Monday, October 22, 2018


▪Zipo Siri nyingi sana za Mafanikio zilizokuwepo, zilizopo, na zitakazoendelea Kuwepo Siku zote maadam Watu Wanaendeleo kufanya Tafiti na kufanikiwĂ .

▪Kufanikiwa Kimaisha hakukuhitaji Kujua kwanza Siri zote za Mafanikio Duniani kwa Sababu hazitawahi kuisha. Cha Muhimu sana ni kuanza kutendea Kazi zìle Siri Kadhaa ambazo Umekwisha kuzifahamu Wakati unaendelea Kujifunza na kufundishwa Siri nyingine nyingi.

○ Pamoja na yayo yote, kuna Jambo la Msingi sana ambalo nawiwa kukujuza kwenye SIRI za MAFANIKIO;


(01) TUMIA AKILI ZAKO
IPASAVYO.



👉🏿 Watu Wengi sana katika Karne hii Wamekuwa Wavivu sana kwenye matumizi ya AKILI zao ipasavyo. Wenğine tangu walipòokoka wakaacha Kutumia Akili zao kwa kigezo cha Kuishi kwa Roho. Cha ajabu sana hata huyo Roho hawamtumii vilivyo.


... Google imeÄ·uwa Msaada wa Watu Wengi sana Siku hizi. Imekuwa mbadala wa matumizi ya Akili - badala ya Watu kutumia AKILI ipasavyo, wanatumia Google Ipasavyo. Siku hizi hata Kijana akiulizwa maana ya neno "Uzalendo au Kamusi" anaingia Kuuliza kwanza Google kwa Sababu Haamini akili zake na wala hazitumii ipasĂ vyo.

... "Tumeanza Sasa kuwa na Kizazi kinachojali sana kuchaji Kila Mara Simu zao kuliko Kuchaji Akili zao." - Lamax.


👉🏿Watu Wote unaowafahamu kwenye Ulingo wa mafanikio (akina Dewji, Bakresa, Mengi, Bill Gates, Donald Trump, Ronaldo, Messi, Samatta, n.k), Sio kwamba Walijaliwa Akili za Kipekee sana Wakati wa Uumbaji, Ila Wao hutumia AKILI zao ipasavyo kabla ya kufanya Jambo, na wakati wa kulifanya. Huku wasiofanikiwa wakiendelea kutumia sana "mihemuko na Hisia."


... Dunia nayo inawathamini sana wale wanaozitumia Akili zao Vyema, kuliko wale wanaotumia sana Nguvu za Mwilini. Ndio maana Watu wanaotumia sana Akili wanalipwa vizuri kuliko wanaotumia Nguvu. Nadhani Wewe ni shahidi Mwaminifu katika Hili. Hata shuleni, wanafunzi wanaotumia Akili zao vyema ndio wanaofaulu na kupata zawadi za pongezi.


... Mwenye hekima mmoja aliwahi kusema ya kwamba, “The world will only mind you when you Use your MIND.” Akiwa na maana ya kwamba, ‘Dunia itakuthamini tu pale utakapotumia Akili.’



Mcheza soka aitwaye Lionel  Messi ukimtazama kwa mwonekano wake wa nje ana mwili wa kawaida, hana mwili mkubwa sana na wala sio baunsa, lakini mambo anayoyafanya uwanjani ni makubwa sana – huwa anawatesa Wachezaji wa timu pinzani kwa sababu ya Utumiaji wake mkubwa sana wa Akili ipasavyo huku wenzake wakitumia nguvu ipasavyo na akili kidogo.

… Waisraeli walikaa Utumwani nchini Misri kwa zaidi ya miaka mia nne kwa sababu ya Uvivu wa kutumia Akili zao ipasavyo, wakaona ni afadhali kuishi kwa kutumia nguvu za mwili. Farao na wamisri wenzake hawakuwa na nguvu kubwa sana zaidi ya Waisraeli, ila waliamua kutumia akili zao ipasavyo kuwatawala wenye nguvu nyingi za mwilini. Na ndivyo ilivyo kwenye jamii yetu, wanaotumia Akili vizuri ndio wanaowaongoza wenye nguvu nyingi za mwilini, ndio wanaolindwa na Mabaunsa, n.k.


Mfalme Sulemani wakati anaandika kitabu chake cha Mithali, alinukuu na maneno ya Aguri mwana wa Yake kwenye sura ya thelathini ndani ya kitabu chake. Aguri alisema ya kwamba, ‘kuna VIUMBE VINNE VIDOGO SANA duniani, lakini VINA AKILI SANA: SISIMIZI: Wadudu wasio na Nguvu, lakini hujihifadhia Chakula wakati wa Kiangazi (Jambo ambalo Halifanywi na watu wengi wanaojiita Watu wazima); PELELE: Wanyama wasio na Uwezo, lakini hujitengenezea Makao Miambani; NZIGE: Hawana Mfalme, lakini wote huenda pamoja kwa Vikosi; MJUSI: Waweza kumshika mkononi, lakini huingia katika Ikulu.’

Ndugu msomaji umeona ambavyo unazidiwa na hao viumbe wane wadogo katika Matumizi ya Akili. Wewe mwenyewe Jichunguze hapo ulipo pamoja na yale unayoyafanya – ikiwa unatumia Akili zako ipasavyo au unaishi tu kwa Mazoea, Mihemuko ya mwili, pamoja na Hisia.


Yapo mambo mengi sana ya kuchambua katika hiki kipengele cha kutumia vyema Akili zako – ikiwa ni pamoja na Namna ya kuamsha akili iliyolala ndani yako, namna ya kutumia akili zako ipasavyo kiuchumi na kimaisha. KARIBU SANA KWENYE SEMINA YA LACKSON TUNGARAZA ya SIKU KUMI (kuanzia terehe 01 Oktoba hadi terehe 10 Oktoba, 2018,) ITAKAYOKUSAIDIA KIUCHUMI NA KIMAISHA KWA UJUMLA. Yapo mambo makubwa sana Unayoweza kuyafanya maishani bila kutumia Nguvu nyingi sana za Mwilini kama watu wanaopasua Miamba kwa mikono.  





Fungua hii Link kwa kubofya haya maandishi yenye rangi ya bluu ili upate kujua hiyo semina ya siku 10 kwa Undani zaidi – Zimebaki siku chache Semina kuanza:


Kwa Mawasiliano ya Simu: 0764-793105 (Ipo pia WhatsApp)
#LamaxDesigns #LamaxQuotes #NewLifeChapter
“LIVING FOR MANY”

SOMA PIA HAPA: DUNIA NI UWANJA WA MAPAMBANO




1 comment:

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI