Showing posts with label BIASHARA YA MTANDAO. Show all posts
Showing posts with label BIASHARA YA MTANDAO. Show all posts

Tuesday, October 25, 2016

*Mwuaji wa Kimya Kimya*

Hahahaa... Nakumbuka wakati nilipokuwa nikitazama Movie za Kivietnam. Komando mmoja anatumwa kwenda kuokoa watu zaidi ya Kumi waliochukuliwa mateka huko Vietnam.
⚜Katika harakati zake za kuingia katika kambi ya adui, anakuwa SILENT KILLER...Anaua Kimya kimya. Anafanya mambo yake kimya kimya hadi anawakomboa watu waliokuwa mateka.
-Baadae ndipo wanashtuka na kushindwa kuwakamata tena.

Inawezekana kabisa kila Unaloshirikisha watu Kulifanya, wanakukatisha Tamaa na hamna anayeonesha dalili ya kukutia Moyo au kuwa sambamba nawe.
-Be a silent Killer.
đź’­Lackson Tungarazađź’­

-Katika hali kama hyo, ninakushauri Leo ya kwamba anza Kufanya Kimya kimya, waone tu jambo lishafanywa.
-Dunia imefika mbali sana na Chuki, Wivu na Uhasama umekuwa Mkubwa kiasi cha kukosekana watu wengi wa Kuwainua wengine.

Henry Ford aliwahi Kusema, *MY BEST FRIEND IS THE ONE WHO BRINGS OUT THE BEST IN ME*
-Fanya, Waone Matokeo
-Kuuliza Uliza watu na Kutangaza-tanga ovyo ndiko kumekufanya hadi sasa haujafika mbali. Maana wengi wao wamekuwa Mizigo na Kipingamizi kwako.

-Actions speak Louder than Words. Matendo yanaongea zaidi ya maneno. Be a Silent Killer.
-Fungua Biashara, Soma hyo Kozi, Fanya jambo hilo na waone matokeo baada ya Kufanya kwako ikiwa wanaokuzunguka wanakukatisha tu tamaa.

SOMA: NJIA ZA KUJENGA KUJIAMINI NDANI YAKO

*Jifunze kwa Huyu Mwanamke

*Luka 8:43-44*

[43]Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, *[aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga]* asipate kuponywa na mtu ye yote,
[44] *alikwenda nyuma yake*, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma.

-Alichukua Maamuzi Binafsi, baadae ndipo wakaona matokeo.
-Angeendelea kusubiri watu wa Kumtia moyo kwanza na kumsindikiza, asingefanikisha kuponywa. Alikwenda Nyuma Ya Yesu yeye Mwenyewe.

STAY AWAY FROM SUCCESS STEALERS
-Kuna watu ni Wezi wa Mafanikio ya wenzao. Hawataki watu wafanikiwe hata Siku moja-Ni Wachawi
-Kuna wakati Utakimbiwa hata na wale uliyokuwa nao. Wakaondoka wote, au wakabaki wachache. Songa mbele, Fanya zaidi.
-Kuna mwingne pia hapa aliyekimbiwa na Watu lakini alisonga mbele bila Kukata tamaa...

*Yohana 6:66-68*

[66]Kwa ajili ya hayo *wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena.*
[67]Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, *Je! Ninyi nanyi mwataka kuondoka?*
[68]Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.

-Mafanikio yanategemea na wewe binafsi ulivyo na Unavyochukulia mambo.
-Anza kufanya, Usisubiri Kutiwa Moyo. Watakuja ukishafanya

    I chose to be a Silent Killer, what of You?
Uwe na wakati mwema
✍Salamu zangu kwako kutoka kwake yeye aliyeniwezesha Kuandika.

Lackson Tungaraza
FANYA SASA. USISUBIRI BAADAE


       📞0764793105
       -WhatsApp/Call
đź‘‚Lackson TungarazĂ 
        "Welcome Again"

http://lacksontungaraza.blogspot.com
www.youtube.com/c/LacksonTungaraza (SUBSCRIBE Kwenye channel yangu ya YouTube)

Saturday, October 1, 2016


 “JINSI YA KUFANYA BIASHARA YAKO KUWA YA TOFAUTI NA YENYE MVUTO MKUBWA”


 Tunashindwa kuongeza vipato vyetu kwa sababu biashara zetu hazina mvuto.

Tunapoendelea kufungua vyanzo vingine vya vipato kwa kutumia mbinu zile zile, tunaendelea kufeli zaidi na hata kukata tamaa kwa sababu ya kukosa wateja kwa kile tunachokifanya

 Hivyo badala ya kukimbilia mikopo kwa ajili ya kuanzisha biashara nyingine, ni bora tukajifunza mbinu za kuifanya biashara yako kuwa ya tofauti na Mvuto Mkubwa kwa Wateja

 Biashara inapokuwa na Mvuto na Utofauti ni rahisi sana kupata Wateja na pato lako kuongezeka

JE! UNAPENDA KUENDELEA NA SOMO HILI?
Haina shida, pakua hapa chini ili ujisomee hata ukiwa hauna intaneti.
PAKUA SOMO ZIMA HAPA (Download)

Kuwa rafiki yangu facebook: www.facebook.com/ltungaraza
 0764793105 [Mawasiliano]

Sunday, September 11, 2016


KIPI NI BORA KWA BIASHARA YAKO?

Kumekuwa na sitofahamu juu ya namna ya kutumia mitandao hii katika kukuza biashara. Ndiyo maana nimekuuliza; Kati ya Facebook na Blog, ni kipi bora kwa Biashara yako?

Jibu lako litaashiria ya kwamba, kwa namna moja ama nyingine utakuwa umepata uzoefu fulani katika hiyo njia unayotumia kulingana na changamoto ambazo umeshakutana nazo. Tuanze uchambuzi wa Facebook na Blog kibiashara;


FACEBOOK.
Facebook inafaida zake, mfano Hakuna gharama katika kufungua Ukurasa wa Biashara na pia ni mtandao wa Kijamii ulio maarufu zaidi maana inazaidi ya watumiaji bilioni 1.35 ambao wako’active’ kila mwezi.

Kama mtu unayetumia Facebook kibiashara, kadri Facebook inavyozidi kukua na kuongezeka watumiaji wake, ndivyo ambavyo inakuwa ngumu kwa wateja kuona Post (Makala) zako. Ndiyo maana unakuta umeandika Posts nyingi Facebook lakini LIKES ni chache zaidi au hazipo kabisa, na wakati ulichoandika ni kizuri kabisa. Tatizo siyo Post zako, bali ni wingi wa Watumiaji wa Facebook.

Hata kwa wale ambao wanalipia ili kufikia watu wengi zaidi {Boosting} unakuta waliosoma post[Post Views] ni chache mno, pamoja na Page Likes[waliopenda ukurasa wako]. Hii ni hasara kwa huyo mtumiaji aliyelipia, na ni faida kwa Mmiliki wa Facebook.

Kuna kipindi name niliBOOST Makala kwa kulipia lakini matokeo yake hayakuwa mazuri….idadi ndogo sana ya waliopenda ukurasa na waliosoma[Post and Page Likes]. Ni hasara, ukizingatia Pesa imetoka kubwa na aidha imeingia ndogo au la.
Haya niliyoyaandika hapo siyo kwamba yametokea kwa kila mtu. La! Hasha. Ni kwa baadhi ya wafanyabiashara, na huwezi jua kama anayefuata baada yao ni wewe hapo. Na hapa ninaelezea upanda wa biashara au jambo lolote ufanyalo ambalo linahitaji wafuasi/wateja.

Kwa ufupi, kwa sasa Facebook imepungua uwezo wake wa kumfanya mtu kukuza biashara yake zaidi kutokana na wingi wa watumiaji wake ambao pia wanaongezeka kila siku. [Lackson Tungaraza].


BLOG.
Aidha ni kwa Biashara au jambo lo lote ambalo unafanya ili kuifikia jamii, Blog ni vyema sana kuwa nayo. Kuna faida nyingi za kuwa na Blog, baadhi ni;

i.             Utakuwa Mwandishi mzuri.
Zaidi ya kuongeza wateja wa biashara yako, utaongeza pia uwezo wako wa kuandika kila siku au mara kwa mara ili kuwavutia wateja/wafuasi wako.

ii.           Utajifunza.
Ili uandike, inabidi usome. Ili uwe mwandishi mzuri itakubidi ufanye vitu viwili tofauti na wengine; Soma sana na Uandike sana.

iii.          Kuonekana Mtaalamu zaidi na Kuaminika.
Mathalani unaandika juu ya upandaji na uvunaji wa kahawa, utaonekana mtaalamu zaidi unayependa kazi yako kuliko yule ambaye hana blog… seen as a Professional expert at your field.
Kwa kadri utakavyokuwa ukiandika makala [blog posts] juu ya unayofanya katika biashara, kampuni au taasisi yako na kuwasaidia watu kutatua Kero zao, ndivyo watavyozidi kukuamini na kuwa Wateja wako wa kudumu.
‘Fully 85% of the happiness and success you enjoy In life will be determined by the Quality of your relationships with others’ –Brian Tracy.

iv.          Kujulikana zaidi.
Kupitia blogs, ni rahisi zaidi kujulikana ukilinganisha na Facebook.
Kwenye Blogs kuna ‘share buttons’ ambapo utaweza kusambaza Post zako katika mitandao mbali mbali ya kijamii moja kwa moja; kama whatsApp, twitter, facebook, linkedln, instagram n.k. Hivyo kutengeneza mtandao mkubwa wa watu, pamoja na wateja wa zamani na wapya.
Itaendelea….

Angalizo: Taasisi ya ‘NYI Movement’ tumetoa punguzo la bei kwa sasa katika kukutengenezea Blog nzuri kulingana na aina ya kazi unayofanya… aidha ni kilimo, afya, michezo, huduma ya injili, mapishi, ufugaji n.k. kama tangazo la hapa chini linavyoonesha. Karibu sana, punguzo hili ni la muda mfupi tu.
Blog ni ya muhimu sana kuwa nayo ikiwa unataka kuwa mtu makini katika kazi au shughuli unayofanya, pamoja na kutengeneza mtandao wa wateja na mashabiki wako ndani na nje ya mipaka yako ya kazi.

Please Share this post[watumie na wengine hili somo].

SOMA: KUJITAMBUA


Mawasiliano: 0764793105 [Lackson Tungaraza]

Jifunze kupitia;


  







Saturday, August 6, 2016

Proudly Sponsored by
N.Y.I MOVEMENT
*Join and Be part of the Change*.


Kuna mambo mbali mbali ambayo wewe kama Kijana mwenzangu unaweza fanya pasipokuwa na pesa kubwa Bali hiyo hiyo uliyonayo hapo .... Akili, maarifa, elimu, ujuzi ni Mitaji pia.... Kwanini bado unalalamika ya kwamba maisha siyo mazuri? Badili sasa mtazamo wako, waliofanikiwa maishani ni watu waliyogundua ya kwamba Mtaji siyo pesa pekee Bali pia uwezo ambao Mungu kakuumbia ndani yako.

Watu kama akina Ronaldinho Gaucho, Barhesa siyo kwamba walikuwa na pesa nyingi pindi wanaanza safari ya kusaka life.. Waliamini ya kwamba kuna zaidi ya Pesa ndani yao. Ni sawa na kuacha migodi Ya dhahabu Tanzania na kwenda kutafuta dhahabu Somalia..
 Huo ni upuuzi. What's your talent, experience, profession, hobby? Then why do you complain about having a hard life? Be a critical Thinker....

Wewe ni zaidi ya Unavyojitazama... Unamadini ndani yako..... Mwandiko wako ni wa kipekee duniani, mboni ya macho yako ni ya kipekee, nyayo za miguu yako ni ya kipekee, alama za mikono yako ni ya kipekee... So what next? You have greatness within you... Use it.
Lackson Tungaraza
www.lacksontungaraza.blogspot.com

Nabii Musa kipindi amefika na wana wa Israeli katika kando ya bahari ya shamu... Watu walianza kumlilia Musa kwa kuwaleta kufa kifo cha aibu na pia Musa akaanza kumlilia Mungu atende jambo... Unajua Mungu alimwambiaje Musa?.... Usinililie, Chukua fimbo yako uinyooshe juu ya bahari... Aliponyoosha, bahari ikawa nchi kavu nao wakapita saa hiyo. Musa alikuwa na Mtaji wa kusogea mbele mkononi mwake lakini hakutambua.
MTAJI SIYO PESA TU, TUMIA UBONGO WAKO VYEMA KUFIKIRI VIZURI.

Mtaji unao hapo hapo ulipo... Siyo kila wakati wakitaja Mtaji unawaza tu pesa.... Ohhhooo nimemaliza chuo sijaanza biashara kwasababu sina mtaji.. Ohooo natamani kulima zao la pamba lakini Mtaji ni kikwazo...

Ni wakati wa akili za watanzania kufunguka na kuwa wazi..... Bado hujaelewa tu ?.... Iko hivi…
Kuna shughuli unaweza Fanya hata kama hauna pesa na ukatengeneza bomba la Pesa....

Unaweza kuwa Mshauri wa mambo ya biashara: Wewe  una uzoefu wa ujasiriamali au umiliki wa biashara? Unajua nini kinahitajika ili uanzishe biashara, kujenga biashara, kuongeza biashara na kukua? Sasa unaweza kuanza kazi ya ushauri wa biashara. Unaweza kusaidia kampuni au biashara mbalimbali kutoka chini ya uvungu na kwa kutoa ushauri na maelekezo muhimu. Unaweza kuwasaidia watu walioajiriwa kuanza kutoka kwenye ajira na kuingia kwenye ujasiriamali kwa malipo.

Hujaelewa tu!! amka wewe.

Sunday, July 10, 2016



Kuna tafsiri mbali mbali katika vichwa vya watu na katika mitandao ya kijamii juu ya dhana ya UJASIRIAMALI. Wengi wamepata tafsiri zilizowapa presha na kuamua kuacha kuwa WAJASIRIAMALI, na baadhi hawatambua ni kwa namna gani wanaweza kuwa Wajasiriamali wakubwa wenye Mafanikio.



UNASUBIRI NINI!! Tazama video hii kwa umakini, naamini hautotoka kapa bali utaelewa UJASIRIAMALI ni nini na Namna ya kuwa mshindi katika sekta hii. Karibu sana.

Whatsapp: 0764793105 [Lackson Tungaraza]

Facebook: www.facebook.com/ltungaraza










Thursday, June 23, 2016

LACKSON TUNGARAZA KATIKA HARAKATI ZAKE ZA KUTOA HUDUMA YA VIATU

Tunashindwa kuongeza vipato vyetu kwa sababu  biashara zetu hazina mvuto

Tunapoendelea kufungua vyanzo vingine vya vipato kwa kutumia mbinu zile zile, tunaendelea kufeli zaidi na hata kukata tamaa kwa sababu ya kukosa wateja kwa kile tunachokifanya


Hivyo badala ya kukimbilia mikopo kwa ajili ya kuanzisha biashara nyingine, ni bora tukajifunza mbinu za kuifanya biashara yako kuwa ya tofauti na Mvuto Mkubwa kwa Wateja

Biashara inapokuwa na Mvuto na Utofauti ni rahisi sana kupata Wateja na pato lako kuongezeka


Zifuatazo ni mbinu utakazotumia ili uwe na Biashara yenye Mvuto na Utofauti Mkubwa dhidi ya Biashara zingine;


     Mbinu Ya Kwanza

      Bei Ya Bidhaa/Huduma Yako Imvutie Mteja

Biashara huanzishwa kwa lengo la kutatua changamoto zilizopo katika jamii, zinaweza zikawa ni ukosefu wa bidhaa au huduma Fulani

Endapo atatokea mtu wa kutatua changamoto hizo, basi Wateja wapo tayari kumpa fedha zao kupata hizo Huduma au Bidhaa

Tatizo linakuja kwenye upangaji wa bei ya Huduma au Bidhaa, na usipolizingatia hili litaangamiza biashara yako kwa kufukuza Wateja

Bei yako isiwe ya ghali ili uweze kuwashawishi watu kuinunua, Usitake faida kubwa au Mafanikio ya mara moja. Wengine husema, “Kulala masikini na Kuamka Tajiri”
Inawezekana Huduma Yako Ikahitajika mahali Fulani, lakini kwa sababu umetanguliza pesa mbele zaidi kuliko Utu au Huduma yako, Utakuwa umekatisha watu tamaa ya kuwa Wateja wako na hutofanikiwa


             Mbinu Ya Pili

             Ubora Wa Huduma/Bidhaa Yako

Wahenga walisema, “Kizuri Chajiuza Na Kibaya Chajitembeza”. Ubora wa Bidhaa/Huduma yako ni jambo la muhimu sana ili kuvutia Wateja

Wateja wanapenda Bidhaa/Huduma ambazo zitawatatulia matatizo yako moja kwa moja bila kuathiri hali zao za kiafya


Bidhaa zako zikiwa na Ubora, zitawavutia watu wengi kwako na utashangaa kuona mauzo yako yakipanda

Ukifanya tofauti na hapo, itabaki historia ya kwamba ulikuwa na Wateja Fulani. Hivyo usiwauzie watu bidhaa feki au zilizopoteza Ubora wake (zilizo expire)

Usijaze bidhaa ambazo sio bora, ni afadhali uwe nazo chache lakini ni bora zaidi.


       Mbinu Ya Tatu

       Muoneshe Mteja au Mpenzi Wa Huduma Yako Kuwa Unamjali

Wanataaluma wengi hupenda kusema, “Kama hauna tabasamu usoni mwako ni vyema usifungue biashara”.

Mtu yeyote Yule anapenda kuonekana wa muhimu na wa thamani zaidi, wengine wanatafuta nafasi hiyo kupitia vyombo vya habari kama TV, redio, Magazeti n.k.


Hii tabia ipo pia ndani ya Wateja, wanapenda kupokelewa kwa tabasamu na uchangamfu mkubwa wanapofika sehemu ya uhitaji wa bidhaa/huduma

Ukifanya hivyo atatamani kuja kwako kila mara, maana wengine huko wanakotoka hawana faraja wala furaha

Zingatia mbinu hii na utaona Wateja wakimiminika kwako zaidi kuliko kwa jirani yako.


           Mbinu Ya Nne

       Usijali Muda Wako Tu, Jali Na Kuthamini Muda Wa Mtu Mwingine Pia

Wazungu wanasema ya kwamba, “Time Is Money”. Kwetu sisi Wabongo, tunaona muda kama ni kitu cha kawaida sana kana kwamba hakiwezi kuleta athari zozote katika maisha yetu na ya wale wanaotuzunguka

Unakuta Mteja anafika dukani kwa mtu, anabisha hodi hadi anachoka, au anamtajia mahitaji yake mwenye duka lakini yeye anakomaa tu na kuchati au kupiga soga


Mteja endapo utamwona bado anakuja kwako, ni kwa sababu hajapata tu sehemu nyingine ya kwenda kupata hiyo huduma/bidhaa. Ikitokea mtu mwingine akaja mwenye kukidhi haja ya moyo wake na kujali muda wake kwa kumsikiliza kwa umakini, huyo Mteja hatorudi tena kwako

Tumia vizuri kwa umakini nafasi ambayo Mteja amekupatia ili apate huduma/bidhaa kutoka kwako.

Mbinu Ya Tano

Tangaza Huduma/Bidhaa Yako

Hamna mwenye alama kichwani ambaye akikutana tu na watu, wanatambua yeye anafanya biashara gani na yuko sehemu gani. Labda tu kama amebeba bango au bidhaa Fulani ambayo ndiyo itakayo mtambulisha

Biashara ni Matangazo na Matangazo ni Biashara.


Matangazo ni gharama lakini tunatumia shilingi kupata shilingi. Lakini usitangaze Huduma ambayo huwezi kuitoa kwa kiwango hicho ulichoahidi, utapoteza Wateja wengi

Tumia njia mbalimbali katika kutangaza bidhaa au huduma yako, unaweza tumia Redio, TV, Magazeti, Mabango,Vipeperushi, Mitandao ya kijamii kama Facebook ambayo inawatumiaji wengi sana duniani na wanazidi kuongezeka kila leo, Twitter, Instagram n.k.


        Fanya Zoezi Hili Fupi

Nakushukuru kwa kusoma Mbinu hizi za kuifanya biashara yako iwe ya tofauti na Yenye Mvuto mkubwa mpaka hatua hii, Ninaamini kabisa una lengo la kubadilisha biashara yako kwenda hatua nyingine. Malizia kwa kufanya zoezi hili fupi;

# Chunguza kwa Umakini kama bidhaa ulizonazo zina ubora sahihi wa kumvutia Mteja. Pia chunguza kwa umakini bidhaa unazonunua kwenye maduka ya jumla, zingine ni feki au zimeshapitiliza muda wa matumizi

# Chunguza kama Bei zako zinaendana na Uchumi wa Wateja wako waliopo katika hilo eneo. Lakini zingatia ya kwamba Ubora wa bidhaa huendana na bei, zenye Ubora mkubwa zina bei kubwa pia


# Je, unamjali Mteja wako na kuthamini muda wake pia?

# Je, unafanya Matangazo ya kutosha kwa bidhaa au huduma ulizonazo?

Kwa Ushauri na Mafunzo yanayohusu kufanya biashara yako kuwa ya tofauti na Mvuto mkubwa, Wasiliana na Ndugu Lackson Tungaraza, +255764793105 au tembelea Website ya lacksontungaraza.blogspot.com

Pia unaweza kupata Nakala ya Kitabu Cha “MBINU ZA KUONGEZA MAUZO KWENYE BIASHARA YAKO,” Kikiwa ni Mwendelezo wa somo hili kama Sehemu Ya Pili Kwa Gharama Nafuu Kabisa. Bila Kusoma Kitabu Hiki Cha Mwendelezo, Biashara Yako bado itakuwa yenye Kuingiza Kipato Kidogo na Cha Kawaida.. Kipo katika softcopy kukuwezesha kukisoma katika simu yako au kompyuta mahali popote pale ulipo   bila kusumbuka kubeba kitabu mkononi mwako.

     07647931059(sms/wasap) [Lackson Tungaraza

PATA KITABU HIKI KWA GHARAMA NAFUU: 5000/- TU.
PUNGUZO HILI LA BEI NI LA MUDA MFUPI TU, HIVYO WAHI MAPEMA.



Tuesday, May 24, 2016

Natumaini wewe ni mzima wa afya na unaendelea vizuri na shughuli zako za kila siku. Ni jambo jema sana la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukupatia siku nyingine tena ukiwa na nguvu tele, una ndugu, una marafiki wazuri, umekula umeshiba, shughuli zako za kila siku zinafanikiwa, familia yako inaamani n.k.

Kumekuwa na mitazamo tofauti tofauti katika jamii kuhusiana na Semina zinazotolewa Mitandaoni; kwa njia ya Telegram, Wasap, Facebook n.k. Wengi wakiona tu tangazo linalotaarifu umma juu ya kuwepo kwa Semina fulani kupitia Whatsapp au Telegram, kichefuchefu kinawaingia na mara hiyo wanaondoka mitandaoni…ni nini tatizo!! Wengine wameshachukulia kama ni Utapeli mtupu, semina gani inayofanyikia mtandaoni tena kwenye Whatsapp? Tena, ingawa hiyo Semina inagusa moja kwa moja tatizo linalomsumbua lakini hawezi kuchukua hatua ya kufuatilia au kulipia gharama zilizowekwa ili kupata semina hiyo kwasababu Akilini mwake ameshaamini ya kwamba ni Utapeli.

Hii ni karne ya kisasa yenye maendeleo ya sayansi na teknolojia, majukumu yamekuwa ni mengi sana na watu wako bize. Wanandoa nao wako bize wakitafuta fedha ili familia isonge mbele, watu wanawahi kuamka asubuhi kuwahi katika shughuli zao na kuchelewa kurudi majumbani mwao, njiani pia foleni ya kutosha kwa wale waliopo kwenye miji mikubwa kama Dar, Mwanza, Arusha na hivyo kufika nyumbani wakiwa wamechoka sana na kupitiliza kulala, siku ya wikendi nayo mtu anapenda awe japo karibu na familia yake au atembelee miradi yake mbalimbali. Muda wa kuhudhuria kwenye Ukumbi wa Semina, anaupata wapi? Muda wa kutoka mkoa mmoja hadi mkoa mwingine ili akapate Semina labda ya Ndoa au biashara unapatikanaje? Hivyo ni baadhi tu ambao wanaweza kupangilia mambo yao vizuri na wakaudhuria Semina kwa wakati. Sasa hao wengine ambao hawapati muda wa kuhudhuria hizo Semina, elimu itawafikiaje?

Katika hali kama hiyo ndipo Umuhimu wa Semina za Mitandaoni zinahitajika ili mtu aweze kupata elimu stahiki kwa wakati sahihi bila kuathiri shughuli zake au muda wake wa kazi. Je! Kuna faida gani za kuhudhuria hizo semina za Mitandaoni, mfano kupitia Whatsap? Zifuatazo ni faida ambazo utazipata;

1.     Unapata Elimu stahiki ukiwa popote pale (Elimu Kiganjani Mwako)
Elimu hiyo unaipata ukiwa nyumbani, ofisini, kazini, safarini au sehemu yoyote ile ukiwa na simu yako au kompyuta inayokubali Intaneti na kuwa na Wasap ndani yake. Karne hii ya kisasa, mafunzo ya mtandaoni yameshika kasi sana kwa kiasi kikubwa. Kuna vyuo mbalimbali vinatoa mafunzo mtandaoni na kumwezesha mtu kupata Stashahada, Shahada, au Masters. Hii itakusaidia kupata masomo kwa uhuru, kwa wakati ambao uko free na sehemu yoyote ile uliyopo bila usumbufu wowote. Unaweza ukatoka ofisini kwako na ukachukua Simu au Kompyuta yako na kuanza kujifunza wakati umepumzika au wakati unakula bila kuathiri muda wako wa kazi.
Miaka ya sasa watu wamekuwa bize sana katika kutafuta maisha bora kutokana na kupanda kwa gharama za maisha, na hivyo inakuwa vigumu kwa watu kuacha shughuli zao na kwenda kwenye ukumbi fulani kuhudhuria Semina kutokana na ufinyu wa muda walionao. Kupitia Semina za mitandaoni, unapata Elimu stahiki kiganjani mwako kama elimu ya biashara na Ndoa mahali popote pale ulipo pasipo kuathiri shughuli zako.

2.     Gharama Nafuu~Low Cost
Badala ya kwenda sehemu na kukaa katika nyumba za wageni (guest house) au kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa gharama kubwa, unaweza kupata hii Semina hapo hapo nyumbani kwako kwa kutozwa kiwango kidogo cha fedha. Ni wewe tu kuwa na Simu au Kompyuta inayokubali intaneti

3.     Unaokoa Muda~Saving Time
Badala ya kusafiri na kutumia muda mwingi njiani, kwenda na kurudi. Lakini pia kuacha shughuli zako za siku na kwenda kwenye kumbi mbalimbali za Semina, sasa utaokoa muda wako kwa kupitia Online Seminars na ukawa unaendelea na kazi yako ya Ualimu, Udaktari, Ujasiriamali n.k.
          “TIME IS MONEY, HOW DO YOU INVEST YOUR TIME?”
Karibu sasa katika Semina yangu itakayoanza tarehe 07/06/2016, naamini ya kwamba hautojutia kabisa. Kuna mambo mengi sana utajifunza kupitia Simu au Kompyuta yako ukiwa hapo hapo kazini, safarini au nyumbani bila kuathiri shughuli zako. Jiandikishe sasa mapema, kwa Ushauri na Maswali binafsi tumia Wasap/sms kwa nambari 0764793105… Utapata elimu stahiki katika maeneo yafuatayo kwa njia ya Whatsapp na Email;

1. Jinsi Ya Kufanikiwa Maishani ikiwa hauna mtaji.

Mtaji ni kilio kwa wengi nawe ukiwa mmoja wao. Kwanini usichukue uwamuzi wa kuyaokoa maisha yako sasa ili upate kujua jinsi ya kuwa na maisha bora na kuzifikia ndoto zako hata kama hauna Mtaji.

2. Jinsi Ya Kupata Wazo Bora la Biashara.

Najua unataka kuanzisha biashara ya kukuinua kiuchumi katika viwango vikubwa lakini hujui ni biashara gani ufanye na kwa njia zipi. Pia unamawazo mengi ya biashara lakini hauna Mtaji na pia hujui lipi ulipe kupaumbele..Sogelea Semina sasa upate kujua

3. Umuhimu wa Maono Kwa Kijana.

Kijana mwenzangu acha kuishi maisha ya kubahatisha. IT'S BETTER TO BE BORN BLIND THAN TO LIVE A LIFE WITHOUT VISION. Ni afadhali ungezaliwa ukiwa kipofu wa macho kuliko kuishi pasipo kuwa na Maono. Maono yatakupa nidhamu nini ufanye na nini usifanye na kwa wakati gani. Ni dira yako ya maisha. Nikuulize, UNAJIONA UKO KATIKA MAISHA GANI BAADA YA MIAKA MITANO? Karibu sasa katika Semina hii ujue zaidi juu Ya Maono kwa kijana

4. Jinsi Ya Kuongeza Mauzo katika Biashara Yako

Mbinu utakazozipata hapa ni nzuri na kwa uhakika zitakusaidia sana..nimekuwa nikizitumia sehemu mbalmbal hata katika mitandao ya kijamii na zmezaa matunda. Usiwe mnyonge kwa sababu biashara yako haina faida ya kutosha, ni siri tu Fulani ambazo hujazipata...karibu sana uchote Maarifa

5. Kutengeneza Kipato cha ziada ukiwa kazini kwako

Hivi unatambua ya kwamba unaweza ukawa unaendesha biashara yako ukiwa hapo hapo kazini? Hamna ya kusubiri hadi upewe likizo au hadi wikendi Ifike...kupitia simu yako, kompyuta yako, mazingira yako ya kazi sasa unakwenda kutengeneza mfereji wa pesa
...usikae maskini kwa sababu ya mshahara mdogo na unatumia nguvu kubwa.

Hata wewe mama wa nyumbani hii siri itakusaidia kutengeneza pesa ukiwa hapo Hapo nyumbani kwako.

Jiandikishe mapema sasa kupitia Wasap kwa namba niliyoitoa hapo juu..semina ni Tsh. 10,000/- tu bila senti. Utaituma kwa nambari 0764793105[M-Pesa] na utaona jina langu Lackson Tungaraza. Ukishatuma utanijulsha kwa Meseji maana wanaotuma ni wengi. Pia Utapata Kitabu cha Biashara Bure.


CHOTA MAARIFA NA LACKSON TUNGARAZA.

www.lacksontungaraza.blogspot.com



Sunday, May 1, 2016

Ni haki yako Kijana Mwenzangu kuwa na Maisha yenye furaha na Mafanikio. Tumia ushauri ufuatao ili uweze kufikia lengo hilo;






Wednesday, March 16, 2016


SIRI INAYOVUTA MAFANIKIO
 Nitakuwa muongo sana kama nikisema ya kwamba hamna mtu anayependa Mafanikio, hata wewe umechukua muda wako kusoma makala hii kwa sababu unapenda kufanikiwa kupitia hii Siri Inayovuta Mafanikio. Je, Mafanikio ni nini? Mafanikio kwa tafsiri ya kawaida ni kutimiza Malengo uliyojiwekea; iwe ni kununua gari, kupata kazi mpya, kuanza biashara, kununua TV, kuwa kiongozi katika Nyanja fulani n.k. Je! Siri hii ya Mafanikio ni ipi?

“Basi Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana na mambo yasiyoonekana”~Ebr 11:1. Ukitaka kufanikiwa katika jambo lolote maishani mwako, ishi maisha ya Imani (Live a life of faith). Natumaini ya kwamba unatamani sana kuwa Tajiri, kuwa Mfanyabiashara mkubwa, kuwa Mkulima wa kimataifa, kuwa Mwimbaji maarufu, kuwa T.O katika masomo yako shuleni, kuwa kiongozi mkuu katika taifa. Je, unafikiaje hayo Malengo yako? Mtaji huna, Umaarufu huna, Wadhamini hauna n.k.

Anza kuishi maisha hayo unayoyataka yatokee katika maisha yako. Ikiwa unataka kuwa Tajiri mkubwa hapa nchini na duniani, anza kuishi maisha kama ya matajiri..Matajiri wananidhamu katika muda, wanavaa mavazi ya heshima, wanapenda kuwafanikisha wanaowazunguka, wanakiu ya kufanikiwa zaidi na zaidi kila siku, changamoto wanazichukulia kama fursa ya kupata fedha na kuongeza Uzoefu katika mambo wayafanyayo, wanasoma vitabu vingi sana vya biashara kila mara, hawana muda wa kulalamika kwa yale waliyoyapoteza bali wanaangalia yaliyobaki na kuweka mikakati ili wasijewakapoteza tena.

~Ukitaka kuwa Mwanamuziki bora katika vipindi vyote, anza kuishi maisha ya Wanamuziki wakubwa..jinsi wanavyofanya mazoezi, wanavyoshirikiana na Wanamuziki wengine, vitabu na vyanzo mbali mbali vya taarifa wanavyotumia kupata maarifa zaidi ya Uanamuziki.

~Ukitaka kuwa Kiongozi katika sehemu yoyote ile katika maisha yako..serikalini, chuoni, taasisi za watu binafsi n.k. Ishi maisha ya Uongozi, huwezi kuwa Kiongozi ikiwa unaisha maisha ya kuongozwa (Mfuasi)..Vaa kama Kiongozi (dress like a leader), tembea kama Kiongozi (walk like a leader), ongea kama kiongozi (talk like a leader), anza kutengeneza wafuasi (start making followers). Vivyo hivyo na katika Nyanja zingine za maisha.

Ukianza kuishi maisha hayo, utavuta maisha unayoyataka kuja kwako. Maisha utakayoishi yatavuta yale mambo ambayo unayataka yatokee katika maisha yako.

~Tangu nilipoanza kutumia Siri hii, maisha yangu Lackson Tungaraza yalibadilika kabisa. Kwa sababu nilikuwa nataka kuwa Mjasiriamali mkubwa, hivyo nikaanza kuishi maisha ya Wajasiriamali wakubwa..vitabu wanavyosoma, muonekano wao wa nje na wa ndani, watu wanaoambatana nao. Baada ya hapo nikashangaa kuanza kuona nawavutia watu wengi kufanya kazi na mimi, wengine kwenda mbali zaidi na kuniita Mjasiriamali mkubwa n.k. Kwa sababu pia nilitaka kuwa Mwandishi katika Blog (Blogger), nilianza kuishi maisha ya ‘Bloggers’.. wanapenda kuikomboa jamii katika matatizo na utashi unaowasumbua katika maisha, wanafanya utafiti katika yale wanayoyaandika, kila mara wanaandika hata kama ni hadithi fupi.. baada ya hapo nikaanza kuwavuta waandishi wengine wa Blog katika maisha yangu na pia kuwa mahiri katika uandishi wa makala zinazovuta hisia za watu wengi.

TENDEA KAZI SIRI HII KUANZIA SASA.
~ Kama mimi Siri hii imenisaidia kufika hapa nilipo leo, naamini hata wewe itakusaidia sana ukianza kuweka katika matendo yale uliyojifunza hapa. Endelea kuwa karibu na mimi Facebook (www.facebook.com/ltungaraza), Instagram/YouTube (Lackson Tungaraza) ili uzidi kupata masomo zaidi ya uelimishaji.


ITAKUWA BORA ZAIDI IKIWA UTATOA MAONI YAKO HAPA (Comment) NA PIA KUSAMBAZA SOMO HILI KATIKA MAKUNDI MBALI MBALI (Share) ILI ELIMU HII IWAFIKIE WATU WENGINE NA KUKOMBOA FIKRA ZAO.

0764793105 Namba yangu. Nitafute kwa kupiga, meseji au wasap.




Thursday, March 10, 2016


UKWELI JUU YA SEMINA ZA MTANDAONI

Natumaini wewe ni mzima wa afya na unaendelea vizuri na shughuli zako za kila siku. Ni jambo jema sana la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukupatia siku nyingine tena ukiwa na nguvu tele, una ndugu, una marafiki wazuri, umekula umeshiba, shughuli zako za kila siku zinafanikiwa, familia yako inaamani n.k.

Kumekuwa na mitazamo tofauti tofauti katika jamii kuhusiana na Semina zinazotolewa Mitandaoni; kwa njia ya Telegram, Wasap, Facebook n.k. Wengi wakiona tu tangazo linalotaarifu umma juu ya kuwepo kwa Semina fulani kupitia Whatsapp au Telegram, kichefuchefu kinawaingia na mara hiyo wanaondoka mitandaoni…ni nini tatizo!! Wengine wameshachukulia kama ni Utapeli mtupu, semina gani inayofanyikia mtandaoni tena kwenye Whatsapp? Tena, ingawa hiyo Semina inagusa moja kwa moja tatizo linalomsumbua lakini hawezi kuchukua hatua ya kufuatilia au kulipia gharama zilizowekwa ili kupata semina hiyo kwasababu Akilini mwake ameshaamini ya kwamba ni Utapeli.

Hii ni karne ya kisasa yenye maendeleo ya sayansi na teknolojia, majukumu yamekuwa ni mengi sana na watu wako bize. Wanandoa nao wako bize wakitafuta fedha ili familia isonge mbele, watu wanawahi kuamka asubuhi kuwahi katika shughuli zao na kuchelewa kurudi majumbani mwao, njiani pia foleni ya kutosha kwa wale waliopo kwenye miji mikubwa kama Dar, Mwanza, Arusha na hivyo kufika nyumbani wakiwa wamechoka sana na kupitiliza kulala, siku ya wikendi nayo mtu anapenda awe japo karibu na familia yake au atembelee miradi yake mbalimbali. Muda wa kuhudhuria kwenye Ukumbi wa Semina, anaupata wapi? Muda wa kutoka mkoa mmoja hadi mkoa mwingine ili akapate Semina labda ya Ndoa au biashara unapatikanaje? Hivyo ni baadhi tu ambao wanaweza kupangilia mambo yao vizuri na wakaudhuria Semina kwa wakati. Sasa hao wengine ambao hawapati muda wa kuhudhuria hizo Semina, elimu itawafikiaje?

Katika hali kama hiyo ndipo Umuhimu wa Semina za Mitandaoni zinahitajika ili mtu aweze kupata elimu stahiki kwa wakati sahihi bila kuathiri shughuli zake au muda wake wa kazi. Je! Kuna faida gani za kuhudhuria hizo semina za Mitandaoni, mfano kupitia Whatsap? Zifuatazo ni faida ambazo utazipata;

1.     Unapata Elimu stahiki ukiwa popote pale (Elimu Kiganjani Mwako)
Elimu hiyo unaipata ukiwa nyumbani, ofisini, kazini, safarini au sehemu yoyote ile ukiwa na simu yako au kompyuta inayokubali Intaneti na kuwa na Wasap ndani yake. Karne hii ya kisasa, mafunzo ya mtandaoni yameshika kasi sana kwa kiasi kikubwa. Kuna vyuo mbalimbali vinatoa mafunzo mtandaoni na kumwezesha mtu kupata Stashahada, Shahada, au Masters. Hii itakusaidia kupata masomo kwa uhuru, kwa wakati ambao uko free na sehemu yoyote ile uliyopo bila usumbufu wowote. Unaweza ukatoka ofisini kwako na ukachukua Simu au Kompyuta yako na kuanza kujifunza wakati umepumzika au wakati unakula bila kuathiri muda wako wa kazi.
Miaka ya sasa watu wamekuwa bize sana katika kutafuta maisha bora kutokana na kupanda kwa gharama za maisha, na hivyo inakuwa vigumu kwa watu kuacha shughuli zao na kwenda kwenye ukumbi fulani kuhudhuria Semina kutokana na ufinyu wa muda walionao. Kupitia Semina za mitandaoni, unapata Elimu stahiki kiganjani mwako kama elimu ya biashara na Ndoa mahali popote pale ulipo pasipo kuathiri shughuli zako.

2.     Gharama Nafuu~Low Cost
Badala ya kwenda sehemu na kukaa katika nyumba za wageni (guest house) au kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa gharama kubwa, unaweza kupata hii Semina hapo hapo nyumbani kwako kwa kutozwa kiwango kidogo cha fedha. Ni wewe tu kuwa na Simu au Kompyuta inayokubali intaneti

3.     Unaokoa Muda~Saving Time
Badala ya kusafiri na kutumia muda mwingi njiani, kwenda na kurudi. Lakini pia kuacha shughuli zako za siku na kwenda kwenye kumbi mbalimbali za Semina, sasa utaokoa muda wako kwa kupitia Online Seminars na ukawa unaendelea na kazi yako ya Ualimu, Udaktari, Ujasiriamali n.k.

          “TIME IS MONEY, HOW DO YOU INVEST YOUR TIME?”


Karibu sasa katika Semina yangu itakayoanza tarehe 21/3/2016, naamini ya kwamba hautojutia kabisa. Kuna mambo mengi sana utajifunza kupitia Simu au Kompyuta yako ukiwa hapo hapo kazini, safarini au nyumbani bila kuathiri shughuli zako. Jiandikishe sasa mapema, kwa Ushauri na Maswali binafsi nipo Wasap kwa nambari 0764793105. Tangazo hili limeelezea vizuri;




MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI