Saturday, September 9, 2017

Asomae na asome kwa Umakini na Kuelewa Lengo la Makala hii.

Kabla ya Hadithi kuanza kusimuliwa, huanza Hadithi! Hadithi! Hapo zamani za Kale… Nami katika Kutafakari jambo hili, nikakumbuka hapo zamani za kale za Mama yao Wana wa Zebedayo aliyemwendea Yesu pamoja na wanawe, akamsujudia na kumwomba neno, kwamba Wanae wawili WAKETI Mmoja mkono wa wake wa Kuume na mmoja mkono wake wa Kushoto katika Ufalme wake. Yesu akajibu akasema, ‘Hamjui Mnaloliomba. Je! Mwaweza KUNYWEA KIKOMBE NITAKACHONYWEA MIMI? Wakamwambia, Twaweza. Akawaambia, hakika Mtakinywea Kikombe changu; lakini Kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, sina amri kuwapa, bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu’

Kikombe alichokuwa ananywea Yesu kilikuwa kimebeba Bidii ya Kufanya Maombi binafsi mlimani pasipokuwa na watu, kukesha, kubezwa, kutokuaminiwa na nduguze, mateso, majaribu, kukanwa na kusalitiwa.

Kuna GHARAMA KUBWA YA KUKETI PAMOJA NA YESU, KUNA GHARAMA KUBWA YA KUKINYWEA KIKOMBE ALICHONYWEA YESU.

Kuna Gharama Kubwa ya Kutaka kuwa kama mtu fulani (Mtume Paulo, Mwl. Mwakasege, Apostle Shemeji Melayeki, Bishop Gwajima, Bishop Moses Kulola, Mwl. Mwambeso, Mwl. Makwaya, Pastor Raphael JL n.k.). Viti vya Kuketi pamoja nao, na vikombe wavinyweavyo vinasiri nzito sana na ngumu. Hivyo hesabu gharama kabla ya kutaka kuketi pamoja nao (upande wa kushoto au wa kulia) na kunywea vikombe vyao.

Kuna gharama ya kuketi pamoja na Lackson Tungaraza, na kunywea kikombe chake. Kwanini? Kwa sababu kuna wakati anabezwa, anasalitiwa, anapitia majaribu, anakesha katika kuutafuta Uso wa Bwana kwa kila namna ikiwa ni pamoja na Kufunga wakati wengine wanaendelea Kula bata. Kuna wakati anajisikia KUKATA TAMAA ya kuendelea Kuandika Masomo yake Mtandaoni kwa yale anayopitia maishani lakini ANAJIPA MOYO kama Kristo alivyosema, huku AKIAMINI kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa na wakata tamaa. Zaidi sana ni juu ya idadi ya watu ambao Mungu amewaandaa ili Wamjue Yeye kupitia Masomo yake ya mtandaoni na ya ana kwa ana. Hivyo akikata tamaa, DAMU yao itakuwa juu yake na atadaiwa na Mwajiri wake (MUNGU) siku ya Kiama.

Mara nyingi amekoswa watu wa Kumtia Moyo katika yale anayoyafanya tofauti na Kristo aliye rafiki yake wa karibu zaidi, na Mshauri wake wa kwanza. Amekutana na akina DELILA wengi kwenye maisha yake, lakini rafiki yake wa karibu zaidi (Yesu Kristo) alimsaidia.

Wewe unayetaka kuwa kama Lackson Tungaraza, Je! Unaweza Kukinywea Kikombe chake? Usione vyaelea, vimeundwa. Remember, ‘Behind any Success there is a Secret to find’ Lackson Tungaraza once wrote in his articles. Nyuma ya mafanikio yo yote yale kuna Siri ya kupata na Kujifunza.



Ni kweli huwa unamfurahia sana Lackson Tungaraza kwa yale ayafanyayo lakini niliyokuandikia leo sio Uongo, kama huamini mtafute umwulize kwa hekima kwa lengo la Kujifunza kwake (0764793105 WhatsApp, SMS). Ni mmoja wa Wapindua Ulimwengu kwa ajili ya Kristo Yesu.

Hakuna marefu yasiyokuwa na Ncha. Tukutane siku nyingine, kwa masomo mengine na kwa siri zingine. Bye bye!!

‘I must first count the price of being like You, Lackson Tungaraza’


WEKA ODA YAKO MAPEMA. KITAANZA KUPATIKANA KWA GHARAMA YA TSH.4000 TU KABLA YA KUZINDULIWA MWISHO WA MWEZI HUU. UTATUMIWA POPOTE PALE.
0764793105

Related Posts:

  • ROLE MODEL WETU WA LEO 16/1/2016 WILLIAM H GATES III    WILLIAM H GATES III William H Gates III , anajulikana kama Bill Gates. Alizaliwa tarehe 28 Oktoba 1955 na kulelewa katika kijiji cha Seattle pamoja na dada zake wawili. Baba yake ni At… Read More
  • "JIFUNZE KWA MWANAMKE MCHAPAKAZI MAZNAT"Jina lake kamili ni Maza Sinare Mchome.    Alipokuwa anaongea katika Kipindi cha Ndoano ndani ya Wanawake live tv ya JOYCE KIRIA, alisema ya kwamba alipokuwa Mdogo alikuwa anaweka 2000 juu ya meza na kuisemeza ya… Read More
  • FIKIRIA NJE YA BOX All the so-called 'Secrets of Success' will not work unless you do--Unknown. Siri za mafanikio ni nyingi sana na utaendelea kuzisikia na kuzisoma sehemu mbali mbali.. Mtandaoni, magazetini, vitabuni nk..... Sidhani kama k… Read More
  • HAKIKA, ANASTAHILI KUPEWA SIFA.Haikuwa jambo jepesi kuacha shughuli zake, Umaarufu wake, Ulinzi, Utajiri na kuja kututembelea huku kwetu. Sidhani kama wewe msomaji ungeweza kufanya hivyo. Yeye aliweza, pasipo manung'uniko wala hamu ya kutamani kurudi huk… Read More
  • JE UNATAKA KUKINYWEA KIKOMBE CHAKE?Asomae na asome kwa Umakini na Kuelewa Lengo la Makala hii. Kabla ya Hadithi kuanza kusimuliwa, huanza Hadithi! Hadithi! Hapo zamani za Kale… Nami katika Kutafakari jambo hili, nikakumbuka hapo zamani za kale za Mama yao Wa… Read More

0 comments:

Post a Comment

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI