Saturday, March 16, 2019

Nakumbuka Wakati nilipokuwa Field ya mwaka wa pili St. John's University of Tanzania  (SJUT) iliyopo Jijini Dodoma, ndiyo Wakati nilipopata wazo  (idea) la Kuandika Kitabu ambacho kitawasaidia Vijana wenzangu Wengi Juu ya Changamoto za Ujanani ambazo zimesheheni Kila Upande kuanzia kwenye familia, Jamii, na Mitandaoni.

Hakikuwa Kitabu changu cha kwanza Kuandika, Ila kwa namna kilivyougusa moyo Wangu niliona Kiwe cha kwanza kutoka halafu ndipo Vitabu vingine vitafuata.

Kilichonisukuma zaidi Kuandika hicho kitabu ni aina ya maisha ambayo niliyapitia katika Ujana Wangu kabla na baada ya kuamua kurudi kwa Mungu. Na pia aina ya maisha ambayo vijana wa Sasa Wameamua kuyaishi bila Kujua ya kwamba Wanapanda mbegu ya kuwaharibu Wao na Kizazi chao.

Wakati naandika hicho Kitabu Nilikuwa naishi kwa Kijana niliyekutana naye huko huko maeneo ya SJUT, na pia alikuwa ni mwanafunzi wa hapo Chuoni. Nadhani Ulikuwa ni mpango wa Mungu kuniruhusu niishi katika Yale Mazingira yaliyopelekea niandike Kitabu. Lakini haikuwa rahisi kihivyo kwa Sababu mwanzoni nilikuwa najilaumu Kuishi katika Yale Mazingira, na pia nilikuwa namwomba sana Mungu awaondoe Machoni pangu Wale Vijana Watukutu waliyokuwa wanakuja na Stori zisizofaa pale nilipokuwa naishi kwa wakati huo.

Asubuhi moja wakati namwomba Mungu ili awazuie Vijana waharibifu kuja pale nilipokuwa naishi, ndani Yangu nikaja WAZO Jipya ambalo Sikulitegemea Kabisa. Niliambiwa hivi, "TATIZO HALIKIMBIWI, TATIZO LINATATULIWA. HAYA YANAYOFANYWA HAPA NA HAWA VIJANA YANAFANYWA PIA NA VIJANA WENGINE WALIYO MBALI NAWE." Baada ya kupata hilo wazo, nikaacha kwanza Kuomba na kuanza kulitafakari. Katika Kutafakari Kwangu, nikaona ni vyema niandike kile ambacho kitawasaidia Vijana Wote  [Wakati huo Nilikuwa Sina wazo la Maandishi hayo kuja kuwa kitabu]. Kwa hiyo nikaondoka na kwenda kuketi mahali kulipokuwa na Kompyuta Yangu ili nianze Kuandika Yaliyomo Moyoni mwangu. Nikaanza kwa kuangalia Changamoto kubwa 5 zinazowasumbua vijana wengi sana. Nikapata hizi hapa:

(1). Peer pressure - Makundi Rika.
(2). Kutaka UMAARUFU.
(3). Kutaka Mafanikio ya haraka.
(4). Tamaa.
(5). Kiburi.

Baada ya Kuandika zote na kuzielezea kwa Kina, nikaona haitakuwa vyema kwa kuziongelea tu bila kuwa na Suluhisho. Hapo nikapata sehemu ya Pili Iitwayo "NAMNA YA KUZIVUKA CHANGAMOTO."


Kisha nikapata tena wazo la kuwaelezea VIJANA ni kwa namna gani wataweza kufikia Hatma zao za Kimaisha  (Destiny), kwa Sababu nilijua Watakuwa na Maswali Mengi mioyoni mwao juu ya namna ya Kuishi baada ya kuzivuka zile Changamoto kubwa za Ujanani. Kwa hiyo nikapata sehemu ya Tatu Iitwayo "IFIKIE HATMA YAKO" (Reach & Fulfill your own Destiny). Kwa Uongozi wa Mungu nikaandika hatua ambazo Kila Mtu anapaswa kuzifuata kama Ana nia ya dhati ya kufikia Ile Mipango ambayo MUNGU anayo kwa ajili Yake.

Sasa Nilipokuwa nataka kuhitimisha, nikapata tena wazo la Kuwasaidia MABINTI kwenye eneo la MAHUSIANO Yao na Mungu, Yao na Wao Wenyewe (Self Relationship), na Yale ya Kimapenzi. Kwa nini nilitakiwa kufanya hivyo? Kwa Sababu niliona namna ambavyo mabinti wengi walikuwa wanadanganywa na vijana wa Mtaa Ule wa SJUT, UDOM, na kwingineko. Na pia niliona ya kwamba Mwanamke akijitambua Vizuri ataifanya pia na Jamii Yake Yote kuwa Imara. Na hapo nikapata sehemu ya Nne Iitwayo "KWAKO BINTI YANGU MPENDWA [Uzuri na Urembo Usiopitwa wa Wakati].

Mwishoni kabisa nikapata Shida ya JINA LA KITABU. Nikaomba USHAURI wa Watu mbali mbali, lakini napo nikaona kama vile Sijaridhika. Baadae ndipo nikapata Jina la "SITARUDI NYUMA TENA." Ambalo nililiona liko poa sana, kwa nini? Kwa Sababu LIMEKAA KWENYE MFUMO WA "KIAPO" ya kwamba MTU aliyekwisha kufahamu anayopaswa kufanya katika Maisha Yake HUPASWI KABISA KURUDI TENA NYUMA kwenye maisha yake ya Awali ambayo hayampeleki ambako Mungu anamtaka awepo.
JOSEPH MSEMBE AKIJISOMEA KITABU


Taratibu za Mwisho zikafuata hadi nikakitoa hicho KITABU changu cha kwanza cha Hard Copy  (Nakala Ngumu) mwezi Oktoba, 2017.

Kwa hayo Yote niliyoyaandika hapo Juu Utakuwa Umejua yaliyokuwa yamejificha NYUMA YA PAZIA hadi hicho Kitabu kuwa Jinsi Unavyokiona Leo. NAKUKARIBISHA SANA KUPATA NAKALA YAKO MOJA YA KITABU HICHO CHA "SITARUDI NYUMA TENA" ILI NAWE "ULE KIAPO" CHA KIMAISHA KWA MAENDELEO YAKO BINAFSI, FAMILIA YAKO, NA JAMII YOTE INAYOKUZUNGUKA. Gharama ya Kitabu ni Tsh. 5000/= tu.

Mawasiliano! 0764793105
@LACKSONTUNGARAZA
AMUA LEO KUWA WA TOFAUTI.

0 comments:

Post a Comment

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI