Showing posts with label ICEFM_KWANINI WATU HAWAFANIKIWI KWENYE MAISHA YA KILA SIKU_Part2 (made with Spreaker). Show all posts
Showing posts with label ICEFM_KWANINI WATU HAWAFANIKIWI KWENYE MAISHA YA KILA SIKU_Part2 (made with Spreaker). Show all posts

Monday, May 6, 2019


Hivi hicho Unachokifanya Sasa Ukiwa peke Yako au ukiwa na mtu mwingine, kama Kesho utakikuta kwenye magazeti Yote ya Mitaani na Mitandaoni, JE UTAKIFURAHIA? JE NDUGU ZAKO WATAENDELEA KUMSHUKURU MUNGU KWA KUWA DAMU MOJA NAWE? JE WAZAZI WAKO WATAKUWA TAYARI KUJISIFIWA YA KWAMBA WEWE NI MTOTO WAO? JE JAMII ITAKUWEKA KWENYE KUMBU KUMBU ZA WATU WALIYOISAIDIA KUSONGA MBELE KIMAENDELEO? JE WATOTO WAKO WATAKIFURAHIA NA KUMSHUKURU MUNGU KWA KUWA NA MAMA au BABA KAMA WEWE? JE LITAMFURAHISHA MUNGU WA MBINGUNI?

Ikiwa unachokifanya Unaona kitakuaibisha kikiwekwa kwenye Magazeti ya kesho au kwenye Vyombo vyote vya Habari Nchini, basi ACHA KABISA KUKIFANYA. ANZA KUFANYA MAMBO MEMA HATA UKIWA MAHALI AMBAPO HAKUNA ANAYEKUONA au ANAYEKUJUA. Haijalishi Uko Gesti, Hotelini, Hosteli za Chuoni, Geto, Kichakani, Porini, Shambani, Sokoni, au pengine pale - SIKU ZOTE JIULIZE HAYA MAMBO KABLA YA KUTENDA JAMBO LO LOTE LILE.

Haya yote yanawezekana, hakuna lisilowezekana. Uwezekano unaanzia kwenye Nia, na Uzuri ni kwamba "Penye NIA pana NJIA."

AMUA LEO KUWA WA TOFAUTI.
#LD-LAMAX DESIGNS tunakutakia Mabadiliko Chanya kwenye Maisha Yako Yote.

"HISTORIA YAKO INAANDIKWA NA WEWE MWENYEWE. WENGINE WATAKUJA TU KUISOMA HADHARANI."

#Mawasiliano: +255 (0) 764 793 105
#Email: lamaxdesigs@gmail.com
#Sponsor: @LACKSONTUNGARAZA

Monday, August 6, 2018

Tangu Uanze kuvunja Laana za UMASKINI, huu ni Mwaka wa ngapi, na Je Umeshaanza kuwa TAJIRI?

Kabla ya Kuanza au Kuendelea tena na Uvunjaji Wako wa Laana za UMASKINI, Tathimini Kwanza ni kwa Jinsi Umejitoa Kulipa Gharama za kuwa TAJIRI; Muda, Nguvu, Fursa, Maarifa, Pesa N.k
... Je Umeshahudhuria Semina ngapi za Kiuchumi-za bure na za Kulipia,?
... Umeshasoma VITABU vingapi vya Kukusaidia Katika eneo Unalotaka Kufanikiwa Kiuchumi,?
... Umeshajifunza kwa Watu gani Waliyokutangulia,?
... Umeshaanza Kufanya mangapi tangu Umalize Kusoma Vitabu na Kuhudhuria Semina Za Kiuchumi,?
... Matumizi Yako  ya Kifedha Yakoje -Nidhamu ya Mapato na Matumizi,?
... Matumizi Yako ya Muda Yakoje - Tangu Unapoamka hadi Unaporudi Kulala,?
... Umetumiaje FURSA ya Kifedha zinazokuzunguka,? Mfano Kutatua Matatizo na Changamoto zilizopo kwenye Jamii Yako; Maji, Chakula, Usafiri, Elimu N.K.
... Umejitoa Kwa Kiasi gani Kujifùnza kwenye Makosa Yako ya Awali,? - Kulalamika na Kuwalaumu Wengine hakuleti Msaada wo Wote.
... Unatumiaje Teknolojia ya Sasa katika Mambo Yako ya KIUCHUMI,?
- "Ukiendelea Kuishi Wakati huu Sasa kama zamani, Utapata Shida sana Kufanikiwa Kiuchumi. Kila Msimu Mpya Unapoingia, Jaribu Kubadilika kiMalengo na Kimkakati, lakini ubaki kwenye MAONO Yako."
- Lamax.

... Je, Una MAONO Yaliyoandikwa,?
- Maono Ni dira ya Maisha Yako... ni Wapi Uelekee na namna gani Uelekee huko.
- "Pasipo Maono WATU HUACHA KUJIZUIA"

... Je, Una Mipango na Mikakati gani ya Kujikomboa Kiuchumi,? - Hii inafuata baada ya Kuwa na Maono Yaliyoandikwa.

Baada ya hapo, ndipo Uendelee au Uache Mambo Yako ya KUVUNJA LAANA ZA UMASKINI. Inawezekana UJINGA Wako ndio Unaowapatia UTAJIRI na UMAARUFU Wale Mitume na Manabii wa Uongo.

. Life Is a Choice
   You Live What you Decide.
  . LACKSON TUNGARAZA

Sunday, October 15, 2017

ICEFM_KWANINI WATU HAWAFANIKIWI KWENYE MAISHA YA KILA SIKU_Part2 (made with Spreaker) Source: http://ift.tt/2zpTKIG kuna mambo kadha wa kadha ambayo huwa kwa namna moja ama nyingine huwafanya watu wasifanikiwe katika maisha yao, licha ya kuwa na BIDII kubwa sana katika matendo. katika somo hili nililofundisha ICE FM RADIO wakati Fulani huko nyuma litakusaidia kuzifahamu Zaidi. jifunze sasa katika sehemu hii ya Pili. USISAHAU KU-SUBSCRIBE

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI