Saturday, September 22, 2018

Mwenye hekima mmoja alisema ya kwamba,
 “sababu ya msingi inayowafanya watu wafeli kwenye maisha ni kutoweka Mipango mipya ya kuwaondoa kwenye Mipango ile ya awali iliyowakwamisha.”

Naamini kuna mipango kadhaa uliyopanga kuitekeleza mwaka uliyopita na ndani ya mwaka huu, lakini hadi sasa bado hujafanikisha hata robo yake. Kuendelea kulalamika ni kuendelea kujichimbia shimo la mateso na majonzi yasiyokwisha. Kuanguka chini kunaweza kuwa ni kwa bahati mbaya, lakini suala la kuamka na kusonga mbele liko mikononi mwako  - unapaswa kusimama, kukung’uta mavumbi na kuendelea na safari yako.  Ikiwa na maana ya kurekebisha hatua zako na kiwango chako cha umakini ili usianguke kwa mara nyingine tena, mtaani wanasema ni aibu kubwa sana kwa mtu mzima kuanguka chini na kulia.

Sisi kama rafiki zako, tumekuandalia semina nzuri sana ya siku 10, ambayo kwa hakika itakuinua mahali ulipoanguka, itakufuta vumbi, na kisha kukuongoza safarini mwako ili usianguke tena hata ukijikwaa kwa njia nyingine.


Semina hiyo itaanza rasmi tarehe 1/11/2018 na kumalizika tarehe 10/11/2018.
Nayo itakuwa inafanywa kwa njia ya mtandao wa WhatsApp.




Semina itakuwa na Mada kuu mbili;




1. MITAJI zaidi ya 30 Unayopaswa kuwa nayo ili Uweze kufanikiwa Kimaisha.


-          Watu wengi wakiulizwa sababu ya kutokufanikiwa kiuchumi na kimaisha, wanasema ni kwa sababu ya KUKOSA MTAJI, na Mtaji wanaoutazamia ni PESA nyingi.

-          Kupitia hii Semina utaifahamu Mitaji zaidi ya 30, huku PESA kama MTAJI ikiwa Mwishoni kabisa. Utaona ni kwa namna gani ambavyo PESA SIO KILA KITU katika ulimwengu wa sasa licha ya kuwa na manufaa  mengi sana kama ya kulipia Ada za shuleni na vyuoni, kununua mavazi na magari, n.k


-          Karibu sana, utaenjoy kwa kweli.


2. Mambo unayopaswa kujua kuhusiana na FURSA, hasa wakati huu ambao zinakuja Fursa za kila aina.


-          Kila siku huwa unapata taarifa redioni na mitandani za uwepo wa fursa mpya mjini ambayo inalipa sana na kutajirisha ndani ya muda mfupi sana bila kufanya kazi za kutoka jasho. Inawezekana ni ya Kilimo cha Matikiti, ufugaji wa kware, kilimo cha Mbao, biashara ya mtandao (Network Marketing), Kubeti, Uuzaji wa Sarafu mtandaoni, n.k

-          Kupitia hii semina utajua ukweli uliopo nyuma ya hizo Fursa, namna ya kutambua Fursa za kweli na za uongo, namna ya kujitengenezea fursa binafsi, hatua za kufuata kabla ya kujiunga kwenye mlolongo wa Fursa mpya, na mengine mengi.


Atakayekufundisha hatua kwa hatua ndani ya hiyo Semina ya siku 10 ni LACKSON TUNGARAZA ambaye Wasifu wake upo kwenye Ujasiriamali, Uandishi wa vitabu kadhaa ikiwa ni pamoja ni vile vya “MWANACHUO DIARY” na “SITARUDI NYUMA TENA”, Mwanzilishi wa Lamax Quotes na Lamax Designs; Injinia wa mifumo ya kompyuta kutoka Chuo kikuu cha Dodoma, ndaki ya Teknolojia na Elimu Angavu (CIVE). Na pia Mwelimishaji wa Masuala ya kijamii kwa vijana kupitia njia za ana kwa ana, redioni, vitabuni, na Mitandaoni. Kwa hiyo, ni Mtu Mzoefu anayejua anachokifanya kwenye jamii.



Gharama za Semina nzima kwa siku zote kumi ni shilingi elfu ishirini za kitanzania (20,000) tu.

“Tarehe 17 hadi 24 Novemba utalipia Tsh. 15,000/= tu kama OFA kwako. Baada ya hapo (Tarehe 25 hadi 31) utalipia
Tsh. 20,000/= ikiwa Utachelewa kujisajili katika kipindi cha Ofa.”





DIRISHA LA USAJILI LIMEFUNGULIWA RASMI terehe 17/10/2018,
 kwa hiyo Hujachelewa kabisa.


Jisajili leo kwa namba za Simu 0764-793105 (M-PESA).
Utaona Jina la “Lackson Tungaraza”

Ukishatuma Pesa yako ya Usajili kwenye hiyo namba ya simu ya 0764-793105, tuma na Jina lako kamili kwa ujumbe wa SMS (Meseji) za kawaida au kwa njia ya WhatsApp kwa ajili ya Uthibitisho.


NAFASI YAKO IPO, KARIBU SANA.
KWA SWALI LOLOTE LILE; tumia hiyo hiyo namba ya simu, au email ya lacksontungaraza@gmail.com


0 comments:

Post a Comment

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI