Mwalimu Emmanuel Makwaya aliwahi
kusema ya kwamba, "HUNUNUI KITABU CHANGU KUNIPA MIMI FAIDA, BALI KUUPA
UFAHAMU WAKO FAIDA"
Kuna Watanzania Wengi Leo ambao
hudhani Kununua Vitabu ni Kuwatajirisha Waandishi wa Vitabu. Utawasikia
wakisema, NGOJA TUKUUNGE KWENYE KITABU CHAKO HIKI!
Laiti kama Waandishi wa Vitabu
wangekuwa wanaandika kwa Lengo la biashara, wasingekuwa Wanaviuza kwa Gharama
ndogo za Tsh. 5000/= au Tsh. 10,000/=
-Waandishi wengi wa Vitabu Wanatoa
HUDUMA kwenye Jamii, Sio kufanya BIASHARA.
Ingekuwa ni kwa Lengo la biashara;
Vitabu vingekuwa vinauzwa hadi laki nane au Milioni Nne. Kwa Sababu wangekuwa
wanakokotoa kwanza FAIDA ambazo Wasomaji wanaenda kuzalisha kupitia hivyo
Vitabu - Results produced by the Book Content.
Fikiria! Kuna
Waandishi ambao Wameandika VITABU vya Kukuza Biashara, Ufugaji wa Samaki au
Sungura... Na kuviuza kwa Gharama ndogo ya Tsh. 10,000/= halafu Wewe Unaenda
kuzalisha zaidi ya Milioni kupitia hivyo Vitabu.
Kwa maisha ya Sasa, Tsh. 5000/= au
Tsh. 10,000/= inaweza Kununua Nguo Moja au Mbili za ndani kulingana na Jinsia
au Mwuzaji, na baada ya Mwezi mmoja Huchakaa sana na kutupwa. Lakini KITABU cha
Gharama hiyo hiyo ni HAZINA YA KUDUMU Kwako, kwa Wajukuu na kwa Uzao wako Wote
KUTEGEMEANA NA UTUNZAJI WAKO.
□ Kwa hiyo, kuanzia Leo Usinunue
Kitabu cha Lackson Tungaraza, Joel Nanauka, Pastor Raphael Lyela, Shemeji
Melayeki, na Wengine Wengi kwa dhana ya KUWAUNGA- KUWASAIDIA WAO.
....KUNUNUA KITABU NI KUJISAIDIA WEWE
MWENYEWE KABLA YA KUMSAIDIA MWANDISHI HUSIKA.
....
KUNUNUA KITABU NI KUJITAJIRISHA WEWE KWANZA, na Sio KUMTAJIRISHA MWANDISHI.
Acha Fikra Potofu, "Nikinunua Kitabu cha Lackson
Tungaraza Nitamtajirisha, na Mimi nitabaki kuwa Maskini."
- Fikra Potofu Ndio Umaskini Wako wa
Kwanza, Ukifuatiwa na Hofu ya Mabadiliko na Uthubutu.
TANZANIA BILA FIKRA POTOFU
INAWEZEKANA!
0 comments:
Post a Comment