Monday, March 4, 2019


Siku Moja nikiwa Nyumbani kwa Wazazi Wangu, nilipata nafasi ya kwenda kusema na Vijana wa Shule Jirani ambayo ilikuwa mbali Kidogo. Kwa dhumuni la kuwahi, nikaamua kutafuta Bodaboda (Pikipiki). Baada ya Muda Mfupi, nikaipata na kuanza safari ya Kuelekea huko Shuleni. Nilipofika, nikamlipa Jamaa PESA Yake, na "kumwomba Namba za Simu" Ili nije nimshitue anifuate baadae.

Tatizo Mojawapo walilonao Watu wa Bodaboda ni "KUTOKUWAPATIA WATEJA NAMBA ZAO ZA SIMU (Mawasiliano)" Kabla ya Kuombwa. Wengi Wanaishi kwa MAZOEA ya Karne ya Kumi na Tisa - Wanataka Wawe Wanatafutwa na Wateja Mara kwa Mara kama vile Dhahabu za Geita.

Baada ya Kupata namba za Simu za Yule Jamaa wa Bodaboda, Nilikuwa namwita mara kwa mara kupitia Simu Anipeleke ninapohitaji. Ikiwa na maana ya kwamba, Alinufaika sana kwa kunipatia namba zake za Simu nilizomwomba badala ya Kunipatia Yeye Mwenyewe. Kumbuka; Wakati huo Ananifuata Nyumbani, wenzake Walikuwa Wamekaa tu VIJIWENI Wakisubiria WATEJA.

Cha Mwisho nilichomshauri Yule Jamaa wa Bodaboda ni "UMUHIMU WA KUWA NA KADI BIASHARA/ KADI KAZI (Business Card)." Nilimwambia, "Business Card" itamsaidia Kuondokana na Tatizo la Kutaja namba zake Kila Wakati, au Kuwaandikia namba kwenye Makaratasi. Na Pia Itamfanya Aonekane Anajitambua, na Anaithamini sana KAZI Yake (Professionalism).

NAWE UNAYEFANYA BIASHARA YA BODABODA au BIASHARA yo yote Ile, nakushauri sana Uwe na "Business Card" - Kitambulisho Chako cha Kibiashara [ambacho Sio cha Kiserikali. Bali ni cha Kukutambulisha Wewe na Biashara Yako].

Kupitia "Business Card", WATU wataijua kwa Urahisi Biashara Yako Mahali Ilipo "physically" na Mitandaoni.

KARIBU SANA KWENYE KAMPUNI YA "LAMAX DESIGNS" UPATE HUDUMA YA "BUSINESS CARD" NZURI NA BORA ZAIDI. Ndani ya Lamax Designs UNAPATA UNACHOSTAHILI.

LAMAX DESIGNS: Providing You What You Deserve.




NJOO LEO UHUDUMIWE.
Mawasiliano! 0764793105

Kumbuka! UTAFUNDISHWA PIA NAMNA YA KUITUMIA "KADI BIASHARA" (Business Card) Yako.

AMUA LEO KUWA WA TOFAUTI. @lacksontungaraza

Related Posts:

  • UNAKIMBIA KWA STAILI GANI? Moja ya tafsiri za Maisha nilizowahi kuzisoma na kuzisikia ni kwamba Maisha ni Mbio. Cha kujiuliza, “Unakimbizana na nani?” Nimegundua ya kwamba Maisha ni Mbio ambayo Mshindani ni wewe mwenyewe… unajipulizia mwenyewe kipen… Read More
  • LIFE IS A PROCESS [Maisha Ni Mlolongo Wa Mambo] Ni nini maana ya neno ‘Maisha?’ Kila mtu anaweza kutoa maana ya neno Maisha kwa yale aliyoyapitia, anayoyapitia au anayotarajia kukutana nayo mbeleni. Maisha yanamaana nyingi sana na kulingana na mtazamo wa kila mtu, ja… Read More
  • UMUHIMU WA RATIBA KATIKA MAISHA YAKO Maisha ya Mwanadamu yana mwanzo na mwisho, ikiwa na maana ya kwamba kuna kuzaliwa na kufariki. Lakini katikati ya kuzaliwa na kufariki kuna mambo ambayo Mwanadamu anatakiwa afanye ili aweze kustahimili hali ya kimwili na… Read More
  • PATA MAARIFA KWA KUWA MKIMYA ~ Wanadamu hata siku moja haitawahi kutokea tukawa sawa kimtazamo, kimienendo..never. Unaweza ukajiulza mbona Mimi ninajiheshima, mpole, mvumilivu lakini huyu ndugu yangu ni mkorofi sana, mlevi, mbeya, mzinzi n.k. Hyo … Read More
  • JE KIJANA UNAHAMU YA KUWA NA MAISHA YENYE FURAHA NA MAFANIKIO? Ni haki yako Kijana Mwenzangu kuwa na Maisha yenye furaha na Mafanikio. Tumia ushauri ufuatao ili uweze kufikia lengo hilo; … Read More

0 comments:

Post a Comment

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI