Kijana mwenzangu kabla hujaanza kusumbuka kutafuta pesa kila
mahala kwaajili ya biashara.
Kwanza Fanya maamuzi ni biashara gani unayohitaji
kufanya, hiyo ni hatua ya kwanza kabisa. Kwanini ufanye uwamuzi kwanza? Ili
kukupa Nidhamu ya pesa.
Pesa pia inahitaji Nidhamu kubwa, hivyo bila nidhamu pesa
yako itapotea bure. Utakuta baada ya kupata pesa unaanza kuwaza sijui nifungue
hoteli au niuze mbao au nichome Mahindi au niuze kitimoto n.k lakini
ukishatambua biashara gani utafanya ukishapata pesa yako, utakuwa na nidhamu
Mara baada ya kuipata pesa hiyo.
Jambo la pili:
baada ya kufahamu ni biashara gani utafanya
baada ya kupata fedha. Ni vyema pia ufanye uchunguzi juu ya uendeshwaji wa hyo
biashara... Kama ikiwezekana nenda hata mtaa wa pili au wilaya nyingine na kutafuta
Mtu ambaye anafanya biashara hyo na umuulize yeye jinsi
alivyoweza kufanikiwa... Kumbuka kuwa na mazungumzo yenye hekima siyo
kukurupuka tu kama mtu aliyeng'atwa na nyoka halafu akatupiwa Jani shingoni.
Acha Aibu, uliza waliokutangulia na ninaona vyema iwe ni mtu ambaye Yuko mbali
na mahali hapo ulipo ili asipate ugumu wa kukupa siri ya mafanikio.
Jambo la Tatu,
Weka Juhudi katika biashara uliyoamua
kuifanya... Kwa moyo wako wote...uipende biashara yako. Focus.
F-Follow
O-One
C-Course
U-Until
S-Successful
Hakikisha unatumia kila mbinu kuifikisha biashara yako
katika hatua kubwa. Siyo Leo unashona nguo, kesho unauza viazi na kesho kutwa
umefungua kibanda cha chips. Wekeza faida katika biashara yako ili iwe kubwa.
Jiulize: unadhani Barhesa hana pesa ya kuanza kutengeneza nguo na kuuza? Anazo
pesa nyingi tu lakini ameamua kuFOCUS... Kufanya kile ulichonacho kuwa uhai
wako. Fanya hiyo baishara kwa ustadi mkubwa na utafanikiwa tu. Love what you do
and you will be successful.
“Success is
not the Key to Happiness. Happiness is the key to Success. If you love what you
are doing, you will be successful” –Albert Schweitzer.
Ahsante sana. Karibu kwa maswali na Mchango wako
WhatsApp: 0764793105 [Lackson Tungaraza]
Facebook: www.facebook.com/ltungaraza
Instagram: LACKSONTUNGARAZA
0 comments:
Post a Comment