Showing posts with label MTAZAMO CHANYA. Show all posts
Showing posts with label MTAZAMO CHANYA. Show all posts

Thursday, January 18, 2018

FANYA JAMBO la Kumfanya MUNGU azidi Kuona  Umuhimu wa Kukuacha Uendelee kuwa HAI hapa duniani.

JAMBO la Kumfanya MUNGU aone KUNA PENGO wakati  wa Kuugua Kwako (Kupatwa na Magonjwa) ili AKUPONYE HARAKA URUDI KAZINI. Jambo la KUMPENDEZA  MUNGU na Kumkumbusha ili Upate UPENDELEO Kwake  {ISA 38:1-5}.


KUNA MAMBO AMBAYO MFALME HEZEKIA ALIFANYA HATA MUNGU AKAONA NI VYEMA AMUONGEZEE MIAKA YA KUISHI;


1: Kwenda Mbele za Mungu katika KWELI na kwa MOYO MKAMILIFU (Hakufanya DHAMBI Kwa SIRI)

2: Kutenda yaliyo MEMA MACHONI PA MUNGU (Hakutaka Kuwafurahisha WANADAMU KWANZA, BALI MUNGU KWANZA).

3: KULIA SANA SANA (Ishara Ya Uhitaji wa Hali ya JUU sana, Kuhurumiwa na BWANA)

{KILA TAWI LISILOZAA (Asiyeleta Mabadiliko Chanya kwenye Jamii Kiroho na Kimwili) HUONDOLEWA/HUKATWA (Yoh 15:2). Bali LIZAALO HUSAFISHWA (Mtu kuinuliwa Viwango hata Viwango, Upako hata Upako, Kibali hata Kibali) ILI LIZIDI KUZAA}

Ni PICHA gani ambayo watu huipata Katika Fahamu au Akili zao, Jina lako Linapotamkwa?

Mfano...
Michael Jordan-Mchezaji bora wa Mpira wa Kikapu.
C.Ronaldo-Mchezaji bora wa Mpira wa miguu
Steven Kanumba-Mwigizaji wa Filamu.
Julius Nyerere-Mwalimu na Mwasisi wa Taifa la Tanzania.

"IF YOU WANT TO BE SUCCESSFUL IN LIFE DON'T SEEK SUCCESS, SEEK TO BECOME A PERSON OF VALUE" -Dr. Myles Munroe

"ONGEZA THAMANI YAKO NA MAFANIKIO YATAKUFUATA MAHALI PO POTE UTAKAPOKUWEPO"

Tafuta Sababu ya KUISHI UWE MIONGONI MWA WAPINDUA ULIMWENGU.



TENDA, USISEME TU.
Lackson Tungaraza.
( www.facebook.com/ltungaraza )
0764793105 Whatsapp, sms.


Saturday, September 30, 2017

Haijalishi una Kazi ama hauna Kazi, kikubwa ni UTAYARI wako pamoja na Kiasi kidogo cha #PESA kuanzia Tsh.4000/=
Sasa Unaweza Kutengeneza Kipato cha Ziada (PESA) kupitia Kitabu changu "SITARUDI NYUMA TENA"
- Sitaki KUFANIKIWA mwenyewe, nataka nawe UFANIKIWE Kiuchumi.

Description: https://static.xx.fbcdn.net/images/emoji.php/v9/f5e/1/16/1f51b.pngUnatengenezaje sasa hicho kipato cha ziada?

Kuanzia tarehe 30/9 hadi tarehe 5/9/2017 Kitabu hiki Kitapatikana kwa Gharama ndogo tu ya Tsh.4000. NAWE UTAENDA KUUZA KWA GHARAMA YAKO AMBAYO ITAKUPATIA FAIDA (Mfano 4500, 4700, 5000 n.k)

Haijalishi Umeajiriwa, Umejiajiri ama Umeajiri, Kutengeneza Kipato cha ziada ni Jambo la Muhimu sana, tena sana.
☆Hii Itakusaidia pia wewe ambaye Hujapata AJIRA.
FAIDA NYINGINE UTAKAZOPATA; 
   1.Wateja Wangu Wote ambao Watakuwa Wanahitaji VITABU katika Mkoa au Wilaya Uliyopo, Nitawaelekeza Kuja kwako.
(Utanipatia Jina lako, Mawasiliano na Mahali Unapopatikana wakati wa kuchukua Vitabu)
Description: https://static.xx.fbcdn.net/images/emoji.php/v9/f51/1/16/1f449.pngNitakusaidia katika KUENDELEA KUTANGAZA KITABU.

   2.Utavirudisha kwangu ikiwa Havijauzika ndani ya Miezi miwili, na Kurudishiwa FEDHA yako (Hili Usiwe na Hofu ama Wasiwasi ya kwamba Utapoteza Fedha kwa Kukosa Wateja)

#ANGALIZO! Vitabu viwe kwenye MAZINGIRA Mazuri kama Ulivyochukua.
    3.Msaada wa namna ya Kuviuza Vitabu katika Maeneo uliyopo.



Description: https://static.xx.fbcdn.net/images/emoji.php/v9/f49/1/16/1f4da.pngKITABU "SITARUDI NYUMA TENA"

   1.Kinasubiriwa na Kupendwa na Watu wengi.
   2.Jina la Kitabu Linamvutia Mteja Kutamani Kujua Yaliyomo ndani yake.
   3.Kimetengenezwa kwa UBORA MZURI kuanzia kwenye COVER (Jalada) ambalo Halitaharibika Kirahisi hata Kikimwagiwa Maji kwa bahati mbaya.
   4.Kinabebeka Kirahisi (Portable) na hivyo Kuweza kwenda nacho po pote pale.
   5.Kina MAJIBU ya Watu Wengi.


Description: https://static.xx.fbcdn.net/images/emoji.php/v9/f28/1/16/1f352.pngKITABU HIKI KINAWAFAA WATU GANI (Wateja Utakaowauzia);

     1.Wanaopitia CHANGAMOTO Mbali mbali katika Maisha (Mfano Kutaka MAFANIKIO ya Kiuchumi, makundi rika n.k) na Namna ya KUZIVUKA.
-Hasa VIJANA (Mtu ye yote Yule ambaye Bado Hajazeeka ni Kijana, Haijalishi yuko kwenye Ndoa ama la)


     2.Ambao Hawajafahamu na Waliyokwisha Kufahamu Hatma yao (Destiny) katika Maisha, yaani Kule wanakotakiwa Kufika na Kuacha Kumbukumbu Chanya duniani.

{Bila Kujua Hatma Yako / Unapoelekea, Utakuwa Unatamani Kila siku kuwa kama Mtu fulani na Kushindana na Watu ambao Kimsingi Hujui Umbali Wanaokimbia. Zipo Hatua za Kukusaidia Kuifikia Hatma Yako}
   3.BINTI Atakaye kuwa na UZURI na UREMBO Usiopitwa na Wakati.
Nimeandika kwa LUGHA Nyepesi Mambo ambayo wanakutana nayo katika Maisha na Yamekuwa Mwiba wa Kuharibu ule UZURI na UREMBO ambao Mungu aliukusudia kwao.


Description: https://static.xx.fbcdn.net/images/emoji.php/v9/f60/1/16/1f51d.pngUnaweza KUJIULIZA Nimeyapata Wapi haya Yote!!

1: UZOEFU ambao Nimeupata Kupitia Mazingira mbali mbali ambayo Niliyapitia na pia Kuyaona.
2. Kwa Uweza wa Mungu mwenyewe.

Unakosaje Kuwa na Vitabu hivi au Kuongeza Kipato cha ziada!! Kazi ni kwako sasa.
Description: https://static.xx.fbcdn.net/images/emoji.php/v9/f51/1/16/1f449.pngBaada ya tarehe 5/10/2017, Kitabu hiki Kitapatikana kwa Gharama ya Tsh.5000/=


Mawasiliano!0764793105
Lackson Tungaraza.
Fb.com/ltungaraza
WAHI SASA KABLA HAVIJAISHA.

 

Sunday, January 22, 2017

Do you Need Success? Do you want a Life of Prosperity? Do you Love walking with God at Higher Standards? Are you Passionate of having a Job or a Business? WHAT DO YOU HAVE? UNA NINI?

Every Now and Then, People Seek New things, IGNORE what they have. Living their Wives to find Virgin Ladies, Living their Husbands to find sexual Satisfaction, withdrawing from one Political Party to another, buying New Clothes of Recent design, etc

Ni kweli ndani yako Mwaka huu Unataka Kuanza Biashara, Kuhubiri Injili, Kuwa Mwanasiasa, Kupata Ajira nk. Na ni Maombi yako kwa Mungu wakati wote.

MUNGU ANAPOKUJA KWENYE MAISHA YAKO, anaangalia "WHAT DO YOU HAVE? UNA NINI?" Ni nini unacho Unapotaka Kuanza hiyo Biashara, Unapotaka Kuoa au Kuolewa, Kupata Ajira, Kufaulu Mitihani? Je ni PESA, AU UTAYARI, AU IMANI, AU MAARIFA? UNA NINI!!
Mwanamke aliyetokwa Damu kwa muda wa  Miaka 12 alikuwa na UTAYARI NA IMANI, MUSA alikuwa na FIMBO MKONONI, PETRO alikuwa na MTUMBWI, SAULI alikuwa na MAARIFA YA TORATI. Wewe Una nini? Ebu angalia Scenario ifuatayo...


#Mathayo 14:15-20
[15]Hata kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na saa imekwisha pita; uwaage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula.
[16]Yesu akawaambia, Hawana haja kwenda zao, wapeni ninyi vyakula.
[17]Wakamwambia, Hamna kitu hapa ila mikate mitano na samaki wawili.
[18]Akasema, Nileteeni hapa.
[19]Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi, wanafunzi wakawapa makutano.
[20]Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, vikapu kumi na viwili, vimejaa.

LACKSON TUNGARAZA
what do you have? 2017:ENTER THROUGH THE
NARROW GATE.
Sentensi waliyosema Wanafunzi wa Yesu "Hamna kitu hapa ila mikate mitano na samaki wawili."  Inaonesha ni kwa Kiwango gani Walikuwa hawathamini Walichokuwanacho kwa wakati huo. Waliona ya kwamba kuna Njia nyingne inayotakiwa ili Makutano waweze kupata chakula, Wakajinunulie Chakula.

Yesu Kristo akawaambia wamletee hiyo mikate Mitano na Samaki wawili. Akashukuru na chakula kikawa cha kusaza, kwa sababu LITTLE IS MUCH WHEN GOD IS IN IT. Today God is Asking you again, WHAT DO YOU HAVE?
GIDEONI alikutwa ana Uwezo ndani yake (Uwezo wa Kupiga vita, Uwezo wa Kufanya Jambo kwa Bidii, Uwezo wa Kuongoza vitani nk). Neno linasema ya kwamba...


      #Waamuzi 6:11-16

[11]Malaika wa BWANA akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani.
[12]Malaika wa BWANA akamtokea, akamwambia, BWANA yu pamoja nawe, Ee shujaa.
[13]Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa BWANA yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba zetu, wakisema, Je! Siye BWANA, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani.
[14]BWANA akamtazama, akasema, Enenda kwa UWEZO wako huu, ukawaokoe Israeli na mkono wa Midiani. Je! Si mimi ninayekutuma?
[15]Akamwambia, Ee Bwana, nitawaokoa Israeli kwa jinsi gani? Tazama, jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase, na mimi ndimi niliye mdogo katika nyumba ya baba yangu.
[16]BWANA akamwambia, Hakika nitakuwa pamoja nawe, nawe utawapiga Wamidiani kama mtu mmoja.

Mungu akamwambia Gideon aenende kwa UWEZO WAKE HUO HUO (alichonacho) na atawapiga Midiani kama Mtu mmoja. How Wonderful!! Wewe una nini ambacho Mungu atakitumia Mwaka huu kukuvusha ng"ambo ya Pili? What do you have?




Inawezekana Unamlilia sana Mungu ili upate Mume, lakini Mungu anapokutaza haoni Kitu. Haoni ukiwa na Maarifa ya Ndoa, haoni ukiwa na Maono ya Familia unayoitaka, haoni ukiwa na Shauku ya kuwa na Ndoa bora ya kiMungu, upo upo tu. Unamlilia akupe Gari na hata Alama za barabarani hujui, kuendesha hujui. Unataka Kuanza biashara na hauna vitabu vya biashara,  hujui biashara gani unahitaji nk. Leo Lackson Tungaraza nakuuliza UNA NINI? Mungu anakuuliza "WHAT DO YOU HAVE TO CONVICE ME TO GIVE YOU A FAVOR?" FICHUKA, DISCOVER YOURSELF IN GOD. DISCOVER THE LOST YOU.

KUWA MUWAZI MBELE ZA MUNGU ITAKUSAIDIA SANA. Inawezekana kabisa HUJATAMBUA UWEZO ULIYONAO, UMEKATA TAMAA AT CETAIN POINTS, UNADHANI YA KWAMBA UWEZO ULIYONAO NI MDOGO SANA. kumbuka tu kwamba LITTLE IS MUCH WHEN GOD IS IN IT. KIDOGO ulichonacho kinaenda Kufanywa KIKUBWA kuanzia sasa. FIMBO ambayo Musa aliona ya kawaida, ILIGEUKA KUWA NYOKA MACHONI PA FARAO, ILIHUSIKA KATIKA KUFANYA BAHARI YA SHAMU KUWA NCHI KAVU NA ISRAELI WAKAPITA. Kikubwa ni Kumhusisha Mungu. Maandiko yanasema....

         #Isaya 40:28-31
[28]Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.
[29] Huwapa nguvu WAZIMIAO, humwongezea nguvu yeye ASIYEKUWA NA UWEZO*
[30]Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka;
[31]bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.


WHAT DO YOU HAVE? UNA NINI? sidhani kama bado utasubiri tena KUSHAWISHIWA ILI USOME VITABU, ILI UHUDHURIE SEMINA NA MAKONGAMANO, ILI UENDE KANISANI KUJIFUNZA, ILI UJIFUNZE KWA WALIYOTANGULIA NA KUFANIKIWA KATIKA ENEO LA MAISHA UNALOTAKA KUFANIKIWA PIA. Mwl. Makwaya anasema TO BE IS TO DO, Fred Msungu anasema BADILI CHANZO CHA TAARIFA, Apostle Shemeji Melayeki anasema TAKE THE FIRST STEP, Pastor Raphael Lyela anasema FICHUKA, Lackson Tungaraza anasema KIPAWA NI KAMA NYWELE KATIKA KICHWA CHA SAMSONI, UKIKILINDA NA KUKITUMIA VYEMA UTAFANIKIWA, USIPOFANYA HIVYO KINAKUANGAMIZA.

Ubarikiwe sana kwa Kupata Maarifa haya. Usiache Kupata Kitabu cha FICHUKA, DISCOVER YOURSELF IN GOD. Usiache kuwa rafiki yangu Facebook ili upate Maarifa zaidi (www.facebook.com/ltungaraza ) na Kuwa karibu na YouTube channel ( www.YouTube.com/c/LacksonTungaraza  ).

2017: ENTER THROUGH THE NARROW GATE.
©Lackson Tungaraza
0764793105 -whatsapp
0652493878

SHARING IS CARING. Shea Ujumbe huu na Wenzako. USIONDOE CHOCHOTE ILI UONEKANE UMEANDIKA WEWE. HUO UTAKUWA NI UFARISAYO WA HALI YA JUU! MUNGU AKUPE UWEZO WAKO BINAFSI. Amen!!!!






Tuesday, October 25, 2016

Ukubali, Ukatae.. Ukweli unabaki pale pale ya kwamba DUNIA NI UWANJA WA MAPAMBANO.

Karibu tupeane Maarifa kidogo hapa, Kujifunza Kitu Kipya Kila Mara ni sifa kubwa ya watu wenye Mafanikio Makubwa maishani.
-Binafsi napenda kujifunza sana Mambo mapya kila Mara.
💡Lackson Tungaraza💡

-Dunia ni Uwanja wa Mapambano kwa sababu Kila jambo unalohitaji kulipata linakuhitaji Kulitafuta kwa kila Namna, liwe dogo ama kubwa bado litahitaji kiwango cha Uhitaji wako ili Kulipata.

-Ikiwa Dunia ni Uwanja wa Mapambano, basi inabidi Kuwa na Silaha nzuri katika Vita.
-Tutakushangaa sana Unakuja na Fimbo/Rungu kwenye Uwanja huu wa vita ikiwa wenzako wanatumia Risasi na Mabomu.
-Na kama unahitaji hilo Rungu lako kummaliza mwenye risasi, itakulazimu Kumwinda akiwa amezubaa au kajisahau.

Silaha hizi siyo za Kumwaga damu. Ninachomaanisha ni MTAJI WAKO. Kitu au Njia unayotumia Kufikia Malengo au Hatma ya Maisha Yako.
-Najua unatamani sana Kufikia hatua kubwa ya Mafanikio katika Maisha yako. Lakini je! Ni silaha ya aina gani uliyoingia nayo katika Uwanja wa Mapambano.

-Wote kwenye Mtaa wako wana maduka ya Kuuza vyakula na bidhaa za Majumbani, wote ni Wanafunzi wa Kozi moja, wote ni wakulima wa mazao, wote ni Waandishi wa blog na Vitabu nk.
-Katika hali kama hiyo, ni Silaha gani unazotumia ili kutoka katika Uwanja huu wa mapambano ukiwa Mshindi? Amua kutumia silaha nzuri na zenye nguvu zaidi.

     🔫 Silaha hiyo yaweza kuwa Ni Kipaji, Kipawa, Ufundi, Ujuzi, Ujanja, Elimu, Maarifa nk.
-Namna utakavyoitumia hiyo Silaha, itaashiria kama Utashinda Mapambano au la.
-Silaha bila Makali au Kujua Kuitumia, bado hautakuwa Mshindi mzuri. Soma Vitabu mbali mbali kulingana na Vita unayopigana, Jifunze kwa waliofanikiwa, Andika katika *Diary au NoteBook* mambo mapya unayojifunza kila wakati.
Akina Bill Gates, Erick Shigongo, Mwl Mwakasege nk.. Wamefika hapo baada ya Kutambua aina ya vita wanayopigana na aina ya silaha ya Kupambania.

    *Don't hunt Something that you cannot Kill*
-Pambana na jambo ambalo Unauwezo wa Kulishinda kulingana na aina ya Silaha na Pambano ulilonalo.
-Mimi nishatambua aina ya Vita ninayopigana na nimeshachagua Silaha za Kupambania ili nimalize salama nikiwa Mshindi, maana *DUNIA NI UWANJA WA MAPAMBANO*

KUMBUKA! Bahati NA Wakati (0pportunity and Time) Kila mtu Kapewa na Mungu.
-Itategemeana tu na USHAPU Wako.
-Mfalme Sulemani anatuambia hapa jambo hilo lenye Faraja kwa màskini na Matajiri pia

   🔦 Mhubiri 9:10-11🔦

[10]Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.

[11]Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini *wakati na bahati huwapata wote*.💡

-Kwahiyo kuwa Mjanja kila unapoingia katika Mapambano ambayo yapo hapa duniani.
-Pigana sana, utapumzika Ukifika mbinguni baada ya Kupambana vyema na Kutetea Imani ya kweli ambayo Mungu kaiweka ndani yako kwa njia ya Wokovu

✍Salamu zangu Kutoka kwake Yeye aliyeñiwezesha Kuziandika✍
Lackson Tungaraza
HAKUNA KURUDI NYUMBA, HADI KIELEWEKE


#MPAMBANÀJI_ATUMAINIYE_KATIKA_UWEZA_WA_BWANA YESU.
⛹Lackson Tungarazà


 (SUBSCRIBE Kwenye Channel yàngu ya YouTube).




Kuwa Rafiki yangu Facebook, tumia;
- www.facebook.com/ltungaraza

💣KIMENUKISWA!!!
*Akasema, YOTE IMEKWISHA.
LIFE is PERFORMANCE. Na Mara unapoanza Kuperfom ndipo unaanza kutambua aina ya wasikilizaji na watazamaji ulionao. Aidha wako pamoja nawe, au la. That's how life is in this world.

Bahati Bukuku anasema SONGA MBELE.. UNAPOIANZA SAFARI wanakutia Moto, UNAPOONESHA MAFANIKIO wanainua Vikwazo. Unaanza kushangaa IMEKUWAJE TENA!!

We chunguza maisha ya wale waliokuwa pamoja nawe kabla ya safari; kabla ya kuanza biashara, kabla ya kukataa umaskini, kabla ya kupata mchumba/mke/mume, kabla ya kupata ajira/kazi, kabla ya kuanza kuonesha dalili za mabadiliko katika maisha yako. WAMEGEUKA UPANDE, WASITAKE KUKUTAZAMA TENA.

Hiyo ni hali ya kawaida kabisa. Upendo wa Kweli hujidhihirisha wakati kama huo...at the Period of transformation.
*Unashangaa ndugu, rafiki, jirani na jamaa hawana mahusiano mazuri tena na wewe.
*Kama walikuwa wanakupigia Simu, huoni tena, mchango wa harusi hawatoi,

*Wakisikia Umefukuzwa chuo, umefeli masomoni, umefukuzwa kazini, umepewa talaka... Wataanza eehee! Tulijua tu hafiki mbali. Mbio za sakafuni huishia Ukingoni. Kwani wangapi wameshindwa! Ye ndiyo uweze!! Limempata la Uso.
*Sahivi wako Kimya wanasubiri wakuone utafikia wapi katika biashara yako hiyo, Huduma au wito ulionao*
Usiogope, Usirudi Nyuma. DO THE PERFORMANCE.


*Hii pia ni sababu ya watu kuendelea kubaki katika hali ile ile ya maisha miaka yote. Mtu akifanikiwa anatengwa! Badala ya kuwekwa karibu na kujifunza kutoka kwake.
YOU WILL NEVER BE RICH UNTIL YOU LOVE THE RICH PEOPLE.
*Rich people are not Greedy to that extent. That's why they solve your daily life problems*

Mabadiliko yanahitaji Self-commitment. Kujitoa mzima mzima bila kujali makele ya watu wasiotaka mabadiliko ya wengne, wanataka kila MTU awe kama wao. KELELE ZA MBU HAZITOBOI NETI.
UTASHANGAA hata ndugu yako wa damu anakuchukia na hata kukupangia kukuua. Kivipi!! Tusome hapa

*Mwanzo 4:1-8*

[1]Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa BWANA.
[2]Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi.
[3]Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa BWANA.
[4]Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake;
[5]bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. *Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.*
[6]BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
[7] *Kama ukitenda vyema, hutapata kibali?* Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.
[8]Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]. Ikawa walipokuwapo uwandani, *Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua.*


CHUKI ni mbaya sana. Inaua kanisa, familia, taifa na dunia kwa ujumla. Umuhimu wake haupo.
Mungu anamwuliza Kaini, *KAMA UKITENDA VYEMA HUTAPATA KIBALI?*
Nawe jiulize swali hilo.

Nawe anza kufanya kazi kwa bidii, kuimba, kaoe/kaolewe, kasome Vitabu na kuhudhuria semina, kajifunze kwa Waliofanikiwa... Na UTAPATA KIBALI NAWE PIA.
CHUKI itakuua mapema, na Mbinguni hautaingia kwame hata kama unafanya kazi ya Mungu kwa kiwango gani.

*Yeye asemaye kwamba Yuko Nuruni, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa* #1 Yoh 2:9

Ubarikiwe sana, na jisemee kwa Kuapa..
*"IT'S NOT OVER UNTIL I WIN"
# I don't stop when I'm Tired, I stop when I'm done.


©Lackson Tungaraza
0764793105 whatsapp
Google plus: www.google.com/+LacksonTungaraza  

Site: http://lacksontungaraza.blogspot.com

Success at Door
#BORN TO MAKE A DIFFERENCE IN YOUR GENERATION
Haikuwa jambo jepesi kuacha shughuli zake, Umaarufu wake, Ulinzi, Utajiri na kuja kututembelea huku kwetu. Sidhani kama wewe msomaji ungeweza kufanya hivyo.
Yeye aliweza, pasipo manung'uniko wala hamu ya kutamani kurudi huko alikotoka kwa haraka. He was happy being with us
Na huyo siyo mwingne, Bali ni Yesu Kristo.

*Najua kuna majina ya watu wengne ambao umeamua kuwafuata ukiamini ya kwamba kwa kufanya hivyo utamwona Mungu kwa uwepesi. WE ALWAYS FOLLOW PEOPLE DEPENDING ON THEIR ABILITY TO SOLVE OUR PROBLEMS.
NDIYO!! Huwa watu wanaamua kumfuata mtu fulani kulingana na uwezo aliyonao katika kutatua Changamoto au Matatizo yao ya kila Mara. Na ndivyo ilivyokwako, ukachagua kumwamini huyo unayemwamini ili umwone Mungu.

ANASTAHILI SIFA HIZI. Kwa Upande wangu; Huyu Mwanaume Yesu alinivutia sana na kuamua kumuamini kwa asilimia kubwa sana... His history made me Inspired.
‼Nitaongelea jambo hili wakati mwingne.

     Namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kuwepo tena Huu mwezi wa Kumi. Sidhani kama ni mazoezi au vyakula nilivyokula. Ni Yeye tu.
    Na kufika mwezi huu, inamaana ya kwamba imebaki tu miezi miwili mwaka kuisha.
     Fikiria umefikisha Asilimia ngapi ya Yale uliyopanga kufanya ndani ya huu mwaka 2016. Inawezekana hata moja hujafanya!!

Kipindi Mwaka unaanza, nilisikia msukumo ndani yangu kwa kiwango kikubwa ya kwamba Mwaka huu utakuwa *mwaka wa Mabadiliko* na nikaandika na kufundisha katika mitandao ya kijamii.
     Walioamini, watakuwa wameshaona nilichomaanisha. Wale akina Tomaso, watakuwa bado wanasubiri kupapasa.

Lackson Tungaraza
KUTOKUKATA TAMAA KUMENIFIKISHA MBALI SANA KIMAISHA. NAWE USIKATE TAMAA, NAFASI YAKO BADO IPO, MUNGU YU HAI KUKUSAIDIA KWA ASILIMIA MIA MOJA.


     Mungu kanipitisha katika mambo makubwa na kunikutanisha na watu mbali mbali walioniongezea thamani... Kwenye basi, hotelini, sokoni... Kote huko Mungu aliwaleta. KUNA NGUVU KUBWA SANA KATIKA IMANI. Increase your Believing percentage.
Na hivyo ninapoelekea mwisho wa Mwaka huu, natazamia neno moja kama Mtume Paulo alivyofanya;

*Wafilipi 3:12-13*

[12] Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.
[13] Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele;

Yes… Nikiyasahau yaliyo ya nyuma (majonzi, hasara, usaliti, changamoto) na kuyachuchumilia yaliyo mbele (Maono, mipango, malengo). HIYO NJOZI HAITASEMA UONGO, IJAPOKAWIA INGOJEE

    Nawe pia sahau yaliyokuumiza tangu mwaka uanze, na utazamie Maono yaliyo ndani yako. GOD ONLY PROMISES A SAFE DESTINATION, DESPITE OF A DANGEROUS JOURNEY
'WHEN YOU LOSE, DONT LOSE THE LESSON.'-Lama.

Mark Twain aliongezea kwa kusema,

*Twenty years from now you will be more disappointed by the things you didn't do than by the ones you did*

     Siri kubwa ya kufeli katika maisha, Ni kujitahidi kumpendeza kila MTU. Ukubali, ukatae ndivyo ilivyo.
‼Ukitakà kumpendeza kila mtu badala ya kumpendeza Mungu na Kutimiza Kazi iliyowekwa ndani yako na Mungu.. You are already a Failure.
Hivyo niliamua kufuata Maono yaliyo ndani pasipokutazamia mazingira yanasemaje, au watu wanawaza nini juu ya maisha Yangu kwa namna wanionavyo.

Hata Yesu walimuoana ndivyo sivyo na hakusumbuka ili awapendeze wajinga;

  *Mathayo 11:18-19*

[18] Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakasema, Yuna pepo.
[19] Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake.

Huwezi kuwapendeza wanadamu katika kila jambo.. Inawezekana hata unavyovaa au kula wanajisikia vibaya. Hawataki hata kukuona ukifanikiwa.!

CHA KUFANYA?
    Jisalimishe katika Mikono salama ya Mungu ili akushindie yote, na kisha fuata Ndoto na Njozi iliyoko ndani yako bila kusita-sita.
AMUA Kufanya jambo ambalo litakuwa katika KUMBUKUMBU ya kwamba mwaka 2016 haukuishi kwa hasara, Bali kwa Faida.

Uwe na Maamuzi mema, Mungu awe nawe.

YOURS SINCERELY,
              ©Lackson Tungaraza
     📞0764793105 (call or whatsapp)
Facebook: www.facebook.com/ltungaraza
Library: http://lacksontungaraza.blogspot.com (CHOTA MAARIFA HAPA).

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI