Tuesday, March 5, 2019


Mwanzoni Uliamini ya kwamba KWA KUJIAJIRI ndipo UTAPATA UHURU WA KIFEDHA na KIUCHUMI. Ukakataa KUAJIRIWA kwa Sababu ya kasoro Yake ya KUWEKEWA UKOMO WA FEDHA UNAYOINGIZA (Income) kutoka kwa MWAJIRI wako.


LAKINI LEO!

Huamini tena kama Ulikuwa Unamaanisha kwa dhati Kutoka moyoni mwako. Na hiyo imekuja baada ya KUISHIWA PESA YOTE YA KUANZISHIA BIASHARA [au MTAJI Kama Wengi Wasemavyo], na KUPATA HASARA ZA MFULULIZO KATIKA BIASHARA au MRADI ULIYOKUWA UKIUTEGEMEA SANA. Yaani, Umekaribia kabisa Kukata Tamaa, na Muda mwingi Unautumia katika KUJILAUMU kwa KUACHA KUCHANGAMKIA FURSA ZA AJIRA zilizokuwa zinakufuata hapo Awali.

Pole sana. Lakini Nikuulize; "WAKATI ULIPOAMUA KUJIAJIRI BADALA YA KUAJIRIWA, ULIDHANI YA KWAMBA KUNA MTEREMKO SANA (Hakuna CHANGAMOTO KUBWA, wala HASARA)??", au Rudi hatua Tatu Nyuma na KUJIULIZA ni kwa nini Uliamua KUJIAJIRI kuliko KUAJIRIWA. Na kama NIA YAKO ilikuwa ni ya dhati Kabisa, kwa nini Sasa Ukate tamaa? Hujui ya kwamba IMANI NDIYO HUJARIBWA? Na KUJARIBIWA KWA IMANI NDIKO KUNALETA SABURI (Ukomavu, Ushupavu, Uhodari)?

Sitaki Uamini ya kwamba Ulikosea kwenye MAAMUZI Yako Ikiwa ULIKUWA NA SABABU ZA MSINGI, PAMOJA NA NIA YA DHATI Kutoka Moyoni mwako. Au PATA MAHALI PA UTULIVU na Kujitathimini kwa Kujiuliza na Kujihoji kama Uliamua kwa dhati kabisa Kutoka moyoni mwako, au Uliamua KUJIAJIRI kwa Sababu ya USHAURI wa Waalimu wa Ujasiriamali, na Wazungumzaji (Motivational Speakers). Au kwa Sababu ya TAMAA YA PESA kwa KUDHANI ya kwamba BIASHARA PEKEE ndiyo NJIA ya Kupata UHURU wa KIFEDHA na KIUCHUMI.

Mwisho kabisa,

SAFARI YA KUJIAJIRI SIO LELEMAMA au MTELEZO; Unaweza ukakutana na HASARA NYINGI za MFULULIZO kuliko hata FAIDA. Au Unaweza ukakutana navyo vyote kwa Wakati Mmoja  (Faida na Hasara). Au Unaweza ukakutana na FAIDA NYINGI za MFULULIZO kuliko hata HASARA  [ambayo Sio kwa Wakati Wote]. Na hiyo haijalishi Ulihudhuria Semina ngapi za Ujasiriamali na Biashara, ulisoma Vitabu vingapi vya Fedha na Uchumi, wala idadi ya Mashauri uliyopokea kutoka kwa manguli wa Ujasiriamali na Biashara. Huwa inatokea tu, na hata Mimi Sina lugha nyepesi ya kuielezea ni kwa nini huwa inakuja tu. Kwa hiyo, Unapaswa KUAMUA kabisa ya kwamba UNATAKA KUJIAJIRI hata kama kuna Changamoto na Hasara ABC. Na kama HUWEZI, basi UTAFUTE NAFASI ZA AJIRA MAPEMA. Kwa maamuzi yo yote Yale, jiapie "SITARUDI NYUMA TENA" kama ilivyoandikwa ndani na nje ya Kitabu changu (Kama huna hicho Kitabu, nijulishe nikutumie - kinapatikana, na kinauzwa).


AMUA LEO KUWA WA TOFAUTI. NIA ni Sababu ya dhati iliyopo nyuma ya maneno na matendo yo yote Yale - haijalishi ni mema au mabaya.

@LACKSONTUNGARAZA (Lamax)
Whatsapp: +255764793105
Bye bye... Uwe na Siku Njema Yenye Ushindi na Amani ya Mwenyezi Mungu aliye hai.


0 comments:

Post a Comment

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI