unamaanisha kwa dhati Kutoka moyoni mwako. Na hiyo imekuja baada ya KUISHIWA PESA YOTE YA KUANZISHIA BIASHARA [au MTAJI Kama Wengi Wasemavyo], na KUPATA HASARA ZA MFULULIZO KATIKA BIASHARA au MRADI ULIYOKUWA UKIUTEGEMEA SANA. Yaani, Umekaribia kabisa Kukata Tamaa, na Muda mwingi Unautumia katika KUJILAUMU kwa KUACHA KUCHANGAMKIA FURSA ZA AJIRA zilizokuwa zinakufuata hapo Awali.

Pole sana. Lakini Nikuulize; "WAKATI ULIPOAMUA KUJIAJIRI BADALA YA KUAJIRIWA, ULIDHANI YA KWAMBA KUNA MTEREMKO SANA (Hakuna CHANGAMOTO KUBWA, wala HASARA)??", au Rudi hatua Tatu Nyuma na KUJIULIZA ni kwa nini Uliamua KUJIAJIRI kuliko KUAJIRIWA. Na kama NIA YAKO ilikuwa ni ya dhati Kabisa, kwa nini Sasa Ukate tamaa? Hujui ya kwamba IMANI NDIYO HUJARIBWA? Na KUJARIBIWA KWA IMANI NDIKO KUNALETA SABURI (Ukomavu, Ushupavu, Uhodari)?

Sitaki Uamini ya kwamba Ulikosea kwenye MAAMUZI Yako Ikiwa ULIKUWA NA SABABU ZA MSINGI, PAMOJA NA NIA YA DHATI Kutoka Moyoni mwako. Au PATA MAHALI PA UTULIVU na Kujitathimini kwa Kujiuliza na Kujihoji kama Uliamua kwa dhati kabisa Kutoka moyoni mwako, au Uliamua KUJIAJIRI kwa Sababu ya USHAURI wa Waalimu wa Ujasiriamali, na Wazungumzaji (Motivational Speakers). Au kwa Sababu ya TAMAA YA PESA kwa KUDHANI ya kwamba BIASHARA PEKEE ndiyo NJIA ya Kupata UHURU wa KIFEDHA na KIUCHUMI.

Mwisho kabisa,

SAFARI YA KUJIAJIRI SIO LELEMAMA au MTELEZO; Unaweza ukakutana na HASARA NYINGI za MFULULIZO kuliko hata FAIDA. Au Unaweza ukakutana navyo vyote kwa Wakati Mmoja  (Faida na Hasara). Au Unaweza ukakutana na FAIDA NYINGI za MFULULIZO kuliko hata HASARA  [ambayo Sio kwa Wakati Wote]. Na hiyo haijalishi Ulihudhuria Semina ngapi za Ujasiriamali na Biashara, ulisoma Vitabu vingapi vya Fedha na Uchumi, wala idadi ya Mashauri uliyopokea kutoka kwa manguli wa Ujasiriamali na Biashara. Huwa inatokea tu, na hata Mimi Sina lugha nyepesi ya kuielezea ni kwa nini huwa inakuja tu. Kwa hiyo, Unapaswa KUAMUA kabisa ya kwamba UNATAKA KUJIAJIRI hata kama kuna Changamoto na Hasara ABC. Na kama HUWEZI, basi UTAFUTE NAFASI ZA AJIRA MAPEMA. Kwa maamuzi yo yote Yale, jiapie "SITARUDI NYUMA TENA" kama ilivyoandikwa ndani na nje ya Kitabu changu (Kama huna hicho Kitabu, nijulishe nikutumie - kinapatikana, na kinauzwa).


AMUA LEO KUWA WA TOFAUTI. NIA ni Sababu ya dhati iliyopo nyuma ya maneno na matendo yo yote Yale - haijalishi ni mema au mabaya.

@LACKSONTUNGARAZA (Lamax)
Whatsapp: +255764793105
Bye bye... Uwe na Siku Njema Yenye Ushindi na Amani ya Mwenyezi Mungu aliye hai.


Monday, March 4, 2019


Siku Moja nikiwa Nyumbani kwa Wazazi Wangu, nilipata nafasi ya kwenda kusema na Vijana wa Shule Jirani ambayo ilikuwa mbali Kidogo. Kwa dhumuni la kuwahi, nikaamua kutafuta Bodaboda (Pikipiki). Baada ya Muda Mfupi, nikaipata na kuanza safari ya Kuelekea huko Shuleni. Nilipofika, nikamlipa Jamaa PESA Yake, na "kumwomba Namba za Simu" Ili nije nimshitue anifuate baadae.

Tatizo Mojawapo walilonao Watu wa Bodaboda ni "KUTOKUWAPATIA WATEJA NAMBA ZAO ZA SIMU (Mawasiliano)" Kabla ya Kuombwa. Wengi Wanaishi kwa MAZOEA ya Karne ya Kumi na Tisa - Wanataka Wawe Wanatafutwa na Wateja Mara kwa Mara kama vile Dhahabu za Geita.

Baada ya Kupata namba za Simu za Yule Jamaa wa Bodaboda, Nilikuwa namwita mara kwa mara kupitia Simu Anipeleke ninapohitaji. Ikiwa na maana ya kwamba, Alinufaika sana kwa kunipatia namba zake za Simu nilizomwomba badala ya Kunipatia Yeye Mwenyewe. Kumbuka; Wakati huo Ananifuata Nyumbani, wenzake Walikuwa Wamekaa tu VIJIWENI Wakisubiria WATEJA.

Cha Mwisho nilichomshauri Yule Jamaa wa Bodaboda ni "UMUHIMU WA KUWA NA KADI BIASHARA/ KADI KAZI (Business Card)." Nilimwambia, "Business Card" itamsaidia Kuondokana na Tatizo la Kutaja namba zake Kila Wakati, au Kuwaandikia namba kwenye Makaratasi. Na Pia Itamfanya Aonekane Anajitambua, na Anaithamini sana KAZI Yake (Professionalism).

NAWE UNAYEFANYA BIASHARA YA BODABODA au BIASHARA yo yote Ile, nakushauri sana Uwe na "Business Card" - Kitambulisho Chako cha Kibiashara [ambacho Sio cha Kiserikali. Bali ni cha Kukutambulisha Wewe na Biashara Yako].

Kupitia "Business Card", WATU wataijua kwa Urahisi Biashara Yako Mahali Ilipo "physically" na Mitandaoni.

KARIBU SANA KWENYE KAMPUNI YA "LAMAX DESIGNS" UPATE HUDUMA YA "BUSINESS CARD" NZURI NA BORA ZAIDI. Ndani ya Lamax Designs UNAPATA UNACHOSTAHILI.

LAMAX DESIGNS: Providing You What You Deserve.




NJOO LEO UHUDUMIWE.
Mawasiliano! 0764793105

Kumbuka! UTAFUNDISHWA PIA NAMNA YA KUITUMIA "KADI BIASHARA" (Business Card) Yako.

AMUA LEO KUWA WA TOFAUTI. @lacksontungaraza


Mwalimu Emmanuel Makwaya aliwahi kusema ya kwamba, "HUNUNUI KITABU CHANGU KUNIPA MIMI FAIDA, BALI KUUPA UFAHAMU WAKO FAIDA"

Kuna Watanzania Wengi Leo ambao hudhani Kununua Vitabu ni Kuwatajirisha Waandishi wa Vitabu. Utawasikia wakisema, NGOJA TUKUUNGE KWENYE KITABU CHAKO HIKI!

Laiti kama Waandishi wa Vitabu wangekuwa wanaandika kwa Lengo la biashara, wasingekuwa Wanaviuza kwa Gharama ndogo za Tsh. 5000/= au Tsh. 10,000/=


-Waandishi wengi wa Vitabu Wanatoa HUDUMA kwenye Jamii, Sio kufanya BIASHARA.
Ingekuwa ni kwa Lengo la biashara; Vitabu vingekuwa vinauzwa hadi laki nane au Milioni Nne. Kwa Sababu wangekuwa wanakokotoa kwanza FAIDA ambazo Wasomaji wanaenda kuzalisha kupitia hivyo Vitabu - Results produced by the Book Content.

Fikiria! Kuna Waandishi ambao Wameandika VITABU vya Kukuza Biashara, Ufugaji wa Samaki au Sungura... Na kuviuza kwa Gharama ndogo ya Tsh. 10,000/= halafu Wewe Unaenda kuzalisha zaidi ya Milioni kupitia hivyo Vitabu.

Kwa maisha ya Sasa, Tsh. 5000/= au Tsh. 10,000/= inaweza Kununua Nguo Moja au Mbili za ndani kulingana na Jinsia au Mwuzaji, na baada ya Mwezi mmoja Huchakaa sana na kutupwa. Lakini KITABU cha Gharama hiyo hiyo ni HAZINA YA KUDUMU Kwako, kwa Wajukuu na kwa Uzao wako Wote KUTEGEMEANA NA UTUNZAJI WAKO.

□ Kwa hiyo, kuanzia Leo Usinunue Kitabu cha Lackson Tungaraza, Joel Nanauka, Pastor Raphael Lyela, Shemeji Melayeki, na Wengine Wengi kwa dhana ya KUWAUNGA- KUWASAIDIA WAO.


....KUNUNUA KITABU NI KUJISAIDIA WEWE MWENYEWE KABLA YA KUMSAIDIA MWANDISHI HUSIKA.

.... KUNUNUA KITABU NI KUJITAJIRISHA WEWE KWANZA, na Sio KUMTAJIRISHA MWANDISHI.

Acha Fikra Potofu, "Nikinunua Kitabu cha Lackson Tungaraza Nitamtajirisha, na Mimi nitabaki kuwa Maskini."

- Fikra Potofu Ndio Umaskini Wako wa Kwanza, Ukifuatiwa na Hofu ya Mabadiliko na Uthubutu.

TANZANIA BILA FIKRA POTOFU INAWEZEKANA!


Tuesday, August 7, 2018

Hakuna asiyelijua hili, ya Kwamba VIJANA Wengi sana HUBADILIKA sana Kitabia wanapofika VYUONI. Kiasi kwamba kuna baadhi ya Wazazi, Walezi, Na Ndugu ambao Husikitika kwa Kuona Watoto Wao Wakichaguliwa Kuingia Vyuoni kwa masomo ya Elimu ya Juu.

.... Kubadilika kwa tabia za Wanavyuo kumefanya Jamii Iwe na Mitazamo mibaya juu ya maisha ya Vyuoni.

I.... Kuna ambao Wameapa Ya kwamba HAWATAOA AU HAWATAOLEWA na WANAVYUO kwa Sababu tu Waliona Picha chafu za kingono za Wanavyuo mbali mbali, Na Pia Kusikia na Kuona Namna Wanavyoishi Katika vyumba vyao.

II... kuna ambao Wameapa Kuacha Kuwapangisha Wanavyuo Katika Nyumba zao za kupangisha kwa Sababu ya tabia zao za Kutembea na Waume au Wake za Watu, Kupiga kelele nyingi za Muziki N.K.

III.... kuna ambao Wameacha Kabisa Kuwaajiri Wanavyuo kwa Kuhofia kuibiwa na kuharibiwa biashara. N.K

INAWEZEKANA KUNA MTU UNAYEMFAHAMU; yaweza kuwa ni MTOTO wako, Rafiki, Ndugu, Jirani, N.k.. ambaye Yuko CHUONI au ANAKARIBIA KUINGIA CHUONI, Ebu mshauri sana Apate KITABU changu KIPYA kiitwacho "MWANACHUO DIARY." Ni Kitabu Kizuri sana ambacho kitamsaidia sana Kujua Yaliyomo Vyuoni ambayo Huwafanya  Wanavyuo wengi kuwa na TABIA mbaya Mara baada ya Kufika huko.

.... Wewe MZAZI au MLEZI nawe Unaweza kupata Kitabu changu ili Ujue namna ya KUWASAIDIA VIJANA WAKO.



ANGALIZO!
......................................
UKIWALETA WATEJA 10 WA KUNUNUA KITABU CHA "MWANACHUO DIARY" BASI WEWE UTAPATA KITABU KIMOJA BURE KABISA. Hivyo, Utapata Matunda Mazuri ya kuwa Sehemu Ya Kuwafikia Vijana ndani na Nje ya Tanzania.
.........................................

Ni Mimi Rafiki Yako,
#Lackson Tungaraza
-Mjasiriamali,
-Mwandishi wa VITABU N.K
 
#Mawasiliano! 0764-793105 au
0656-197242.

Thursday, January 18, 2018

All the so-called 'Secrets of Success' will not work unless you do--Unknown.

Siri za mafanikio ni nyingi sana na utaendelea kuzisikia na kuzisoma sehemu mbali mbali.. Mtandaoni, magazetini, vitabuni nk..... Sidhani kama kuna mtu humu ambaye hajawahi kutamani Mafanikio na kufikia kiwango cha kutafuta Siri yake kwenye vyanzo mbali mbali.
Nimekutana na Vijana wengi sana, wengine ni ndugu zangu... Wamesoma vitabu kadhaa vya mafanikio. Mfano WHY WE WANT YOU TO BE RICH, RICH DAD POOR DAD, THINK BIG, THINK AND GROW RICH, MIDAS TOUCH n.k....

~~~Wengne wameenda mbali zaidi hadi kuhudhuria Semina za waandishi wa Vitabu hivyo ili waipate ladha halisi... Kama kunywa Togwa ambayo haijachacha. Why are they not Successful!!!!!"



Lackson Tungaraza nimejifunza vingi kwenye vitabu mbali mbali nilivyosoma, awali nilikuwa siyo msomaji wa Vitabu kama baadhi ya wapuuzi wanavyosema ya kwamba WATANZANIA HAWAWEZI KUSOMA VITABU HATA UFANYAJE. Baada ya kusota na maisha kwa muda, siku moja nilikwenda kwa rafiki yangu kuongea naye mambo fulani ... Kipindi ananionesha baadhi ya nondo alizonazo kwenye Kompyuta, ghafla nikakiona kitabu cha THE BUSINESS OF 21st CENTURY cha Robert Kiyosaki. Nilikichukua na kuanza kukisoma ukurasa kwa ukurasa pamoja na kunakili vitu vya Muhimu.

~~Aissseh! Macho yangu yalitiwa Nuru kuanzia siku hiyo.. Cha kwanza ilikuwa ni juu ya MAPATO NA MATUMIZI. Namna ambavyo wengne wanakuwa matajiri zaidi na wengne maskini zaidi... Assets vs Liabilities.

~Success Secret brings results to those working on it. Bila kufanyia kazi ulichosoma utabaki tu vivyo hvyo kama anayejitazama ktk kioo akaondoka na baadae kusahau alivyo na kurudi tena kujitazama. JIFUNZE KUENDESHA GARI BARABARANI SIYO KWENYE KOMPYUTA KWA KUCHEZA GEMU. Umenipata hapo?

~~Kuwa Mtendaji wa yapo Mema unayoyaona na kuyasikia.. Hamna tofauti ya mtu aliyesomea Kilimo na hajui hata kushika jembe na yule ambaye hakusomea hicho... Tunahitaji kuona kitu kimetokea siyo kimetabiriwa.

---Kwa Leo tuishie hapa, Maoni yako yanakaribishwa kabisa.
TENDA, USISEME TU.
Lackson Tungaraza.
( www.facebook.com/ltungaraza )
0764793105 Whatsapp, sms.


FANYA JAMBO la Kumfanya MUNGU azidi Kuona  Umuhimu wa Kukuacha Uendelee kuwa HAI hapa duniani.

JAMBO la Kumfanya MUNGU aone KUNA PENGO wakati  wa Kuugua Kwako (Kupatwa na Magonjwa) ili AKUPONYE HARAKA URUDI KAZINI. Jambo la KUMPENDEZA  MUNGU na Kumkumbusha ili Upate UPENDELEO Kwake  {ISA 38:1-5}.


KUNA MAMBO AMBAYO MFALME HEZEKIA ALIFANYA HATA MUNGU AKAONA NI VYEMA AMUONGEZEE MIAKA YA KUISHI;


1: Kwenda Mbele za Mungu katika KWELI na kwa MOYO MKAMILIFU (Hakufanya DHAMBI Kwa SIRI)

2: Kutenda yaliyo MEMA MACHONI PA MUNGU (Hakutaka Kuwafurahisha WANADAMU KWANZA, BALI MUNGU KWANZA).

3: KULIA SANA SANA (Ishara Ya Uhitaji wa Hali ya JUU sana, Kuhurumiwa na BWANA)

{KILA TAWI LISILOZAA (Asiyeleta Mabadiliko Chanya kwenye Jamii Kiroho na Kimwili) HUONDOLEWA/HUKATWA (Yoh 15:2). Bali LIZAALO HUSAFISHWA (Mtu kuinuliwa Viwango hata Viwango, Upako hata Upako, Kibali hata Kibali) ILI LIZIDI KUZAA}

Ni PICHA gani ambayo watu huipata Katika Fahamu au Akili zao, Jina lako Linapotamkwa?

Mfano...
Michael Jordan-Mchezaji bora wa Mpira wa Kikapu.
C.Ronaldo-Mchezaji bora wa Mpira wa miguu
Steven Kanumba-Mwigizaji wa Filamu.
Julius Nyerere-Mwalimu na Mwasisi wa Taifa la Tanzania.

"IF YOU WANT TO BE SUCCESSFUL IN LIFE DON'T SEEK SUCCESS, SEEK TO BECOME A PERSON OF VALUE" -Dr. Myles Munroe

"ONGEZA THAMANI YAKO NA MAFANIKIO YATAKUFUATA MAHALI PO POTE UTAKAPOKUWEPO"

Tafuta Sababu ya KUISHI UWE MIONGONI MWA WAPINDUA ULIMWENGU.



TENDA, USISEME TU.
Lackson Tungaraza.
( www.facebook.com/ltungaraza )
0764793105 Whatsapp, sms.


Sunday, November 26, 2017

Usisubiri hadi Uzeeke, ndipo uanze kupata hamasa ya kutimiza ndoto... Rasilimali kubwa uliyonayo sasa ni Kwamba wewe ni kijana, unanguvu nyingi, afya njema. Usitumie nguvu zako vibaya katika kufanya mapenzi kiholela... Kadri unavyotumia hzo nguvu zako vibaya ndivyo unavyokaribisha Uzee .


Ndiyo maana kuna vijana ukiwatazama ni kama wazee... Sura zimekomaa hadi macho yameingia ndani, midomo imekauka kaukau... Kijana Shughulika sahivi.... Time is Limited.

Katika muda huo huo wa masaa 24, wengine wanatengeneza pesa nyingi na wewe hauna uhakika hata wa kuingiza shilingi mia. Time Is Money, how do you Invest your time?

Amka sasa bado mapema... Usidanganywe eti Kula ujana na wakati wanaokwambia kufanya hivyo wenyewe wanafanya kazi na wanauhakika wa kuingia pesa kila siku hata wasipoingia kazi... Cash flow.


KITABU NI Tsh. 5000/=
0764 793105


    NYI
    Lackson Tungaraza
     0764793105 whatsApp

Saturday, September 30, 2017

Haijalishi una Kazi ama hauna Kazi, kikubwa ni UTAYARI wako pamoja na Kiasi kidogo cha #PESA kuanzia Tsh.4000/=
Sasa Unaweza Kutengeneza Kipato cha Ziada (PESA) kupitia Kitabu changu "SITARUDI NYUMA TENA"
- Sitaki KUFANIKIWA mwenyewe, nataka nawe UFANIKIWE Kiuchumi.

Description: https://static.xx.fbcdn.net/images/emoji.php/v9/f5e/1/16/1f51b.pngUnatengenezaje sasa hicho kipato cha ziada?

Kuanzia tarehe 30/9 hadi tarehe 5/9/2017 Kitabu hiki Kitapatikana kwa Gharama ndogo tu ya Tsh.4000. NAWE UTAENDA KUUZA KWA GHARAMA YAKO AMBAYO ITAKUPATIA FAIDA (Mfano 4500, 4700, 5000 n.k)

Haijalishi Umeajiriwa, Umejiajiri ama Umeajiri, Kutengeneza Kipato cha ziada ni Jambo la Muhimu sana, tena sana.
☆Hii Itakusaidia pia wewe ambaye Hujapata AJIRA.
FAIDA NYINGINE UTAKAZOPATA; 
   1.Wateja Wangu Wote ambao Watakuwa Wanahitaji VITABU katika Mkoa au Wilaya Uliyopo, Nitawaelekeza Kuja kwako.
(Utanipatia Jina lako, Mawasiliano na Mahali Unapopatikana wakati wa kuchukua Vitabu)
Description: https://static.xx.fbcdn.net/images/emoji.php/v9/f51/1/16/1f449.pngNitakusaidia katika KUENDELEA KUTANGAZA KITABU.

   2.Utavirudisha kwangu ikiwa Havijauzika ndani ya Miezi miwili, na Kurudishiwa FEDHA yako (Hili Usiwe na Hofu ama Wasiwasi ya kwamba Utapoteza Fedha kwa Kukosa Wateja)

#ANGALIZO! Vitabu viwe kwenye MAZINGIRA Mazuri kama Ulivyochukua.
    3.Msaada wa namna ya Kuviuza Vitabu katika Maeneo uliyopo.



Description: https://static.xx.fbcdn.net/images/emoji.php/v9/f49/1/16/1f4da.pngKITABU "SITARUDI NYUMA TENA"

   1.Kinasubiriwa na Kupendwa na Watu wengi.
   2.Jina la Kitabu Linamvutia Mteja Kutamani Kujua Yaliyomo ndani yake.
   3.Kimetengenezwa kwa UBORA MZURI kuanzia kwenye COVER (Jalada) ambalo Halitaharibika Kirahisi hata Kikimwagiwa Maji kwa bahati mbaya.
   4.Kinabebeka Kirahisi (Portable) na hivyo Kuweza kwenda nacho po pote pale.
   5.Kina MAJIBU ya Watu Wengi.


Description: https://static.xx.fbcdn.net/images/emoji.php/v9/f28/1/16/1f352.pngKITABU HIKI KINAWAFAA WATU GANI (Wateja Utakaowauzia);

     1.Wanaopitia CHANGAMOTO Mbali mbali katika Maisha (Mfano Kutaka MAFANIKIO ya Kiuchumi, makundi rika n.k) na Namna ya KUZIVUKA.
-Hasa VIJANA (Mtu ye yote Yule ambaye Bado Hajazeeka ni Kijana, Haijalishi yuko kwenye Ndoa ama la)


     2.Ambao Hawajafahamu na Waliyokwisha Kufahamu Hatma yao (Destiny) katika Maisha, yaani Kule wanakotakiwa Kufika na Kuacha Kumbukumbu Chanya duniani.

{Bila Kujua Hatma Yako / Unapoelekea, Utakuwa Unatamani Kila siku kuwa kama Mtu fulani na Kushindana na Watu ambao Kimsingi Hujui Umbali Wanaokimbia. Zipo Hatua za Kukusaidia Kuifikia Hatma Yako}
   3.BINTI Atakaye kuwa na UZURI na UREMBO Usiopitwa na Wakati.
Nimeandika kwa LUGHA Nyepesi Mambo ambayo wanakutana nayo katika Maisha na Yamekuwa Mwiba wa Kuharibu ule UZURI na UREMBO ambao Mungu aliukusudia kwao.


Description: https://static.xx.fbcdn.net/images/emoji.php/v9/f60/1/16/1f51d.pngUnaweza KUJIULIZA Nimeyapata Wapi haya Yote!!

1: UZOEFU ambao Nimeupata Kupitia Mazingira mbali mbali ambayo Niliyapitia na pia Kuyaona.
2. Kwa Uweza wa Mungu mwenyewe.

Unakosaje Kuwa na Vitabu hivi au Kuongeza Kipato cha ziada!! Kazi ni kwako sasa.
Description: https://static.xx.fbcdn.net/images/emoji.php/v9/f51/1/16/1f449.pngBaada ya tarehe 5/10/2017, Kitabu hiki Kitapatikana kwa Gharama ya Tsh.5000/=


Mawasiliano!0764793105
Lackson Tungaraza.
Fb.com/ltungaraza
WAHI SASA KABLA HAVIJAISHA.

 

Saturday, September 2, 2017

Watu wengi hawataki kuwa huru kabisa.  Watu wengi hawataki kuachana na UTUMWA. Wakiambiwa, hawaamini, na Kudhani ya kwamba wanafatiliwa maisha yao.

Kati ya mambo yaliyomtia hamasa Mwalimu  Nyerere kuacha Ualimu na kuingia kwenye ulingo wa Siasa, ni Kupata Uhuru (wa watu pamoja na Nchi yao).

๐Ÿ‘‰Je wewe bado unataka uhuru, Una uhuru, au hutaki kuutumia vyema uhuru??

Uhuru ni jambo la msingi sana na la muhimu kabisa.

Kuna watu wengi sana ambao bado ni WAFUNGWA WA MAISHA YAO YA NYUMA (Historia). Kila wakitaka kupiga hatua moja mbele kuelekea kwenye maisha ya UBORA, wanakumbuka waliyoyapitia huko nyuma na namna walivyokuwa (mienendo), na hujishika tama na kukata tamaa. Hawako tayari kutumia maisha hayo kama Ndoano ya kunasa FURSA na KUWASAIDIA Watu wengine katika Jamii.

๐Ÿ‘‰Hilo janga Lipo hata kwa watu ambao wanasema ya kwamba WAMEOKOKA. Licha ya kwamba wanasema ya kwamba wamesafishwa kwa DAMU ya Kristo YESU,  lakini bado hawaamini kama ni Wasafi na hata maisha yao ya nyuma HAYAWEZI Kuwachafua tena. Wamekuwa WAFUNGWA wanaojimiliki. Wanajidai ya kwamba hawakuwahi kupitia maisha fulani hivi ya Uharibifu na yasiyo mpendeza Mungu. Hahaha!

Ikiwa bado Unajihukumu kwa kwa sababu hapo nyuma ulikuwa Mlevi, Kahaba, Mwongo, Mzinzi, Mwasherati, Mchawi, Shoga, Fisadi, Jambazi, Kibaka..

 Wewe ni MFUNGWA wa aina yake, hata kama unasema ya kwamba Kristo kakuweka Huru. "UHURU USIOKUWA NA NURU NI GUNDU"

Kama unaamimi kabisa ya kwamba Mtu anapokuwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe KIPYA na ya kale yamepita, kwa nini bado Umefungwa na HISTORIA ya maisha yako?? Kwa nini bado hujiamini!! Kwa nini bado una mashaka na kufadhaika moyoni mwako?

๐Ÿ‘‰Kupata UHURU ni tofauti na Kuutumia na Kuishi maisha ya Uhuru. Wewe umeupata, lakini huutumii na Kuuishi.

TUMIA hali ya maisha yako ya awali kama FURSA ya KUWASAIDIA wengine walio katika hali hiyo hiyo.

๐Ÿ‘‰Kuna #walevi ambao wanataka kuelimishwa na watu ambao washawahi kuwa Walevi pia. Vivyo hivyo kwa Wadada wanaojiuza, Waoga wa Kufanya BIASHARA, Washindwao Kuishi bila kuiba au kufanya NGONO n.k. Hao wote ni fursa yako, itumie.

Kwanini Usishuhudie namna ulivyopambana na hali ya Kushindwa Kusoma Biblia na Vitabu vingine, Ulivyoamka tena kibiashara baada ya kupata hasara, ulivyofaulu tena baada ya KUFELI mitihani mfululizo!! N.K

●(TUMIA ZAIDI HEKIMA YA MUNGU KATIKA KUFANYA YOTE)

"Be not a Prisoner of your Past Life style. Just be a Conquerer of it" 
Lackson Tungaraza.

Amรนa Leo Kumeza Dawa ya KUBADILIKA na KUWASAIDIA WENGINE.

Mtume Paulo alitumia hali ya maisha yake ya awali kama FURSA ya KUWASAIDIA wengine walio kwama papo hapo, waliokuwa hawaamini kama Inawezekana kuwa kiumbe KIPYA kabisa ndani ya Kristo... Nami Lackson Tungaraza Natumia Vivyo hivyo ili nawe utumie.

Acha mgomo baridi, unajipotezea MUDA. 

Na Lackson Tungaraza
Fb.com/ltungaraza


"Heri mtu Yule ayasikiaye maneno hayo na KUYAFANYA..."

( www.youtube.com/c/lacksontungaraza )

#Tukutane wakati ujao.
Shea na wenzako huu UJUMBE. Sharing is CARING.

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI