KUJIAMINI Ni uwezo wa kuwa na uthubutu juu ya mambo pasipo kuwa na
hofu wala uwoga, wala kutegemea msukumo kutoka kwa ndugu, jamaa au rafiki.
Kujiamini
kunaweza kujengeka ndani ya mtu kwa:
Uwamuzi Binafsi. Nadhani wewe hapo ulipo hujawahi
kulazimishwa kuvuta hewa... Unavuta kwasababu umeamua kufanya hvyo na hata
akitokea mtu akakwambia acha kuvuta hewa, utamshangaa sana na uhenda ukamhisi
ni mchawi. Vivyo hivyo KUJIAMINI Ni Uwamuzi ambao mtu binafsi anapaswa
kuamua kuishi.. Katika kila eneo la Maisha yako, amua Kujiamini. Fanya Uwamuzi
binafsi kuanzia sasa.
Utendaji.
INORDER TO
BE EXPERIENCED YOU HAVE TO TRY MANY THINGS AS MUCH AS YOU CAN, MEET CHALLENGES
AND LEARN FROM THEN.
KUJIAMINI hujengwa kwa Kufanya jambo tena na
tena, kutana na changamoto na Kujifunza kupitia hizo Changamoto.
Mtu
aliyefanya mitihani mingi ya shuleni, huwa anakuwa na hali ya Kujiamini ndani
yake kuliko ambaye kafanya michache au ambaye hajafanya kabisa wakiwa wanaenda
kufanya Mtihani wa Taifa.
Mfano
unafanya shughuli za kuuza Viatu, mwanzoni unaweza ukawa na wasiwasi Au hofu
lakini kwa kadri ya muda utakavyozidi kwenda utaanza Kujiamini na hata ikitokea
unahojiwa sehemu, utakuwa hauna mashaka yoyote. HUWEZI JIFUNZA KUENDESHA
BAISKELI KWA KUSOMA KITABU AU KWA KUANGALIA IGOLIZO; BALI KWA KUTENDA. Anza
kutenda, Kujiamini kutajengeka ndani Yako.
Jitambue:
Ukijua
unakokwenda, utaweza kuchagua aina nzuri ya Usafiri wa Kutumia
... Kama ni
Usafiri wa baiskeli, gari, train au ndege. Nitashangaa kukuona uko stendi ya
basi unasubiria usafiri na hujui unakokwenda.
Jitaambue;
unatĂ ka kufanya jambo gani kwenye Maisha.. Kwa kufanya hvyo utaumba KUJIAMINI
ndani Yako.
0764793105
whatsApp
www.lacksontungaraza.blogspot.com
Mwonekano-
Your Grooming.
Unaweza ukawahujaelewa hii pointi na
hata kuanza kushangaa, ni kwa namna gani Mwonekano ukajenga Kujiamini ndani ya
mtu… Kuwa mpole, tuwe pamoja ndugu. Mwonekano wa mtu huanzia katika Mavazi
aliyovaa… ndani ya sekunde kumi za mwanzoni unapokutana na mtu kwa mara ya
kwanza, aina ya Mavazi utakayokuwa umevaa ndiyo yataashiria akupokeeje.
Chukulia mfano uko sehemu umepumzika
halafu anakuja mtu amevaa haya mavazi ya sahivi ya kimwendokasi… shati na
suruali kama dekio, halafu anakuomba simu yako mara moja awasiliane na nduguye
maana yeye ni mgeni eneo hilo na hanasimu… sidhani kama utamuamini. Licha ya
kwamba Mavazi hujenga Kujiamini, humpatia pia mtu Kibali/Kukubalika machoni pa
wengine.
MWONEKANO HUJENGA KUJIAMINI.[Lackson Tungaraza] |
MAVAZI HULETA KIBALI MACHONI PA WATU.[Lackson Tungaraza] |
Asilimia kubwa, huwezi kuvaa mavazi ambayo
hayaendani na tabia yako ya sirini… ukiona mdada anavaa nguo za kumuonesha
mapaja au maungo yake, basi fahamu hiyo ndiyo hali yake ya ndani moyoni na
hivyo pia jamii itamtafsiri kwa mwonekano wake, wanaume watakaomchumbia
watakuwa na aina yake hiyo hiyo. Sasa
Mavazi yanajengaje Kujiamini!! Hii ndiyo pointi ya msingi hapa.
Unapokuwa
umevaa vizuri kiimaadili, siyo kuvaa tu ilimradi umekutana na nguo kabatini
kwako… Unakuwa na uhuru wa kutembea njiani kwa Kujiamini, kusimama mbele ya
watu pasipokuwa na wasiwasi…. Ndiyo maana vyuoni wakati wa ‘presentation’
wanafunzi wanaaswa kujitahidi kuvaa vizuri kimaadili, kwanini? Kujenga
Kujiamini katika hatua ya kwanza. Ukivaa vinguo vimekubana makalio, hata ukiwa
njiani unajishitukia kama utapigiwa mluzi na wanaume na hata kukaa kwenye kiti
unajikunja kama paka aliyenyeshewa mvua na wakati vazi ni lako. Mimi binafsi [Lackson
Tungaraza] huwa nahisi Kujiamini sana pale ninapovaa vyema kimaadili zaidi.
Capture that!!
Ambatana
na watu sahihi.
Kunamsemo usemao, ndege ambaye hanambawa
akiwa katika kundi la ndege wenye mbawa, naye hujiona kuwa na uwezo wa kuruka
au kupaa na hivyo humpelekea kujaribu kuruka kama wenzake. Why!! Birds of the same feathers flock
together. Therefore, [associate yourself with confident people and you’ll
develop a sense of confidence in yourself, and eventually you’ll begin to
practice that sense of confidence to the outside world]-said Lackson Tungaraza.
Amua leo Kuifuata Ndoto yako bila kujali watu watasemaje..Inawezekana. |
Lastly
but not least, Neno La MUNGU
YES, Neno la MUNGU. GOD is the beginning
and the end, the source and the destination.
*tena mtaifahamu
kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru- Yoh
8:32* Kwahiyo Neno la Mungu ambaye ndiye Mungu anakujulisha maarifa ambayo
umepungukiwa ndani yako ili kujenga Kujiamini.. aliyekuumba, anafahamu udhaifu
wako na nguvu yako. Kweli hiyo ni ipi sasa!!
*Maana Mungu hakutupa roho ya woga,
bali ya nguvu, na ya upendo na ya moyo wa kiasi- 2Tim 1:7*
Huu ndiyo ukweli wa Neno lake, uwoga hautoki kwa Mungu bali kwa shetani. Ndiyo
maana YESU KRISTO anawaambia wanafunzi wake [Msiwaogope wauuao mwili,
wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na
roho pia katika jehanum- Mathayo 10:28]…
Anawajengea Kujiamini ndani yao, wasiwaogope wanadamu bali wamuogope Mungu.
Kujua kama kweli Mungu hakutuumbia roho
ya Uwoga, soma hapa… “Bali
waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi,
na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo
moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”
–Ufunuo 21:8. Waoga hapo inamaanisha wenye roho ya uoga, hivyo Mungu
hawezi akakuumbia roho ya uwoga halafu tena akuangamize… ni roho itokayo kwa
shetani. Dawa yake? Mwamini YESU KRISTO na ukubariki akuongoze katika maisha
yako yote na yale uyafanyayo… Mwambie ulikosea mwanzoni lakini sasa umetambua
na unarudi kundini mwake. WORD OF GOD IS THE BREATHE OF LIFE
Tembelea: www.jesusisalive2016.wordpress.com kumjua MUNGU zaidi |
©Lackson
Tungaraza
0764793105
whatsApp
www.lacksontungaraza.blogspot.com
www.facebook.com/ltungaraza on facebook[Follow me]
Hizo ni baadhi
ya njia za Kuweza KUJIAMINI. Fanyia kazi.... Kuwa Ni Kutenda. Actions speak
Louder than Words.
WE ARE THE
CHOSEN GENERATION [N.T.I MOVEMENT].
Ebu tushirikishe njia nyingine ambayo huwa unatumia kujenga hali ya KUJIAMINI ndani yako .... karibu sana, tunasubiria wazo lako
ReplyDelete