Showing posts with label UNAJUA KWA NINI UMEKWAMA KIMAISHA? Sikiliza Hapa. Show all posts
Showing posts with label UNAJUA KWA NINI UMEKWAMA KIMAISHA? Sikiliza Hapa. Show all posts

Monday, May 6, 2019


A- Kwenye biashara kuna kukuru kakara nyingi sana. Unaweza Ukapoteza pesa zako zote ulizoanzishia.

B- Fursa yo yote Ile ina Hatari ya kupata HASARA kabla ya FAIDA, tofauti Ipo kwenye Asilimia.

C- Mradi/BIASHARA yenye FAIDA kubwa sana ina hatari/vikwazo Vikubwa pia. Na kama FAIDA ni Ndogo, basi na hatari zake ni za kawaida. UNAWEZA UKAFUGA KUKU NA WAKAFA WOTE AU KUIBIWA

Ndivyo BIASHARA zilivyo.Matajiri wakubwa kama Donald Trump nao Walishakumbwa na hiyo mikasa - kuna Kipindi aliwekeza na kufilisika kabisa.

Kwa hiyo: "kabla ya kujiingiza kwenye biashara au FURSA, tathimini kama una Uwezo wa kustahimili hasara yo yote Ile utakayoipata huko mbeleni." - Lamax.


"USHUHUDA WANGU."

- Nilipokuwa Chuo Kikuu cha Dodoma mwaka wa Pili, nilipata WAZO la kuanza kuuza viatu vya Kiume. Kwa hiyo nikachukua pea kadhaa za viatu Dar na kwenda navyo chuoni, nikiamini ya kwamba Vitapendwa na kuuzika Fasta. Nilipofika nikaandaa Tangazo na kubandika sehemu mbali mbali chuoni, na Pia Kusambaza kwenye Makundi ya WhatsApp.

Baada ya hapo nikaanza kusubiria Wateja. Mungu Sio Athumani, Wakaanza kuja, lakini Kila kiatu wanachopima wanasema Hawapendi Rangi, Hawapendi Muundo, au Hakuna vya Kuwatosha (Kwa maana ya size). Jambo hilo likawa linaniuma sana. Lakini nikaendelea kuwa na Uvumilivu. Baada ya Muda vikanunuliwa viatu kadhaa na vingine kubaki vikiwa vinanikodolea tu macho.

Baada ya Kuona ya kwamba Vinanijazia tu nafasi Chumbani kwangu na haviuziki, nikamtafuta jamaa niliyekuwa najuana naye, nikampatia hivyo viatu aviuze. Wakati wa Likizo, Jamaa akavichukua viatu vyote na kwenda navyo nyumbani kwao kijijini. Nilipomwuliza Baada ya Muda fulani, jamaa akaniambia Wadogo zake walivichukua na kuvivaa. Hilo Jambo lilinikera sana ajabu. Lakini nikamwacha nilipoona ya kwamba shida ilikuwa kwangu kwa kumwamini mtu asiyejua kuwa makini na biashara. Kwahiyo nikapoteza zaidi ya laki moja.

"WATU WENGI WANASHINDWA KUNUFAIKA KWENYE FURSA NA BIASHARA WANAZOZICHAGUA kwa Sababu ya MIHEMUKO MINGI YA KUONA YA KWAMBA WATAFANIKIWA HARAKA HARAKA. Na hiyo yote inatokana na MAHESABU YA KWENYE MAKARATASI."

Naamini Kuna Jambo Zuri sana ulilojifunza hapa, basi Litendee Kazi. Na kama Unahitaji Vitabu vyangu LACKSON TUNGARAZA usisite kuwasiliana nami moja kwa moja WhatsApp kwa kubofya hii LINK: https://wa.me/255764793105 . UNAWEZA KUPATA VITABU VYA HARD COPY (Nakala Ngumu) na SOFT COPY (Nakala Laini ya kusomea kwenye Simu au Kompyuta yako.




By Lackson Tungaraza.
@LACKSONTUNGARAZA.
AMUA LEO KUWA WA TOFAUTI.


TAJIRI MKUBWA SANA DUNIANI AITWAYE SULEMANI Alisema hivi;

A) Atendaye Mambo kwa Mkono mlegevu huwa Maskini  (Kwa hiyo kuwa Maskini ni Matokeo ya kufanya mambo kwa Ulegevu/Unyonge/Liwalo na Liwe); Bali MKONO WAKE ALIYE NA BIDII HUTAJIRISHA (kila aliyetajirika ni kwa sababu ya kufanya kazi Yake kwa BIDII - sio kwa Kujaribu Jaribu).

B) Katika KILA KAZI "MNA FAIDA"; Bali Maneno ya Midomo huleta HASARA tu (Yaani kuongea tu bila kufanya KAZI ni kujiletea hasara maishani).

C) Alimaye Shamba lake atakuwa na Chakula TELE; Bali afuataye Mambo ya Upuuzi ATAPATA UMASKINI WA KUMTOSHA (Huo UMASKINI Utakuwa wa VIWANGO vya 4G au zaidi).

D) Je! Wamwona Mtu mwenye BIDII katika KAZI Yake? Huyo Atasimama mbele ya Wafalme ( atapata KIBALI kwa Watu waliofanikiwa zaidi. Hao Watu ndio watakuwa Watu wake wa karibu); Hatasimama mbele ya Watu Wasio na Cheo (hutamkuta kwa Watu wasiopenda kazi).

By Lackson Tungaraza.

Kupata Vitabu vya Lackson Tungaraza kama Cha SITARUDI NYUMA TENA, MWANACHUO DIARY, MBINU 16 ZA KUONGEZA MAUZO KWENYE BIASHARA YAKO, NAMNA YA KUSOMA KITABU, n.k. njoo WhatsApp kwa kubofya hii LINK: https://wa.me/255764793105



Saturday, March 16, 2019

Watu Wengi huwa Wananunua Vifurushi vya Intaneti Ili Waelimike Mtandaoni, Lakini huwa hawafikii hayo Malengo Yao.

- Unakuta Mtu anaingia YouTube ili apate Elimu ya kumsaidia Kukua Kiroho au Kiuchumi, lakini anaishia kuangalia Comedy  (Vichekesho), Mieleka ya WWE, Video za Ngono  (Pornography), Udaku, Series, Taarifa ya Habari, N.k.



- KIFURUSHI KINAPOISHA, au kinapokaribia kuisha, ndipo Wanakumbuka walichokuwa wanataka Kujifunza. Na tabia hiyo hujirudia tena na tena baada ya Kununua Vifurushi vingine vya Intaneti. Nami Lackson Tungaraza nilikuwa Vivyo hivyo hapo Awali.


UNAJUA SHIDA NI NINI??

- SHIDA ni kwamba hawajui kwa Kina wanachotaka Kujifunza, kwa nini wanataka Kujifunza hicho wanachotaka Kujifunza  (Nia na Sababu ya kujifunza), na kutokuwa na Nidhamu binafsi (Self-Discipline) ya Kujiongoza.

Inawezekana kabisa nawe unayesoma huu ujumbe ni Muhanga  (Victim) wa hilo, Usihofu Ikiwa utaamua Kubadilika kuanzia Sasa. Sasa FANYA YAFUATAYO KABLA YA KUINGIA FACEBOOK, INSTAGRAM, YOUTUBE, N.K;

(I) Fahamu Unataka Kujifunza nini na kwa Nani (Mtu anayefundisha Unachokitaka, au Kama ni Page au Channel ya YouTube).

(II) Fahamu ni KWA NINI Unataka Kujifunza  (Nia na Sababu Yako ya Kujifunza).

(III) ANDIKA Mahali Yale Yote Unayotaka Kujifunza YouTube. Mfano!
- Jinsi ya Kutengeneza Sabini ya Unga.
- Faida za Nyama tamu ya Sungura. N.k.

(IV) Ingia Mtandaoni na kuanza kutekeleza hatua hiyo ya (III) hapo Juu. Ikiwa na maana ya kwamba UWE NA NIDHAMU BINAFSI YA KUJISIMAMIA, KUJIZUIA USIANGALIE au USIFANYE AMBAYO HUKUPANGA, na Kuweza KUJIONGOZA  (Leading Yourself).
Kumbuka kutumia "SEARCH BUTTON" (Kitufe cha Kutafutia unachokitaka) Kupata Yale uliyopanga Kujifunza YouTube.

(V) Ondoka Mtandaoni UKAFANYIE KAZI ULICHOJIFUNZA au ULICHOPAKUA MTANDAONI  (What you Downloaded from the Internet).


KWA KUFANYA HIVYO;

(I) Utakuwa unaokoa muda wako mwingi (Time saving).

(II)  Utakuwa unatumia vyema Vifurushi vya Intaneti kama ulivyokusudia. Na Pia

(III) Utakuwa Mbali na mambo yasiyokuhusu ambayo yangekupotezea Muda Wako na Kuharibu Tabia Yako njema - kwa Sababu Mazungumzo mabaya na Marafiki Wabaya huaribu tabia Njema.


Naamini Utakuwa umejifunza Jambo la Kukusaidia unapokuwa Mtandaoni. Usisahau kutendea kazi na Kushea hili Somo Zuri sana kwa Rafiki zako waliyopo Facebook, Messenger, Instagram, WhatsApp, Twitter, n.k. Uwe na Siku njema sana. Ni Mimi Rafiki Yako Lackson Tungaraza  (Lamax).

AMUA LEO KUWA WA TOFAUTI.
@LACKSONTUNGARAZA
0764793105 - WhatsApp

Friday, March 8, 2019


Furahia Kila Siku Mpya ambayo Unapewa na Mwenyezi Mungu. Usipofurahia Leo uliyopewa na Mungu, Unadhani Kesho na Kesho kutwa zina nini cha Ajabu sana ambacho Kitakupa Furaha.?

Hata Kama Unawaza sana Juu ya Kupata Pesa ya Kulipa Kodi ya Nyumba, Ada za Watoto Shuleni, Mahari, Mkopo wa Benki... Furaha Isikuondoke Kabisa, hasa Furaha ya BWANA - Kwa Sababu Furaha ya BWANA ndiyo NGUVU Yako.


Kuna Wakati Unaweza Ukadhani ya kwamba Ukipata Aina fulani ya Simu, Gari, Nyumba, Mavazi, Watu, au Kiwango fulani cha Pesa, ndipo Utapata Furaha Isiyokuwa Kifani. Lakini huo Uongo mkubwa sana. Nakuhakikishia ya kwamba Utabaki kuwa vile vile hata Kama Utavipata Kupita Ulivyotarajia. Kuwa na Furaha ni Kuamua kutokea Ndani Yako hata Kama huna pesa, Mali, Umaarufu, n.k.

Wengi Mlitamani Kufika Vyuo vikuu na Kupata Digrii kwa Kuamini ya Kwamba Ndipo Mtapata Heshima Kubwa Kwenye Jamii na Kuwa na Furaha Isiyokuwa Kifani, Lakini baada ya Kufika huko Vyuoni na Kisha Kuhitimu, Mmegundua ya Kwamba MAMBO NI YALE YALE Kama ya Shule ya Msingi, Sekondari, na Mtaani. Wengine Mlidhani Mkioa na Kuolewa ndipo Mtakuwa na Furaha, Mlidhani Mkiajiriwa Kwenye Kampuni Kubwa na Kupata Mishahara Minono ndipo Mtayafurahia Maisha... hahahaha! Yote Yamekuwa Ubatili Mtupu kwa Sasa! Mmegundua ya kwamba Mlikuwa Mnakimbiza Upepo Msiojua Utakako wala Uendako.

Lengo Sio Kumkebehi yeyote Yule, Bali Kukushauri Uwe na Furaha ya BWANA hata Kama huna Yale Unayodhani Unayahitaji kwa Sasa. Furaha ni ya Muhimu sana. WaPo Wenye pesa nyingi na Mali lakini Hawana Furaha kwa Sababu hawana Afya Njema. Wewe uliye na Afya Njema lakini huna pesa na Mali, Mshukuru Yehovah Yahweh kwa hilo. Maadam Uko hai na una Afya Njema, Unaweza Ukapata vingine Kama Kawaida.

USIKUBALI KUTOKUWA NA FURAHA KWA SABABU YA MATOKEO MABAYA YA SHULENI, KUKOSA AJIRA, MSHAHARA MDOGO, KUTOKUOLEWA, KUTOKUWA NA PESA YA KUFANYIA BIASHARA, KUTOKUWA NA WATU WA KUKUTIA MOYO, N.K.

MAISHA NDIYO HAYA HAYA, YAFURAHIE KATIKA BWANA. Imeandikwa, "MAISHA ni zaidi ya CHAKULA, na MWILI zaidi ya MAVAZI."

IFURAHIE LEO, KESHO ITAAKISI FURAHA YAKO YA LEO.

       ..Ahsante sana.
Mawasiliano: +255-764793105.
@lacksontungaraza
AMUA LEO KUWA WA TOFAUTI.

Saturday, August 18, 2018

UNAJUA KWA NINI UMEKWAMA KIMAISHA? Sikiliza Hapa Kukwama Kimaisha limekuwa jambo endelevu katika Jamii zetu za Afrika. Je Wajua ni Kwanini? Sikiliza hapa kisha toa maoni yako. USISAHAU Ku_SUBSCRIBE na Kushea. https://ift.tt/2GO1hEL

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI