Tuesday, October 25, 2016

*Akasema, YOTE IMEKWISHA.
LIFE is PERFORMANCE. Na Mara unapoanza Kuperfom ndipo unaanza kutambua aina ya wasikilizaji na watazamaji ulionao. Aidha wako pamoja nawe, au la. That's how life is in this world.

Bahati Bukuku anasema SONGA MBELE.. UNAPOIANZA SAFARI wanakutia Moto, UNAPOONESHA MAFANIKIO wanainua Vikwazo. Unaanza kushangaa IMEKUWAJE TENA!!

We chunguza maisha ya wale waliokuwa pamoja nawe kabla ya safari; kabla ya kuanza biashara, kabla ya kukataa umaskini, kabla ya kupata mchumba/mke/mume, kabla ya kupata ajira/kazi, kabla ya kuanza kuonesha dalili za mabadiliko katika maisha yako. WAMEGEUKA UPANDE, WASITAKE KUKUTAZAMA TENA.

Hiyo ni hali ya kawaida kabisa. Upendo wa Kweli hujidhihirisha wakati kama huo...at the Period of transformation.
*Unashangaa ndugu, rafiki, jirani na jamaa hawana mahusiano mazuri tena na wewe.
*Kama walikuwa wanakupigia Simu, huoni tena, mchango wa harusi hawatoi,

*Wakisikia Umefukuzwa chuo, umefeli masomoni, umefukuzwa kazini, umepewa talaka... Wataanza eehee! Tulijua tu hafiki mbali. Mbio za sakafuni huishia Ukingoni. Kwani wangapi wameshindwa! Ye ndiyo uweze!! Limempata la Uso.
*Sahivi wako Kimya wanasubiri wakuone utafikia wapi katika biashara yako hiyo, Huduma au wito ulionao*
Usiogope, Usirudi Nyuma. DO THE PERFORMANCE.


*Hii pia ni sababu ya watu kuendelea kubaki katika hali ile ile ya maisha miaka yote. Mtu akifanikiwa anatengwa! Badala ya kuwekwa karibu na kujifunza kutoka kwake.
YOU WILL NEVER BE RICH UNTIL YOU LOVE THE RICH PEOPLE.
*Rich people are not Greedy to that extent. That's why they solve your daily life problems*

Mabadiliko yanahitaji Self-commitment. Kujitoa mzima mzima bila kujali makele ya watu wasiotaka mabadiliko ya wengne, wanataka kila MTU awe kama wao. KELELE ZA MBU HAZITOBOI NETI.
UTASHANGAA hata ndugu yako wa damu anakuchukia na hata kukupangia kukuua. Kivipi!! Tusome hapa

*Mwanzo 4:1-8*

[1]Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa BWANA.
[2]Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi.
[3]Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa BWANA.
[4]Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake;
[5]bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. *Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.*
[6]BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
[7] *Kama ukitenda vyema, hutapata kibali?* Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.
[8]Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]. Ikawa walipokuwapo uwandani, *Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua.*


CHUKI ni mbaya sana. Inaua kanisa, familia, taifa na dunia kwa ujumla. Umuhimu wake haupo.
Mungu anamwuliza Kaini, *KAMA UKITENDA VYEMA HUTAPATA KIBALI?*
Nawe jiulize swali hilo.

Nawe anza kufanya kazi kwa bidii, kuimba, kaoe/kaolewe, kasome Vitabu na kuhudhuria semina, kajifunze kwa Waliofanikiwa... Na UTAPATA KIBALI NAWE PIA.
CHUKI itakuua mapema, na Mbinguni hautaingia kwame hata kama unafanya kazi ya Mungu kwa kiwango gani.

*Yeye asemaye kwamba Yuko Nuruni, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa* #1 Yoh 2:9

Ubarikiwe sana, na jisemee kwa Kuapa..
*"IT'S NOT OVER UNTIL I WIN"
# I don't stop when I'm Tired, I stop when I'm done.


©Lackson Tungaraza
0764793105 whatsapp
Google plus: www.google.com/+LacksonTungaraza  

Site: http://lacksontungaraza.blogspot.com

Success at Door
#BORN TO MAKE A DIFFERENCE IN YOUR GENERATION

0 comments:

Post a Comment

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI