Alipokuwa
anaongea katika Kipindi cha Ndoano ndani ya Wanawake live tv ya JOYCE KIRIA,
alisema ya kwamba alipokuwa Mdogo alikuwa anaweka 2000 juu ya meza na kuisemeza
ya kwamba hataitumia hadi iwe 4000.
Pengine ilichangiwa na aina ya wazazi aliokuwa nao,
maana walikuwa ni wachapakazi sana. Mamake alikuwa Fashion designer na Fundi
Cherehani mzuri, na babaye alikuwa Daktari wa Mifugo.
MAZNAT
alisoma sana na kupata vyeti kadhaa vya kiheshima, lakini MWISHO wa siku
aliamua kuweka Vyeti pembeni na Kuanza KUJIAJIRI.
Nilijifunza
mambo kadhaa kutoka kwake kama ifuatavyo;
1.
MTAZAMO
MAZNAT
alikulia maisha ya kuwa na Mtazamo Chanya katika Kila jambo alilokuwa akikutana
nalo. Mtazamo huo ulimwezesha Kupiga hatua sana Kimaisha, na Mtazamo huo
ulichangiwa pia na aina ya watu waliokuwa wakimzunguka kwanzia kwenye familia
yao na kwingine.
☆Hivyo ni muhimu sana kuwa na MTAZAMO CHANYA.
Haijalishi Aina ya FURSA unayopata, pesa unazoingiza, nafasi yako katika Jamii.
JAMBO kubwa ni Mtazamo, una Mtazamo gani??
2. DHARAU
Dharau ya
jambo lolote ni mbaya. MAZNAT alishawahi kuuza Vocha, Ubuju, Maji, Big G,
mitumbe, house Girl n.k.
#Chochote ambacho
hakimkosei Mungu ni vyema kukifanya pasipo kukidharau. Hata kama kinakuingizia
Fedha ndogo au kubwa, kiheshimu kabisa. Acha kudharau hicho kidogo unachofanya
leo. Wajasiriamali wakubwa unaowaona, nao walikuwa wadogo hapo awali.
Kumbuka MAZNAT alikuwa akiheshimu hata biashara ya Big G, kusaga Unga wa Watoto n.k.
3.
UTHAMINI.
MAZNAT
alikuwa msomi, lakini hakujali hilo, akaanza kufanya biashara ndogo ndogo kwa
kuzithamini sana. MWISHO wa siku zikamtoa Kimaisha.
☆Hivyo ni vyema kuthamini biashara au kazi ufanyayo
hata kama hailingani na vyeti vyako au haiendani na Mtazamo wa watu kwako. Kuna
walioanza kuuza Vitumbua na sasa ni wamiliki wa Hoteli kubwa, walianza kucheza
mpira wa mchangani na sasa wanacheza Ligi kuu TANZANIA bara na wengine wako
Ulaya. Kila kitu ni hatua. Nyumba ya ghorofa 30 huanza kwa Tofali moja. Wazungu
husema, "ROME WASN'T BUILT IN A SINGLE DAY." Kwahyo THAMINI
unachofanya sasa, uwe na UVUMILIVU na IMANI juu ya mambo YATARAJIWAYO bayana na
Yale Yasiyoonekana kwa sasa.
KWA upande
mwingine, MAZNAT alikulia maisha ya kubanwa sana na WAZAZI wake. Alikuwa hapati
MUDA WA kukaa KIHASARA HASARA wakati wa Likizo. Alikuwa anapewa pesa baada ya
KUFANYA KAZI KWANZA. Siku moja alifanya kazi vizuri sana na KUPEWA Tsh. 10,000.
Akaichukua hiyo Fedha na kuanzisha Home English Tuition Center, akapata
wanafunzi kadhaa aliokuwa akiwafundisha Kiingereza hapo kwao. Kwa sasa ni
Mfanyabiashara Mkubwa anayemiliki MAZNAT BRIDAL CARE nk
☆Hivyo WAZAZI nao wana NAFASI kubwa sana ya
Kuwafanya watoto wao kuwa Wachapakazi na wajasiriamali wakubwa. Waswahili
husema,"Mtoto Umleavyo ndivyo Akuavyo, SAMAKI MKUNJE ANGALI MBICHI"
na Wazungu husema, "CHARITY BEGINS AT HOME"
KWA yote
hayo niliyoandika hapa, MAZNAT ni mfano mzuri sana wa wanawake wa kuigwa katika
Jamii. Ni mfano mzuri kwa MABINTI na wamama ambao wanajiona Hawafai au Hawawezi
kufanya mambo makubwa katika Jamii zao. Pia ni mfano kwa VIJANA ambao walidhani
ya kwamba Wanawake wote ni Wadhaifu kikazi nk.
Aliyeandika
haya ni Lackson Tungaraza
Facebook!
fb.com/ltungaraza
WhatsApp!0764793105
☆NI WAKATI WA KUACHA LAWAMA NA KUPIGA KAZI. HUU NI
MSIMU WA 'HAPA KAZI TU'
Watumie
na wenzako Wajifunze pia.
0 comments:
Post a Comment