All
the so-called 'Secrets of Success' will not work unless you do--Unknown.
Siri za mafanikio ni nyingi
sana na utaendelea kuzisikia na kuzisoma sehemu mbali mbali.. Mtandaoni,
magazetini, vitabuni nk..... Sidhani kama kuna mtu humu ambaye hajawahi
kutamani Mafanikio na kufikia kiwango cha kutafuta Siri yake kwenye vyanzo
mbali mbali.
Nimekutana na Vijana wengi
sana, wengine ni ndugu zangu... Wamesoma vitabu kadhaa vya mafanikio. Mfano WHY
WE WANT YOU TO BE RICH, RICH DAD POOR DAD, THINK BIG, THINK AND GROW RICH,
MIDAS TOUCH n.k....
~~~Wengne wameenda mbali
zaidi hadi kuhudhuria Semina za waandishi wa Vitabu hivyo ili waipate ladha
halisi... Kama kunywa Togwa ambayo haijachacha. Why are they not
Successful!!!!!"
Lackson Tungaraza
nimejifunza vingi kwenye vitabu mbali mbali nilivyosoma, awali nilikuwa siyo
msomaji wa Vitabu kama baadhi ya wapuuzi wanavyosema ya kwamba WATANZANIA
HAWAWEZI KUSOMA VITABU HATA UFANYAJE. Baada ya kusota na maisha kwa muda, siku
moja nilikwenda kwa rafiki yangu kuongea naye mambo fulani ... Kipindi
ananionesha baadhi ya nondo alizonazo kwenye Kompyuta, ghafla nikakiona kitabu
cha THE BUSINESS OF 21st CENTURY cha Robert Kiyosaki. Nilikichukua na kuanza
kukisoma ukurasa kwa ukurasa pamoja na kunakili vitu vya Muhimu.
~~Aissseh! Macho yangu
yalitiwa Nuru kuanzia siku hiyo.. Cha kwanza ilikuwa ni juu ya MAPATO NA
MATUMIZI. Namna ambavyo wengne wanakuwa matajiri zaidi na wengne maskini
zaidi... Assets vs Liabilities.
~Success Secret brings
results to those working on it. Bila kufanyia kazi ulichosoma utabaki tu vivyo
hvyo kama anayejitazama ktk kioo akaondoka na baadae kusahau alivyo na kurudi
tena kujitazama. JIFUNZE KUENDESHA GARI BARABARANI SIYO KWENYE KOMPYUTA KWA
KUCHEZA GEMU. Umenipata hapo?
~~Kuwa Mtendaji wa yapo Mema
unayoyaona na kuyasikia.. Hamna tofauti ya mtu aliyesomea Kilimo na hajui hata
kushika jembe na yule ambaye hakusomea hicho... Tunahitaji kuona kitu kimetokea
siyo kimetabiriwa.
---Kwa Leo tuishie hapa, Maoni
yako yanakaribishwa kabisa.
TENDA, USISEME TU.
Lackson Tungaraza.
( www.facebook.com/ltungaraza )
0764793105 Whatsapp, sms.
0 comments:
Post a Comment