Saturday, August 6, 2016

Proudly Sponsored by
N.Y.I MOVEMENT
*Join and Be part of the Change*.


Kuna mambo mbali mbali ambayo wewe kama Kijana mwenzangu unaweza fanya pasipokuwa na pesa kubwa Bali hiyo hiyo uliyonayo hapo .... Akili, maarifa, elimu, ujuzi ni Mitaji pia.... Kwanini bado unalalamika ya kwamba maisha siyo mazuri? Badili sasa mtazamo wako, waliofanikiwa maishani ni watu waliyogundua ya kwamba Mtaji siyo pesa pekee Bali pia uwezo ambao Mungu kakuumbia ndani yako.

Watu kama akina Ronaldinho Gaucho, Barhesa siyo kwamba walikuwa na pesa nyingi pindi wanaanza safari ya kusaka life.. Waliamini ya kwamba kuna zaidi ya Pesa ndani yao. Ni sawa na kuacha migodi Ya dhahabu Tanzania na kwenda kutafuta dhahabu Somalia..
 Huo ni upuuzi. What's your talent, experience, profession, hobby? Then why do you complain about having a hard life? Be a critical Thinker....

Wewe ni zaidi ya Unavyojitazama... Unamadini ndani yako..... Mwandiko wako ni wa kipekee duniani, mboni ya macho yako ni ya kipekee, nyayo za miguu yako ni ya kipekee, alama za mikono yako ni ya kipekee... So what next? You have greatness within you... Use it.
Lackson Tungaraza
www.lacksontungaraza.blogspot.com

Nabii Musa kipindi amefika na wana wa Israeli katika kando ya bahari ya shamu... Watu walianza kumlilia Musa kwa kuwaleta kufa kifo cha aibu na pia Musa akaanza kumlilia Mungu atende jambo... Unajua Mungu alimwambiaje Musa?.... Usinililie, Chukua fimbo yako uinyooshe juu ya bahari... Aliponyoosha, bahari ikawa nchi kavu nao wakapita saa hiyo. Musa alikuwa na Mtaji wa kusogea mbele mkononi mwake lakini hakutambua.
MTAJI SIYO PESA TU, TUMIA UBONGO WAKO VYEMA KUFIKIRI VIZURI.

Mtaji unao hapo hapo ulipo... Siyo kila wakati wakitaja Mtaji unawaza tu pesa.... Ohhhooo nimemaliza chuo sijaanza biashara kwasababu sina mtaji.. Ohooo natamani kulima zao la pamba lakini Mtaji ni kikwazo...

Ni wakati wa akili za watanzania kufunguka na kuwa wazi..... Bado hujaelewa tu ?.... Iko hivi…
Kuna shughuli unaweza Fanya hata kama hauna pesa na ukatengeneza bomba la Pesa....

Unaweza kuwa Mshauri wa mambo ya biashara: Wewe  una uzoefu wa ujasiriamali au umiliki wa biashara? Unajua nini kinahitajika ili uanzishe biashara, kujenga biashara, kuongeza biashara na kukua? Sasa unaweza kuanza kazi ya ushauri wa biashara. Unaweza kusaidia kampuni au biashara mbalimbali kutoka chini ya uvungu na kwa kutoa ushauri na maelekezo muhimu. Unaweza kuwasaidia watu walioajiriwa kuanza kutoka kwenye ajira na kuingia kwenye ujasiriamali kwa malipo.

Hujaelewa tu!! amka wewe.

Related Posts:

  • SIRI AMBAZO MFANYA BIASHARA HUJAZIJUA  “JINSI YA KUFANYA BIASHARA YAKO KUWA YA TOFAUTI NA YENYE MVUTO MKUBWA”  Tunashindwa kuongeza vipato vyetu kwa sababu biashara zetu hazina mvuto. Tunapoendelea kufungua vyanzo vingine vya vipato kwa kut… Read More
  • HAKIKA, ANASTAHILI KUPEWA SIFA.Haikuwa jambo jepesi kuacha shughuli zake, Umaarufu wake, Ulinzi, Utajiri na kuja kututembelea huku kwetu. Sidhani kama wewe msomaji ungeweza kufanya hivyo. Yeye aliweza, pasipo manung'uniko wala hamu ya kutamani kurudi huk… Read More
  • BE A SILENT KILLER*Mwuaji wa Kimya Kimya* Hahahaa... Nakumbuka wakati nilipokuwa nikitazama Movie za Kivietnam. Komando mmoja anatumwa kwenda kuokoa watu zaidi ya Kumi waliochukuliwa mateka huko Vietnam. ⚜Katika harakati zake za kuingia ka… Read More
  • FACEBOOK VS BLOG KIPI NI BORA KWA BIASHARA YAKO? Kumekuwa na sitofahamu juu ya namna ya kutumia mitandao hii katika kukuza biashara. Ndiyo maana nimekuuliza; Kati ya Facebook na Blog, ni kipi bora kwa Biashara yako? Jibu lako litaash… Read More
  • WHAT DO YOU WANT TO BE REMEMBERED FOR?  Kwa kawaida kila mtu huwa anatamani na anapenda ya kwamba akitenda jambo, baadae Akumbukwe kwalo. Ikiwezekana hata watu kadhaa watoe shuhuda za jambo hilo. This a human character. Unataka kukumbukwa kwa lipi… Read More

2 comments:

  1. wewe kama Kijana mwenzangu, unawaza nini juu ya MTAJI? Toa maoni yako hapa

    ReplyDelete
  2. wewe kama Kijana mwenzangu, unawaza nini juu ya MTAJI? Toa maoni yako hapa

    ReplyDelete

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI