Tuesday, October 25, 2016

*Mwuaji wa Kimya Kimya*

Hahahaa... Nakumbuka wakati nilipokuwa nikitazama Movie za Kivietnam. Komando mmoja anatumwa kwenda kuokoa watu zaidi ya Kumi waliochukuliwa mateka huko Vietnam.
Katika harakati zake za kuingia katika kambi ya adui, anakuwa SILENT KILLER...Anaua Kimya kimya. Anafanya mambo yake kimya kimya hadi anawakomboa watu waliokuwa mateka.
-Baadae ndipo wanashtuka na kushindwa kuwakamata tena.

Inawezekana kabisa kila Unaloshirikisha watu Kulifanya, wanakukatisha Tamaa na hamna anayeonesha dalili ya kukutia Moyo au kuwa sambamba nawe.
-Be a silent Killer.
💭Lackson Tungaraza💭

-Katika hali kama hyo, ninakushauri Leo ya kwamba anza Kufanya Kimya kimya, waone tu jambo lishafanywa.
-Dunia imefika mbali sana na Chuki, Wivu na Uhasama umekuwa Mkubwa kiasi cha kukosekana watu wengi wa Kuwainua wengine.

Henry Ford aliwahi Kusema, *MY BEST FRIEND IS THE ONE WHO BRINGS OUT THE BEST IN ME*
-Fanya, Waone Matokeo
-Kuuliza Uliza watu na Kutangaza-tanga ovyo ndiko kumekufanya hadi sasa haujafika mbali. Maana wengi wao wamekuwa Mizigo na Kipingamizi kwako.

-Actions speak Louder than Words. Matendo yanaongea zaidi ya maneno. Be a Silent Killer.
-Fungua Biashara, Soma hyo Kozi, Fanya jambo hilo na waone matokeo baada ya Kufanya kwako ikiwa wanaokuzunguka wanakukatisha tu tamaa.

SOMA: NJIA ZA KUJENGA KUJIAMINI NDANI YAKO

*Jifunze kwa Huyu Mwanamke

*Luka 8:43-44*

[43]Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, *[aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga]* asipate kuponywa na mtu ye yote,
[44] *alikwenda nyuma yake*, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma.

-Alichukua Maamuzi Binafsi, baadae ndipo wakaona matokeo.
-Angeendelea kusubiri watu wa Kumtia moyo kwanza na kumsindikiza, asingefanikisha kuponywa. Alikwenda Nyuma Ya Yesu yeye Mwenyewe.

STAY AWAY FROM SUCCESS STEALERS
-Kuna watu ni Wezi wa Mafanikio ya wenzao. Hawataki watu wafanikiwe hata Siku moja-Ni Wachawi
-Kuna wakati Utakimbiwa hata na wale uliyokuwa nao. Wakaondoka wote, au wakabaki wachache. Songa mbele, Fanya zaidi.
-Kuna mwingne pia hapa aliyekimbiwa na Watu lakini alisonga mbele bila Kukata tamaa...

*Yohana 6:66-68*

[66]Kwa ajili ya hayo *wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena.*
[67]Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, *Je! Ninyi nanyi mwataka kuondoka?*
[68]Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.

-Mafanikio yanategemea na wewe binafsi ulivyo na Unavyochukulia mambo.
-Anza kufanya, Usisubiri Kutiwa Moyo. Watakuja ukishafanya

    I chose to be a Silent Killer, what of You?
Uwe na wakati mwema
Salamu zangu kwako kutoka kwake yeye aliyeniwezesha Kuandika.

Lackson Tungaraza
FANYA SASA. USISUBIRI BAADAE


       📞0764793105
       -WhatsApp/Call
👂Lackson Tungarazà
        "Welcome Again"

http://lacksontungaraza.blogspot.com
www.youtube.com/c/LacksonTungaraza (SUBSCRIBE Kwenye channel yangu ya YouTube)

Related Posts:

  • WHY ONLINE SEMINARS? UKWELI JUU YA SEMINA ZA MTANDAONI Natumaini wewe ni mzima wa afya na unaendelea vizuri na shughuli zako za kila siku. Ni jambo jema sana la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukupatia siku nyingine tena ukiwa na nguvu tel… Read More
  • MTAJI KWA KIJANA NI UPI...! Proudly Sponsored by N.Y.I MOVEMENT *Join and Be part of the Change*. Kuna mambo mbali mbali ambayo wewe kama Kijana mwenzangu unaweza fanya pasipokuwa na pesa kubwa Bali hiyo hiyo uliyonayo hapo .... Akili, maarifa… Read More
  • NJIA ZA KUJENGA KUJIAMINI NDANI YAKO KUJIAMINI Ni uwezo wa kuwa na uthubutu juu ya mambo pasipo kuwa na hofu wala uwoga, wala kutegemea msukumo kutoka kwa ndugu, jamaa au rafiki. Kujiamini kunaweza kujengeka ndani ya mtu kwa: Uwamuzi Binafsi. Nadhani … Read More
  • MAISHA NI SAFARI NDEFU, UMEFIKA WAPI? Kuna siku niliandika hapa juu ya mada inayoitwa LIFE IS A PROCESS… Katika hiyo mada nilitoa mfano wa Mti ambao huanza kama mche baada ya mbegu kuwekwa ardhini. Hakuna mti ambao umetokea tu kuwepo hapo ulipo, ulianzia katik… Read More
  • MAMBO MATATU MUHIMU YA KUFANYA KIJANA KABLA YA KUANZA KUTAFUTA PESA YA KUFANYA BIASHARA Kijana mwenzangu kabla hujaanza kusumbuka kutafuta pesa kila mahala kwaajili ya biashara.  Kwanza Fanya maamuzi ni biashara gani unayohitaji kufanya, hiyo ni hatua ya kwanza kabisa. Kwanini ufanye uwamuzi kwanza? Ili k… Read More

0 comments:

Post a Comment

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI