WILLIAM H GATES III
William H Gates III , anajulikana kama Bill Gates. Alizaliwa tarehe 28 Oktoba 1955 na kulelewa katika
kijiji cha Seattle pamoja na dada
zake wawili. Baba yake ni Attoney na marehemu mama yake alikuwa mwalimu tu wa
kawaida wa shule. Katika umri wake mdogo Bill Gates alivutiwa na utengenezaji
wa programu akiwa katika mojawapo wa shule kijijini Seattle. Akiwa huko shuleni
Seattle, Bill Gates alikutana na Paul Allen , mwanafunzi mwenzake wakawa
marafiki.Hapo ndipo wakaanza kutumia tarakilishi ndogo ya shule kuendeleza
ujuzi wao, kama ambavyo pia wanafunzi mbalmbal duniani wanavyotumia elimu ya darasan
na elimu ya kijamii kuvumbua mitandao mbalmbal ya kijamii n.k.
Baadaye Bill Gates akaenda kujiunga na Chuo Kikuu cha Harvard kwa masomo ya elimu ya
juu. Kwa mara nyingine tena akajiunga pamoja na Paulo kuandika toleo jipya la
programu ya Msingi wa lugha ya kwanza ya kompyuta ya kibinafsi, iitwayo Altair
8800. Kampuni iliyotumia program hiyo iliridhishwa na kazi ambayo Bill Gates na
Paul Allen waliofanya na programu hiyo ikapewa leseni.
Jambo hili liliwachangia Gates na Allen Kuanzisha
kampuni ya Microsoft, iliyokuwa ikitengenezea kampuni zingine programu. Bill
Gates aliacha masomo yake katika chuo kikuu cha Harvard na kujishughulisha muda
wake wote katika biashara.
MICROSOFT COMPANY YA BWANA BILL GATES NA PAUL ALLEN |
Funzo: Fanya lile jambo unalolipenda maishan kwa
juhudi kubwa, usiige ya engine kwa sababu umeona wamefanya jambo Fulani. Mungu
kakupatia jambo la kipekee ndani yako, usijidharau. YOU ARE GENIOUS, INVEST ON
YOUR TALENTS.
Mafanikio yao yalikuja walipotengeneza mfumo wa
kuendesha kompyuta uitwao MS-DOS uliotumika katika kompyuta ya kwanza ya kibinafsi
ya IBM. Baadaye waliweza kuzishawishi kampuni zingine zinazotengeneza kompyuta
kutumia mfumo huo wa MS-DOS. Mfumo huu mpya wa MS-DOS ulipata umaarufu katika
soko miaka ya 1980.
Kipindi cha miaka mitano baadaye Microsoft ilitoa
mifumo mipya ya Windows 2.0 iliyokuwa bora zaidi kuliko mifumo ya hapo awali.
Kampuni ya Microsoft iliweza kupata umaarufu zaidi katika soko la hisa, na
akiwa umri wa miaka 31, Bill Gates aliweza kuwa bilionea mchanga zaidi katika
historia ya Marekani.
MAGARI YAKE YALIYOPO NYUMBANI |
BAADHI YA MAENEO ANAYOMILIKI BWN. BILL GATES |
Bill Gates alifunga ndoa na Melinda French Gates mwaka
wa 1994 na wakabarikiwa na watoto watatu, Jennifer, Rory na Fibi. Wote wawili Bill na Melinda ni
waanzilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali. Waliweza kulianzisha shirika la
Bill na Melinda Gates Foundation ambalo limesaidia kutoa michango mbalmbal ya
kuiendeleza jamii pamoja na watu wasiojiweza. Ubunifu wa Bill Gates wa
kutengeneza programu umekuwa mchango wake katika mapinduzi ya kompyuta na
sayansi ya kompyuta.
Tangu Mwaka 1995 amekua namba moja katika orodha ya
matajiri wakuu (forbes) duniani isipokua mwaka 2008 ambapo alikua namba 3 akiwa
na utajiri wa takribani dola bilioni 58 za kimarekani. Mwaka huo Bw. Warren
Buffet ndio alikua mtu namba mmoja akiwa na utajiri takribani dola za
kimarekani bilioni 62 akifuatiwa na Bw.Carlos Slim akiwa na utajiri wa takribani
dola bilioni 60 za kimarekani. Unaweza usijue lakini kila sekunde Bill Gates
anaingiza takribani dola 250 za kimarekani, Na kwa dakika nzima anaingiza takribani
dola 15000. Unashangaa?? . Bill Gates anaweza akagawa Dola 15 za kimarekani kwa
kila mtu duniani na bado akabakiwa na dola milioni 5 za kimarekani mfukoni. Kama
akiangusha dola 1000 za kimarekani hana haja ya kuziokota kwa sababu ndani ya
sekunde 4 ambazo angeweza kuziokota angekuwa tayari amesha zirudisha . Ukiachana
na kompyuta, pia Bill Gates ni muandishi. Mpaka sasa ana vitabu viwili amabavyo
ni ”The Road Ahead'” na ‘Business at the Speed of Thought’.
BAADHI YA PESA ZA JAMAA, SIYO UCHAWI, NI REAL |
Kwa Leo, hayo yanatosha kujifunza kutoka kwa Role
Model wetu, Bwn. Bill Gates. Unalipi la kuongezea juu ya huyu jamaa, Mr. Bill
Gates?.. Unaweza changia hapa na pia kuwashirikisha na wengine wajifunze (share)
MORAL
OF THIS:
1: Kuna wakati ambapo
sisi kama wanadamu tunatenda mambo ambayo hatuyapendi kutoka moyoni; bali kwa
sababu ya tamaa zetu binafsi. Watu wanafanya kazi ambazo hawazipendi kutoka
mioyoni ila kwa sababu mishahara ya hizo kazi ni minono.
2.
Ukitenda jambo ambalo hulipendi kutoka moyoni, tambua ya kwamba hutopata
mafanikio ambayo ulipaswa kupata katika maisha yako na pia hayo mafanikio
hayatakuwa ya kudumu. Bwana Bill Gates na wengine wengi wamekuwa na mafanikio
makubwa sana hadi hii leo kwa sababu waliweza kutenda yale ambazo waliyapenda
kutoka mioyoni mwao. Anza leo kuwekeza nguvu kubwa katika fani, kipaji na ujuzi
ulionao. Elimu ya shuleni ni daraja tu la kukutanisha na vitu fulani ambavyo
Mungu anataka uvijue kabla ya kufika kule unakotaka kwenda. Usiitegemee sana kuliko kipaji chako.
3.
Watu waliowekeza katika fani, ujuzi na vipaji vyao wamefika mbali sana kimafanikio.
Mfano Lionel Messi, Christian Ronaldo, Samatta, Diamond, Ambwene, Rose Muhando
n.k. Japo kuwa elimu zao za darasani siyo kubwa kivile
4.
Naamini kabisa ya kwamba 2016, Mwaka Wa Mabadiliko na kuinuliwa na Bwana katika
maisha yako. Wekeza pia katika kutafuta elimu ya kiMungu katika maisha yako.
Hvyo unaweza kuungana name katika kampeni ya kuleta ukombozi katika maisha yao
kuanzia mwaka huu. Kampeni yangu inaitwa 2016,
MWAKA WA MABADILIKO NA KUINULIWA kama ambavyo picha hii ya chini
inavyoelezea;
USIPITWE NA MAONO HAYA JUU YA MAISHA YAKO, 2016, YEAR OF VICTORY. |
HUYU JAMAA KAFANYA MAISHA KUWA RAHISI KWA NAFASI KUBWA SANA, WEWE KAMA MPENDA MAENDELEO, UNALIPI LA KUSEMA JUU YA HUYU BILL GATES?
ReplyDeleteToa maoni yako hapa.