Showing posts with label ROLE MODEL WETU WA LEO. Show all posts
Showing posts with label ROLE MODEL WETU WA LEO. Show all posts

Thursday, January 18, 2018

All the so-called 'Secrets of Success' will not work unless you do--Unknown.

Siri za mafanikio ni nyingi sana na utaendelea kuzisikia na kuzisoma sehemu mbali mbali.. Mtandaoni, magazetini, vitabuni nk..... Sidhani kama kuna mtu humu ambaye hajawahi kutamani Mafanikio na kufikia kiwango cha kutafuta Siri yake kwenye vyanzo mbali mbali.
Nimekutana na Vijana wengi sana, wengine ni ndugu zangu... Wamesoma vitabu kadhaa vya mafanikio. Mfano WHY WE WANT YOU TO BE RICH, RICH DAD POOR DAD, THINK BIG, THINK AND GROW RICH, MIDAS TOUCH n.k....

~~~Wengne wameenda mbali zaidi hadi kuhudhuria Semina za waandishi wa Vitabu hivyo ili waipate ladha halisi... Kama kunywa Togwa ambayo haijachacha. Why are they not Successful!!!!!"



Lackson Tungaraza nimejifunza vingi kwenye vitabu mbali mbali nilivyosoma, awali nilikuwa siyo msomaji wa Vitabu kama baadhi ya wapuuzi wanavyosema ya kwamba WATANZANIA HAWAWEZI KUSOMA VITABU HATA UFANYAJE. Baada ya kusota na maisha kwa muda, siku moja nilikwenda kwa rafiki yangu kuongea naye mambo fulani ... Kipindi ananionesha baadhi ya nondo alizonazo kwenye Kompyuta, ghafla nikakiona kitabu cha THE BUSINESS OF 21st CENTURY cha Robert Kiyosaki. Nilikichukua na kuanza kukisoma ukurasa kwa ukurasa pamoja na kunakili vitu vya Muhimu.

~~Aissseh! Macho yangu yalitiwa Nuru kuanzia siku hiyo.. Cha kwanza ilikuwa ni juu ya MAPATO NA MATUMIZI. Namna ambavyo wengne wanakuwa matajiri zaidi na wengne maskini zaidi... Assets vs Liabilities.

~Success Secret brings results to those working on it. Bila kufanyia kazi ulichosoma utabaki tu vivyo hvyo kama anayejitazama ktk kioo akaondoka na baadae kusahau alivyo na kurudi tena kujitazama. JIFUNZE KUENDESHA GARI BARABARANI SIYO KWENYE KOMPYUTA KWA KUCHEZA GEMU. Umenipata hapo?

~~Kuwa Mtendaji wa yapo Mema unayoyaona na kuyasikia.. Hamna tofauti ya mtu aliyesomea Kilimo na hajui hata kushika jembe na yule ambaye hakusomea hicho... Tunahitaji kuona kitu kimetokea siyo kimetabiriwa.

---Kwa Leo tuishie hapa, Maoni yako yanakaribishwa kabisa.
TENDA, USISEME TU.
Lackson Tungaraza.
( www.facebook.com/ltungaraza )
0764793105 Whatsapp, sms.


Saturday, September 9, 2017

Asomae na asome kwa Umakini na Kuelewa Lengo la Makala hii.

Kabla ya Hadithi kuanza kusimuliwa, huanza Hadithi! Hadithi! Hapo zamani za Kale… Nami katika Kutafakari jambo hili, nikakumbuka hapo zamani za kale za Mama yao Wana wa Zebedayo aliyemwendea Yesu pamoja na wanawe, akamsujudia na kumwomba neno, kwamba Wanae wawili WAKETI Mmoja mkono wa wake wa Kuume na mmoja mkono wake wa Kushoto katika Ufalme wake. Yesu akajibu akasema, ‘Hamjui Mnaloliomba. Je! Mwaweza KUNYWEA KIKOMBE NITAKACHONYWEA MIMI? Wakamwambia, Twaweza. Akawaambia, hakika Mtakinywea Kikombe changu; lakini Kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, sina amri kuwapa, bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu’

Kikombe alichokuwa ananywea Yesu kilikuwa kimebeba Bidii ya Kufanya Maombi binafsi mlimani pasipokuwa na watu, kukesha, kubezwa, kutokuaminiwa na nduguze, mateso, majaribu, kukanwa na kusalitiwa.

Kuna GHARAMA KUBWA YA KUKETI PAMOJA NA YESU, KUNA GHARAMA KUBWA YA KUKINYWEA KIKOMBE ALICHONYWEA YESU.

Kuna Gharama Kubwa ya Kutaka kuwa kama mtu fulani (Mtume Paulo, Mwl. Mwakasege, Apostle Shemeji Melayeki, Bishop Gwajima, Bishop Moses Kulola, Mwl. Mwambeso, Mwl. Makwaya, Pastor Raphael JL n.k.). Viti vya Kuketi pamoja nao, na vikombe wavinyweavyo vinasiri nzito sana na ngumu. Hivyo hesabu gharama kabla ya kutaka kuketi pamoja nao (upande wa kushoto au wa kulia) na kunywea vikombe vyao.

Kuna gharama ya kuketi pamoja na Lackson Tungaraza, na kunywea kikombe chake. Kwanini? Kwa sababu kuna wakati anabezwa, anasalitiwa, anapitia majaribu, anakesha katika kuutafuta Uso wa Bwana kwa kila namna ikiwa ni pamoja na Kufunga wakati wengine wanaendelea Kula bata. Kuna wakati anajisikia KUKATA TAMAA ya kuendelea Kuandika Masomo yake Mtandaoni kwa yale anayopitia maishani lakini ANAJIPA MOYO kama Kristo alivyosema, huku AKIAMINI kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa na wakata tamaa. Zaidi sana ni juu ya idadi ya watu ambao Mungu amewaandaa ili Wamjue Yeye kupitia Masomo yake ya mtandaoni na ya ana kwa ana. Hivyo akikata tamaa, DAMU yao itakuwa juu yake na atadaiwa na Mwajiri wake (MUNGU) siku ya Kiama.

Mara nyingi amekoswa watu wa Kumtia Moyo katika yale anayoyafanya tofauti na Kristo aliye rafiki yake wa karibu zaidi, na Mshauri wake wa kwanza. Amekutana na akina DELILA wengi kwenye maisha yake, lakini rafiki yake wa karibu zaidi (Yesu Kristo) alimsaidia.

Wewe unayetaka kuwa kama Lackson Tungaraza, Je! Unaweza Kukinywea Kikombe chake? Usione vyaelea, vimeundwa. Remember, ‘Behind any Success there is a Secret to find’ Lackson Tungaraza once wrote in his articles. Nyuma ya mafanikio yo yote yale kuna Siri ya kupata na Kujifunza.



Ni kweli huwa unamfurahia sana Lackson Tungaraza kwa yale ayafanyayo lakini niliyokuandikia leo sio Uongo, kama huamini mtafute umwulize kwa hekima kwa lengo la Kujifunza kwake (0764793105 WhatsApp, SMS). Ni mmoja wa Wapindua Ulimwengu kwa ajili ya Kristo Yesu.

Hakuna marefu yasiyokuwa na Ncha. Tukutane siku nyingine, kwa masomo mengine na kwa siri zingine. Bye bye!!

‘I must first count the price of being like You, Lackson Tungaraza’


WEKA ODA YAKO MAPEMA. KITAANZA KUPATIKANA KWA GHARAMA YA TSH.4000 TU KABLA YA KUZINDULIWA MWISHO WA MWEZI HUU. UTATUMIWA POPOTE PALE.
0764793105

Saturday, September 2, 2017

Jina lake kamili ni Maza Sinare Mchome. 
 
Alipokuwa anaongea katika Kipindi cha Ndoano ndani ya Wanawake live tv ya JOYCE KIRIA, alisema ya kwamba alipokuwa Mdogo alikuwa anaweka 2000 juu ya meza na kuisemeza ya kwamba hataitumia hadi iwe 4000. 

Pengine ilichangiwa na aina ya wazazi aliokuwa nao, maana walikuwa ni wachapakazi sana. Mamake alikuwa Fashion designer na Fundi Cherehani mzuri, na babaye alikuwa Daktari wa Mifugo.


MAZNAT alisoma sana na kupata vyeti kadhaa vya kiheshima, lakini MWISHO wa siku aliamua kuweka Vyeti pembeni na Kuanza KUJIAJIRI. 


Nilijifunza mambo kadhaa kutoka kwake kama ifuatavyo;


1. MTAZAMO

MAZNAT alikulia maisha ya kuwa na Mtazamo Chanya katika Kila jambo alilokuwa akikutana nalo. Mtazamo huo ulimwezesha Kupiga hatua sana Kimaisha, na Mtazamo huo ulichangiwa pia na aina ya watu waliokuwa wakimzunguka kwanzia kwenye familia yao na kwingine. 

☆Hivyo ni muhimu sana kuwa na MTAZAMO CHANYA. Haijalishi Aina ya FURSA unayopata, pesa unazoingiza, nafasi yako katika Jamii. JAMBO kubwa ni Mtazamo, una Mtazamo gani??


2. DHARAU
Dharau ya jambo lolote ni mbaya. MAZNAT alishawahi kuuza Vocha, Ubuju, Maji, Big G, mitumbe, house Girl n.k. 

#Chochote ambacho hakimkosei Mungu ni vyema kukifanya pasipo kukidharau. Hata kama kinakuingizia Fedha ndogo au kubwa, kiheshimu kabisa. Acha kudharau hicho kidogo unachofanya leo. Wajasiriamali wakubwa unaowaona, nao walikuwa wadogo hapo awali.

Kumbuka MAZNAT alikuwa akiheshimu hata biashara ya Big G, kusaga Unga wa Watoto n.k.


3. UTHAMINI.

MAZNAT alikuwa msomi, lakini hakujali hilo, akaanza kufanya biashara ndogo ndogo kwa kuzithamini sana. MWISHO wa siku zikamtoa Kimaisha.

☆Hivyo ni vyema kuthamini biashara au kazi ufanyayo hata kama hailingani na vyeti vyako au haiendani na Mtazamo wa watu kwako. Kuna walioanza kuuza Vitumbua na sasa ni wamiliki wa Hoteli kubwa, walianza kucheza mpira wa mchangani na sasa wanacheza Ligi kuu TANZANIA bara na wengine wako Ulaya. Kila kitu ni hatua. Nyumba ya ghorofa 30 huanza kwa Tofali moja. Wazungu husema, "ROME WASN'T BUILT IN A SINGLE DAY." Kwahyo THAMINI unachofanya sasa, uwe na UVUMILIVU na IMANI juu ya mambo YATARAJIWAYO bayana na Yale Yasiyoonekana kwa sasa.

KWA upande mwingine, MAZNAT alikulia maisha ya kubanwa sana na WAZAZI wake. Alikuwa hapati MUDA WA kukaa KIHASARA HASARA wakati wa Likizo. Alikuwa anapewa pesa baada ya KUFANYA KAZI KWANZA. Siku moja alifanya kazi vizuri sana na KUPEWA Tsh. 10,000. Akaichukua hiyo Fedha na kuanzisha Home English Tuition Center, akapata wanafunzi kadhaa aliokuwa akiwafundisha Kiingereza hapo kwao. Kwa sasa ni Mfanyabiashara Mkubwa anayemiliki MAZNAT BRIDAL CARE nk

☆Hivyo WAZAZI nao wana NAFASI kubwa sana ya Kuwafanya watoto wao kuwa Wachapakazi na wajasiriamali wakubwa. Waswahili husema,"Mtoto Umleavyo ndivyo Akuavyo, SAMAKI MKUNJE ANGALI MBICHI" na Wazungu husema, "CHARITY BEGINS AT HOME"

KWA yote hayo niliyoandika hapa, MAZNAT ni mfano mzuri sana wa wanawake wa kuigwa katika Jamii. Ni mfano mzuri kwa MABINTI na wamama ambao wanajiona Hawafai au Hawawezi kufanya mambo makubwa katika Jamii zao. Pia ni mfano kwa VIJANA ambao walidhani ya kwamba Wanawake wote ni Wadhaifu kikazi nk.

Aliyeandika haya ni Lackson Tungaraza
Facebook! fb.com/ltungaraza
WhatsApp!0764793105

☆NI WAKATI WA KUACHA LAWAMA NA KUPIGA KAZI. HUU NI MSIMU WA 'HAPA KAZI TU'
Watumie na wenzako Wajifunze pia.

Tuesday, October 25, 2016

Haikuwa jambo jepesi kuacha shughuli zake, Umaarufu wake, Ulinzi, Utajiri na kuja kututembelea huku kwetu. Sidhani kama wewe msomaji ungeweza kufanya hivyo.
Yeye aliweza, pasipo manung'uniko wala hamu ya kutamani kurudi huko alikotoka kwa haraka. He was happy being with us
Na huyo siyo mwingne, Bali ni Yesu Kristo.

*Najua kuna majina ya watu wengne ambao umeamua kuwafuata ukiamini ya kwamba kwa kufanya hivyo utamwona Mungu kwa uwepesi. WE ALWAYS FOLLOW PEOPLE DEPENDING ON THEIR ABILITY TO SOLVE OUR PROBLEMS.
NDIYO!! Huwa watu wanaamua kumfuata mtu fulani kulingana na uwezo aliyonao katika kutatua Changamoto au Matatizo yao ya kila Mara. Na ndivyo ilivyokwako, ukachagua kumwamini huyo unayemwamini ili umwone Mungu.

ANASTAHILI SIFA HIZI. Kwa Upande wangu; Huyu Mwanaume Yesu alinivutia sana na kuamua kumuamini kwa asilimia kubwa sana... His history made me Inspired.
‼Nitaongelea jambo hili wakati mwingne.

     Namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kuwepo tena Huu mwezi wa Kumi. Sidhani kama ni mazoezi au vyakula nilivyokula. Ni Yeye tu.
    Na kufika mwezi huu, inamaana ya kwamba imebaki tu miezi miwili mwaka kuisha.
     Fikiria umefikisha Asilimia ngapi ya Yale uliyopanga kufanya ndani ya huu mwaka 2016. Inawezekana hata moja hujafanya!!

Kipindi Mwaka unaanza, nilisikia msukumo ndani yangu kwa kiwango kikubwa ya kwamba Mwaka huu utakuwa *mwaka wa Mabadiliko* na nikaandika na kufundisha katika mitandao ya kijamii.
     Walioamini, watakuwa wameshaona nilichomaanisha. Wale akina Tomaso, watakuwa bado wanasubiri kupapasa.

Lackson Tungaraza
KUTOKUKATA TAMAA KUMENIFIKISHA MBALI SANA KIMAISHA. NAWE USIKATE TAMAA, NAFASI YAKO BADO IPO, MUNGU YU HAI KUKUSAIDIA KWA ASILIMIA MIA MOJA.


     Mungu kanipitisha katika mambo makubwa na kunikutanisha na watu mbali mbali walioniongezea thamani... Kwenye basi, hotelini, sokoni... Kote huko Mungu aliwaleta. KUNA NGUVU KUBWA SANA KATIKA IMANI. Increase your Believing percentage.
Na hivyo ninapoelekea mwisho wa Mwaka huu, natazamia neno moja kama Mtume Paulo alivyofanya;

*Wafilipi 3:12-13*

[12] Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.
[13] Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele;

Yes… Nikiyasahau yaliyo ya nyuma (majonzi, hasara, usaliti, changamoto) na kuyachuchumilia yaliyo mbele (Maono, mipango, malengo). HIYO NJOZI HAITASEMA UONGO, IJAPOKAWIA INGOJEE

    Nawe pia sahau yaliyokuumiza tangu mwaka uanze, na utazamie Maono yaliyo ndani yako. GOD ONLY PROMISES A SAFE DESTINATION, DESPITE OF A DANGEROUS JOURNEY
'WHEN YOU LOSE, DONT LOSE THE LESSON.'-Lama.

Mark Twain aliongezea kwa kusema,

*Twenty years from now you will be more disappointed by the things you didn't do than by the ones you did*

     Siri kubwa ya kufeli katika maisha, Ni kujitahidi kumpendeza kila MTU. Ukubali, ukatae ndivyo ilivyo.
‼UkitakĂ  kumpendeza kila mtu badala ya kumpendeza Mungu na Kutimiza Kazi iliyowekwa ndani yako na Mungu.. You are already a Failure.
Hivyo niliamua kufuata Maono yaliyo ndani pasipokutazamia mazingira yanasemaje, au watu wanawaza nini juu ya maisha Yangu kwa namna wanionavyo.

Hata Yesu walimuoana ndivyo sivyo na hakusumbuka ili awapendeze wajinga;

  *Mathayo 11:18-19*

[18] Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakasema, Yuna pepo.
[19] Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake.

Huwezi kuwapendeza wanadamu katika kila jambo.. Inawezekana hata unavyovaa au kula wanajisikia vibaya. Hawataki hata kukuona ukifanikiwa.!

CHA KUFANYA?
    Jisalimishe katika Mikono salama ya Mungu ili akushindie yote, na kisha fuata Ndoto na Njozi iliyoko ndani yako bila kusita-sita.
AMUA Kufanya jambo ambalo litakuwa katika KUMBUKUMBU ya kwamba mwaka 2016 haukuishi kwa hasara, Bali kwa Faida.

Uwe na Maamuzi mema, Mungu awe nawe.

YOURS SINCERELY,
              ©Lackson Tungaraza
     📞0764793105 (call or whatsapp)
Facebook: www.facebook.com/ltungaraza
Library: http://lacksontungaraza.blogspot.com (CHOTA MAARIFA HAPA).

Saturday, January 16, 2016


WILLIAM H GATES III 

 
WILLIAM H GATES III
William H Gates III , anajulikana kama Bill Gates. Alizaliwa tarehe 28 Oktoba 1955 na kulelewa katika kijiji cha Seattle pamoja na dada zake wawili. Baba yake ni Attoney na marehemu mama yake alikuwa mwalimu tu wa kawaida wa shule. Katika umri wake mdogo Bill Gates alivutiwa na utengenezaji wa programu akiwa katika mojawapo wa shule kijijini Seattle. Akiwa huko shuleni Seattle, Bill Gates alikutana na Paul Allen , mwanafunzi mwenzake wakawa marafiki.Hapo ndipo wakaanza kutumia tarakilishi ndogo ya shule kuendeleza ujuzi wao, kama ambavyo pia wanafunzi mbalmbal duniani wanavyotumia elimu ya darasan na elimu ya kijamii kuvumbua mitandao mbalmbal ya kijamii n.k.

Baadaye Bill Gates akaenda kujiunga na  Chuo Kikuu cha Harvard kwa masomo ya elimu ya juu. Kwa mara nyingine tena akajiunga pamoja na Paulo kuandika toleo jipya la programu ya Msingi wa lugha ya kwanza ya kompyuta ya kibinafsi, iitwayo Altair 8800. Kampuni iliyotumia program hiyo iliridhishwa na kazi ambayo Bill Gates na Paul Allen waliofanya na programu hiyo ikapewa leseni.
Jambo hili liliwachangia Gates na Allen Kuanzisha kampuni ya Microsoft, iliyokuwa ikitengenezea kampuni zingine programu. Bill Gates aliacha masomo yake katika chuo kikuu cha Harvard na kujishughulisha muda wake wote katika biashara.
MICROSOFT COMPANY YA BWANA BILL GATES NA PAUL ALLEN

Funzo: Fanya lile jambo unalolipenda maishan kwa juhudi kubwa, usiige ya engine kwa sababu umeona wamefanya jambo Fulani. Mungu kakupatia jambo la kipekee ndani yako, usijidharau. YOU ARE GENIOUS, INVEST ON YOUR TALENTS.
Mafanikio yao yalikuja walipotengeneza mfumo wa kuendesha kompyuta uitwao MS-DOS uliotumika katika kompyuta ya kwanza ya kibinafsi ya IBM. Baadaye waliweza kuzishawishi kampuni zingine zinazotengeneza kompyuta kutumia mfumo huo wa MS-DOS. Mfumo huu mpya wa MS-DOS ulipata umaarufu katika soko miaka ya 1980.

Kipindi cha miaka mitano baadaye Microsoft ilitoa mifumo mipya ya Windows 2.0 iliyokuwa bora zaidi kuliko mifumo ya hapo awali. Kampuni ya Microsoft iliweza kupata umaarufu zaidi katika soko la hisa, na akiwa umri wa miaka 31, Bill Gates aliweza kuwa bilionea mchanga zaidi katika historia ya Marekani.
MAGARI YAKE YALIYOPO NYUMBANI

BAADHI YA MAENEO ANAYOMILIKI BWN. BILL GATES

Bill Gates alifunga ndoa na Melinda French Gates mwaka wa 1994 na wakabarikiwa na watoto watatu, Jennifer, Rory na  Fibi. Wote wawili Bill na Melinda ni waanzilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali. Waliweza kulianzisha shirika la Bill na Melinda Gates Foundation ambalo limesaidia kutoa michango mbalmbal ya kuiendeleza jamii pamoja na watu wasiojiweza. Ubunifu wa Bill Gates wa kutengeneza programu umekuwa mchango wake katika mapinduzi ya kompyuta na sayansi ya kompyuta.
Tangu Mwaka 1995 amekua namba moja katika orodha ya matajiri wakuu (forbes) duniani isipokua mwaka 2008 ambapo alikua namba 3 akiwa na utajiri wa takribani dola bilioni 58 za kimarekani. Mwaka huo Bw. Warren Buffet ndio alikua mtu namba mmoja akiwa na utajiri takribani dola za kimarekani bilioni 62 akifuatiwa na Bw.Carlos Slim akiwa na utajiri wa takribani dola bilioni 60 za kimarekani. Unaweza usijue lakini kila sekunde Bill Gates anaingiza takribani dola 250 za kimarekani, Na kwa dakika nzima anaingiza takribani dola 15000. Unashangaa?? . Bill Gates anaweza akagawa Dola 15 za kimarekani kwa kila mtu duniani na bado akabakiwa na dola milioni 5 za kimarekani mfukoni. Kama akiangusha dola 1000 za kimarekani hana haja ya kuziokota kwa sababu ndani ya sekunde 4 ambazo angeweza kuziokota angekuwa tayari amesha zirudisha . Ukiachana na kompyuta, pia Bill Gates ni muandishi. Mpaka sasa ana vitabu viwili amabavyo ni ”The Road Ahead'” na ‘Business at the Speed of Thought’.
BAADHI YA PESA ZA JAMAA, SIYO UCHAWI, 
NI REAL



Kwa Leo, hayo yanatosha kujifunza kutoka kwa Role Model wetu, Bwn. Bill Gates. Unalipi la kuongezea juu ya huyu jamaa, Mr. Bill Gates?.. Unaweza changia hapa na pia kuwashirikisha na wengine wajifunze (share)

MORAL OF THIS:
1: Kuna wakati ambapo sisi kama wanadamu tunatenda mambo ambayo hatuyapendi kutoka moyoni; bali kwa sababu ya tamaa zetu binafsi. Watu wanafanya kazi ambazo hawazipendi kutoka mioyoni ila kwa sababu mishahara ya hizo kazi ni minono.

2. Ukitenda jambo ambalo hulipendi kutoka moyoni, tambua ya kwamba hutopata mafanikio ambayo ulipaswa kupata katika maisha yako na pia hayo mafanikio hayatakuwa ya kudumu. Bwana Bill Gates na wengine wengi wamekuwa na mafanikio makubwa sana hadi hii leo kwa sababu waliweza kutenda yale ambazo waliyapenda kutoka mioyoni mwao. Anza leo kuwekeza nguvu kubwa katika fani, kipaji na ujuzi ulionao. Elimu ya shuleni ni daraja tu la kukutanisha na vitu fulani ambavyo Mungu anataka uvijue kabla ya kufika kule unakotaka  kwenda. Usiitegemee sana kuliko kipaji chako.

3. Watu waliowekeza katika fani, ujuzi na vipaji vyao wamefika mbali sana kimafanikio. Mfano Lionel Messi, Christian Ronaldo, Samatta, Diamond, Ambwene, Rose Muhando n.k. Japo kuwa elimu zao za darasani siyo kubwa kivile

4. Naamini kabisa ya kwamba 2016, Mwaka Wa Mabadiliko na kuinuliwa na Bwana katika maisha yako. Wekeza pia katika kutafuta elimu ya kiMungu katika maisha yako. Hvyo unaweza kuungana name katika kampeni ya kuleta ukombozi katika maisha yao kuanzia mwaka huu. Kampeni yangu inaitwa 2016, MWAKA WA MABADILIKO NA KUINULIWA kama ambavyo picha hii ya chini inavyoelezea;
USIPITWE NA MAONO HAYA JUU YA MAISHA YAKO, 2016, YEAR OF VICTORY.



Thursday, January 14, 2016


JULIUS K. NYERERE


Tunayo mengi ya kujifunza na kujivunia kwa mwalimu nyerere, Mwasisi na Baba wa taifa la Tanzania.
MWL. JK NYERERE 

AKIWA NA RAIS WA AWAMU YA NNE, DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, 
MZEE WA ARI MPYA, NGUVU MPYA NA KASI  MPYA

Kuzaliwa na Malezi
Julius Kambarage Nyerere alizaliwa April 12/1922 katika ardhi ya Tanganyika, na alifariki tarehe 14/10/1999 mjini wa London Uingereza. Alizaliwa katika kijiji cha Butiama, karibu na pwani ya mashariki ya Ziwa la Victoria. Nyerere alikuwa mmoja wa watoto ishirini na sita wa baba yake, Nyerere Burito. Baba yake alikuwa kiongozi wa kabila la Zanaki. Pia baba yake alikuwa na fedha nyingi lakini hakuwa na  elimu kubwa.

Wakati wa utoto wake, Julius Nyerere alichunga mifugo na alikuwa na maisha ya kawaida. Nyerere alikuwa mfuasi wa dini ya Katholiki, alihudhuria misa mara kwa mara. Watu wanasema alipenda sana kucheza na kufanya mizaha. Pia alichonga meno yake ya mbele na msumeno kuonyesha utamaduni wa kabila lake.

Elimu
Julius Nyerere alijiunga na Shule ya Msingi ya Serikali katika mji wa Musoma wakati alipokuwa na miaka kumi na miwili. Alimaliza masomo ya miaka minne kwa miaka mitatu kwa sababu alikuwa na akili sana, alienda kusoma Shule ya Upili ya Serikali ya Tabora. Huko, alipata udhamini wa kwenda Chuo Kikuu cha Makerere. Ni muhimu kujua wakati alipopata udhamini huo, Makerere kilikuwa Chuo Kikuu cha pekee katika Afrika ya Mashariki. Alipata shahada yake hapo.

Baada ya chuo kikuu, Nyerere alirudi Tanganyika na alifanya kazi katika Shule ya Upili ya St. Mary katika mji wa Tabora. Shule ya St. Mary, ilikuwa shule ya katoliki. Huko, alifundisha masomo ya Biolojia na Kiingereza. Mwaka 1949, alipata udhamini wa kwenda kusoma katika Chuo Kikuu cha Edinburgh, hivyo akawa Mtanzania wa kwanza kusoma chuo kikuu nchini Wingereza na Mtanzania wa pili kupata digrii nje ya Afrika.

Katika chuo kikuu cha Edinburgh, Nyerere alipata Shahada ya juu ya Sanaa katika Historia na Uchumi, mwaka 1952. Akiwa Edinburgh, alisoma mkondo wa kufikiri unaoitwa “Fabian.” Mkondo wa “Fabian”, ulijumuisha kundi la wataalamu wa Ujamaa wa Uingereza. Azimio la “Fabian” ni kuendeleza mawazo ya kijamaa. Kwa sababu alijifunza mawazo ya “Fabian,” alianza kufikiri mabadiliko mazuri sana yangepatikana ikiwa angeweza kuunganisha ujamaa na maisha ya Afrika. Wakati wa maisha yake, Nyerere aliitwa “mwalimu” kwa sababu ya kazi zake za uelimishaji.

Ndoa na Familia
Kabla ya maisha yake ya kuwa mwanasiasa, alioa mwanamke aliyeitwa Maria Magige. Maria alitoka kabila tofauti. Wanahistoria walisema alioa mwanamke wa kabila lingine kuonyesha dunia,ilikuwa muhimu sana kusahau tofauti baina ya makabila na kuwa wamoja.

Mchango Katika Jamii
Mchango mkuu wa Nyerere katika jamii ni kazi aliyofanyia serikali. Lakini kwanza tusisahau kwamba, Nyerere alikuwa mwalimu wa historia, Kiingereza, na Kiswahili. Hivyo alianza shughuli za kisiasa alipokianzisha chama cha TANU (Tanganyika African National Union) kupigania uhuru kwa nchi za Tanganyika. Ndani ya mwaka mmoja tu, TANU ilikuwa na watu wengi wapya na ilikuwa ikiongoza  miradi ya kisiasa Tanganyika. Kwa sababu Nyerere alianza kujihusisha na siasa, hivyo alihitaji kuamua baina ya maisha ya uwalimu au ya uwanasiasa. Alijiuzulu kutoka kufundisha, na kuwa Mwanasiasa .

Alisafiri ndani ya Tanganyika kuzungumza na watu wengi na viongozi tofauti, kujaribu kupata msaada katika harakati za uhuru wa Tanganyika. Katika mwaka 1954, alifaulu kuunganisha jamii mbalimbali kitaifa pamoja kusaidia harakati za uhuru.  Nyerere alikuwa na ujasiri wakuzungumza, ujasiriuliomsaidia alipozungumza na UN (Umoja wa Mataifa) kuhusu uhuru wa Tanganyika. Mwaka 1958, aljiunga na Colonial Legislative. Tarehe 9/12/1961, Nyerere alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika baaada ya kupata Uhuru.
UHURU WA TANGANYIKA, NYERERE NA WANANCHI WAKISHEREKEA 

 Baada ya mwaka mmoja yaani mwaka 1962, Nyerere alishinda uchaguzi na kuwa rais wa Tanganyika. Pia  ni muhimu kujua kwamba Nyerere alifaulu kuunganisha kisiwa cha Zanzibar na Tanganyika  pamoja kuunda nchi ya Tanzania katika mwaka 1964, baada ya mapigano huko Zanzibar yaliyomaliza utawala wa Jamshid bin Abdullah, kiongozi wa Zanzibar.
KUUNDWA KWA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Nyerere aliendelea kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mpaka mwaka1985. Akiwa Rais, Nyerere alikumbwa na matatizo mengi kwa sababu mwaka 1960 Tanzania ilikuwa nchi maskini sana ukilinganisha na nchi zingine duniani, hivyo kuwa na deni kubwa sana na pia kulikuwepo na mfumuko mkubwa wa bei. Katika kusaidia nchi yake, Nyerere aliamua kujaribu ujamaa na maisha ya pamoja vijijini, na utaifishaji. Aliandika dhana zake katika Azimio la Arusha la Mwaka 1967. Watu walihimizwa kuishi na kufanya kazi pamoja katika vijiji vilivyokusudiwa kusambaza desturi ya utamaduni wa Tanzania na kuunda umoja.

JK. NYERERE AKIWA KWENYE BAISKELI YAKE,
 HAKUPENDA KUJILIMBIKIZIA MALI
ALIKUWA MTU WA WATU
Baada ya shughuli zake za urais, Nyerere aliendelea kusaidia jamii yake. Alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM).  Miaka michache baadae, aliacha shughuli za kisiasa kwa sababu ya umri wake. Alirudi kupumzika katika kijiji chake huko Butiama alipozaliwa. Tarehe 14/10/1999, alifariki mjini London alipokuwa amelazwa kwa matatizo ya kiafya.  Je, wewe kama Mtanzania unalipi la kusema juu ya Mwasisi wa taifa letu Mwl. JK Nyerere?
MWL. JK NYERERE AKIWA AKITA UBORA WAKE, 
A MAN OF VISIONS 
Toa maoni yako hapa na pia washirikishe wengine (share)

Imeandaliwa na rafiki yako mpendwa, Mr. Lackson Tungaraza
Blogger & Motivator
0764793105 (whatsapp/sms/call).

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI