Wednesday, March 16, 2016


SIRI INAYOVUTA MAFANIKIO
 Nitakuwa muongo sana kama nikisema ya kwamba hamna mtu anayependa Mafanikio, hata wewe umechukua muda wako kusoma makala hii kwa sababu unapenda kufanikiwa kupitia hii Siri Inayovuta Mafanikio. Je, Mafanikio ni nini? Mafanikio kwa tafsiri ya kawaida ni kutimiza Malengo uliyojiwekea; iwe ni kununua gari, kupata kazi mpya, kuanza biashara, kununua TV, kuwa kiongozi katika Nyanja fulani n.k. Je! Siri hii ya Mafanikio ni ipi?

Basi Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana na mambo yasiyoonekana”~Ebr 11:1. Ukitaka kufanikiwa katika jambo lolote maishani mwako, ishi maisha ya Imani (Live a life of faith). Natumaini ya kwamba unatamani sana kuwa Tajiri, kuwa Mfanyabiashara mkubwa, kuwa Mkulima wa kimataifa, kuwa Mwimbaji maarufu, kuwa T.O katika masomo yako shuleni, kuwa kiongozi mkuu katika taifa. Je, unafikiaje hayo Malengo yako? Mtaji huna, Umaarufu huna, Wadhamini hauna n.k.

Anza kuishi maisha hayo unayoyataka yatokee katika maisha yako. Ikiwa unataka kuwa Tajiri mkubwa hapa nchini na duniani, anza kuishi maisha kama ya matajiri..Matajiri wananidhamu katika muda, wanavaa mavazi ya heshima, wanapenda kuwafanikisha wanaowazunguka, wanakiu ya kufanikiwa zaidi na zaidi kila siku, changamoto wanazichukulia kama fursa ya kupata fedha na kuongeza Uzoefu katika mambo wayafanyayo, wanasoma vitabu vingi sana vya biashara kila mara, hawana muda wa kulalamika kwa yale waliyoyapoteza bali wanaangalia yaliyobaki na kuweka mikakati ili wasijewakapoteza tena.

~Ukitaka kuwa Mwanamuziki bora katika vipindi vyote, anza kuishi maisha ya Wanamuziki wakubwa..jinsi wanavyofanya mazoezi, wanavyoshirikiana na Wanamuziki wengine, vitabu na vyanzo mbali mbali vya taarifa wanavyotumia kupata maarifa zaidi ya Uanamuziki.

~Ukitaka kuwa Kiongozi katika sehemu yoyote ile katika maisha yako..serikalini, chuoni, taasisi za watu binafsi n.k. Ishi maisha ya Uongozi, huwezi kuwa Kiongozi ikiwa unaisha maisha ya kuongozwa (Mfuasi)..Vaa kama Kiongozi (dress like a leader), tembea kama Kiongozi (walk like a leader), ongea kama kiongozi (talk like a leader), anza kutengeneza wafuasi (start making followers). Vivyo hivyo na katika Nyanja zingine za maisha.

Ukianza kuishi maisha hayo, utavuta maisha unayoyataka kuja kwako. Maisha utakayoishi yatavuta yale mambo ambayo unayataka yatokee katika maisha yako.

~Tangu nilipoanza kutumia Siri hii, maisha yangu Lackson Tungaraza yalibadilika kabisa. Kwa sababu nilikuwa nataka kuwa Mjasiriamali mkubwa, hivyo nikaanza kuishi maisha ya Wajasiriamali wakubwa..vitabu wanavyosoma, muonekano wao wa nje na wa ndani, watu wanaoambatana nao. Baada ya hapo nikashangaa kuanza kuona nawavutia watu wengi kufanya kazi na mimi, wengine kwenda mbali zaidi na kuniita Mjasiriamali mkubwa n.k. Kwa sababu pia nilitaka kuwa Mwandishi katika Blog (Blogger), nilianza kuishi maisha ya ‘Bloggers’.. wanapenda kuikomboa jamii katika matatizo na utashi unaowasumbua katika maisha, wanafanya utafiti katika yale wanayoyaandika, kila mara wanaandika hata kama ni hadithi fupi.. baada ya hapo nikaanza kuwavuta waandishi wengine wa Blog katika maisha yangu na pia kuwa mahiri katika uandishi wa makala zinazovuta hisia za watu wengi.

TENDEA KAZI SIRI HII KUANZIA SASA.
~ Kama mimi Siri hii imenisaidia kufika hapa nilipo leo, naamini hata wewe itakusaidia sana ukianza kuweka katika matendo yale uliyojifunza hapa. Endelea kuwa karibu na mimi Facebook (www.facebook.com/ltungaraza), Instagram/YouTube (Lackson Tungaraza) ili uzidi kupata masomo zaidi ya uelimishaji.


ITAKUWA BORA ZAIDI IKIWA UTATOA MAONI YAKO HAPA (Comment) NA PIA KUSAMBAZA SOMO HILI KATIKA MAKUNDI MBALI MBALI (Share) ILI ELIMU HII IWAFIKIE WATU WENGINE NA KUKOMBOA FIKRA ZAO.

0764793105 Namba yangu. Nitafute kwa kupiga, meseji au wasap.




0 comments:

Post a Comment

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI