By Lackson Tungaraza
0764793105 whatsapp.
Habari yako rafiki
yangu mpendwa?
Baada ya kuwa
tumejifunza mada mbalimbali za ukombozi wa fikra na mafanikio ya kiuchumi. Napenda
kukushukuru kwa ufuatiliaji wako katika masomo yangu na pia kwa kuhudhuria
semina zangu za Ujasiriamali kwa njia ya Email na Whatsapp. Pia ni matumaini
yangu ya kwamba utakuwa umepiga hatua kiMaisha. Leo tutajifunza jinsi ya kuweka
Malengo na Njia za kufanikisha Malengo yako;
1. NAMNA YA KUWEKA MALENGO
YANAYOFIKIKA;
Malengo ni Mipango ya
muda mfupi; yaweza kuwa ni siku, wiki, mwezi au mwaka. Moja ya sifa kubwa ya
Malengo ni lazima yawe SMART;
S-Specific
(Malengo yako yawe wazi)
M-Measurable
(Yenye Uwezo wa kupimika kujua ni nguvu na jitihada kiasi vinahitajika ili kuyafikia)
A-Attainable
(Yenye kufikika, usipange ambayo huwezi kutimiza)
R-Realistic
(Yaweze kuakisi Uhalisia)
T-
Timed (Yenye kutimia ndani ya muda fulani).
Kila mmoja wetu kwa
namna moja ama nyingine huwa anajiwekea malengo ambayo anatamani baada ya muda fulani
yawe yametimia, yaweza kuwa ni malengo ya kiroho au kimwili. Utofauti unakuja
kwenye namna ya kuweka hayo malengo, kuna wanaotumia nguvu nyingi na wengine nguvu
kidogo. Nitakupa njia fupi hii leo;
Ili kuyafikia Malengo
yako kwa urahisi, ni vyema ukatumia SHORTEST PLAN ili usiwahi kuchoka njiani.
Weka Malengo yako katika Vipengele vidogo vidogo. Inawezekana unataka kuwa
Mwandishi mkubwa wa vitabu, ni vyema ukaliweka hilo lengo lako katika
Vipengele. Anza kuandika kila siku hata
hadithi moja au Insha yoyote ile ili kuweka ufahamu wako sawa. Kwa
kufanya hivyo utapiga hatua fulani kila siku kwa urahisi zaidi, utajikuta baada
ya miezi kadhaa unahadithi nyingi na Insha na unaweza kuwa na kitabu chako.
Mimi binafsi Lackson
Tungaraza, njia hii imenisaidia sana kuyafikia Malengo yangu na bado ninaitumia
kila siku. Sitaki kutenda yale yale kila siku, kila siku ninajipangia jambo
jipya la kufanya; Yaweza kuwa ni kuweka Blog yangu vizuri na kuweka Makala,
kuongeza ujuzi wa kutumia mitandao kibiashara, kusoma vitabu mbali mbali n.k.
Hii yote ili baadae niwe Gwiji na Sumaku katika Masoko ya biashara.
“Don’t think about what can happen
in a month or a year, focus on the 24 hours ahead of you and do what you can to
get closer to where you want to be”
2. NAMNA YA KUFANIKISHA MALENGO YAKO;
Baada ya kujifunza
namna ya kuweka Malengo yanayofikika kwa urahisi, naamini ya kwamba umeanza
kuweka elimu hii katika matendo. Kumbuka kuyaandika Malengo na vipengele vyake
katika daftari la kumbukumbu (notebook) au kwenye simu, kompyuta na kuweka
mahali ambapo panafikika. Yaani mahali ambapo ni rahisi kwako kuyaona na
kujikumbusha kila mara ili kuamsha nguvu mpya ndani yako; Yaweza kuwa ni
chumbani, sebuleni, kwenye gari, dressing table n.k.
Tutajifunza namna ya
kufanikisha Malengo yako ambayo umekwisha kuyaweka katika vipengele na
kuhifadhi mahali ambapo ni rahisi kufikika. Fuata hatua hizi chache tu;
i. Uwe na Nidhamu~ Have Discipline
Nidhamu/discipline ni
neno pana sana kwa sababu linatumika kila mahali kwa wakati wake. Shuleni ili
mwanafunzi afaulu vizuri inabidi awe na nidhamu nzuri, vivyo hivyo Maofisini na
Serikalini. Kumbe Nidhamu ni jambo la muhimu sana!! Tia bidii katika kutimiza
malengo yako, usiwe mtu wa visingizio na kughairi kila wakati, kumbuka umri
unaenda na muda haukusubiri. Huyo mzee unayemwona hapo, kuna wakati naye
alikuwa ni kijana kama wewe.
Rafiki yangu mpendwa,
unatakiwa kuwa na nidhamu ili Malengo yako yapate kutimia ndani ya muda
ulioweka. Nidhamu ya kujali muda wako, nidhamu ya kuthamini mwili wako na pia
watu unaochangamana nao. Ikiwa lengo lako ni la mwezi mmoja, basi hakikisha unalitimiza
ndani ya mwezi huo.
ii. Jiamini~ Have Confidence in
yourself
Kijana mmoja mdogo Daudi
alimwua Goliathi, bonge la mtu lenye miraba mine kwa sababu ya kujiamini.
Unapojiamini, ule uwezo uliyoko ndani yako unapata nafasi ya kujidhihirisha
wazi wazi. Jiamini ya kwamba unaweza kuyatimiza Malengo yako ndani ya muda
uliyojipangia. Usitolewe katika mstari wa mafanikio na watu wasiojua mbele wala
nyuma, wapo wapo tu, kumbuka kuwa mtendaji siyo msomaji tu wa post na kukaa
kimya
iii. Kuwa na Shauku/Msukumo wa
kuyatimiza Malengo yako~ Burning desire.
Chukulia mfano wa mtu
ambaye amezidiwa na maji ziwani, yanamzamisha na kutaka kumwua, jinsi mtu huyo
anavyotapa tapa huku na kule ilia pate hewa ya Oxygen na pia ili asife. Hiyo
ndiyo “burning desire.” Ukiwa na Msukumo
ndani yako, rafiki yangu mpendwa hakuna jambo litakalokukatisha tamaa kusonga
mbele. Utakuwa kama bondia unakwepa, unakinga na kutupia ngumi (Rolling with
punches) unakuwa ‘Unstoppable’. Hata zije ngurumo, radi, kiangazi ama masika,
wewe bado utasonga tu mbele. Kwa hiyo natamani sana uwe na shauku/msukumo ndani
yako kwanza ndipo uanze kuona mafanikio katika yale yote utakayoyapanga.
Ahsante sana kwa muda
wako uliotumia kusoma hii post, ubarikiwe na Bwana.
Kwa lolote, usisite kunijulisha kwa nambari 0764793105 ambayo pia ipo Whatsapp.
0 comments:
Post a Comment