Thursday, May 9, 2019


- USIPOPATA AMANI YA MOYO, LICHUNGUZE AU LIACHE KABISA.

#Mfano! Umeambiwa Kilimo cha Papai kinalipa sana mwaka huu 2019. Usiwahi tu kwenda kukopa kwa ndugu zako au mahali po pote pale na kuanza kulima. Unapaswa kufanya TAFITI ZA KINA JUU YA GHARAMA ZA Kuanzisha na kuendesha, Changamoto zake, Masoko Yake, Mauzo, n.k.


Kabla ya Kuanza biashara yako ya Kilimo;

1- Andika Maono Yako  ( Unaona nini juu ya hiyo biashara ndani ya mwaka Mmoja, miaka miwili, n.k. Na je Unataka Ikue kwa kiwango gani - Je ni kwa upana wa Kuihudumia tu Jamii Yako ya hapo karibu au kwenda na miji  na Mikoa mwingine?).

2- Andika Malengo yako.

3- Andika Mikakati Yako (Hatua kwa Hatua ya namna utakavyoitekeleza hiyo biashara Kila Siku. Mfano ni Lazima uweke Wazi ni kwa namna gani Utasafirisha Mazao yako kutoka Shambani Ikiwa Wateja watataka uwapelekee. N.k).

Na vivyo hivyo kwa biashara zingine Utakazohusishwa au utakazoanzisha wewe Mwenyewe.

UNAJUA MAISHA NI FURSA. BILA FURSA NI NGUMU SANA KUKUA KIMAISHA. Na tunapoongelea FURSA, HATUGUSII TU KWENYE BIASHARA. Hata kwako Wewe unayetaka kuwa Mwandishi mkubwa, mwibaji, Mchoraji, Mwinjilisti, Mwalimu wa Neno la MUNGU, Mchezaji, Mchekeshaji, Msusi, n.k.

KILA MTU ANASTAWI KUPITIA FURSA Hata Wale waliyoolewa ni kwamba walijua namna ya Kuidaka hiyo Fursa na kuifanyia kazi moja kwa moja.

SASA, FURSA ZIPO KILA MAHALI DUNIANI. Hapo Ulipo zipo nyingi sana Ila huzioni, hapa nilipo zipo pia.

- Haijalishi uko Tanzania au Ulaya, "Fursa zipo po pote pale. Tofauti ipo kwenye kuziona, na kuzifanyia Kazi."

#Mwenye HEKIMA Mmoja aliwahi Kusema ya kwamba,
"AN OPPORTUNITY KNOCKS ONLY ONCE. THE NEXT ONE MAY BE BETTER OR WORSE, BUT NEVER THE SAME ONE. THAT'S WHY IT'S SO CRUCIAL TO MAKE RIGHT DECISION AT THE RIGHT TIME - BECAUSE A RIGHT DECISION AT THE WRONG TIME BECOMES A WRONG DECISION."

Naamini Kuna Jambo Zuri sana ulilojifunza hapa, basi Litendee Kazi kwa Bidii. Na kama Wahitaji Vitabu vya Lackson Tungaraza bofya hii LINK ya WhatsApp: https://wa.me/255764793105 .

By Lackson Tungaraza.
AMUA LEO KUWA WA TOFAUTI.


0 comments:

Post a Comment

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI