Natumaini wewe ni mzima
wa afya na unaendelea vizuri na shughuli zako za kila siku. Ni jambo jema sana
la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukupatia siku nyingine tena ukiwa na nguvu
tele, una ndugu, una marafiki wazuri, umekula umeshiba, shughuli zako za kila
siku zinafanikiwa, familia yako inaamani n.k.
Kumekuwa na mitazamo
tofauti tofauti katika jamii kuhusiana na Semina zinazotolewa Mitandaoni; kwa
njia ya Telegram, Wasap, Facebook n.k. Wengi wakiona tu tangazo linalotaarifu
umma juu ya kuwepo kwa Semina fulani kupitia Whatsapp au Telegram, kichefuchefu
kinawaingia na mara hiyo wanaondoka mitandaoni…ni nini tatizo!! Wengine
wameshachukulia kama ni Utapeli mtupu, semina gani inayofanyikia mtandaoni tena
kwenye Whatsapp? Tena, ingawa hiyo Semina inagusa moja kwa moja tatizo
linalomsumbua lakini hawezi kuchukua hatua ya kufuatilia au kulipia gharama
zilizowekwa ili kupata semina hiyo kwasababu Akilini mwake ameshaamini ya
kwamba ni Utapeli.
Hii ni karne ya kisasa
yenye maendeleo ya sayansi na teknolojia, majukumu yamekuwa ni mengi sana na
watu wako bize. Wanandoa nao wako bize wakitafuta fedha ili familia isonge
mbele, watu wanawahi kuamka asubuhi kuwahi katika shughuli zao na kuchelewa
kurudi majumbani mwao, njiani pia foleni ya kutosha kwa wale waliopo kwenye
miji mikubwa kama Dar, Mwanza, Arusha na hivyo kufika nyumbani wakiwa wamechoka
sana na kupitiliza kulala, siku ya wikendi nayo mtu anapenda awe japo karibu na
familia yake au atembelee miradi yake mbalimbali. Muda wa kuhudhuria kwenye
Ukumbi wa Semina, anaupata wapi? Muda wa kutoka mkoa mmoja hadi mkoa mwingine
ili akapate Semina labda ya Ndoa au biashara unapatikanaje? Hivyo ni baadhi tu
ambao wanaweza kupangilia mambo yao vizuri na wakaudhuria Semina kwa wakati.
Sasa hao wengine ambao hawapati muda wa kuhudhuria hizo Semina, elimu
itawafikiaje?
Katika hali kama hiyo
ndipo Umuhimu wa Semina za Mitandaoni zinahitajika ili mtu aweze kupata elimu
stahiki kwa wakati sahihi bila kuathiri shughuli zake au muda wake wa kazi. Je!
Kuna faida gani za kuhudhuria hizo semina za Mitandaoni, mfano kupitia Whatsap?
Zifuatazo ni faida ambazo utazipata;
1.
Unapata
Elimu stahiki ukiwa popote pale (Elimu Kiganjani Mwako)
Elimu hiyo unaipata
ukiwa nyumbani, ofisini, kazini, safarini au sehemu yoyote ile ukiwa na simu
yako au kompyuta inayokubali Intaneti na kuwa na Wasap ndani yake. Karne hii ya
kisasa, mafunzo ya mtandaoni yameshika kasi sana kwa kiasi kikubwa. Kuna vyuo
mbalimbali vinatoa mafunzo mtandaoni na kumwezesha mtu kupata Stashahada,
Shahada, au Masters. Hii itakusaidia kupata masomo kwa uhuru, kwa wakati ambao
uko free na sehemu yoyote ile uliyopo bila usumbufu wowote. Unaweza ukatoka
ofisini kwako na ukachukua Simu au Kompyuta yako na kuanza kujifunza wakati
umepumzika au wakati unakula bila kuathiri muda wako wa kazi.
Miaka ya sasa watu
wamekuwa bize sana katika kutafuta maisha bora kutokana na kupanda kwa gharama
za maisha, na hivyo inakuwa vigumu kwa watu kuacha shughuli zao na kwenda
kwenye ukumbi fulani kuhudhuria Semina kutokana na ufinyu wa muda walionao.
Kupitia Semina za mitandaoni, unapata Elimu stahiki kiganjani mwako kama elimu
ya biashara na Ndoa mahali popote pale ulipo pasipo kuathiri shughuli zako.
2.
Gharama
Nafuu~Low Cost
Badala ya kwenda sehemu
na kukaa katika nyumba za wageni (guest house) au kusafiri kutoka sehemu moja
kwenda nyingine kwa gharama kubwa, unaweza kupata hii Semina hapo hapo nyumbani
kwako kwa kutozwa kiwango kidogo cha fedha. Ni wewe tu kuwa na Simu au Kompyuta
inayokubali intaneti
3.
Unaokoa
Muda~Saving Time
Badala ya kusafiri na
kutumia muda mwingi njiani, kwenda na kurudi. Lakini pia kuacha shughuli zako
za siku na kwenda kwenye kumbi mbalimbali za Semina, sasa utaokoa muda wako kwa
kupitia Online Seminars na ukawa unaendelea na kazi yako ya Ualimu, Udaktari,
Ujasiriamali n.k.
“TIME IS MONEY, HOW DO YOU INVEST YOUR TIME?”
Karibu sasa katika
Semina yangu itakayoanza tarehe 07/06/2016, naamini ya kwamba hautojutia
kabisa. Kuna mambo mengi sana utajifunza kupitia Simu au Kompyuta yako ukiwa hapo
hapo kazini, safarini au nyumbani bila kuathiri shughuli zako. Jiandikishe sasa mapema, kwa Ushauri na
Maswali binafsi tumia Wasap/sms kwa nambari 0764793105… Utapata elimu
stahiki katika maeneo yafuatayo kwa njia ya Whatsapp na Email;
1. Jinsi Ya Kufanikiwa Maishani ikiwa hauna mtaji.
Mtaji ni kilio kwa wengi nawe ukiwa mmoja wao.
Kwanini usichukue uwamuzi wa kuyaokoa maisha yako sasa ili upate kujua jinsi ya
kuwa na maisha bora na kuzifikia ndoto zako hata kama hauna Mtaji.
2. Jinsi Ya Kupata Wazo Bora la Biashara.
Najua unataka kuanzisha biashara ya kukuinua
kiuchumi katika viwango vikubwa lakini hujui ni biashara gani ufanye na kwa
njia zipi. Pia unamawazo mengi ya biashara lakini hauna Mtaji na pia hujui lipi
ulipe kupaumbele..Sogelea Semina sasa upate kujua
3. Umuhimu wa Maono Kwa Kijana.
Kijana mwenzangu acha kuishi maisha ya kubahatisha.
IT'S BETTER TO BE BORN BLIND THAN TO LIVE A LIFE WITHOUT VISION. Ni afadhali
ungezaliwa ukiwa kipofu wa macho kuliko kuishi pasipo kuwa na Maono. Maono yatakupa
nidhamu nini ufanye na nini usifanye na kwa wakati gani. Ni dira yako ya
maisha. Nikuulize, UNAJIONA UKO KATIKA MAISHA GANI BAADA YA MIAKA MITANO?
Karibu sasa katika Semina hii ujue zaidi juu Ya Maono kwa kijana
4. Jinsi Ya Kuongeza Mauzo katika Biashara Yako
Mbinu utakazozipata hapa ni nzuri na kwa uhakika
zitakusaidia sana..nimekuwa nikizitumia sehemu mbalmbal hata katika mitandao ya
kijamii na zmezaa matunda. Usiwe mnyonge kwa sababu biashara yako haina faida
ya kutosha, ni siri tu Fulani ambazo hujazipata...karibu sana uchote Maarifa
5. Kutengeneza Kipato cha ziada ukiwa kazini kwako
Hivi unatambua ya kwamba unaweza ukawa unaendesha
biashara yako ukiwa hapo hapo kazini? Hamna ya kusubiri hadi upewe likizo au
hadi wikendi Ifike...kupitia simu yako, kompyuta yako, mazingira yako ya kazi
sasa unakwenda kutengeneza mfereji wa pesa
...usikae maskini kwa sababu ya mshahara mdogo na
unatumia nguvu kubwa.
Hata wewe mama wa nyumbani hii siri itakusaidia
kutengeneza pesa ukiwa hapo Hapo nyumbani kwako.
Jiandikishe mapema sasa kupitia Wasap kwa namba
niliyoitoa hapo juu..semina ni Tsh. 10,000/- tu bila senti. Utaituma kwa
nambari 0764793105[M-Pesa] na utaona jina langu Lackson Tungaraza. Ukishatuma
utanijulsha kwa Meseji maana wanaotuma ni wengi. Pia Utapata Kitabu cha
Biashara Bure.
CHOTA MAARIFA NA LACKSON TUNGARAZA.
www.lacksontungaraza.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment