MADHARA YA KUKATA
TAMAA
Habari yako rafiki yangu mpendwa?
Nakupa pongezi kwa kuendelea kutafuta maarifa mbali
mbali ya kuweza kubadili maisha yako katika mtazamo uliochanya, ni wengi
wanatamani lakini hawachukui hatua wanabaki kulalamika kila siku. Kwahiyo
mshukuru Mungu wako.
Baada ya kujifunza mambo mengi kwa habari ya namna
ya kuweka Malengo na jinsi ya
kuyafanikisha na masomo mengine mengi juu ya Mafanikio katika Maisha yetu ya
kila siku. Leo napenda tuangalie hili suala la kukata tamaa. Watu wengi,
wanamuziki, waalimu, wanasheria, wanafunzi, mawaziri, wafanyabiashara,
wanandoa, wachumba, wachungaji wameingia katika ramani ya maisha ambayo
hawakuwa nayo awali kwa sababu ya kukata tamaa. Kukata tamaa ni adui namba moja
aliyewapeleka wengi makaburini kabla ya wakati wao, aliyewafanya wengi
waonekane ni wazee wakati bado ni vijana, aliyewafanya wengi waone kama maisha
hayana maana yoyote kwao. KUKATA TAMAA
NI NINI?
Kukata
tamaa ni hali ya kupoteza matumaini. Hali hii hutokea
pale ambapo mtu anapoteza imani juu ya matarajio yake ya sasa na ya baadae ya
kupata kitu fulani alichojipangia. Kuna wanaofahamu kuwa wamekata tamaa na
wengine hawafahamu kama wamekata tamaa. Kama una dalili zifuatazo, basi gundua
ya kuwa umeshakata tamaa;
i.
Kukosa msukumo wa ndani. Ili mtu yeyote
yule aweze kufanikiwa anahitajika kuwa na msukumo wa ndani (burning desire),
huu msukumo haupo ndani ya aliyekata tamaa.
ii.
Kufanya Maamuzi ya haraka
iii.
Kupoteza hamu juu ya jambo Fulani. Inawezekana kuna jambo
ulikuwa unalifanya kwa furaha na uzuri lakini ghafla unaanza kupoteza hamu juu
ya jambo hilo.
iv.
Kupoteza Ujasiri. Mwanzoni ulikuwa
unatenda jambo kwa ujasiri lakini sasa ujasiri huo umepotea ghafla.
v.
Kujihisi hufai kabisa. Unajichukulia kama
mtu usiye na thamani yoyote ile hapa duniani.
vi.
Mabadiliko ya Tabia. Kutoka tabia nzuri
hadi mbaya
vii.
Kupungua kwa juhudi katika jambo
ulitendalo. Mwanzoni ulikuwa unafanya kazi kwa bidii lakini sasa unajifariji ya
kwamba unapumzika kidogo au utafanya baadae.
viii.
Maneno na vitendo vinavyoashiria kukata
tamaa kama matumizi ya madawa ya kulevya, Ukahaba, Sidhani kama nitaweza,
kujitenga n.k
Nadhani sasa utakuwa umejitambua kama ulikuwa
umekata tamaa au la. Madhara ya kukata tamaa ni makubwa japokuwa watu
wanajifariji, kama;
I. Kupoteza
Dira ya Maisha. Ili mwanadamu aweze kufanikiwa hapa
duniani, anatakiwa kuwa na dira (maono). Lakini mtu anapokata tamaa, dira hii
hupotea ghafla na hivyo kujikuta akitenda mambo ya ajabu hata kama mwanzoni
alikuwa mtu mwema na mwadilifu
I II. Kutokufikia
Malengo yako ndani ya Wakati. Katika video iliyopita
nilielezea juu ya sifa mojawapo ya Malengo, lazima yawe na muda maalumu; kama
ni wiki, mwezi, mwaka au zaidi ya hapo. Hivyo mtu anapokata tamaa, Malengo hayo
huwekwa pembeni kwanza na kusababisha upotevu wa muda uliopangwa
III. Kufanya
Maamuzi ya Haraka. Kama mtu alikuwa mtumishi wa Mungu,
basi anajiingiza katika masuala ya Uzinzi, matumizi ya madawa ya kulevya.
Mwanafunzi aliyefeli kujiua, Wanandoa kupeana taraka, Wanawake kutoa Mimba n.k
pasipo kufikiria kwanza.
IV. Jamii
na Taifa kukoswa Maendeleo. Waziri, Mzazi anapokata tamaa,
basi hawezi kuleta maendeleo yoyote kwa sababu ameshajiona yeye siyo wa thamani
na hata hatokuwepo, kwa nia ya kujiua .
KUMBUKA MAMBO YAFUATAYO IKIWA UNATAKA KUKATA TAMAA;
HAMNA MWENYE UWEZO WA KUZUIA NDOTO YAKO IKIWA HUJAWAPA NAFASI YA KUITAWALA, SONGA MBELE SIKU ZOTE, USIKATE TAMAA, MAMBO MAZURI ZAIDI YANAKUJA MBELENI. |
Nakushukuru sana kwa muda uliyotoa kusoma Makala hii
ya leo, Unaweza changia lolote lile ambalo unaona kwa upande wako litasaidia
jamii yetu kusonga mbele. Pia kumbuka kuSHARE ili kuwafikia ndugu na rafiki
zetu wengi. Ubarikiwe na Bwana.
Ni Mimi Rafiki Yako Mpendwa,
Lakson Tungaraza.
0764793105
(whatsapp/piga simu)
Ukizijua principles za maisha, hutopata shida...usikate tamaa.
ReplyDeleteToa maoni yako hapa