Showing posts with label KWANINI WATU HAWAFANIKIWI KWENYE MAISHA YA KILA SIKU-Tungaraza (made with Spreaker). Show all posts
Showing posts with label KWANINI WATU HAWAFANIKIWI KWENYE MAISHA YA KILA SIKU-Tungaraza (made with Spreaker). Show all posts

Monday, May 6, 2019


Leo ukimwuliza Mtoto wa Darasa la Kwanza 1-5 (Moja kutoa Tano) ni Sawa sawa na ngapi, atakwambia haiwezekani, ni Lazima pawepo mahali pa kukopa. Lakini ukimwuliza hilo hilo Swali aliye Darasa la Tano atakwambia ni Sawa sawa na -4 (hasi Nne). Wanafunzi ni wale wale lakini Majibu tofauti. Na Kila Mmoja yuko Sahihi kulingana na kiwango cha Maarifa alichonacho kwa wakati huo.

Ni jambo gani ninalotaka ujifunze kupitia huo mfamo wa hapo Juu? Sikiliza, kwenye maisha yako Yote ya hapa Duniani, usitegemee ya kwamba kuna Siku Watu wote watakuwa na Mtazamo kama wako, Akili kama zako, wala kiwango cha Maarifa kama ulichonacho. Never. Unaweza Ukaandika, ukasema,  au ukatenda Jambo ambalo ni Sahihi lakini Ukapingwa sana kana kwamba hauko Sahihi, na waliokupinga ndiyo wako Sahihi. Hiyo isikutishe sana. Inawezekana Wameamua kupinga kwa Sababu ndiyo kazi inayowaweka Mjini (Siku zote wapo kwenye kambi ya Upinzani kwa Kila Jambo), au hawajui walitendalo kwa Sababu ya Kiwango cha Maarifa na aina ya Usahihi walionao, au hawataki Ukweli ujulikane  (wanataka Watu Wengi waendelee kutembea gizani katika upofu, na wao wanufaike zaidi).

Kumbuka ya kwamba, kupingwa kwa Jambo Sahihi hakuondoi Usahihi wa hilo Jambo hata kama waliyolipinga watashinda.

Aiseeeh! Songa mbele, wasikutishie nyau. Unajua hata waliyokuwa wanapinga ujio wa Simu Janja  (Smartphone) kwa kusema ya kwamba ni za Freemason na zinanyonya Damu za Watu za Mikononi, ndiyo WANAOONGOZA Leo kwa kutumia hizo Simu. Kupingwa Sio kuzuiliwa. Yesu alipingwa ya kwamba Sio Mwana Pekee wa Mungu Ingawa Ishara zote zilionesha ndiye. Hata hivyo kupinga Kwao hakukuondoa Ukweli kwamba Yeye ndiye Mwana wa Mungu aliye hai. John Magufuli alipingwa sana wakati wa kampeni za Uchaguzi mwaka 2015 wakisema ya kwamba hawezi kuwa Rais wa Nchi kwa Sababu alifanya Makosa ABC alipokuwa Waziri. Kwani kupinga kwao kulimfanya asiwe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Hahahaha, Jibu unalo.

"Ukishindwa kusonga Mbele kwa Sababu ya kupingwa, basi Ujue ya kwamba Ulikuwa Hujui ulitendalo hata kabla ya kuanza kulitenda ulitendalo Leo." - LAMAX.


AMUA LEO KUWA WA TOFAUTI. Kuwa Yule unayetakiwa kuwa. Usiwe Yule anayetakiwa Kuwa kwa Sababu ya matakwa ya Watu fulani fulani.

Tukutane baadae.
By Lackson Tungaraza (Mwandishi wa Vitabu Kadhaa ambavyo Unaweza ukavipata Leo na ukaweza kunoa Uwezo uliyomo ndani Yako).

@LACKSONTUNGARAZA
#0764793105 WhatsApp.
https://lacksontungaraza.blogspot.com
#LamaxQuotes #LIVING4MANY #LamaxLibrary

Friday, March 8, 2019


Furahia Kila Siku Mpya ambayo Unapewa na Mwenyezi Mungu. Usipofurahia Leo uliyopewa na Mungu, Unadhani Kesho na Kesho kutwa zina nini cha Ajabu sana ambacho Kitakupa Furaha.?

Hata Kama Unawaza sana Juu ya Kupata Pesa ya Kulipa Kodi ya Nyumba, Ada za Watoto Shuleni, Mahari, Mkopo wa Benki... Furaha Isikuondoke Kabisa, hasa Furaha ya BWANA - Kwa Sababu Furaha ya BWANA ndiyo NGUVU Yako.


Kuna Wakati Unaweza Ukadhani ya kwamba Ukipata Aina fulani ya Simu, Gari, Nyumba, Mavazi, Watu, au Kiwango fulani cha Pesa, ndipo Utapata Furaha Isiyokuwa Kifani. Lakini huo Uongo mkubwa sana. Nakuhakikishia ya kwamba Utabaki kuwa vile vile hata Kama Utavipata Kupita Ulivyotarajia. Kuwa na Furaha ni Kuamua kutokea Ndani Yako hata Kama huna pesa, Mali, Umaarufu, n.k.

Wengi Mlitamani Kufika Vyuo vikuu na Kupata Digrii kwa Kuamini ya Kwamba Ndipo Mtapata Heshima Kubwa Kwenye Jamii na Kuwa na Furaha Isiyokuwa Kifani, Lakini baada ya Kufika huko Vyuoni na Kisha Kuhitimu, Mmegundua ya Kwamba MAMBO NI YALE YALE Kama ya Shule ya Msingi, Sekondari, na Mtaani. Wengine Mlidhani Mkioa na Kuolewa ndipo Mtakuwa na Furaha, Mlidhani Mkiajiriwa Kwenye Kampuni Kubwa na Kupata Mishahara Minono ndipo Mtayafurahia Maisha... hahahaha! Yote Yamekuwa Ubatili Mtupu kwa Sasa! Mmegundua ya kwamba Mlikuwa Mnakimbiza Upepo Msiojua Utakako wala Uendako.

Lengo Sio Kumkebehi yeyote Yule, Bali Kukushauri Uwe na Furaha ya BWANA hata Kama huna Yale Unayodhani Unayahitaji kwa Sasa. Furaha ni ya Muhimu sana. WaPo Wenye pesa nyingi na Mali lakini Hawana Furaha kwa Sababu hawana Afya Njema. Wewe uliye na Afya Njema lakini huna pesa na Mali, Mshukuru Yehovah Yahweh kwa hilo. Maadam Uko hai na una Afya Njema, Unaweza Ukapata vingine Kama Kawaida.

USIKUBALI KUTOKUWA NA FURAHA KWA SABABU YA MATOKEO MABAYA YA SHULENI, KUKOSA AJIRA, MSHAHARA MDOGO, KUTOKUOLEWA, KUTOKUWA NA PESA YA KUFANYIA BIASHARA, KUTOKUWA NA WATU WA KUKUTIA MOYO, N.K.

MAISHA NDIYO HAYA HAYA, YAFURAHIE KATIKA BWANA. Imeandikwa, "MAISHA ni zaidi ya CHAKULA, na MWILI zaidi ya MAVAZI."

IFURAHIE LEO, KESHO ITAAKISI FURAHA YAKO YA LEO.

       ..Ahsante sana.
Mawasiliano: +255-764793105.
@lacksontungaraza
AMUA LEO KUWA WA TOFAUTI.

Sunday, November 26, 2017


"MAFANIKIO hayaji kwa Ukubwa au Udogo wa kile Ulichonacho, bali kwa namna Unavyotumia kile Ulichonacho" ~Lamax

Kila siku nikikumbuka Hatua nilizopitia Kufika hapa nilipo Leo Kimaisha, ninapata hamasa ya Kumshukuru Mungu kwa kunifundisha kwa Kila Hali. Nami sio wa Kwanza, kwani hata Mtume Paulo alifundishwa na Mungu KUSTAHIMILI Kila hali; kushiba na Kuona njaa, Kufanikiwa na kutofanikiwa, kuwa na Vingi na Kupungukiwa, na mwisho wa mafundisho hayo akasema kwa hakika Niliyaweza mambo yote katika yeye anitiaye Nguvu.


Muda Kadhaa Uliyopita Nilikuwa natumia Simu ya Tecno S3 (pichani) katika Kuandaa Masomo (Audio, Video, Nukuu, Makala) Mengi niliyokuwa nikiweka Mtandaoni. Screen yake ilikuwa ndogo, UBORA wa picha ulikuwa wa kawaida sana, RAM na Memory nazo zilikuwa ndogo. Lakini Licha ya hayo yote Nilikuwa nikiandika hata Makala yenye Maneno zaidi ya Mia tano  (500) na kuweka Facebook na katika Blog yangu, na Kuanza kusomwa na Watu waliokuwa wakitumia Simu za Gharama kubwa kama IPhone, IPad, Samsung, Nokia n.k. Watu  Wengi walikuwa Wanastaajabu wakiniona nayo hiyo Simu. Wengine wakawa wananiuliza "HIVI HUWA UNATUMIA NINI KUANDIKA YALE MASOMO YAKO YA WHATSAPP?" na nikawa nawajibu "NI HII SIMU NILIYONAYO." Wakawa hawaamini kama ni kweli, maana walitarajia ya kwamba Ningekuwa na Bonge la Simu.
SIMU YANGU-TECNO S3


Baada ya Wengine Kuona aina hiyo ya Simu niliyokuwa nikitumia, wakaanza kuniambia ya kwamba Ninajiaibisha, hiyo Simu sio ya Hadhi yangu; Screen yake ni ndogo sana na ninaandika kwa Shida Sana. Nikawa nikiwasikiliza tu na kisha kuendelea na Mipango yangu, kwa sababu kwangu Haikuwa Adhabu Bali Kipindi cha Mpito. 

Nikaendelea na UAMINIFU huo kwa Miaka mitatu (2014-2017). Nikawa nikifanya Kazi ya Uandishi kwa Ustadi na kuwasaidia Wengi.


Kilichokuwa kinanisaidia sana ni Neema ya MUNGU, #MAONO yaliyonipatia NIDHAMU na UVUMILIVU, Pamoja na Kutumia kwa UBORA kile kidogo nilichokuwanacho kwa Wakati huo. Na mwisho wa Siku nikazidi kuwa bora zaidi kwa sababu MATENDO yananguvu kuliko MANENO, ACTIONS Speak Louder than WORDS. Na kisha baadae nikapata Simu ya Kisasa ya Samsung Galaxy Grand Prime Plus. 

Maandiko matakatifu yanasema "Aliye Mwaminifu kwa Madogo/Machache huwa MWAMINIFU Pia kwa Makubwa/Mengi"


Hivyo Usisumbuke sana katika kutafuta Makubwa ama Mengi ili kupata Mafanikio katika yake Uyafanyayo, kikubwa ni Kufanya kwa UAMINIFU, UVUMILIVU na Ustadi kwa Madogo/Machache uliyonayo ili Kupata Makubwa/Mengi Uyatakayo.




"Uwe MWAMINIFU"

"I have Never Seen a Great Person with an Easy Past. Your Present Situation is not your Final Destination, the Best is yet to Come. Keep Moving Forward while fully believing in Christ Jesus"



Lackson Tungaraza

lacksontungaraza.blogspot.com

0764793105

Sunday, October 15, 2017

KWANINI WATU HAWAFANIKIWI KWENYE MAISHA YA KILA SIKU-Tungaraza (made with Spreaker) Source: http://ift.tt/2gbY85E kuna mambo kadha wa kadha ambayo huwa kwa namna moja ama nyingine huwafanya watu wasifanikiwe katika maisha yao, licha ya kuwa na BIDII kubwa sana katika matendo. katika somo hili nililofundisha ICE FM RADIO wakati Fulani huko nyuma litakusaidia kuzifahamu Zaidi. jifunze sasa

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI