KIPI NI BORA KWA
BIASHARA YAKO?
Kumekuwa na
sitofahamu juu ya namna ya kutumia mitandao hii katika kukuza biashara. Ndiyo
maana nimekuuliza; Kati ya Facebook na Blog, ni kipi bora kwa Biashara yako?
Jibu lako litaashiria
ya kwamba, kwa namna moja ama nyingine utakuwa umepata uzoefu fulani katika
hiyo njia unayotumia kulingana na changamoto ambazo umeshakutana nazo. Tuanze
uchambuzi wa Facebook na Blog kibiashara;
FACEBOOK.
Facebook inafaida
zake, mfano Hakuna gharama katika kufungua Ukurasa wa Biashara na pia ni
mtandao wa Kijamii ulio maarufu zaidi maana inazaidi ya watumiaji bilioni 1.35
ambao wako’active’ kila mwezi.
Kama mtu unayetumia
Facebook kibiashara, kadri Facebook inavyozidi kukua na kuongezeka watumiaji
wake, ndivyo ambavyo inakuwa ngumu kwa wateja kuona Post (Makala) zako. Ndiyo
maana unakuta umeandika Posts nyingi Facebook lakini LIKES ni chache zaidi au
hazipo kabisa, na wakati ulichoandika ni kizuri kabisa. Tatizo siyo Post zako,
bali ni wingi wa Watumiaji wa Facebook.
Hata kwa wale ambao
wanalipia ili kufikia watu wengi zaidi {Boosting} unakuta waliosoma post[Post
Views] ni chache mno, pamoja na Page Likes[waliopenda ukurasa wako]. Hii ni
hasara kwa huyo mtumiaji aliyelipia, na ni faida kwa Mmiliki wa Facebook.
Kuna kipindi name niliBOOST
Makala kwa kulipia lakini matokeo yake hayakuwa mazuri….idadi ndogo sana ya
waliopenda ukurasa na waliosoma[Post and Page Likes]. Ni hasara, ukizingatia
Pesa imetoka kubwa na aidha imeingia ndogo au la.
Haya niliyoyaandika
hapo siyo kwamba yametokea kwa kila mtu. La! Hasha. Ni kwa baadhi ya
wafanyabiashara, na huwezi jua kama anayefuata baada yao ni wewe hapo. Na hapa
ninaelezea upanda wa biashara au jambo lolote ufanyalo ambalo linahitaji
wafuasi/wateja.
Kwa ufupi, kwa sasa Facebook imepungua uwezo wake wa kumfanya mtu
kukuza biashara yake zaidi kutokana na wingi wa watumiaji wake ambao pia
wanaongezeka kila siku. [Lackson Tungaraza].
BLOG.
Aidha ni kwa Biashara
au jambo lo lote ambalo unafanya ili kuifikia jamii, Blog ni vyema sana kuwa
nayo. Kuna faida nyingi za kuwa na Blog, baadhi ni;
i.
Utakuwa Mwandishi mzuri.
Zaidi
ya kuongeza wateja wa biashara yako, utaongeza pia uwezo wako wa kuandika kila
siku au mara kwa mara ili kuwavutia wateja/wafuasi wako.
ii.
Utajifunza.
Ili
uandike, inabidi usome. Ili uwe mwandishi mzuri itakubidi ufanye vitu viwili tofauti
na wengine; Soma sana na Uandike sana.
iii.
Kuonekana Mtaalamu zaidi na
Kuaminika.
Mathalani unaandika
juu ya upandaji na uvunaji wa kahawa, utaonekana mtaalamu zaidi unayependa kazi
yako kuliko yule ambaye hana blog… seen as a Professional expert at your field.
Kwa kadri
utakavyokuwa ukiandika makala [blog posts] juu ya unayofanya katika biashara,
kampuni au taasisi yako na kuwasaidia watu kutatua Kero zao, ndivyo watavyozidi
kukuamini na kuwa Wateja wako wa kudumu.
‘Fully 85% of the happiness and success you enjoy In life will be
determined by the Quality of your relationships with others’ –Brian Tracy.
iv.
Kujulikana zaidi.
Kupitia blogs, ni
rahisi zaidi kujulikana ukilinganisha na Facebook.
Kwenye Blogs kuna ‘share
buttons’ ambapo utaweza kusambaza Post zako katika mitandao mbali mbali ya
kijamii moja kwa moja; kama whatsApp, twitter, facebook, linkedln, instagram
n.k. Hivyo kutengeneza mtandao mkubwa wa watu, pamoja na wateja wa zamani na
wapya.
Itaendelea….
Angalizo:
Taasisi
ya ‘NYI Movement’ tumetoa punguzo la bei kwa sasa katika kukutengenezea Blog
nzuri kulingana na aina ya kazi unayofanya… aidha ni kilimo, afya, michezo,
huduma ya injili, mapishi, ufugaji n.k. kama tangazo la hapa chini
linavyoonesha. Karibu sana, punguzo hili ni la muda mfupi tu.
Blog
ni ya muhimu sana kuwa nayo ikiwa unataka kuwa mtu makini katika kazi au
shughuli unayofanya, pamoja na kutengeneza mtandao wa wateja na mashabiki wako
ndani na nje ya mipaka yako ya kazi.
Mawasiliano:
0764793105 [Lackson Tungaraza]
Email: lacksontungaraza@gmail.com
Facebok: www.facebook.com/ltungaraza
Jifunze
kupitia;
0 comments:
Post a Comment