Saturday, August 20, 2016


Karibu sana rafiki yangu mpendwa katika mfululizo wa masomo yangu kwa njia ya mtandao. Wakati uliyopita, nilifundisha juu ya MTAJI KWA KIJANA NI UPI!! Maana neno MTAJI limekuwa maarufu sana kwetu vijana hasa katika karne hii ya sayansi na teknolojia/taarifa tofauti na karne ile ya viwanda [industrial age]. Kama ulipitia somo hilo, nadhani utakuwa umepata jambo zuri sana la kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi… Kama bado, soma hapa kwa kubofya maandishi haya: MTAJI KWA KIJANA NI UPI!!

Leo tujifunze jambo jingine jipya ambao kwa nafasi yake litatusaidia kuwa makini zaidi kuelekea katika maisha ya mafanikio, ambayo tunayaona katika fikra kila tulalapo na tuamkapo. Karibu sasa, tuwe pamoja.

Ubunifu, Kipaji, Karama au Uwezo uliyopo ndani yako huwa unaonekana zaidi unapokuwa karibu na watu wengi[kwa kuongeza watu] au unapokuwa mwenyewe[unapokuwa faragha]? Jiulize, Jijibu. Hii itakusaidia sana katika safari yako ya kuifikia Ndoto iliyoko ndani yako ambayo Mungu kakupatia.
Kuna watu ambao hadi sasa hawajaona Vipaji vyao vikiwaletea manufaa kwa sababu hawajajichunguza, hawajajitathmini na kujitambua. Self-Discovery is the foundation, it comes first and others follow.


Ukiona ya kwamba Ideas[mawazo] ya kufanya mambo makubwa zinakuja ukiwa karibu na watu wengi kila mara, endelea kufanya hivyo na uwe makini usipitwe. Ikiwa ni ukiwa mwenyewe chumbani kwako au sehemu umepumzika, tia bidii katika Kujitenga na marafiki/watu ambao wanakupotezea muda mwingi na utumie muda huo kuandika hizo ideas punde zinapokuja ndani yako… Sir. Isack Newton aligundua ‘gravitational force’ alipokuwa amepumzika chini ya mti, WEWE JE?

Mara nyingi nimekuwa nikipata masomo mbali mbali ya kufundisha hapa pamoja na kuwa mbunifu katika mambo mbali mbali ninapokuwa faragha. Blog yangu hii {www.lacksontungaraza.blogspot.com} pamoja na ile nyingine {jesusisalive2016.wordpress.com} nilizitengeneza wakati nilipokuwa faragha, sikuweza kufanya hivyo nilipokuwa na watu wengi. Design nyingi nimezifanya nikiwa peke yangu, tofauti na pale ninapokuwa karibu na watu mbali mbali.

Nawe pia jitathmini vyema ili ujue ni eneo gani unatakiwa kuliwekea nguvu na umakini mkubwa zaidi. Isiwe kwamba Mungu anataka kukupa maarifa na ubunifu ukiwa peke yako, halafu wewe huo muda ndiyo unautumia kutafuta watu wa kuchati nao mtandaoni au unaenda kwa jirani kutafuta wa kupiga nae soga.

Kwa leo naomba kuishia hapa, tutaendelea na somo hili wakati mwingine kama Mungu atakavyotujalia Uzima na afya. Kama unambinu nyingine nzuri na unapenda jamii ifahamu, toa maoni yako hapa {Comment}. Unaweza pia kunipata katika maeneo yafuatayo kwa ukaribu;

Twitter: @lacksonthecoach
Instagram: LACKSONTUNGARAZA
WhatsApp/sms: 0764793105
TWENTY YEARS TO COME BEGINS TODAY, MAKE EVERY MINUTE COUNTABLE. WASTE NOT YOUR TIME





Related Posts:

  • UJASIRIAMALI NI NINI? Kuna tafsiri mbali mbali katika vichwa vya watu na katika mitandao ya kijamii juu ya dhana ya UJASIRIAMALI. Wengi wamepata tafsiri zilizowapa presha na kuamua kuacha kuwa WAJASIRIAMALI, na baadhi hawatambua ni kwa namna gan… Read More
  • JINSI YA KUWEKA MALENGO NA NAMNA YA KUFANIKISHA MALENGO YAKO  By Lackson Tungaraza 0764793105 whatsapp. Habari yako rafiki yangu mpendwa? Baada ya kuwa tumejifunza mada mbalimbali za ukombozi wa fikra na mafanikio ya kiuchumi. Napenda kukushukuru kwa ufuatiliaji wako katik… Read More
  • MAONGEZI YENYE MAANA NI YAPI HAYO... Tungaraza na Kijana Joseph katika Mjadala. Kila mara watu tunajikuta tupo au tunaingia wenyewe katika Mazungumzo, na hayo mazungumzo yanaweza yakawa yenye kuleta Matokeo chanya au hasi. Hivyo uhalali wa matokeo ya mazungumzo unategemeana na wahusika binafsi. Leo… Read More
  • MAISHA NI SAFARI NDEFU, UMEFIKA WAPI? Kuna siku niliandika hapa juu ya mada inayoitwa LIFE IS A PROCESS… Katika hiyo mada nilitoa mfano wa Mti ambao huanza kama mche baada ya mbegu kuwekwa ardhini. Hakuna mti ambao umetokea tu kuwepo hapo ulipo, ulianzia katik… Read More
  • UKWELI JUU YA SEMINA ZA MTANDAONI Natumaini wewe ni mzima wa afya na unaendelea vizuri na shughuli zako za kila siku. Ni jambo jema sana la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukupatia siku nyingine tena ukiwa na nguvu tele, una ndugu, una marafiki wazuri, umekul… Read More

1 comment:

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI