Maisha ya Mwanadamu
yana mwanzo na mwisho, ikiwa na maana ya kwamba kuna kuzaliwa na kufariki.
Lakini katikati ya kuzaliwa na kufariki kuna mambo ambayo Mwanadamu anatakiwa
afanye ili aweze kustahimili hali ya kimwili na kiroho pia.
.
Dira ndiyo inayomwongoza
Rubani kuifikisha Ndege mahala salama, pasipokuwa na Dira Rubani anaweza kwenda
mahala pasipo sahihi na hata wakati mwingine kupata ajali. Kama wanadamu
tunaoishi duniani, pasipokuwa na Dira inayotuongoza ni rahisi sana kupoteza
muda mwingi katika kufanya mambo ambayo hatutakiwi kufanya, hatimaye kuangamia
katika Uharibifu
Ulishawahi kuona siku nzima inapita katika maisha yako na
huoni jambo la muhimu ulilofanya, au ulifanya ambayo hukutakiwa kufanya? That’s
lack of Direction/Daily Schedule
Nimejifanyia utafiti
binafsi [Lackson Tungaraza], kati ya kuishi maisha ya Ratiba na yasiyo na
ratiba. Ndugu yangu unayesoma taarifa hii, Maisha yasiyo na Ratiba ni sawa na
Samaki pasipokuwa na maji. Nilikuwa namaliza siku nzima wakati mwingine
pasipokufanya jambo lolote ambalo linaendana na Malengo yangu ya muda fulani.
Ukitaka siku yako iwe
yenye thamani na hata ukatamani ijirudie tena, uwe na Dira inayokuongoza kila
siku kwasababu siku huzaa wiki na wiki huzaa mwezi na miezi huzaa miaka na
miaka huzaa urefu wa maisha ya mtu.
Anza kidogo kidogo,
haba na haba hujaza kibaba. Kila siku jioni andika mambo hata matatu/matano
ambayo kwa siku inayofuata utayafanya kwa Ufasaha na kuyamaliza ndani ya siku
husika.
MFANO WA UPANGAJI WA RATIBA KWA SIKU INAYOFUATA. WEWE NDIYE RUBANI WA MAISHA YAKO.... KUWA MPYA KILA SIKU. |
Kumbuka; Hayo mambo
ambayo unayapanga kufanya, yawe yanaendana na Ndoto uliyonayo juu ya maisha
yako ya baadae. Kama hayaendani na kule unakotaka kufika, yaache hata kama ni
yenye kufurahisha kwa wakati huo
Mfano.. Una ndoto ya
kuwa Mfanyabiashara mkubwa baadae ambaye utakuwa ukiwashauri watu jinsi ya
kutumia fedha vyema halafu Rafiki zako wanakuambia muende kwenye kumbi za
starehe kutafuta mwanawake wa kulala nao, acha kabisa kwasababu utapoteza
Nidhamu ya Pesa na pia Afya yako kuwa katika hali ya hatari kupata Magonjwa
hatarishi. Na ukishakuwa na Afya mbovu, hutofurahia mafanikio ambayo utapata
katika maisha yako… Afya Bora ni Msingi Imara wa kukufikisha kule unakohitaji
kwenda… huwezi kufanya kazi kwa muda mrefu ikiwa Afya yako siyo Imara… Ishi kwa
tahadhari… Kinga ni bora kuliko Tiba.
Ahsante sana kwa muda
uliyoutumia kusoma makala haya, naamini ya kwamba kuanzia sasa utakuwa na
maisha yenye furaha na thamani kila siku kwasababu utakuwa na Dira ya
kukuongoza… shea na rafiki zako ujumbe huu na kutoa maoni yako…
0764793105
WhatsApp/call/sms.
Kama mpenda maendeleo, unamaoni gani juu ya hili?
ReplyDelete