Yeye
aliweza, pasipo manung'uniko wala hamu ya kutamani kurudi huko alikotoka kwa
haraka. He was happy being with us
Na
huyo siyo mwingne, Bali ni Yesu Kristo.
*Najua
kuna majina ya watu wengne ambao umeamua kuwafuata ukiamini ya kwamba kwa
kufanya hivyo utamwona Mungu kwa uwepesi. WE ALWAYS FOLLOW PEOPLE DEPENDING ON
THEIR ABILITY TO SOLVE OUR PROBLEMS.
NDIYO!!
Huwa watu wanaamua kumfuata mtu fulani kulingana na uwezo aliyonao katika
kutatua Changamoto au Matatizo yao ya kila Mara. Na ndivyo ilivyokwako,
ukachagua kumwamini huyo unayemwamini ili umwone Mungu.
ANASTAHILI
SIFA HIZI. Kwa Upande wangu; Huyu Mwanaume Yesu alinivutia sana na kuamua
kumuamini kwa asilimia kubwa sana... His history made me Inspired.
‼Nitaongelea
jambo hili wakati mwingne.
Namshukuru
sana Mungu kwa kuniwezesha kuwepo tena Huu mwezi wa Kumi. Sidhani kama ni
mazoezi au vyakula nilivyokula. Ni Yeye tu.
Na kufika mwezi huu, inamaana ya kwamba
imebaki tu miezi miwili mwaka kuisha.
Fikiria
umefikisha Asilimia ngapi ya Yale uliyopanga kufanya ndani ya huu mwaka 2016.
Inawezekana hata moja hujafanya!!
Kipindi
Mwaka unaanza, nilisikia msukumo ndani yangu kwa kiwango kikubwa ya kwamba
Mwaka huu utakuwa *mwaka wa Mabadiliko* na nikaandika na kufundisha katika
mitandao ya kijamii.
Walioamini, watakuwa wameshaona
nilichomaanisha. Wale akina Tomaso, watakuwa bado wanasubiri kupapasa.
KUTOKUKATA TAMAA KUMENIFIKISHA MBALI SANA KIMAISHA. NAWE USIKATE TAMAA, NAFASI YAKO BADO IPO, MUNGU YU HAI KUKUSAIDIA KWA ASILIMIA MIA MOJA. |
Mungu
kanipitisha katika mambo makubwa na kunikutanisha na watu mbali mbali
walioniongezea thamani... Kwenye basi, hotelini, sokoni... Kote huko Mungu
aliwaleta. KUNA NGUVU KUBWA SANA KATIKA IMANI. Increase your Believing
percentage.
Na
hivyo ninapoelekea mwisho wa Mwaka huu, natazamia neno moja kama Mtume Paulo
alivyofanya;
*Wafilipi
3:12-13*
[12]
Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza
mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo
Yesu.
[13]
Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja
tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele;
Yes…
Nikiyasahau yaliyo ya nyuma (majonzi, hasara, usaliti, changamoto) na
kuyachuchumilia yaliyo mbele (Maono, mipango, malengo). HIYO NJOZI HAITASEMA
UONGO, IJAPOKAWIA INGOJEE
Nawe
pia sahau yaliyokuumiza tangu mwaka uanze, na utazamie Maono yaliyo ndani yako.
GOD ONLY PROMISES A SAFE DESTINATION, DESPITE OF A DANGEROUS JOURNEY
'WHEN
YOU LOSE, DONT LOSE THE LESSON.'-Lama.
Mark
Twain aliongezea kwa kusema,
*Twenty years from now you will be more disappointed
by the things you didn't do than by the ones you did*
Siri
kubwa ya kufeli katika maisha, Ni kujitahidi kumpendeza kila MTU. Ukubali,
ukatae ndivyo ilivyo.
‼Ukitakà
kumpendeza kila mtu badala ya kumpendeza Mungu na Kutimiza Kazi iliyowekwa
ndani yako na Mungu.. You are already a Failure.
Hivyo
niliamua kufuata Maono yaliyo ndani pasipokutazamia mazingira yanasemaje, au
watu wanawaza nini juu ya maisha Yangu kwa namna wanionavyo.
Hata
Yesu walimuoana ndivyo sivyo na hakusumbuka ili awapendeze wajinga;
*Mathayo 11:18-19*
[18]
Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakasema, Yuna pepo.
[19]
Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki
yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi
zake.
Huwezi
kuwapendeza wanadamu katika kila jambo.. Inawezekana hata unavyovaa au kula
wanajisikia vibaya. Hawataki hata kukuona ukifanikiwa.!
CHA
KUFANYA?
Jisalimishe
katika Mikono salama ya Mungu ili akushindie yote, na kisha fuata Ndoto na
Njozi iliyoko ndani yako bila kusita-sita.
AMUA
Kufanya jambo ambalo litakuwa katika KUMBUKUMBU ya kwamba mwaka 2016 haukuishi
kwa hasara, Bali kwa Faida.
Uwe
na Maamuzi mema, Mungu awe nawe.
YOURS
SINCERELY,
©Lackson Tungaraza
📞0764793105
(call or whatsapp)
Facebook:
www.facebook.com/ltungaraza
Library:
http://lacksontungaraza.blogspot.com (CHOTA MAARIFA HAPA).
0 comments:
Post a Comment