Showing posts with label BORESHA BIASHARA YAKO. Show all posts
Showing posts with label BORESHA BIASHARA YAKO. Show all posts

Thursday, May 9, 2019


- USIPOPATA AMANI YA MOYO, LICHUNGUZE AU LIACHE KABISA.

#Mfano! Umeambiwa Kilimo cha Papai kinalipa sana mwaka huu 2019. Usiwahi tu kwenda kukopa kwa ndugu zako au mahali po pote pale na kuanza kulima. Unapaswa kufanya TAFITI ZA KINA JUU YA GHARAMA ZA Kuanzisha na kuendesha, Changamoto zake, Masoko Yake, Mauzo, n.k.


Kabla ya Kuanza biashara yako ya Kilimo;

1- Andika Maono Yako  ( Unaona nini juu ya hiyo biashara ndani ya mwaka Mmoja, miaka miwili, n.k. Na je Unataka Ikue kwa kiwango gani - Je ni kwa upana wa Kuihudumia tu Jamii Yako ya hapo karibu au kwenda na miji  na Mikoa mwingine?).

2- Andika Malengo yako.

3- Andika Mikakati Yako (Hatua kwa Hatua ya namna utakavyoitekeleza hiyo biashara Kila Siku. Mfano ni Lazima uweke Wazi ni kwa namna gani Utasafirisha Mazao yako kutoka Shambani Ikiwa Wateja watataka uwapelekee. N.k).

Na vivyo hivyo kwa biashara zingine Utakazohusishwa au utakazoanzisha wewe Mwenyewe.

UNAJUA MAISHA NI FURSA. BILA FURSA NI NGUMU SANA KUKUA KIMAISHA. Na tunapoongelea FURSA, HATUGUSII TU KWENYE BIASHARA. Hata kwako Wewe unayetaka kuwa Mwandishi mkubwa, mwibaji, Mchoraji, Mwinjilisti, Mwalimu wa Neno la MUNGU, Mchezaji, Mchekeshaji, Msusi, n.k.

KILA MTU ANASTAWI KUPITIA FURSA Hata Wale waliyoolewa ni kwamba walijua namna ya Kuidaka hiyo Fursa na kuifanyia kazi moja kwa moja.

SASA, FURSA ZIPO KILA MAHALI DUNIANI. Hapo Ulipo zipo nyingi sana Ila huzioni, hapa nilipo zipo pia.

- Haijalishi uko Tanzania au Ulaya, "Fursa zipo po pote pale. Tofauti ipo kwenye kuziona, na kuzifanyia Kazi."

#Mwenye HEKIMA Mmoja aliwahi Kusema ya kwamba,
"AN OPPORTUNITY KNOCKS ONLY ONCE. THE NEXT ONE MAY BE BETTER OR WORSE, BUT NEVER THE SAME ONE. THAT'S WHY IT'S SO CRUCIAL TO MAKE RIGHT DECISION AT THE RIGHT TIME - BECAUSE A RIGHT DECISION AT THE WRONG TIME BECOMES A WRONG DECISION."

Naamini Kuna Jambo Zuri sana ulilojifunza hapa, basi Litendee Kazi kwa Bidii. Na kama Wahitaji Vitabu vya Lackson Tungaraza bofya hii LINK ya WhatsApp: https://wa.me/255764793105 .

By Lackson Tungaraza.
AMUA LEO KUWA WA TOFAUTI.


Wednesday, May 8, 2019


Mtu anakwambia "HII FURSA HAIKUHITAJI KUFANYA KAZI KWA BIDII. WEWE UKISHAJIUNGA, MAMBO MENGINE YOTE TUTAKUFANYIA SISI." Hapo Umeliwa.
VIJANA Wengi sana wa kitanzania HATUPENDI KUFANYA KAZI KWA BIDII NDIO MAANA HUWA TUNAKAMATIKA KIRAHISI SANA.

Na hiyo ni sababu kubwa sana ya BIASHARA YA KUBETI KUSHIKA SANA KASI NCHINI MWETU. Kila Siku unasikia namna mpya ya Kubeti.

#Zaidi ya Yote: Ikiwa Unataka Elimu kama hizi za biashara na Fursa, JIPATIE KITABU CHA "MBINU 16 ZA KUONGEZA MAUZO KWENYE BIASHARA YAKO" kwa Gharama nafuu kabisa. Njoo WhatsApp kwa kubofya hii LINK ili kupata Kitabu: https://wa.me/255764793105.

Monday, May 6, 2019


Kitabu cha Kwanza: "MBINU 16 ZA KUONGEZA MAUZO KWENYE BIASHARA YAKO.".



- Ndani ya Kitabu hiki Utapata Mbinu 16 za uhakika za Kukusaidia katika Kuongeza Mauzo (SALES) kwenye Biashara Yako yo yote Ile uifanyayo Mtandaoni au nje ya Mitandao. Ni zaidi ya mwaka tangu kilipozinduliwa rasmi, na kimekwisha Kuwasaidia Watu Wengi Kibiashara.

Wewe Unasubiri nini Kukua KIFEDHA wakati huu ambao Watu wanasema ya kwamba VYUMA VIMEKAZA (Hali ya Kiuchumi ni Ngumu, na hakuna Faida kwenye Biashara)?? KITABU HIKI NI MKOMBOZI WAKO. JIPATIE NAKALA YAKO LEO KWA "SOFT COPY" (pdf) po pote pale Ulipo Duniani. Ni Tsh 10,000/= tu.

- Bofya hii LINK kuwasiliana nasi moja kwa moja kwa WhatsApp: https://wa.me/255764793105.


Kitabu cha Pili: "NAMNA YA KUSOMA KITABU - How to Read A book.".


- Ndani ya hiki Kitabu utakutana na mambo mazuri sana ya Kukusaidia kupata hamu ya Kusoma Vitabu kwa ufasaha na kuweza Kuishi Ndoto Yako.

- Ndani yake utayapata "MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZA USOMAJI WA VITABU, NAMNA YA KUSOMA KITABU, SHUHUDA NA MASHAURI YA WASOMAJI MAARUFU WA VITABU, pamoja na MASWALI KUMI YA MUHIMU."
.
- Unaanzaje Kukosa hiki Kitabu?? AMUA LEO KUWA WA TOFAUTI, Mr. Lamax aliwahi kusema ya kwamba; "Usomaji wa Vitabu Sio Kipaji, ni TABIA Inayotengenezwa na Mtu Mwenyewe Kila Siku."

-Bofya hii LINK kuwasiliana nasi moja kwa moja WhatsApp: https://wa.me/255764793105. Utakipata kwa Tsh. 5000/= tu katika Mfumo wa "SOFT COPY  (pdf)."


MWANDISHI WA VITABU VYOTE ni LACKSON TUNGARAZA. Unaweza Kumjua zaidi kwa Undani na Yote ayafanyayo kwa KUBOFYA hii LINK: https://lacksontungaraza.blogspot.com/2019/03/lackson-tungaraza-ni-nani-haswa.html?m=1.


KARIBU SANA LEO.
- Kwa Mawasiliano ya Kawaida: +255 (0) 764 793 105.

Wednesday, March 6, 2019


"UKITAKA KUWA MC (Master Of Ceremony) UNAYEPENDWA ZAIDI MJINI, Unapaswa Kuwa na SIFA Mbili Kuu;

(I) Uwezo wa Kuwafurahisha Watu, Hata kama ni kwa Mambo ya Kijinga na Yasiyokuwa na maana.

(II) Uwezo wa Kuwafanya Watu WATOE PESA zaidi (Cash), Hata Kama ni Kwa Kukopa Kwa Majirani zao. Ili hizo Pesa Ziweze Kufidia Gharama zilizotumika Kwenye maandalizi ya Harusi, Sherehe, au Uzinduzi.

Mwonekano wa MC Sio Kigezo Kikubwa sana. Kitafuata mbeleni huko." - LAMAX.


Kwa hiyo, Kama huna hizo Sifa Mbili Kuu, Tafuta Kazi Nyingine ya Kufanya Mjini. Furaha + Pesa ndio Habari ya Mjini kwa Sasa.
@lacksontungaraza

Monday, March 4, 2019


Siku Moja nikiwa Nyumbani kwa Wazazi Wangu, nilipata nafasi ya kwenda kusema na Vijana wa Shule Jirani ambayo ilikuwa mbali Kidogo. Kwa dhumuni la kuwahi, nikaamua kutafuta Bodaboda (Pikipiki). Baada ya Muda Mfupi, nikaipata na kuanza safari ya Kuelekea huko Shuleni. Nilipofika, nikamlipa Jamaa PESA Yake, na "kumwomba Namba za Simu" Ili nije nimshitue anifuate baadae.

Tatizo Mojawapo walilonao Watu wa Bodaboda ni "KUTOKUWAPATIA WATEJA NAMBA ZAO ZA SIMU (Mawasiliano)" Kabla ya Kuombwa. Wengi Wanaishi kwa MAZOEA ya Karne ya Kumi na Tisa - Wanataka Wawe Wanatafutwa na Wateja Mara kwa Mara kama vile Dhahabu za Geita.

Baada ya Kupata namba za Simu za Yule Jamaa wa Bodaboda, Nilikuwa namwita mara kwa mara kupitia Simu Anipeleke ninapohitaji. Ikiwa na maana ya kwamba, Alinufaika sana kwa kunipatia namba zake za Simu nilizomwomba badala ya Kunipatia Yeye Mwenyewe. Kumbuka; Wakati huo Ananifuata Nyumbani, wenzake Walikuwa Wamekaa tu VIJIWENI Wakisubiria WATEJA.

Cha Mwisho nilichomshauri Yule Jamaa wa Bodaboda ni "UMUHIMU WA KUWA NA KADI BIASHARA/ KADI KAZI (Business Card)." Nilimwambia, "Business Card" itamsaidia Kuondokana na Tatizo la Kutaja namba zake Kila Wakati, au Kuwaandikia namba kwenye Makaratasi. Na Pia Itamfanya Aonekane Anajitambua, na Anaithamini sana KAZI Yake (Professionalism).

NAWE UNAYEFANYA BIASHARA YA BODABODA au BIASHARA yo yote Ile, nakushauri sana Uwe na "Business Card" - Kitambulisho Chako cha Kibiashara [ambacho Sio cha Kiserikali. Bali ni cha Kukutambulisha Wewe na Biashara Yako].

Kupitia "Business Card", WATU wataijua kwa Urahisi Biashara Yako Mahali Ilipo "physically" na Mitandaoni.

KARIBU SANA KWENYE KAMPUNI YA "LAMAX DESIGNS" UPATE HUDUMA YA "BUSINESS CARD" NZURI NA BORA ZAIDI. Ndani ya Lamax Designs UNAPATA UNACHOSTAHILI.

LAMAX DESIGNS: Providing You What You Deserve.




NJOO LEO UHUDUMIWE.
Mawasiliano! 0764793105

Kumbuka! UTAFUNDISHWA PIA NAMNA YA KUITUMIA "KADI BIASHARA" (Business Card) Yako.

AMUA LEO KUWA WA TOFAUTI. @lacksontungaraza

Monday, October 22, 2018


▪Zipo Siri nyingi sana za Mafanikio zilizokuwepo, zilizopo, na zitakazoendelea Kuwepo Siku zote maadam Watu Wanaendeleo kufanya Tafiti na kufanikiwĂ .

▪Kufanikiwa Kimaisha hakukuhitaji Kujua kwanza Siri zote za Mafanikio Duniani kwa Sababu hazitawahi kuisha. Cha Muhimu sana ni kuanza kutendea Kazi zìle Siri Kadhaa ambazo Umekwisha kuzifahamu Wakati unaendelea Kujifunza na kufundishwa Siri nyingine nyingi.

○ Pamoja na yayo yote, kuna Jambo la Msingi sana ambalo nawiwa kukujuza kwenye SIRI za MAFANIKIO;


(01) TUMIA AKILI ZAKO
IPASAVYO.



👉🏿 Watu Wengi sana katika Karne hii Wamekuwa Wavivu sana kwenye matumizi ya AKILI zao ipasavyo. Wenğine tangu walipòokoka wakaacha Kutumia Akili zao kwa kigezo cha Kuishi kwa Roho. Cha ajabu sana hata huyo Roho hawamtumii vilivyo.


... Google imeÄ·uwa Msaada wa Watu Wengi sana Siku hizi. Imekuwa mbadala wa matumizi ya Akili - badala ya Watu kutumia AKILI ipasavyo, wanatumia Google Ipasavyo. Siku hizi hata Kijana akiulizwa maana ya neno "Uzalendo au Kamusi" anaingia Kuuliza kwanza Google kwa Sababu Haamini akili zake na wala hazitumii ipasĂ vyo.

... "Tumeanza Sasa kuwa na Kizazi kinachojali sana kuchaji Kila Mara Simu zao kuliko Kuchaji Akili zao." - Lamax.


👉🏿Watu Wote unaowafahamu kwenye Ulingo wa mafanikio (akina Dewji, Bakresa, Mengi, Bill Gates, Donald Trump, Ronaldo, Messi, Samatta, n.k), Sio kwamba Walijaliwa Akili za Kipekee sana Wakati wa Uumbaji, Ila Wao hutumia AKILI zao ipasavyo kabla ya kufanya Jambo, na wakati wa kulifanya. Huku wasiofanikiwa wakiendelea kutumia sana "mihemuko na Hisia."


... Dunia nayo inawathamini sana wale wanaozitumia Akili zao Vyema, kuliko wale wanaotumia sana Nguvu za Mwilini. Ndio maana Watu wanaotumia sana Akili wanalipwa vizuri kuliko wanaotumia Nguvu. Nadhani Wewe ni shahidi Mwaminifu katika Hili. Hata shuleni, wanafunzi wanaotumia Akili zao vyema ndio wanaofaulu na kupata zawadi za pongezi.


... Mwenye hekima mmoja aliwahi kusema ya kwamba, “The world will only mind you when you Use your MIND.” Akiwa na maana ya kwamba, ‘Dunia itakuthamini tu pale utakapotumia Akili.’



Mcheza soka aitwaye Lionel  Messi ukimtazama kwa mwonekano wake wa nje ana mwili wa kawaida, hana mwili mkubwa sana na wala sio baunsa, lakini mambo anayoyafanya uwanjani ni makubwa sana – huwa anawatesa Wachezaji wa timu pinzani kwa sababu ya Utumiaji wake mkubwa sana wa Akili ipasavyo huku wenzake wakitumia nguvu ipasavyo na akili kidogo.

… Waisraeli walikaa Utumwani nchini Misri kwa zaidi ya miaka mia nne kwa sababu ya Uvivu wa kutumia Akili zao ipasavyo, wakaona ni afadhali kuishi kwa kutumia nguvu za mwili. Farao na wamisri wenzake hawakuwa na nguvu kubwa sana zaidi ya Waisraeli, ila waliamua kutumia akili zao ipasavyo kuwatawala wenye nguvu nyingi za mwilini. Na ndivyo ilivyo kwenye jamii yetu, wanaotumia Akili vizuri ndio wanaowaongoza wenye nguvu nyingi za mwilini, ndio wanaolindwa na Mabaunsa, n.k.


Mfalme Sulemani wakati anaandika kitabu chake cha Mithali, alinukuu na maneno ya Aguri mwana wa Yake kwenye sura ya thelathini ndani ya kitabu chake. Aguri alisema ya kwamba, ‘kuna VIUMBE VINNE VIDOGO SANA duniani, lakini VINA AKILI SANA: SISIMIZI: Wadudu wasio na Nguvu, lakini hujihifadhia Chakula wakati wa Kiangazi (Jambo ambalo Halifanywi na watu wengi wanaojiita Watu wazima); PELELE: Wanyama wasio na Uwezo, lakini hujitengenezea Makao Miambani; NZIGE: Hawana Mfalme, lakini wote huenda pamoja kwa Vikosi; MJUSI: Waweza kumshika mkononi, lakini huingia katika Ikulu.’

Ndugu msomaji umeona ambavyo unazidiwa na hao viumbe wane wadogo katika Matumizi ya Akili. Wewe mwenyewe Jichunguze hapo ulipo pamoja na yale unayoyafanya – ikiwa unatumia Akili zako ipasavyo au unaishi tu kwa Mazoea, Mihemuko ya mwili, pamoja na Hisia.


Yapo mambo mengi sana ya kuchambua katika hiki kipengele cha kutumia vyema Akili zako – ikiwa ni pamoja na Namna ya kuamsha akili iliyolala ndani yako, namna ya kutumia akili zako ipasavyo kiuchumi na kimaisha. KARIBU SANA KWENYE SEMINA YA LACKSON TUNGARAZA ya SIKU KUMI (kuanzia terehe 01 Oktoba hadi terehe 10 Oktoba, 2018,) ITAKAYOKUSAIDIA KIUCHUMI NA KIMAISHA KWA UJUMLA. Yapo mambo makubwa sana Unayoweza kuyafanya maishani bila kutumia Nguvu nyingi sana za Mwilini kama watu wanaopasua Miamba kwa mikono.  





Fungua hii Link kwa kubofya haya maandishi yenye rangi ya bluu ili upate kujua hiyo semina ya siku 10 kwa Undani zaidi – Zimebaki siku chache Semina kuanza:


Kwa Mawasiliano ya Simu: 0764-793105 (Ipo pia WhatsApp)
#LamaxDesigns #LamaxQuotes #NewLifeChapter
“LIVING FOR MANY”

SOMA PIA HAPA: DUNIA NI UWANJA WA MAPAMBANO




Thursday, January 18, 2018

All the so-called 'Secrets of Success' will not work unless you do--Unknown.

Siri za mafanikio ni nyingi sana na utaendelea kuzisikia na kuzisoma sehemu mbali mbali.. Mtandaoni, magazetini, vitabuni nk..... Sidhani kama kuna mtu humu ambaye hajawahi kutamani Mafanikio na kufikia kiwango cha kutafuta Siri yake kwenye vyanzo mbali mbali.
Nimekutana na Vijana wengi sana, wengine ni ndugu zangu... Wamesoma vitabu kadhaa vya mafanikio. Mfano WHY WE WANT YOU TO BE RICH, RICH DAD POOR DAD, THINK BIG, THINK AND GROW RICH, MIDAS TOUCH n.k....

~~~Wengne wameenda mbali zaidi hadi kuhudhuria Semina za waandishi wa Vitabu hivyo ili waipate ladha halisi... Kama kunywa Togwa ambayo haijachacha. Why are they not Successful!!!!!"



Lackson Tungaraza nimejifunza vingi kwenye vitabu mbali mbali nilivyosoma, awali nilikuwa siyo msomaji wa Vitabu kama baadhi ya wapuuzi wanavyosema ya kwamba WATANZANIA HAWAWEZI KUSOMA VITABU HATA UFANYAJE. Baada ya kusota na maisha kwa muda, siku moja nilikwenda kwa rafiki yangu kuongea naye mambo fulani ... Kipindi ananionesha baadhi ya nondo alizonazo kwenye Kompyuta, ghafla nikakiona kitabu cha THE BUSINESS OF 21st CENTURY cha Robert Kiyosaki. Nilikichukua na kuanza kukisoma ukurasa kwa ukurasa pamoja na kunakili vitu vya Muhimu.

~~Aissseh! Macho yangu yalitiwa Nuru kuanzia siku hiyo.. Cha kwanza ilikuwa ni juu ya MAPATO NA MATUMIZI. Namna ambavyo wengne wanakuwa matajiri zaidi na wengne maskini zaidi... Assets vs Liabilities.

~Success Secret brings results to those working on it. Bila kufanyia kazi ulichosoma utabaki tu vivyo hvyo kama anayejitazama ktk kioo akaondoka na baadae kusahau alivyo na kurudi tena kujitazama. JIFUNZE KUENDESHA GARI BARABARANI SIYO KWENYE KOMPYUTA KWA KUCHEZA GEMU. Umenipata hapo?

~~Kuwa Mtendaji wa yapo Mema unayoyaona na kuyasikia.. Hamna tofauti ya mtu aliyesomea Kilimo na hajui hata kushika jembe na yule ambaye hakusomea hicho... Tunahitaji kuona kitu kimetokea siyo kimetabiriwa.

---Kwa Leo tuishie hapa, Maoni yako yanakaribishwa kabisa.
TENDA, USISEME TU.
Lackson Tungaraza.
( www.facebook.com/ltungaraza )
0764793105 Whatsapp, sms.


Saturday, September 30, 2017

Haijalishi una Kazi ama hauna Kazi, kikubwa ni UTAYARI wako pamoja na Kiasi kidogo cha #PESA kuanzia Tsh.4000/=
Sasa Unaweza Kutengeneza Kipato cha Ziada (PESA) kupitia Kitabu changu "SITARUDI NYUMA TENA"
- Sitaki KUFANIKIWA mwenyewe, nataka nawe UFANIKIWE Kiuchumi.

Description: https://static.xx.fbcdn.net/images/emoji.php/v9/f5e/1/16/1f51b.pngUnatengenezaje sasa hicho kipato cha ziada?

Kuanzia tarehe 30/9 hadi tarehe 5/9/2017 Kitabu hiki Kitapatikana kwa Gharama ndogo tu ya Tsh.4000. NAWE UTAENDA KUUZA KWA GHARAMA YAKO AMBAYO ITAKUPATIA FAIDA (Mfano 4500, 4700, 5000 n.k)

Haijalishi Umeajiriwa, Umejiajiri ama Umeajiri, Kutengeneza Kipato cha ziada ni Jambo la Muhimu sana, tena sana.
☆Hii Itakusaidia pia wewe ambaye Hujapata AJIRA.
FAIDA NYINGINE UTAKAZOPATA; 
   1.Wateja Wangu Wote ambao Watakuwa Wanahitaji VITABU katika Mkoa au Wilaya Uliyopo, Nitawaelekeza Kuja kwako.
(Utanipatia Jina lako, Mawasiliano na Mahali Unapopatikana wakati wa kuchukua Vitabu)
Description: https://static.xx.fbcdn.net/images/emoji.php/v9/f51/1/16/1f449.pngNitakusaidia katika KUENDELEA KUTANGAZA KITABU.

   2.Utavirudisha kwangu ikiwa Havijauzika ndani ya Miezi miwili, na Kurudishiwa FEDHA yako (Hili Usiwe na Hofu ama Wasiwasi ya kwamba Utapoteza Fedha kwa Kukosa Wateja)

#ANGALIZO! Vitabu viwe kwenye MAZINGIRA Mazuri kama Ulivyochukua.
    3.Msaada wa namna ya Kuviuza Vitabu katika Maeneo uliyopo.



Description: https://static.xx.fbcdn.net/images/emoji.php/v9/f49/1/16/1f4da.pngKITABU "SITARUDI NYUMA TENA"

   1.Kinasubiriwa na Kupendwa na Watu wengi.
   2.Jina la Kitabu Linamvutia Mteja Kutamani Kujua Yaliyomo ndani yake.
   3.Kimetengenezwa kwa UBORA MZURI kuanzia kwenye COVER (Jalada) ambalo Halitaharibika Kirahisi hata Kikimwagiwa Maji kwa bahati mbaya.
   4.Kinabebeka Kirahisi (Portable) na hivyo Kuweza kwenda nacho po pote pale.
   5.Kina MAJIBU ya Watu Wengi.


Description: https://static.xx.fbcdn.net/images/emoji.php/v9/f28/1/16/1f352.pngKITABU HIKI KINAWAFAA WATU GANI (Wateja Utakaowauzia);

     1.Wanaopitia CHANGAMOTO Mbali mbali katika Maisha (Mfano Kutaka MAFANIKIO ya Kiuchumi, makundi rika n.k) na Namna ya KUZIVUKA.
-Hasa VIJANA (Mtu ye yote Yule ambaye Bado Hajazeeka ni Kijana, Haijalishi yuko kwenye Ndoa ama la)


     2.Ambao Hawajafahamu na Waliyokwisha Kufahamu Hatma yao (Destiny) katika Maisha, yaani Kule wanakotakiwa Kufika na Kuacha Kumbukumbu Chanya duniani.

{Bila Kujua Hatma Yako / Unapoelekea, Utakuwa Unatamani Kila siku kuwa kama Mtu fulani na Kushindana na Watu ambao Kimsingi Hujui Umbali Wanaokimbia. Zipo Hatua za Kukusaidia Kuifikia Hatma Yako}
   3.BINTI Atakaye kuwa na UZURI na UREMBO Usiopitwa na Wakati.
Nimeandika kwa LUGHA Nyepesi Mambo ambayo wanakutana nayo katika Maisha na Yamekuwa Mwiba wa Kuharibu ule UZURI na UREMBO ambao Mungu aliukusudia kwao.


Description: https://static.xx.fbcdn.net/images/emoji.php/v9/f60/1/16/1f51d.pngUnaweza KUJIULIZA Nimeyapata Wapi haya Yote!!

1: UZOEFU ambao Nimeupata Kupitia Mazingira mbali mbali ambayo Niliyapitia na pia Kuyaona.
2. Kwa Uweza wa Mungu mwenyewe.

Unakosaje Kuwa na Vitabu hivi au Kuongeza Kipato cha ziada!! Kazi ni kwako sasa.
Description: https://static.xx.fbcdn.net/images/emoji.php/v9/f51/1/16/1f449.pngBaada ya tarehe 5/10/2017, Kitabu hiki Kitapatikana kwa Gharama ya Tsh.5000/=


Mawasiliano!0764793105
Lackson Tungaraza.
Fb.com/ltungaraza
WAHI SASA KABLA HAVIJAISHA.

 

Tuesday, October 25, 2016

Ukubali, Ukatae.. Ukweli unabaki pale pale ya kwamba DUNIA NI UWANJA WA MAPAMBANO.

Karibu tupeane Maarifa kidogo hapa, Kujifunza Kitu Kipya Kila Mara ni sifa kubwa ya watu wenye Mafanikio Makubwa maishani.
-Binafsi napenda kujifunza sana Mambo mapya kila Mara.
đź’ˇLackson Tungarazađź’ˇ

-Dunia ni Uwanja wa Mapambano kwa sababu Kila jambo unalohitaji kulipata linakuhitaji Kulitafuta kwa kila Namna, liwe dogo ama kubwa bado litahitaji kiwango cha Uhitaji wako ili Kulipata.

-Ikiwa Dunia ni Uwanja wa Mapambano, basi inabidi Kuwa na Silaha nzuri katika Vita.
-Tutakushangaa sana Unakuja na Fimbo/Rungu kwenye Uwanja huu wa vita ikiwa wenzako wanatumia Risasi na Mabomu.
-Na kama unahitaji hilo Rungu lako kummaliza mwenye risasi, itakulazimu Kumwinda akiwa amezubaa au kajisahau.

Silaha hizi siyo za Kumwaga damu. Ninachomaanisha ni MTAJI WAKO. Kitu au Njia unayotumia Kufikia Malengo au Hatma ya Maisha Yako.
-Najua unatamani sana Kufikia hatua kubwa ya Mafanikio katika Maisha yako. Lakini je! Ni silaha ya aina gani uliyoingia nayo katika Uwanja wa Mapambano.

-Wote kwenye Mtaa wako wana maduka ya Kuuza vyakula na bidhaa za Majumbani, wote ni Wanafunzi wa Kozi moja, wote ni wakulima wa mazao, wote ni Waandishi wa blog na Vitabu nk.
-Katika hali kama hiyo, ni Silaha gani unazotumia ili kutoka katika Uwanja huu wa mapambano ukiwa Mshindi? Amua kutumia silaha nzuri na zenye nguvu zaidi.

     🔫 Silaha hiyo yaweza kuwa Ni Kipaji, Kipawa, Ufundi, Ujuzi, Ujanja, Elimu, Maarifa nk.
-Namna utakavyoitumia hiyo Silaha, itaashiria kama Utashinda Mapambano au la.
-Silaha bila Makali au Kujua Kuitumia, bado hautakuwa Mshindi mzuri. Soma Vitabu mbali mbali kulingana na Vita unayopigana, Jifunze kwa waliofanikiwa, Andika katika *Diary au NoteBook* mambo mapya unayojifunza kila wakati.
Akina Bill Gates, Erick Shigongo, Mwl Mwakasege nk.. Wamefika hapo baada ya Kutambua aina ya vita wanayopigana na aina ya silaha ya Kupambania.

    *Don't hunt Something that you cannot Kill*
-Pambana na jambo ambalo Unauwezo wa Kulishinda kulingana na aina ya Silaha na Pambano ulilonalo.
-Mimi nishatambua aina ya Vita ninayopigana na nimeshachagua Silaha za Kupambania ili nimalize salama nikiwa Mshindi, maana *DUNIA NI UWANJA WA MAPAMBANO*

KUMBUKA! Bahati NA Wakati (0pportunity and Time) Kila mtu Kapewa na Mungu.
-Itategemeana tu na USHAPU Wako.
-Mfalme Sulemani anatuambia hapa jambo hilo lenye Faraja kwa mĂ skini na Matajiri pia

   🔦 Mhubiri 9:10-11🔦

[10]Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.

[11]Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini *wakati na bahati huwapata wote*.đź’ˇ

-Kwahiyo kuwa Mjanja kila unapoingia katika Mapambano ambayo yapo hapa duniani.
-Pigana sana, utapumzika Ukifika mbinguni baada ya Kupambana vyema na Kutetea Imani ya kweli ambayo Mungu kaiweka ndani yako kwa njia ya Wokovu

✍Salamu zangu Kutoka kwake Yeye aliyeñiwezesha Kuziandika✍
Lackson Tungaraza
HAKUNA KURUDI NYUMBA, HADI KIELEWEKE


#MPAMBANĂ€JI_ATUMAINIYE_KATIKA_UWEZA_WA_BWANA YESU.
⛹Lackson TungarazĂ 


 (SUBSCRIBE Kwenye Channel yĂ ngu ya YouTube).




Kuwa Rafiki yangu Facebook, tumia;
- www.facebook.com/ltungaraza

đź’ŁKIMENUKISWA!!!

Saturday, October 1, 2016


 “JINSI YA KUFANYA BIASHARA YAKO KUWA YA TOFAUTI NA YENYE MVUTO MKUBWA”


 Tunashindwa kuongeza vipato vyetu kwa sababu biashara zetu hazina mvuto.

Tunapoendelea kufungua vyanzo vingine vya vipato kwa kutumia mbinu zile zile, tunaendelea kufeli zaidi na hata kukata tamaa kwa sababu ya kukosa wateja kwa kile tunachokifanya

 Hivyo badala ya kukimbilia mikopo kwa ajili ya kuanzisha biashara nyingine, ni bora tukajifunza mbinu za kuifanya biashara yako kuwa ya tofauti na Mvuto Mkubwa kwa Wateja

 Biashara inapokuwa na Mvuto na Utofauti ni rahisi sana kupata Wateja na pato lako kuongezeka

JE! UNAPENDA KUENDELEA NA SOMO HILI?
Haina shida, pakua hapa chini ili ujisomee hata ukiwa hauna intaneti.
PAKUA SOMO ZIMA HAPA (Download)

Kuwa rafiki yangu facebook: www.facebook.com/ltungaraza
 0764793105 [Mawasiliano]

Sunday, September 11, 2016


KIPI NI BORA KWA BIASHARA YAKO?

Kumekuwa na sitofahamu juu ya namna ya kutumia mitandao hii katika kukuza biashara. Ndiyo maana nimekuuliza; Kati ya Facebook na Blog, ni kipi bora kwa Biashara yako?

Jibu lako litaashiria ya kwamba, kwa namna moja ama nyingine utakuwa umepata uzoefu fulani katika hiyo njia unayotumia kulingana na changamoto ambazo umeshakutana nazo. Tuanze uchambuzi wa Facebook na Blog kibiashara;


FACEBOOK.
Facebook inafaida zake, mfano Hakuna gharama katika kufungua Ukurasa wa Biashara na pia ni mtandao wa Kijamii ulio maarufu zaidi maana inazaidi ya watumiaji bilioni 1.35 ambao wako’active’ kila mwezi.

Kama mtu unayetumia Facebook kibiashara, kadri Facebook inavyozidi kukua na kuongezeka watumiaji wake, ndivyo ambavyo inakuwa ngumu kwa wateja kuona Post (Makala) zako. Ndiyo maana unakuta umeandika Posts nyingi Facebook lakini LIKES ni chache zaidi au hazipo kabisa, na wakati ulichoandika ni kizuri kabisa. Tatizo siyo Post zako, bali ni wingi wa Watumiaji wa Facebook.

Hata kwa wale ambao wanalipia ili kufikia watu wengi zaidi {Boosting} unakuta waliosoma post[Post Views] ni chache mno, pamoja na Page Likes[waliopenda ukurasa wako]. Hii ni hasara kwa huyo mtumiaji aliyelipia, na ni faida kwa Mmiliki wa Facebook.

Kuna kipindi name niliBOOST Makala kwa kulipia lakini matokeo yake hayakuwa mazuri….idadi ndogo sana ya waliopenda ukurasa na waliosoma[Post and Page Likes]. Ni hasara, ukizingatia Pesa imetoka kubwa na aidha imeingia ndogo au la.
Haya niliyoyaandika hapo siyo kwamba yametokea kwa kila mtu. La! Hasha. Ni kwa baadhi ya wafanyabiashara, na huwezi jua kama anayefuata baada yao ni wewe hapo. Na hapa ninaelezea upanda wa biashara au jambo lolote ufanyalo ambalo linahitaji wafuasi/wateja.

Kwa ufupi, kwa sasa Facebook imepungua uwezo wake wa kumfanya mtu kukuza biashara yake zaidi kutokana na wingi wa watumiaji wake ambao pia wanaongezeka kila siku. [Lackson Tungaraza].


BLOG.
Aidha ni kwa Biashara au jambo lo lote ambalo unafanya ili kuifikia jamii, Blog ni vyema sana kuwa nayo. Kuna faida nyingi za kuwa na Blog, baadhi ni;

i.             Utakuwa Mwandishi mzuri.
Zaidi ya kuongeza wateja wa biashara yako, utaongeza pia uwezo wako wa kuandika kila siku au mara kwa mara ili kuwavutia wateja/wafuasi wako.

ii.           Utajifunza.
Ili uandike, inabidi usome. Ili uwe mwandishi mzuri itakubidi ufanye vitu viwili tofauti na wengine; Soma sana na Uandike sana.

iii.          Kuonekana Mtaalamu zaidi na Kuaminika.
Mathalani unaandika juu ya upandaji na uvunaji wa kahawa, utaonekana mtaalamu zaidi unayependa kazi yako kuliko yule ambaye hana blog… seen as a Professional expert at your field.
Kwa kadri utakavyokuwa ukiandika makala [blog posts] juu ya unayofanya katika biashara, kampuni au taasisi yako na kuwasaidia watu kutatua Kero zao, ndivyo watavyozidi kukuamini na kuwa Wateja wako wa kudumu.
‘Fully 85% of the happiness and success you enjoy In life will be determined by the Quality of your relationships with others’ –Brian Tracy.

iv.          Kujulikana zaidi.
Kupitia blogs, ni rahisi zaidi kujulikana ukilinganisha na Facebook.
Kwenye Blogs kuna ‘share buttons’ ambapo utaweza kusambaza Post zako katika mitandao mbali mbali ya kijamii moja kwa moja; kama whatsApp, twitter, facebook, linkedln, instagram n.k. Hivyo kutengeneza mtandao mkubwa wa watu, pamoja na wateja wa zamani na wapya.
Itaendelea….

Angalizo: Taasisi ya ‘NYI Movement’ tumetoa punguzo la bei kwa sasa katika kukutengenezea Blog nzuri kulingana na aina ya kazi unayofanya… aidha ni kilimo, afya, michezo, huduma ya injili, mapishi, ufugaji n.k. kama tangazo la hapa chini linavyoonesha. Karibu sana, punguzo hili ni la muda mfupi tu.
Blog ni ya muhimu sana kuwa nayo ikiwa unataka kuwa mtu makini katika kazi au shughuli unayofanya, pamoja na kutengeneza mtandao wa wateja na mashabiki wako ndani na nje ya mipaka yako ya kazi.

Please Share this post[watumie na wengine hili somo].

SOMA: KUJITAMBUA


Mawasiliano: 0764793105 [Lackson Tungaraza]

Jifunze kupitia;


  







MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI