Tuesday, October 25, 2016

Ukubali, Ukatae.. Ukweli unabaki pale pale ya kwamba DUNIA NI UWANJA WA MAPAMBANO.

Karibu tupeane Maarifa kidogo hapa, Kujifunza Kitu Kipya Kila Mara ni sifa kubwa ya watu wenye Mafanikio Makubwa maishani.
-Binafsi napenda kujifunza sana Mambo mapya kila Mara.
💡Lackson Tungaraza💡

-Dunia ni Uwanja wa Mapambano kwa sababu Kila jambo unalohitaji kulipata linakuhitaji Kulitafuta kwa kila Namna, liwe dogo ama kubwa bado litahitaji kiwango cha Uhitaji wako ili Kulipata.

-Ikiwa Dunia ni Uwanja wa Mapambano, basi inabidi Kuwa na Silaha nzuri katika Vita.
-Tutakushangaa sana Unakuja na Fimbo/Rungu kwenye Uwanja huu wa vita ikiwa wenzako wanatumia Risasi na Mabomu.
-Na kama unahitaji hilo Rungu lako kummaliza mwenye risasi, itakulazimu Kumwinda akiwa amezubaa au kajisahau.

Silaha hizi siyo za Kumwaga damu. Ninachomaanisha ni MTAJI WAKO. Kitu au Njia unayotumia Kufikia Malengo au Hatma ya Maisha Yako.
-Najua unatamani sana Kufikia hatua kubwa ya Mafanikio katika Maisha yako. Lakini je! Ni silaha ya aina gani uliyoingia nayo katika Uwanja wa Mapambano.

-Wote kwenye Mtaa wako wana maduka ya Kuuza vyakula na bidhaa za Majumbani, wote ni Wanafunzi wa Kozi moja, wote ni wakulima wa mazao, wote ni Waandishi wa blog na Vitabu nk.
-Katika hali kama hiyo, ni Silaha gani unazotumia ili kutoka katika Uwanja huu wa mapambano ukiwa Mshindi? Amua kutumia silaha nzuri na zenye nguvu zaidi.

     🔫 Silaha hiyo yaweza kuwa Ni Kipaji, Kipawa, Ufundi, Ujuzi, Ujanja, Elimu, Maarifa nk.
-Namna utakavyoitumia hiyo Silaha, itaashiria kama Utashinda Mapambano au la.
-Silaha bila Makali au Kujua Kuitumia, bado hautakuwa Mshindi mzuri. Soma Vitabu mbali mbali kulingana na Vita unayopigana, Jifunze kwa waliofanikiwa, Andika katika *Diary au NoteBook* mambo mapya unayojifunza kila wakati.
Akina Bill Gates, Erick Shigongo, Mwl Mwakasege nk.. Wamefika hapo baada ya Kutambua aina ya vita wanayopigana na aina ya silaha ya Kupambania.

    *Don't hunt Something that you cannot Kill*
-Pambana na jambo ambalo Unauwezo wa Kulishinda kulingana na aina ya Silaha na Pambano ulilonalo.
-Mimi nishatambua aina ya Vita ninayopigana na nimeshachagua Silaha za Kupambania ili nimalize salama nikiwa Mshindi, maana *DUNIA NI UWANJA WA MAPAMBANO*

KUMBUKA! Bahati NA Wakati (0pportunity and Time) Kila mtu Kapewa na Mungu.
-Itategemeana tu na USHAPU Wako.
-Mfalme Sulemani anatuambia hapa jambo hilo lenye Faraja kwa màskini na Matajiri pia

   🔦 Mhubiri 9:10-11🔦

[10]Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.

[11]Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini *wakati na bahati huwapata wote*.💡

-Kwahiyo kuwa Mjanja kila unapoingia katika Mapambano ambayo yapo hapa duniani.
-Pigana sana, utapumzika Ukifika mbinguni baada ya Kupambana vyema na Kutetea Imani ya kweli ambayo Mungu kaiweka ndani yako kwa njia ya Wokovu

Salamu zangu Kutoka kwake Yeye aliyeñiwezesha Kuziandika
Lackson Tungaraza
HAKUNA KURUDI NYUMBA, HADI KIELEWEKE


#MPAMBANÀJI_ATUMAINIYE_KATIKA_UWEZA_WA_BWANA YESU.
Lackson Tungarazà


 (SUBSCRIBE Kwenye Channel yàngu ya YouTube).




Kuwa Rafiki yangu Facebook, tumia;
- www.facebook.com/ltungaraza

💣KIMENUKISWA!!!

0 comments:

Post a Comment

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI