Kati ya mambo yaliyomtia hamasa
Mwalimu Nyerere kuacha Ualimu na kuingia
kwenye ulingo wa Siasa, ni Kupata Uhuru (wa watu pamoja na Nchi yao).
๐Je
wewe bado unataka uhuru, Una uhuru, au hutaki kuutumia vyema uhuru??
Uhuru ni jambo la msingi sana na la muhimu kabisa.
Kuna
watu wengi sana ambao bado ni WAFUNGWA WA MAISHA YAO YA NYUMA (Historia). Kila
wakitaka kupiga hatua moja mbele kuelekea kwenye maisha ya UBORA, wanakumbuka
waliyoyapitia huko nyuma na namna walivyokuwa (mienendo), na hujishika tama na
kukata tamaa. Hawako tayari kutumia maisha hayo kama Ndoano ya kunasa FURSA na
KUWASAIDIA Watu wengine katika Jamii.
๐Hilo
janga Lipo hata kwa watu ambao wanasema ya kwamba WAMEOKOKA. Licha ya kwamba
wanasema ya kwamba wamesafishwa kwa DAMU ya Kristo YESU, lakini bado hawaamini kama ni Wasafi na hata
maisha yao ya nyuma HAYAWEZI Kuwachafua tena. Wamekuwa WAFUNGWA wanaojimiliki.
Wanajidai ya kwamba hawakuwahi kupitia maisha fulani hivi ya Uharibifu na
yasiyo mpendeza Mungu. Hahaha!
Ikiwa
bado Unajihukumu kwa kwa sababu hapo nyuma ulikuwa Mlevi, Kahaba, Mwongo,
Mzinzi, Mwasherati, Mchawi, Shoga, Fisadi, Jambazi, Kibaka..
Wewe ni MFUNGWA wa aina yake, hata kama
unasema ya kwamba Kristo kakuweka Huru. "UHURU USIOKUWA NA NURU NI
GUNDU"
Kama unaamimi kabisa ya kwamba Mtu
anapokuwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe KIPYA na ya kale yamepita, kwa nini bado
Umefungwa na HISTORIA ya maisha yako?? Kwa nini bado hujiamini!! Kwa nini bado
una mashaka na kufadhaika moyoni mwako?
๐Kupata
UHURU ni tofauti na Kuutumia na Kuishi maisha ya Uhuru. Wewe umeupata, lakini
huutumii na Kuuishi.
TUMIA
hali ya maisha yako ya awali kama FURSA ya KUWASAIDIA wengine walio katika hali
hiyo hiyo.
๐Kuna
#walevi ambao wanataka kuelimishwa na watu ambao washawahi kuwa Walevi pia.
Vivyo hivyo kwa Wadada wanaojiuza, Waoga wa Kufanya BIASHARA, Washindwao Kuishi
bila kuiba au kufanya NGONO n.k. Hao wote ni fursa yako, itumie.
Kwanini
Usishuhudie namna ulivyopambana na hali ya Kushindwa Kusoma Biblia na Vitabu
vingine, Ulivyoamka tena kibiashara baada ya kupata hasara, ulivyofaulu tena
baada ya KUFELI mitihani mfululizo!! N.K
●(TUMIA ZAIDI HEKIMA YA MUNGU KATIKA KUFANYA YOTE)
"Be not a Prisoner of your Past Life style.
Just be a Conquerer of it"
Lackson Tungaraza.
Amรนa
Leo Kumeza Dawa ya KUBADILIKA na KUWASAIDIA WENGINE.
Mtume
Paulo alitumia hali ya maisha yake ya awali kama FURSA ya KUWASAIDIA wengine
walio kwama papo hapo, waliokuwa hawaamini kama Inawezekana kuwa kiumbe KIPYA
kabisa ndani ya Kristo... Nami Lackson Tungaraza Natumia Vivyo hivyo ili nawe
utumie.
Acha mgomo baridi, unajipotezea MUDA.
Na Lackson Tungaraza
Fb.com/ltungaraza
"Heri mtu Yule ayasikiaye maneno hayo na
KUYAFANYA..."
( www.youtube.com/c/lacksontungaraza )
#Tukutane wakati ujao.
Shea na wenzako huu UJUMBE. Sharing is CARING.
0 comments:
Post a Comment