UKWELI
JUU YA SEMINA ZA MTANDAONI
Natumaini wewe ni mzima
wa afya na unaendelea vizuri na shughuli zako za kila siku. Ni jambo jema sana
la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukupatia siku nyingine tena ukiwa na nguvu
tele, una ndugu, una marafiki wazuri, umekula umeshiba, shughuli zako za kila
siku zinafanikiwa, familia yako inaamani n.k.
Kumekuwa na mitazamo
tofauti tofauti katika jamii kuhusiana na Semina zinazotolewa Mitandaoni; kwa
njia ya Telegram, Wasap, Facebook n.k. Wengi wakiona tu tangazo linalotaarifu
umma juu ya kuwepo kwa Semina fulani kupitia Whatsapp au Telegram, kichefuchefu
kinawaingia na mara hiyo wanaondoka mitandaoni…ni nini tatizo!! Wengine wameshachukulia
kama ni Utapeli mtupu, semina gani inayofanyikia mtandaoni tena kwenye
Whatsapp? Tena, ingawa hiyo Semina inagusa moja kwa moja tatizo linalomsumbua
lakini hawezi kuchukua hatua ya kufuatilia au kulipia gharama zilizowekwa ili
kupata semina hiyo kwasababu Akilini mwake ameshaamini ya kwamba ni Utapeli.
Hii ni karne ya kisasa
yenye maendeleo ya sayansi na teknolojia, majukumu yamekuwa ni mengi sana na
watu wako bize. Wanandoa nao wako bize wakitafuta fedha ili familia isonge
mbele, watu wanawahi kuamka asubuhi kuwahi katika shughuli zao na kuchelewa
kurudi majumbani mwao, njiani pia foleni ya kutosha kwa wale waliopo kwenye
miji mikubwa kama Dar, Mwanza, Arusha na hivyo kufika nyumbani wakiwa wamechoka
sana na kupitiliza kulala, siku ya wikendi nayo mtu anapenda awe japo karibu na
familia yake au atembelee miradi yake mbalimbali. Muda wa kuhudhuria kwenye
Ukumbi wa Semina, anaupata wapi? Muda wa kutoka mkoa mmoja hadi mkoa mwingine
ili akapate Semina labda ya Ndoa au biashara unapatikanaje? Hivyo ni baadhi tu ambao
wanaweza kupangilia mambo yao vizuri na wakaudhuria Semina kwa wakati. Sasa hao
wengine ambao hawapati muda wa kuhudhuria hizo Semina, elimu itawafikiaje?
Katika hali kama hiyo
ndipo Umuhimu wa Semina za Mitandaoni zinahitajika ili mtu aweze kupata elimu
stahiki kwa wakati sahihi bila kuathiri shughuli zake au muda wake wa kazi. Je!
Kuna faida gani za kuhudhuria hizo semina za Mitandaoni, mfano kupitia Whatsap?
Zifuatazo ni faida ambazo utazipata;
1.
Unapata
Elimu stahiki ukiwa popote pale (Elimu Kiganjani Mwako)
Elimu hiyo unaipata
ukiwa nyumbani, ofisini, kazini, safarini au sehemu yoyote ile ukiwa na simu
yako au kompyuta inayokubali Intaneti na kuwa na Wasap ndani yake. Karne hii ya
kisasa, mafunzo ya mtandaoni yameshika kasi sana kwa kiasi kikubwa. Kuna vyuo
mbalimbali vinatoa mafunzo mtandaoni na kumwezesha mtu kupata Stashahada,
Shahada, au Masters. Hii itakusaidia kupata masomo kwa uhuru, kwa wakati ambao
uko free na sehemu yoyote ile uliyopo bila usumbufu wowote. Unaweza ukatoka ofisini
kwako na ukachukua Simu au Kompyuta yako na kuanza kujifunza wakati umepumzika
au wakati unakula bila kuathiri muda wako wa kazi.
Miaka ya sasa watu
wamekuwa bize sana katika kutafuta maisha bora kutokana na kupanda kwa gharama
za maisha, na hivyo inakuwa vigumu kwa watu kuacha shughuli zao na kwenda
kwenye ukumbi fulani kuhudhuria Semina kutokana na ufinyu wa muda walionao.
Kupitia Semina za mitandaoni, unapata Elimu stahiki kiganjani mwako kama elimu ya
biashara na Ndoa mahali popote pale ulipo pasipo kuathiri shughuli zako.
2.
Gharama
Nafuu~Low Cost
Badala ya kwenda sehemu
na kukaa katika nyumba za wageni (guest house) au kusafiri kutoka sehemu moja
kwenda nyingine kwa gharama kubwa, unaweza kupata hii Semina hapo hapo nyumbani
kwako kwa kutozwa kiwango kidogo cha fedha. Ni wewe tu kuwa na Simu au Kompyuta
inayokubali intaneti
3.
Unaokoa
Muda~Saving Time
Badala ya kusafiri na
kutumia muda mwingi njiani, kwenda na kurudi. Lakini pia kuacha shughuli zako
za siku na kwenda kwenye kumbi mbalimbali za Semina, sasa utaokoa muda wako kwa
kupitia Online Seminars na ukawa unaendelea na kazi yako ya Ualimu, Udaktari,
Ujasiriamali n.k.
“TIME IS MONEY, HOW DO YOU INVEST YOUR TIME?”
Karibu sasa katika
Semina yangu itakayoanza tarehe 21/3/2016, naamini ya kwamba hautojutia kabisa.
Kuna mambo mengi sana utajifunza kupitia Simu au Kompyuta yako ukiwa hapo hapo
kazini, safarini au nyumbani bila kuathiri shughuli zako. Jiandikishe sasa mapema, kwa Ushauri na Maswali binafsi nipo Wasap kwa
nambari 0764793105. Tangazo hili limeelezea vizuri;
0 comments:
Post a Comment