Monday, May 6, 2019


TAJIRI MKUBWA SANA DUNIANI AITWAYE SULEMANI Alisema hivi;

A) Atendaye Mambo kwa Mkono mlegevu huwa Maskini  (Kwa hiyo kuwa Maskini ni Matokeo ya kufanya mambo kwa Ulegevu/Unyonge/Liwalo na Liwe); Bali MKONO WAKE ALIYE NA BIDII HUTAJIRISHA (kila aliyetajirika ni kwa sababu ya kufanya kazi Yake kwa BIDII - sio kwa Kujaribu Jaribu).

B) Katika KILA KAZI "MNA FAIDA"; Bali Maneno ya Midomo huleta HASARA tu (Yaani kuongea tu bila kufanya KAZI ni kujiletea hasara maishani).

C) Alimaye Shamba lake atakuwa na Chakula TELE; Bali afuataye Mambo ya Upuuzi ATAPATA UMASKINI WA KUMTOSHA (Huo UMASKINI Utakuwa wa VIWANGO vya 4G au zaidi).

D) Je! Wamwona Mtu mwenye BIDII katika KAZI Yake? Huyo Atasimama mbele ya Wafalme ( atapata KIBALI kwa Watu waliofanikiwa zaidi. Hao Watu ndio watakuwa Watu wake wa karibu); Hatasimama mbele ya Watu Wasio na Cheo (hutamkuta kwa Watu wasiopenda kazi).

By Lackson Tungaraza.

Kupata Vitabu vya Lackson Tungaraza kama Cha SITARUDI NYUMA TENA, MWANACHUO DIARY, MBINU 16 ZA KUONGEZA MAUZO KWENYE BIASHARA YAKO, NAMNA YA KUSOMA KITABU, n.k. njoo WhatsApp kwa kubofya hii LINK: https://wa.me/255764793105



0 comments:

Post a Comment

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI