LACKSON TUNGARAZA KATIKA HARAKATI ZAKE ZA KUTOA HUDUMA YA VIATU |
Tunashindwa kuongeza vipato vyetu kwa sababu biashara zetu hazina mvuto
Tunapoendelea kufungua vyanzo vingine
vya vipato kwa kutumia mbinu zile zile, tunaendelea kufeli zaidi na hata kukata
tamaa kwa sababu ya kukosa wateja kwa kile tunachokifanya
Hivyo badala ya kukimbilia mikopo kwa
ajili ya kuanzisha biashara nyingine, ni bora tukajifunza mbinu za kuifanya
biashara yako kuwa ya tofauti na Mvuto Mkubwa kwa Wateja
Biashara inapokuwa na Mvuto na
Utofauti ni rahisi sana kupata Wateja na pato lako kuongezeka
Zifuatazo ni mbinu utakazotumia ili
uwe na Biashara yenye Mvuto na Utofauti Mkubwa dhidi ya Biashara zingine;
Mbinu Ya Kwanza
Bei Ya Bidhaa/Huduma Yako Imvutie Mteja
Biashara huanzishwa kwa lengo la
kutatua changamoto zilizopo katika jamii, zinaweza zikawa ni ukosefu wa bidhaa
au huduma Fulani
Endapo atatokea mtu wa kutatua
changamoto hizo, basi Wateja wapo tayari kumpa fedha zao kupata hizo Huduma au Bidhaa
Tatizo linakuja kwenye upangaji wa
bei ya Huduma au Bidhaa, na usipolizingatia hili litaangamiza biashara yako kwa
kufukuza Wateja
Bei yako isiwe ya ghali ili uweze
kuwashawishi watu kuinunua, Usitake faida kubwa au Mafanikio ya mara moja.
Wengine husema, “Kulala masikini na Kuamka Tajiri”
Inawezekana Huduma Yako Ikahitajika
mahali Fulani, lakini kwa sababu umetanguliza pesa mbele zaidi kuliko Utu au
Huduma yako, Utakuwa umekatisha watu tamaa ya kuwa Wateja wako na hutofanikiwa
Mbinu Ya Pili
Ubora Wa Huduma/Bidhaa Yako
Wahenga
walisema, “Kizuri Chajiuza Na Kibaya Chajitembeza”. Ubora wa Bidhaa/Huduma yako
ni jambo la muhimu sana ili kuvutia Wateja
Wateja
wanapenda Bidhaa/Huduma ambazo zitawatatulia matatizo yako moja kwa moja bila
kuathiri hali zao za kiafya
Bidhaa
zako zikiwa na Ubora, zitawavutia watu wengi kwako na utashangaa kuona mauzo
yako yakipanda
Ukifanya
tofauti na hapo, itabaki historia ya kwamba ulikuwa na Wateja Fulani. Hivyo
usiwauzie watu bidhaa feki au zilizopoteza Ubora wake (zilizo expire)
Usijaze
bidhaa ambazo sio bora, ni afadhali uwe nazo chache lakini ni bora zaidi.
Mbinu Ya Tatu
Muoneshe Mteja au Mpenzi Wa Huduma Yako Kuwa Unamjali
Wanataaluma wengi hupenda kusema,
“Kama hauna tabasamu usoni mwako ni vyema usifungue biashara”.
Mtu yeyote Yule anapenda kuonekana wa
muhimu na wa thamani zaidi, wengine wanatafuta nafasi hiyo kupitia vyombo vya
habari kama TV, redio, Magazeti n.k.
Hii tabia ipo pia ndani ya Wateja,
wanapenda kupokelewa kwa tabasamu na uchangamfu mkubwa wanapofika sehemu ya
uhitaji wa bidhaa/huduma
Ukifanya hivyo atatamani kuja kwako
kila mara, maana wengine huko wanakotoka hawana faraja wala furaha
Zingatia mbinu hii na utaona Wateja
wakimiminika kwako zaidi kuliko kwa jirani yako.
Mbinu Ya Nne
Usijali Muda Wako Tu, Jali Na Kuthamini Muda Wa Mtu Mwingine Pia
Wazungu wanasema ya kwamba, “Time Is
Money”. Kwetu sisi Wabongo, tunaona muda kama ni kitu cha kawaida sana kana kwamba
hakiwezi kuleta athari zozote katika maisha yetu na ya wale wanaotuzunguka
Unakuta Mteja anafika dukani kwa mtu,
anabisha hodi hadi anachoka, au anamtajia mahitaji yake mwenye duka lakini yeye
anakomaa tu na kuchati au kupiga soga
Mteja endapo utamwona bado anakuja
kwako, ni kwa sababu hajapata tu sehemu nyingine ya kwenda kupata hiyo
huduma/bidhaa. Ikitokea mtu mwingine akaja mwenye kukidhi haja ya moyo wake na
kujali muda wake kwa kumsikiliza kwa umakini, huyo Mteja hatorudi tena kwako
Tumia vizuri kwa umakini nafasi
ambayo Mteja amekupatia ili apate huduma/bidhaa kutoka kwako.
Mbinu Ya Tano
Tangaza Huduma/Bidhaa Yako
Hamna mwenye alama kichwani ambaye
akikutana tu na watu, wanatambua yeye anafanya biashara gani na yuko sehemu
gani. Labda tu kama amebeba bango au bidhaa Fulani ambayo ndiyo itakayo
mtambulisha
Biashara ni Matangazo na Matangazo ni
Biashara.
Matangazo ni gharama lakini tunatumia
shilingi kupata shilingi. Lakini usitangaze Huduma ambayo huwezi kuitoa kwa
kiwango hicho ulichoahidi, utapoteza Wateja wengi
Tumia njia mbalimbali katika
kutangaza bidhaa au huduma yako, unaweza tumia Redio, TV, Magazeti,
Mabango,Vipeperushi, Mitandao ya kijamii kama Facebook ambayo inawatumiaji
wengi sana duniani na wanazidi kuongezeka kila leo, Twitter, Instagram n.k.
Fanya Zoezi Hili Fupi
Nakushukuru kwa kusoma Mbinu hizi
za kuifanya biashara yako iwe ya tofauti na Yenye Mvuto mkubwa mpaka hatua
hii, Ninaamini kabisa una lengo la kubadilisha biashara yako kwenda hatua
nyingine. Malizia kwa kufanya zoezi hili fupi;
# Chunguza kwa Umakini kama bidhaa
ulizonazo zina ubora sahihi wa kumvutia Mteja. Pia chunguza kwa umakini bidhaa
unazonunua kwenye maduka ya jumla, zingine ni feki au zimeshapitiliza muda wa
matumizi
# Chunguza kama Bei zako zinaendana na
Uchumi wa Wateja wako waliopo katika hilo eneo. Lakini zingatia ya kwamba Ubora
wa bidhaa huendana na bei, zenye Ubora mkubwa zina bei kubwa pia
# Je, unamjali Mteja wako na kuthamini
muda wake pia?
# Je, unafanya Matangazo ya kutosha kwa
bidhaa au huduma ulizonazo?
Kwa Ushauri na Mafunzo yanayohusu
kufanya biashara yako kuwa ya tofauti na Mvuto mkubwa, Wasiliana na Ndugu Lackson Tungaraza, +255764793105 au tembelea Website ya lacksontungaraza.blogspot.com
07647931059(sms/wasap) [Lackson Tungaraza
PATA KITABU HIKI KWA GHARAMA NAFUU: 5000/- TU. PUNGUZO HILI LA BEI NI LA MUDA MFUPI TU, HIVYO WAHI MAPEMA. |
Wahi sasa, muda wa punguzo la bei umekaribia kufika mwisho.
ReplyDelete0764793105 [Lackson Tungaraza].
Nini maoni yako juu ya masomo ninayofundisha hapa?