Showing posts with label KUJULIKANA POPOTE. Show all posts
Showing posts with label KUJULIKANA POPOTE. Show all posts

Tuesday, October 23, 2018

Wakati uliopita tuliangalia namna ambavyo Akili ikitumika ipasavyo inaweza ikamfanya mtu akatumikiwa na wenye nguvu nyingi za Mwilini. Tuliona namna ambavyo Lionel Messi huwatesa Wachezaji wengi wa timu pinzani kwa sababu ya kiwango kikubwa cha uwekezaji aliyoufanya kwenye Akili zake. Ikiwa nawe unahitaji kufanikiwa kama Messi kwenye eneo lo lote lile, huna budi kuwekeza kwenye Akili yako – unao uwezo mkubwa sana wa kuifanya Akili yako ilale au iamke, ikimbie au itembee, isinyae au istawi na kuchanua, izae au iwe tasa.


Kama ulipitwa na sehemu ya kwanza ya Siri za Mafanikio - Tumia Akili zako ipasavyo, huna budi kujifunza kwanza kupitia hii link yenye maandishi ya bluu hapa chini ili twende sambamba;


Sasa, siku hii ya leo ninawiwa kukuletea siri ya pili ya mafanikio iliyotumiwa na akina Bakresa, Mo Dewji, Reginald Mengi, Shabiby, Maznat, Oprah, Dangote, Masanja Mkandamizaji, na wengine wengi unaowajua na kuwasikia. Ikiwa wao walio binadamu kama sisi waliweza kufanikiwa, hata nasi inawezekana kwa kutumia siri walizozitumia wao. Ili nisikuchoshe, siri yenyewe hii hapa chini;



(02) FANYA KAZI
KWA BIDII.



Mojawapo ya majanga makubwa yanayoitesa Afrika ni Uvivu unaoambatana na ufanyaji wa kazi kimazoea – kufanya kidhaifu kama akina fulani na kutegemea matokeo makubwa. Vijana wengi wa kitanzania, au wa kiafrika wanapenda sana kuweka bidii ndogo sana kwenye jambo na kutegemea Mavuno makubwa. Matokeo yanapokuwa madogo, wanaanza kusema ya kwamba Wamelogwa, au wanafuatiliwa na roho za kiukoo za Umaskini. Na ndio maana hata waonapo wengine wamefanikiwa wanaanza kuwashutumu ya kwamba wanatumia Mazingaombwe, Freemason, Mazindiko na Kafara. Nadhani nawe ni shahidi mwaminifu katika hili.


Baada ya wajasiriamali wa nje kuona vijana wengi wa kiafrika hawapendi kufanya jambo lo lote lile kwa bidii ili kuwa na hali nzuri za kiuchumi na kimaisha; wakaja na kampeni za kubeti kwa pesa kidogo ili kuvuna mamilioni, wakaja na kampeni za biashara ya mtandao – network marketing, ya kuwaaminisha ya kwamba wanaweza kuwa mamilionea wapya bila kufanya kazi kwa bidii – wenyewe ni kulala tu na kufanya mambo yao mengine huku pesa zikiendelea kuingia na kujaa kwenye akaunti zao za kwenye simu na benki. Mamia ya vijana wakatumia fedha zao za akiba kujiingiza huko kichwa kichwa, baada ya muda wakaanza kurudi na misemo ya ‘Ningejua! Ningejua’ na kuchukia michezo ya kubahatisha. Ingawa wengine bado wanajiingiza huko.


Ndugu msomaji,
“mtu ye yote Yule ambaye atakuletea FURSA mpya ya kukufanikisha kifedha bila kufanya kazi kwa bidii, mkimbie na umwogope kama dhambi. Hakuna uhuru wa kiuchumi usiomwitaji mtu kufanya kazi kwa bidii, kama huamini kawaulize matajiri wote unaowafahamu.” – Lamax

 – utawakuta wanafanya kazi kwa bidii kuliko maskini walio wengi. Kufanya kwao kazi kwa bidii hakumaanishi ya kwamba wanauchu sana na Utajiri usiokuwa na mwisho, ila kwa sababu kazi ni Utu. Kuishi bila kufanya kazi ni kufa bila kujielewa.

Ulishawahi kujiuliza ni kwa nini Walokole wengi wana hali ngumu za kiuchumi licha ya kusema ya kwamba Mungu wao anamiliki fedha na dhahabu zote, naye alikwisha kuwabariki!! Ni kwa sababu ya kutokufanya KAZI kwa BIDII. Wengi wao wanadhani MAOMBI ndio njia ya MKATO ya kuwafikisha kwenye Uhuru wa KIFEDHA. Kumbe sivyo!

Mungu hawezi akamfanikisha mtu ye yote Yule asiyefanya kazi kwa bidii – Yeye huliangalia neno lake apate kulitimiza. Anasema ya kwamba, ‘Atendaye mambo kwa Mkono mlegevu huwa Maskini; Bali mkono wake aliye na BIDII HUTAJIRISHA.’

Tena anaongezea kwa kusema, ‘Akusanyaye wakati wa Hari ni mwana mwenye Hekima; Bali asinziaye wakati wa Mavuno ni mwana mwenye Kuaibisha.’

Ndugu msomaji; unataka kuwa mwandishi kama Emmanuel Makwaya au Lackson Tungaraza, Mwalimu kama Dickson Kabigumila au Raphael Lyela, Mwamasishaji kama Joel Nanauka au Paul Mashauri, Mchekeshaji kama Joti au Masanja, Mwimbaji kama Angel Benard au Ambwene, Mwanasoka kama Ronaldo au Samatta, Kiongozi kama Nyerere au Nelson Mandera, Mwanasiasa kama Tundu Lissu au Zitto Kabwe, Mhubiri kama Reginald Bonke au Fred Msungu, na wengine wengi?
Siri mojawapo ni KUFANYA KAZI YAKO KWA BIDII.

Kama ni kuimba, imba kwa bidii. Kama ni kuandika, andika kwa bidii. Kama ni kucheza mpira, cheza kwa bidii. Kama ni kusoma, soma kwa bidii. Unajua ni kwa nini ufanye hivyo? Kwa sababu ndio siri itakayokuketisha na Wakuu.



Mwenye Hekima mmoja aitwaye Sulemani alisema ya kwamba,
‘LO LOTE MKONO WAKO UTAKALOLIPATA KULIFANYA, ULIFANYE KWA NGUVU ZAKO
 – KWA BIDII’


Tukutane baadae kwa mwendelezo wa Somo la SIRI ZA MAFANIKIO. Hata hiyo Siri ya kufanya kazi kwa Bidii sio kwamba nimegusia kila kitu, ila nimekupatia maeneo ya Msingi zaidi.


Unaweza kujipatia VITABU vya Lackson Tungaraza, aidha cha ‘SITARUDI NYUMA TENA’ au cha ‘MWANACHUO DIARY’- Bofya hapa chini kujua kwa Undani kitabu cha Mwanachuo Diary;



Pia unaweza kujipatia Somo ambalo liko kwenye mfumo wa Sauti (audio) liitwalo ‘KIJANA NA UMAARUFU – Kuna Raha ya Kuwa Maarufu’ – utaweza kulipata kwa kutumiwa Mtandaoni.



Mawasiliano ya kupata Vitabu na Somo la Audio:

0764-793105 (ipo pia WhatsApp)

Zaidi: JIFUNZE
 Facebook Page ( @tungarazalackson )

Saturday, September 22, 2018

Mwenye hekima mmoja alisema ya kwamba,
 “sababu ya msingi inayowafanya watu wafeli kwenye maisha ni kutoweka Mipango mipya ya kuwaondoa kwenye Mipango ile ya awali iliyowakwamisha.”

Naamini kuna mipango kadhaa uliyopanga kuitekeleza mwaka uliyopita na ndani ya mwaka huu, lakini hadi sasa bado hujafanikisha hata robo yake. Kuendelea kulalamika ni kuendelea kujichimbia shimo la mateso na majonzi yasiyokwisha. Kuanguka chini kunaweza kuwa ni kwa bahati mbaya, lakini suala la kuamka na kusonga mbele liko mikononi mwako  - unapaswa kusimama, kukung’uta mavumbi na kuendelea na safari yako.  Ikiwa na maana ya kurekebisha hatua zako na kiwango chako cha umakini ili usianguke kwa mara nyingine tena, mtaani wanasema ni aibu kubwa sana kwa mtu mzima kuanguka chini na kulia.

Sisi kama rafiki zako, tumekuandalia semina nzuri sana ya siku 10, ambayo kwa hakika itakuinua mahali ulipoanguka, itakufuta vumbi, na kisha kukuongoza safarini mwako ili usianguke tena hata ukijikwaa kwa njia nyingine.


Semina hiyo itaanza rasmi tarehe 1/11/2018 na kumalizika tarehe 10/11/2018.
Nayo itakuwa inafanywa kwa njia ya mtandao wa WhatsApp.




Semina itakuwa na Mada kuu mbili;




1. MITAJI zaidi ya 30 Unayopaswa kuwa nayo ili Uweze kufanikiwa Kimaisha.


-          Watu wengi wakiulizwa sababu ya kutokufanikiwa kiuchumi na kimaisha, wanasema ni kwa sababu ya KUKOSA MTAJI, na Mtaji wanaoutazamia ni PESA nyingi.

-          Kupitia hii Semina utaifahamu Mitaji zaidi ya 30, huku PESA kama MTAJI ikiwa Mwishoni kabisa. Utaona ni kwa namna gani ambavyo PESA SIO KILA KITU katika ulimwengu wa sasa licha ya kuwa na manufaa  mengi sana kama ya kulipia Ada za shuleni na vyuoni, kununua mavazi na magari, n.k


-          Karibu sana, utaenjoy kwa kweli.


2. Mambo unayopaswa kujua kuhusiana na FURSA, hasa wakati huu ambao zinakuja Fursa za kila aina.


-          Kila siku huwa unapata taarifa redioni na mitandani za uwepo wa fursa mpya mjini ambayo inalipa sana na kutajirisha ndani ya muda mfupi sana bila kufanya kazi za kutoka jasho. Inawezekana ni ya Kilimo cha Matikiti, ufugaji wa kware, kilimo cha Mbao, biashara ya mtandao (Network Marketing), Kubeti, Uuzaji wa Sarafu mtandaoni, n.k

-          Kupitia hii semina utajua ukweli uliopo nyuma ya hizo Fursa, namna ya kutambua Fursa za kweli na za uongo, namna ya kujitengenezea fursa binafsi, hatua za kufuata kabla ya kujiunga kwenye mlolongo wa Fursa mpya, na mengine mengi.


Atakayekufundisha hatua kwa hatua ndani ya hiyo Semina ya siku 10 ni LACKSON TUNGARAZA ambaye Wasifu wake upo kwenye Ujasiriamali, Uandishi wa vitabu kadhaa ikiwa ni pamoja ni vile vya “MWANACHUO DIARY” na “SITARUDI NYUMA TENA”, Mwanzilishi wa Lamax Quotes na Lamax Designs; Injinia wa mifumo ya kompyuta kutoka Chuo kikuu cha Dodoma, ndaki ya Teknolojia na Elimu Angavu (CIVE). Na pia Mwelimishaji wa Masuala ya kijamii kwa vijana kupitia njia za ana kwa ana, redioni, vitabuni, na Mitandaoni. Kwa hiyo, ni Mtu Mzoefu anayejua anachokifanya kwenye jamii.



Gharama za Semina nzima kwa siku zote kumi ni shilingi elfu ishirini za kitanzania (20,000) tu.

“Tarehe 17 hadi 24 Novemba utalipia Tsh. 15,000/= tu kama OFA kwako. Baada ya hapo (Tarehe 25 hadi 31) utalipia
Tsh. 20,000/= ikiwa Utachelewa kujisajili katika kipindi cha Ofa.”





DIRISHA LA USAJILI LIMEFUNGULIWA RASMI terehe 17/10/2018,
 kwa hiyo Hujachelewa kabisa.


Jisajili leo kwa namba za Simu 0764-793105 (M-PESA).
Utaona Jina la “Lackson Tungaraza”

Ukishatuma Pesa yako ya Usajili kwenye hiyo namba ya simu ya 0764-793105, tuma na Jina lako kamili kwa ujumbe wa SMS (Meseji) za kawaida au kwa njia ya WhatsApp kwa ajili ya Uthibitisho.


NAFASI YAKO IPO, KARIBU SANA.
KWA SWALI LOLOTE LILE; tumia hiyo hiyo namba ya simu, au email ya lacksontungaraza@gmail.com


Thursday, March 1, 2018

KUJULIKANA POPOTE KILA MWANADAMU huwa na ile hali ya kuhitaji KUJULIKANA aidha kwa Mema au Mabaya ambayo ameamua kuyatenda katika Ubora wa Ujinga au Hekima aliyonayo. Lakini hapa tutatazamia upande wa Mema, NAMNA YA KUJULIKANA POPOTE PALE KATIKA YALE UYATENDAYO. Karibu sana.... Usisahau ku_Subscribe na kuwasambazia na wenzako KUPATA VITABU VYANGU Mf. cha 'SITARUDI NYUMA TENA' 0764-793105 Lackson Tungaraza fb.com/ltungaraza

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI