Monday, January 25, 2016

       MADHARA YA KUKATA TAMAA

Habari yako rafiki yangu mpendwa?
Nakupa pongezi kwa kuendelea kutafuta maarifa mbali mbali ya kuweza kubadili maisha yako katika mtazamo uliochanya, ni wengi wanatamani lakini hawachukui hatua wanabaki kulalamika kila siku. Kwahiyo mshukuru Mungu wako.

Baada ya kujifunza mambo mengi kwa habari ya namna ya  kuweka Malengo na jinsi ya kuyafanikisha na masomo mengine mengi juu ya Mafanikio katika Maisha yetu ya kila siku. Leo napenda tuangalie hili suala la kukata tamaa. Watu wengi, wanamuziki, waalimu, wanasheria, wanafunzi, mawaziri, wafanyabiashara, wanandoa, wachumba, wachungaji wameingia katika ramani ya maisha ambayo hawakuwa nayo awali kwa sababu ya kukata tamaa. Kukata tamaa ni adui namba moja aliyewapeleka wengi makaburini kabla ya wakati wao, aliyewafanya wengi waonekane ni wazee wakati bado ni vijana, aliyewafanya wengi waone kama maisha hayana maana yoyote kwao. KUKATA TAMAA NI NINI?

Kukata tamaa ni hali ya kupoteza matumaini. Hali hii hutokea pale ambapo mtu anapoteza imani juu ya matarajio yake ya sasa na ya baadae ya kupata kitu fulani alichojipangia. Kuna wanaofahamu kuwa wamekata tamaa na wengine hawafahamu kama wamekata tamaa. Kama una dalili zifuatazo, basi gundua ya kuwa umeshakata tamaa;

       i.            Kukosa msukumo wa ndani. Ili mtu yeyote yule aweze kufanikiwa anahitajika kuwa na msukumo wa ndani (burning desire), huu msukumo haupo ndani ya aliyekata tamaa.

     ii.            Kufanya Maamuzi ya haraka

  iii.            Kupoteza hamu  juu ya jambo Fulani. Inawezekana kuna jambo ulikuwa unalifanya kwa furaha na uzuri lakini ghafla unaanza kupoteza hamu juu ya jambo hilo.

  iv.            Kupoteza Ujasiri. Mwanzoni ulikuwa unatenda jambo kwa ujasiri lakini sasa ujasiri huo umepotea ghafla.

     v.            Kujihisi hufai kabisa. Unajichukulia kama mtu usiye na thamani yoyote ile hapa duniani.

  vi.            Mabadiliko ya Tabia. Kutoka tabia nzuri hadi mbaya

vii.            Kupungua kwa juhudi katika jambo ulitendalo. Mwanzoni ulikuwa unafanya kazi kwa bidii lakini sasa unajifariji ya kwamba unapumzika kidogo au utafanya baadae.

viii.            Maneno na vitendo vinavyoashiria kukata tamaa kama matumizi ya madawa ya kulevya, Ukahaba, Sidhani kama nitaweza, kujitenga n.k
          
Nadhani sasa utakuwa umejitambua kama ulikuwa umekata tamaa au la. Madhara ya kukata tamaa ni makubwa japokuwa watu wanajifariji, kama;

                          I.  Kupoteza Dira ya Maisha. Ili mwanadamu aweze kufanikiwa hapa duniani, anatakiwa kuwa na dira (maono). Lakini mtu anapokata tamaa, dira hii hupotea ghafla na hivyo kujikuta akitenda mambo ya ajabu hata kama mwanzoni alikuwa mtu mwema na mwadilifu
          
     I           II. Kutokufikia Malengo yako ndani ya Wakati. Katika video iliyopita nilielezea juu ya sifa mojawapo ya Malengo, lazima yawe na muda maalumu; kama ni wiki, mwezi, mwaka au zaidi ya hapo. Hivyo mtu anapokata tamaa, Malengo hayo huwekwa pembeni kwanza na kusababisha upotevu wa muda uliopangwa
         
              III.   Kufanya Maamuzi ya Haraka. Kama mtu alikuwa mtumishi wa Mungu, basi anajiingiza katika masuala ya Uzinzi, matumizi ya madawa ya kulevya. Mwanafunzi aliyefeli kujiua, Wanandoa kupeana taraka, Wanawake kutoa Mimba n.k pasipo kufikiria kwanza.

              IV. Jamii na Taifa kukoswa Maendeleo. Waziri, Mzazi anapokata tamaa, basi hawezi kuleta maendeleo yoyote kwa sababu ameshajiona yeye siyo wa thamani na hata hatokuwepo, kwa nia ya kujiua .


         KUMBUKA MAMBO YAFUATAYO IKIWA UNATAKA KUKATA TAMAA;



HAMNA MWENYE UWEZO WA KUZUIA NDOTO YAKO IKIWA HUJAWAPA NAFASI YA KUITAWALA, SONGA MBELE SIKU ZOTE, 
USIKATE TAMAA, 
MAMBO MAZURI ZAIDI YANAKUJA MBELENI.


Nakushukuru sana kwa muda uliyotoa kusoma Makala hii ya leo, Unaweza changia lolote lile ambalo unaona kwa upande wako litasaidia jamii yetu kusonga mbele. Pia kumbuka kuSHARE ili kuwafikia ndugu na rafiki zetu wengi. Ubarikiwe na Bwana.

Ni Mimi Rafiki Yako Mpendwa,
Lakson Tungaraza.

0764793105 (whatsapp/piga simu)




Thursday, January 21, 2016


AMUA LEO NI NANI ATAKAYEKUWA MSHAURI WAKO

MSHAURI MZURI NI YULE ANAYEKUPA MAWAIDHA MEMA

Habari yako rafiki yangu mpendwa?
Karibu tena katika mfululizo wa masomo yetu kupitia mitandao ya kijamii, jipongeze kwa afya na uhai uliopewa na Mungu hadi siku hii ya leo kwa sababu ni wengi walitamani kuwepo katika nafasi kama hiyo yako lakini hawajawezi na pia wengine walishaaga dunia. Kumbe siyo jambo la kujivunia, ila ni la kushukuru na kusema Ahsante Mungu.

Napenda leo tuangalie hili suala la kuchagua Mshauri katika maisha. Mwanadamu yeyote yule timamu ni kawaida kupitia vipindi vya magonjwa, kushindwa, ajali, misiba,kufeli mitihani, kukoswa ajira n.k. Lakini katika hayo yote mtu anahitaji kuwa na Mshauri ili aweze kufanya maamuzi yaliyo sahihi kwa ajili ya hatima ya maisha yake ya sasa nay a baadaye. Je, Mshauri wako ni yupi?

CHAGUA MSHAURI ANAYEFAA. UTAKUGHARIMU UKIKOSEA.
Inawezeka ni kweli unaye mtu ambaye huwa ana kushauri katika mambo mbali mbali ya kimwili na kiroho, lakini, Je! Ushauri anaokupa ni sahihi au ni wa kukunufaisha kwa muda na kisha baadae kuumia zaidi? AKILI YA KUAMBIWA, JUMLISHA NA YA KWAKO, uone kama unafaa au la. Siyo kila ushauri ni wa kufanyia kazi papo hapo bila kufanya utafiti, natumaini utanielewa tu kidogo kidogo hadi tufike.

Ngoja nikupe mfano kutoka katika maandiko matakatifu. Kulikuwa na mfalme aitwae Herode, huyu mfalme alimwoa mke wa nduguye Filipo. Jambo hilo halikumpendeza Yohana na hivyo akamwambia Herode, siyo halali yeye kuwa na mke wa nduguye. Naye Herodia (mke wa Herode, aliyechukuliwa kutoka kwa Filipo) akawa akimvizia Yohana ili amwue kwa sababu ya kuongea ukweli.

Siku moja Herode akawa anafanya karamu kwa ajili ya siku yake ya kuzaliwa na aliwaalika majemadari na watu wenye vyeo wa Galilaya. Binti yake Herodia aliingia, akacheza kwa ufanisi mkubwa na kumfurahisha Herode sana. Herode akamwambia aombe lolote atakalo na atapewa, hata ikiwa ni nusu ya ufalme wake.
Binti akaenda kumuliza mamake, aombe nini? Akamwambia, aombe kichwa cha Yohana Mbatizaji. Kwa sababu ya kiapo cha Herode mbele ya wageni, Yohana akakatwa kichwa. Tunajifunza nini hapa?

YOHANA KUKATWA KICHWA KWA SABABU YA MSHAURI MBAYA


Herodia ndiye aliyekuwa mshauri wa binti yake, na ndiyo maana binti yake alimfuata baada ya kupata jambo jipya. Lakini, Je! Ushauri ulikuwa mzuri? La hasha. Kuna watu ambao wapo kwa ajili ya kuwapoteza wengine kwa manufaa yao binafsi. Inawezekana unataka kuoa na ukamwomba rafiki yako akushauri, naye akakushauri uachane na mchumba wako halafu baadaye unamkuta naye. Wengi wamelizwa sana kutokana na Washauri waliowachagua katika maisha yao. Jiulize, anayekushauri juu ya biashara, ndoa, elimu, afya ni Mshauri sahihi au ndiye anayekupoteza katika dira ya maisha?

Chukua hatua leo ya kufanya tathimini katika maisha yako na wale ambao unawaendea kupata Ushauri kutoka kwao, ikiwa hawafai tengana nao mapema.
Nakushukuru sana kwa kusoma makala hii hadi mwisho, ubarikiwe na Bwana na uwe na hekima ya kuchagua Mshauri mwema.

Ni mimi rafiki yako mpendwa,
Lackson Tungaraza.
0764793105, kwa jambo lolote nijulishe (whatsapp,call).
WHO IS YOUR BEST ADVISOR? IT NEEDS ENOUGH KNOWLEDGE TO CHOOSE 
Join Lackson Tungaraza 
Whatsapp: 0764793105
Facebook/instagram: Lackson Tungaraza. 
HAVE A NICE DAY.




Saturday, January 16, 2016


WILLIAM H GATES III 

 
WILLIAM H GATES III
William H Gates III , anajulikana kama Bill Gates. Alizaliwa tarehe 28 Oktoba 1955 na kulelewa katika kijiji cha Seattle pamoja na dada zake wawili. Baba yake ni Attoney na marehemu mama yake alikuwa mwalimu tu wa kawaida wa shule. Katika umri wake mdogo Bill Gates alivutiwa na utengenezaji wa programu akiwa katika mojawapo wa shule kijijini Seattle. Akiwa huko shuleni Seattle, Bill Gates alikutana na Paul Allen , mwanafunzi mwenzake wakawa marafiki.Hapo ndipo wakaanza kutumia tarakilishi ndogo ya shule kuendeleza ujuzi wao, kama ambavyo pia wanafunzi mbalmbal duniani wanavyotumia elimu ya darasan na elimu ya kijamii kuvumbua mitandao mbalmbal ya kijamii n.k.

Baadaye Bill Gates akaenda kujiunga na  Chuo Kikuu cha Harvard kwa masomo ya elimu ya juu. Kwa mara nyingine tena akajiunga pamoja na Paulo kuandika toleo jipya la programu ya Msingi wa lugha ya kwanza ya kompyuta ya kibinafsi, iitwayo Altair 8800. Kampuni iliyotumia program hiyo iliridhishwa na kazi ambayo Bill Gates na Paul Allen waliofanya na programu hiyo ikapewa leseni.
Jambo hili liliwachangia Gates na Allen Kuanzisha kampuni ya Microsoft, iliyokuwa ikitengenezea kampuni zingine programu. Bill Gates aliacha masomo yake katika chuo kikuu cha Harvard na kujishughulisha muda wake wote katika biashara.
MICROSOFT COMPANY YA BWANA BILL GATES NA PAUL ALLEN

Funzo: Fanya lile jambo unalolipenda maishan kwa juhudi kubwa, usiige ya engine kwa sababu umeona wamefanya jambo Fulani. Mungu kakupatia jambo la kipekee ndani yako, usijidharau. YOU ARE GENIOUS, INVEST ON YOUR TALENTS.
Mafanikio yao yalikuja walipotengeneza mfumo wa kuendesha kompyuta uitwao MS-DOS uliotumika katika kompyuta ya kwanza ya kibinafsi ya IBM. Baadaye waliweza kuzishawishi kampuni zingine zinazotengeneza kompyuta kutumia mfumo huo wa MS-DOS. Mfumo huu mpya wa MS-DOS ulipata umaarufu katika soko miaka ya 1980.

Kipindi cha miaka mitano baadaye Microsoft ilitoa mifumo mipya ya Windows 2.0 iliyokuwa bora zaidi kuliko mifumo ya hapo awali. Kampuni ya Microsoft iliweza kupata umaarufu zaidi katika soko la hisa, na akiwa umri wa miaka 31, Bill Gates aliweza kuwa bilionea mchanga zaidi katika historia ya Marekani.
MAGARI YAKE YALIYOPO NYUMBANI

BAADHI YA MAENEO ANAYOMILIKI BWN. BILL GATES

Bill Gates alifunga ndoa na Melinda French Gates mwaka wa 1994 na wakabarikiwa na watoto watatu, Jennifer, Rory na  Fibi. Wote wawili Bill na Melinda ni waanzilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali. Waliweza kulianzisha shirika la Bill na Melinda Gates Foundation ambalo limesaidia kutoa michango mbalmbal ya kuiendeleza jamii pamoja na watu wasiojiweza. Ubunifu wa Bill Gates wa kutengeneza programu umekuwa mchango wake katika mapinduzi ya kompyuta na sayansi ya kompyuta.
Tangu Mwaka 1995 amekua namba moja katika orodha ya matajiri wakuu (forbes) duniani isipokua mwaka 2008 ambapo alikua namba 3 akiwa na utajiri wa takribani dola bilioni 58 za kimarekani. Mwaka huo Bw. Warren Buffet ndio alikua mtu namba mmoja akiwa na utajiri takribani dola za kimarekani bilioni 62 akifuatiwa na Bw.Carlos Slim akiwa na utajiri wa takribani dola bilioni 60 za kimarekani. Unaweza usijue lakini kila sekunde Bill Gates anaingiza takribani dola 250 za kimarekani, Na kwa dakika nzima anaingiza takribani dola 15000. Unashangaa?? . Bill Gates anaweza akagawa Dola 15 za kimarekani kwa kila mtu duniani na bado akabakiwa na dola milioni 5 za kimarekani mfukoni. Kama akiangusha dola 1000 za kimarekani hana haja ya kuziokota kwa sababu ndani ya sekunde 4 ambazo angeweza kuziokota angekuwa tayari amesha zirudisha . Ukiachana na kompyuta, pia Bill Gates ni muandishi. Mpaka sasa ana vitabu viwili amabavyo ni ”The Road Ahead'” na ‘Business at the Speed of Thought’.
BAADHI YA PESA ZA JAMAA, SIYO UCHAWI, 
NI REAL



Kwa Leo, hayo yanatosha kujifunza kutoka kwa Role Model wetu, Bwn. Bill Gates. Unalipi la kuongezea juu ya huyu jamaa, Mr. Bill Gates?.. Unaweza changia hapa na pia kuwashirikisha na wengine wajifunze (share)

MORAL OF THIS:
1: Kuna wakati ambapo sisi kama wanadamu tunatenda mambo ambayo hatuyapendi kutoka moyoni; bali kwa sababu ya tamaa zetu binafsi. Watu wanafanya kazi ambazo hawazipendi kutoka mioyoni ila kwa sababu mishahara ya hizo kazi ni minono.

2. Ukitenda jambo ambalo hulipendi kutoka moyoni, tambua ya kwamba hutopata mafanikio ambayo ulipaswa kupata katika maisha yako na pia hayo mafanikio hayatakuwa ya kudumu. Bwana Bill Gates na wengine wengi wamekuwa na mafanikio makubwa sana hadi hii leo kwa sababu waliweza kutenda yale ambazo waliyapenda kutoka mioyoni mwao. Anza leo kuwekeza nguvu kubwa katika fani, kipaji na ujuzi ulionao. Elimu ya shuleni ni daraja tu la kukutanisha na vitu fulani ambavyo Mungu anataka uvijue kabla ya kufika kule unakotaka  kwenda. Usiitegemee sana kuliko kipaji chako.

3. Watu waliowekeza katika fani, ujuzi na vipaji vyao wamefika mbali sana kimafanikio. Mfano Lionel Messi, Christian Ronaldo, Samatta, Diamond, Ambwene, Rose Muhando n.k. Japo kuwa elimu zao za darasani siyo kubwa kivile

4. Naamini kabisa ya kwamba 2016, Mwaka Wa Mabadiliko na kuinuliwa na Bwana katika maisha yako. Wekeza pia katika kutafuta elimu ya kiMungu katika maisha yako. Hvyo unaweza kuungana name katika kampeni ya kuleta ukombozi katika maisha yao kuanzia mwaka huu. Kampeni yangu inaitwa 2016, MWAKA WA MABADILIKO NA KUINULIWA kama ambavyo picha hii ya chini inavyoelezea;
USIPITWE NA MAONO HAYA JUU YA MAISHA YAKO, 2016, YEAR OF VICTORY.



Thursday, January 14, 2016


JULIUS K. NYERERE


Tunayo mengi ya kujifunza na kujivunia kwa mwalimu nyerere, Mwasisi na Baba wa taifa la Tanzania.
MWL. JK NYERERE 

AKIWA NA RAIS WA AWAMU YA NNE, DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, 
MZEE WA ARI MPYA, NGUVU MPYA NA KASI  MPYA

Kuzaliwa na Malezi
Julius Kambarage Nyerere alizaliwa April 12/1922 katika ardhi ya Tanganyika, na alifariki tarehe 14/10/1999 mjini wa London Uingereza. Alizaliwa katika kijiji cha Butiama, karibu na pwani ya mashariki ya Ziwa la Victoria. Nyerere alikuwa mmoja wa watoto ishirini na sita wa baba yake, Nyerere Burito. Baba yake alikuwa kiongozi wa kabila la Zanaki. Pia baba yake alikuwa na fedha nyingi lakini hakuwa na  elimu kubwa.

Wakati wa utoto wake, Julius Nyerere alichunga mifugo na alikuwa na maisha ya kawaida. Nyerere alikuwa mfuasi wa dini ya Katholiki, alihudhuria misa mara kwa mara. Watu wanasema alipenda sana kucheza na kufanya mizaha. Pia alichonga meno yake ya mbele na msumeno kuonyesha utamaduni wa kabila lake.

Elimu
Julius Nyerere alijiunga na Shule ya Msingi ya Serikali katika mji wa Musoma wakati alipokuwa na miaka kumi na miwili. Alimaliza masomo ya miaka minne kwa miaka mitatu kwa sababu alikuwa na akili sana, alienda kusoma Shule ya Upili ya Serikali ya Tabora. Huko, alipata udhamini wa kwenda Chuo Kikuu cha Makerere. Ni muhimu kujua wakati alipopata udhamini huo, Makerere kilikuwa Chuo Kikuu cha pekee katika Afrika ya Mashariki. Alipata shahada yake hapo.

Baada ya chuo kikuu, Nyerere alirudi Tanganyika na alifanya kazi katika Shule ya Upili ya St. Mary katika mji wa Tabora. Shule ya St. Mary, ilikuwa shule ya katoliki. Huko, alifundisha masomo ya Biolojia na Kiingereza. Mwaka 1949, alipata udhamini wa kwenda kusoma katika Chuo Kikuu cha Edinburgh, hivyo akawa Mtanzania wa kwanza kusoma chuo kikuu nchini Wingereza na Mtanzania wa pili kupata digrii nje ya Afrika.

Katika chuo kikuu cha Edinburgh, Nyerere alipata Shahada ya juu ya Sanaa katika Historia na Uchumi, mwaka 1952. Akiwa Edinburgh, alisoma mkondo wa kufikiri unaoitwa “Fabian.” Mkondo wa “Fabian”, ulijumuisha kundi la wataalamu wa Ujamaa wa Uingereza. Azimio la “Fabian” ni kuendeleza mawazo ya kijamaa. Kwa sababu alijifunza mawazo ya “Fabian,” alianza kufikiri mabadiliko mazuri sana yangepatikana ikiwa angeweza kuunganisha ujamaa na maisha ya Afrika. Wakati wa maisha yake, Nyerere aliitwa “mwalimu” kwa sababu ya kazi zake za uelimishaji.

Ndoa na Familia
Kabla ya maisha yake ya kuwa mwanasiasa, alioa mwanamke aliyeitwa Maria Magige. Maria alitoka kabila tofauti. Wanahistoria walisema alioa mwanamke wa kabila lingine kuonyesha dunia,ilikuwa muhimu sana kusahau tofauti baina ya makabila na kuwa wamoja.

Mchango Katika Jamii
Mchango mkuu wa Nyerere katika jamii ni kazi aliyofanyia serikali. Lakini kwanza tusisahau kwamba, Nyerere alikuwa mwalimu wa historia, Kiingereza, na Kiswahili. Hivyo alianza shughuli za kisiasa alipokianzisha chama cha TANU (Tanganyika African National Union) kupigania uhuru kwa nchi za Tanganyika. Ndani ya mwaka mmoja tu, TANU ilikuwa na watu wengi wapya na ilikuwa ikiongoza  miradi ya kisiasa Tanganyika. Kwa sababu Nyerere alianza kujihusisha na siasa, hivyo alihitaji kuamua baina ya maisha ya uwalimu au ya uwanasiasa. Alijiuzulu kutoka kufundisha, na kuwa Mwanasiasa .

Alisafiri ndani ya Tanganyika kuzungumza na watu wengi na viongozi tofauti, kujaribu kupata msaada katika harakati za uhuru wa Tanganyika. Katika mwaka 1954, alifaulu kuunganisha jamii mbalimbali kitaifa pamoja kusaidia harakati za uhuru.  Nyerere alikuwa na ujasiri wakuzungumza, ujasiriuliomsaidia alipozungumza na UN (Umoja wa Mataifa) kuhusu uhuru wa Tanganyika. Mwaka 1958, aljiunga na Colonial Legislative. Tarehe 9/12/1961, Nyerere alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika baaada ya kupata Uhuru.
UHURU WA TANGANYIKA, NYERERE NA WANANCHI WAKISHEREKEA 

 Baada ya mwaka mmoja yaani mwaka 1962, Nyerere alishinda uchaguzi na kuwa rais wa Tanganyika. Pia  ni muhimu kujua kwamba Nyerere alifaulu kuunganisha kisiwa cha Zanzibar na Tanganyika  pamoja kuunda nchi ya Tanzania katika mwaka 1964, baada ya mapigano huko Zanzibar yaliyomaliza utawala wa Jamshid bin Abdullah, kiongozi wa Zanzibar.
KUUNDWA KWA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Nyerere aliendelea kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mpaka mwaka1985. Akiwa Rais, Nyerere alikumbwa na matatizo mengi kwa sababu mwaka 1960 Tanzania ilikuwa nchi maskini sana ukilinganisha na nchi zingine duniani, hivyo kuwa na deni kubwa sana na pia kulikuwepo na mfumuko mkubwa wa bei. Katika kusaidia nchi yake, Nyerere aliamua kujaribu ujamaa na maisha ya pamoja vijijini, na utaifishaji. Aliandika dhana zake katika Azimio la Arusha la Mwaka 1967. Watu walihimizwa kuishi na kufanya kazi pamoja katika vijiji vilivyokusudiwa kusambaza desturi ya utamaduni wa Tanzania na kuunda umoja.

JK. NYERERE AKIWA KWENYE BAISKELI YAKE,
 HAKUPENDA KUJILIMBIKIZIA MALI
ALIKUWA MTU WA WATU
Baada ya shughuli zake za urais, Nyerere aliendelea kusaidia jamii yake. Alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM).  Miaka michache baadae, aliacha shughuli za kisiasa kwa sababu ya umri wake. Alirudi kupumzika katika kijiji chake huko Butiama alipozaliwa. Tarehe 14/10/1999, alifariki mjini London alipokuwa amelazwa kwa matatizo ya kiafya.  Je, wewe kama Mtanzania unalipi la kusema juu ya Mwasisi wa taifa letu Mwl. JK Nyerere?
MWL. JK NYERERE AKIWA AKITA UBORA WAKE, 
A MAN OF VISIONS 
Toa maoni yako hapa na pia washirikishe wengine (share)

Imeandaliwa na rafiki yako mpendwa, Mr. Lackson Tungaraza
Blogger & Motivator
0764793105 (whatsapp/sms/call).

Wednesday, January 13, 2016

KWANINI SOKO LA AJIRA LIMEPUNGUA SANA KWA KASI KARNE HII?


Habari yako rafiki yangu mpendwa?
Napenda nikupe pongezi kwa kufuatilia masomo yetu mbali mbali katika mitandao ya jamii na kuhudhuria semina zetu za Ujasiriamali kwa njia ya Whatsapp na barua pepe. Leo tutajifunza mada uliyoisoma hapo juu katika kichwa cha habari.


KILA SIKU WATU WANAKESHA MITANDAONI NA KATIKA BAO ZA MATANGAZO
KUTAFUTA NAFASI ZA AJIRA

NAFASI ZA AJIRA KILA SIKU ZINAPUNGUA KWA KASI YA AJABU
NINI TATIZO?


WANAVYUO WANA PRESHA YA INTERVIEW ILI WAWEZE KUPATA AJIRA
JE, SULUHISHO NI SERIKALI?


Kila mara utawasikia wagombea Ubunge, udiwani, uraisi wakisema, “Mkituchagua sisi kwa hakika soko la ajira kwa vijana litapanda kutoka asilimia fulani hadi asilimia fulani.” Pia vijana wa kike na wa kiume masikioni mwao hupenda kusikia maneno kama hayo, lakini mambo hubadilika kuwa ndivyo sivyo pindi viongozi hao wanapoingia madarakani na kumaliza vipindi vyao vya uongozi bila kutimiza ahadi yao hiyo kwa vijana ambao ndiyo walio wengi nchini. Nini tatizo?
Lackson Tungaraza, baada ya utafiti wake ameweza kubaini kuwa tatizo siyo viongozi wala mfumo wa elimu nchini kama wengi wanavyolalamika, wakiwemo watu mashuhuri na maarufu nchini.

Tatizo ni “Sayansi na teknolojia”. Unaweza  shangaa au kukataa ni kwanini iwe Sayansi na teknolojia na siyo Serikali!!?
Ukuaji wa Sayansi na teknolojia nchihi na duniani kote unaathiri sana soko la ajira hata kwa wasomi kila siku, ndiyo maana wenye vyeti ni wengi kuliko wenye ajira.
Jiulize mambo yafuatayo;

1.     Wako wapi waliokuwa wanavusha watu ziwani kwa mitumbwi na mashua?
2.     Idadi kubwa ya vijana waliokuwa wanaishi kwa kuwarushia watu nyimbo kwenye simu zao kutoka kwenye Kompyuta,imeenda wapi?
3.     Idadi kubwa ya vijana waliokuwa wanasafisha mchanga migodini na kuchimba madini, imekimbilia wapi?
4.     Idadi kubwa ya watu waliokuwa wanalima mashamba yaw engine kwa jembe la mkono, imeenda wapi?

Utagundua kuwa  baada ya ugunduzi wa meli/boti, smartphones, bulldozers, tractors, robot n.k. Idadi kubwa ya watu wameondolewa katika sehemu zao za ajira za mwanzo. Mfano, kazi ambazo wangeliajiri watu 200 kiwandani kubeba vyuma na bidhaa zingine, hufanywa na Roboti mmoja au idadi kubwa ya watu ambao wangeliajiriwa na serikali kubeba moramu, mchanga, kuponda kokoto, hufanywa kwa mashine ambayo inaendeshwa na watu wachache sana. Na mambo mengine mengi kama hayo.
Ni wakati wako dada, kaka, mjomba, shangazi, baba, mama kufanya biashara inayoendana na ukuaji wa Sayansi na teknolojia. Wakati unasumbuka kutafuta fremu/pango kwa ajili ya kufungua biashara, wateja wengine wanafikishiwa bidhaa zilizo bora zaidi hadi milangoni mwao, atakuja saa ngapi kwako?
NI WAKATI WA KUCHUKUA MAAMUZI YA KUTAFUTA SULUHISHO LA
TATIZO LA AJIRA KATIKA MAISHA YAKO
USITEGEMEE SERIKALI
MUNGU KAWEKA KITU CHA THAMANI NDANI YAKO

Biashara ya Mtandao au Network Marketing ni biashara inayoweza kuleta mapinduzi ya kimtazamo na kiuchumi kwako kama ilivyofanya kwa wengine, bila kujali kiwango cha elimu, uzoefu bali ni msukumo uliyomo ndani yako kuyafikia malengo yako ya kifedha. Wasiliana nasi kupitia Whatsapp kwa nambari 0764793105 kuifahamu biashara hii na uendeshwaji wake.

Kama tayari una biashara na unapenda kuifanya kuwa ya tofauti na yenye mvuto mkubwa, kuna kitabu ambacho tunakitoa bure kabisa ili uweze kukuza biashara yako. Kimeandikwa “JINSI YA KUFANYA BIASHARA YAKO KUWA YA TOFAUTI NA YENYE MVUTO MKUBWA.” Ili kupata Nakala ya kitabu hicho, tuma Jina lako na Anuani ya barua pepe (Email address) kwenda namba 0764793105 au kwenye Email ya lacksontungaraza@gmail.com


Usisite kuuliza jambo lolote lile pale unapopata utata, wewe ni mtu wa maana sana kwetu. Pia unaweza kuwatumia na wengine taarifa hii au kutoa maoni yako hapa .Ahsante sana na ubarikiwe na Bwana.

Friday, January 8, 2016

ZAWADI YANGU KWAKO MFANYABIASHARA NA MJASIRIAMALI WA KWELI


Habari yako Mfanyabiashara na Mjasiriamali?
Namrudishia Mungu sifa, utukufu na heshima kwa kunilinda hadi siku hii ya leo na pia kukulinda wewe Mjasiriamali na Mfanyabiashara. Kwa hakika tusingeliweza kufika mahali hapa tulipo kama isingelikuwa ni rehema zake kwetu, tumepitia visa na mikasa mbali mbali ya kukatisha tamaa, kuchoa machozi, kufiwa, kufilisiwa, vitisho. Lakini katika yote hayo, tumeibuka washindi na sasa bado tunasonga mbele tena huu mwaka. Inawezekana unapitia maisha magumu ya kukatisha tamaa na hata huoni msaada mwingine. Ndugu, jamaa na rafiki wamekukimbia, nakuomba usikate tamaa na umwamini yeye aliyekuweka hai hadi hii siku ya leo. Kuna jambo ambalo Mungu atatenda muda siyo mrefu katika maisha yako ikiwa hutokata tamaa na ukiendelea kumwamini.

Katika mwaka huu mpya tuliyouanza siku kadhaa zilizopita, kila mmoja wetu kajiwekea Malengo ya kufikia kabla ya mwaka kuisha. Inawezekana mipango uliyonayo umeiga au ni kwa tamaa tu, usihofu mwaka huu ni Mwaka wa Mabadiliko ukichukua hatua ya imani ya kutaka kubadilisha maisha yako kuanzia muda huu. Ili kuleta Mabadiliko hayo chanya katika maisha yako, inakubidi kuwa mtu wa vitendo na siyo maneno. Katika kukusaidia kuleta Mabadiliko katika maisha yako, ikiwemo suala ya kiuchumi, nimekuandalia kitabu cha biashara kilichopewa jina la “JINSI YA KUFANYA BIASHARA YAKO KUWA YA TOFAUTI NA YENYE MVUTO MKUBWA” Kikiwa ni sehemu ya kwanza ya Mada ya “SIRI AMBAZO MFANYA BIASHARA HUJAZIJUA.”

Hii Ofa ni kwa wale wote ambao watajiunga na Semina ya biashara itakayoanza kesho tarehe 8 January. Nafasi hii ni yako wewe Mfanyabiashara na Mjasiriamali makini, fanya maamuzi sahihi ya kuleta mabadiliko katika maisha yako ndani ya mwaka huu. Isiishi maisha ya kubahatisha kila mwaka, biashara pia inahitaji kuwa na elimu yake na maarifa. Usipochukua hatua nzuri mwanzoni mwa mwaka, utapata shida huko mbeleni. NYOTA NJEMA HUONEKANA ASUBUHI.

Nakukumbusha juu ya semina ya mwaka wa mafaniko wa 2016, itakayoanza tarehe 8 Januari kesho kwenye makundi ya wasap na Email(barua pepe). Hivyo ni vyema ukalipia mapema gharama za semina kabla ya muda kufika ili kuleta mafanikio ya kiuchumi, kimtazamo na kiroho mwaka 2016. Mada zilizopo ni;

1.      Jinsi ya kupata Wazo bora la Biashara
Kuna watu wengi ambao wana Mitaji lakini hawajui wafanye biashara gani itakayowapa mafanikio

2.     Siri itakayo badilisha maisha yako mwaka 2016
Hii Siri itakupa ushindi wa kiuchumi na katika mfumo wako wa maisha

3.     Jinsi ya kuweka Malengo na njia za kufanikisha Malengo yako mwaka 2016
Utapata Mbinu zilizofupi na za Uhakika

4.     Mambo ya kuepuka ili ufanikiwe kiuchumi mwaka 2016
Kuna mambo  mengi ambayo yamekuwa  yakiwazuia watu kufanikiwa kiuchumi, yamechambuliwa vizuri. Pia baada ya Semina utapata Bure copy ya kitabu kiitwacho “SIRI AMBAZO MFANYA BIASHARA HUJAZIJUA” sehemu ya kwanza iliyopewa jina la “JINSI YA KUFANYA BIASHARA YAKO KUWA YA TOFAUTI NA YENYE MVUTO MKUBWA.”

PATA COPY YA KITABU HIKI BURE KABISA
BAADA YA SEMINA
0764793105
Lackson Tungaraza


Gharama ni Tsh. 10,000/- tu na Semina itafanyika wiki nzima kuanzia tarehe 8 Januari. Hivyo wahi mapema nafasi hii muhimu kwa kutuma pesa yako kwenda namba 0764793105, utaona jina limeandikwa Lackson Tungaraza . Usisahau kutuma Jina lako kwa ajili ya uhakiki na barua pepe(Email Address) kwa njia ya SMS. Ikiwa hauna Wasap au Barua pepe, nijulishe ili upate masomo kwa njia ya Inbox yako ya Facebook. FANYA UWAMUZI SAHIHI. Usisite kuSHARE na kuCOMMENT hapa.

FURAHIA FURSA AMBAZO MUNGU ANAKUPATIA
HUWEZI KUFANIKIWA KWA UBINAFSI
Karibu  Nikupe Semina Ya Ujasiriamali
2016, Mwaka Wa Mabadiliko



Tuesday, January 5, 2016

NGUVU YA MANENO YATOKAYO KATIKA VINYWA VYETU


Walisema manabii na mitume, “Atakaye kupenda maisha na kuona siku njema auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isinene hila” (1 Petro 3:10). Wengine wakaongezea”Mtu atakula mema kwa matunda ya kinywa chake” (Mith 13:2). Hayo yote yalitokea ili sisi tupate kujifunza namna gani tunaweza kuwa sehemu salama kwa kuwa makini nay ale tunayoyatamka kutoka katika vinywa vyetu.
Walisema, nimeamini na mimi nakwambia leo “MANENO NI SILAA” tena silaa yenye nguvu zaidi ya bunduki, mabomu au wanyama wakali wa mwituni. Wananchi wameingia katika balaa la kupigwa na Askari ovyo kwa sababu ya maneno mabaya ambayo viongozi fulani waliyatamka. Ndoa zimevunjika, zimetengana, yote sababu ya maneno waliyoyatamka wana ndoa hao.

Wanafunzi shuleni wanaendelea kufeli mitihani yao, afya za wagonjwa kuzidi kuwa mbaya kila siku kisa maneno waliyojitamkia. Wanasema, “Mimi ni wa kufeli tu”, “hatuna historia ya kudumu kwenye ndoa”, “umasikini tumeumbiwa”, “huu ugonjwa ni wa kwangu” n.k.

Tukibadili aina ya maneno yanayotoka vinywani mwetu, tutakuwa na amani, umoja, furaha na maendeleo katika jamii na kwetu pia kwa sababu hapatakuwepo na kauli mbaya za kuleta misuguano
Tofauti iliyopo kati ya waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa au tajiri na masikini, ni aina ya maneno yanayotoka katika vinywa vyao. Matajiri wanatamka maneno ya ushindi hata kama wako katika hali ngumu, wanajiamini hata kama mazingira waliyopo yanaleta hofu, waamini katika kutimiza malengo hata kama wengine wanakata tamaa, na maneno yao yanaashiria hivyo.

Baada ya kusoma juu ya nguvu iliyopo katika maneno tunayoyatamka kutoka  vinywani mwetu, mithiri ya kuleta umasikini, magonjwa, vifo katika maisha yetu. Kuanzia leo chukua hatua ya kuchunguza yale unayoyatamka juu ya maisha yako na juu ya watu wanaokuzunguka, kwa kufanya hivyo utapata mabadiliko ambayo hukutegemea hata katika biashara yako.
Hili somo limewasaidia wengi na kubadili aina ya maisha waliyokuwa nayo hapo awali, akiwemo Bwn. Lackson Tungaraza, blogger wa makala za kuikimboa jamii na Motivator, pia wanafunzi wa vyuo vikuu nchini. Wasiliana nae kujua zaidi, yale anayoyajua hadi sasa..Elimu haina Mwisho.

Nakukumbusha juu ya semina ya mwaka wa mafaniko wa 2016, itakayoanza tarehe 8 Januari kwenye makundi ya wasap na Email(barua pepe). Hivyo ni vyema ukalipia mapema gharama za semina kabla ya muda kufika ili kuleta mafanikio ya kiuchumi, kimtazamo na kiroho mwaka 2016. Mada zilizopo ni;

1.      Jinsi ya kupata Wazo bora la Biashara
Kuna watu wengi ambao wana Mitaji lakini hawajui wafanye biashara gani itakayowapa mafanikio

2.     Siri itakayo badilisha maisha yako mwaka 2016
Hii Siri itakupa ushindi wa kiuchumi na katika mfumo wako wa maisha

3.     Jinsi ya kuweka Malengo na njia za kufanikisha Malengo yako mwaka 2016
Utapata Mbinu zilizofupi na za Uhakika

4.     Mambo ya kuepuka ili ufanikiwe kiuchumi mwaka 2016
Kuna mambo  mengi ambayo yamekuwa  yakiwazuia watu kufanikiwa kiuchumi, yamechambuliwa vizuri. Pia baada ya Semina utapata Bure copy ya kitabu kiitwacho “SIRI AMBAZO MFANYA BIASHARA HUJAZIJUA” sehemu ya kwanza iliyopewa jina la “JINSI YA KUFANYA BIASHARA YAKO KUWA YA TOFAUTI NA YENYE MVUTO MKUBWA.”


Gharama ni Tsh. 10,000/- tu na Semina itafanyika wiki nzima kuanzia tarehe 8 Januari. Hivyo wahi mapema nafasi hii muhimu kwa kutuma pesa yako kwenda namba 0764793105, utaona jina limeandikwa Lackson Tungaraza . Usisahau kutuma Jina lako kwa ajili ya uhakiki na barua pepe(Email Address) kwa njia ya SMS. Ikiwa hauna Wasap au Barua pepe, nijulishe ili upate masomo kwa njia ya Inbox yako ya Facebook. FANYA UWAMUZI SAHIHI. Usisite kuSHARE na kuCOMMENT hapa.


JIFUNZE KUJIAJIRI NA KUJITENGENEZEA KIPATO CHA ZIADA
Lackson Tungaraza
Blogger & Motivator
0764793105
USIPITWE NA SEMINA HII MUHIMU
2016, MWAKA WA MABADILIKO

Saturday, January 2, 2016

JITAMBUE KUANZIA LEO


Heshima na Shukrani za dhati zikufikie wewe msomaji wa Makala zangu za Uelimishaji kupitia Mitandao ya Kijamii ya Facebook, Twitter, Linkedln, Instagram pamoja na blog yangu (lacksontungaraza.blogspot.com) kwani umekuwa msaada wangu kusonga mbele ndani ya mwaka 2015 na sasa tena uko pamoja nami mwaka 2016. Nimejipanga  huu mwaka kukupa Masomo na Semina mbali mbali ambazo zitakuwezesha kujitambua na kufanikiwa ndani ya huu mwaka ili itakapofika tarehe 31 Disemba ziwepo shuhuda nyingi za mafanikio kwa kila mmoja wetu, hivyo usiache kufuatilia masomo yangu na pia kuwa rafiki yangu facebook ( www.facebook.com/ltungaraza ).
Leo nitazungumzia suala la mtu kujitambua ana tabia ya aina gani maishani ili afanye mabadiliko na kusonga mbele. Nimezitenga hizo tabia katika makundi matatu ambayo kwa uhakika na wewe umo kama ukijitathimini baada ya kusoma. Makundi hayo ni;

Ø MTU WA KUIGA
Kama wewe ulikuwa msomaji mzuri wa hadithi zaSungura na Fisi, utagundua ya kwaamba fisi alikuwa anaiga mambo mengi kutoka kwa Sungura; njia alizokuwa akitumia Sungura kupata chakula wakati wa njaa, Ujanja n.k. Na hivyo kupelekea Sungura kuonekana ni Mjanja zaidi ya Fisi. Fisi alijikuta yuko matatani kwa kuwa na tabia ya kuiga.
Katika mfumo wa maisha ya mwanadamu, kuna watu ambao wao wapo kwa ajili ya kuiga ya wengine, hawana ya kwao. Inawezekana na wewe upo katika kundi hili lakini endelea kusoma, utagundua cha kufanya.

Unamkuta mtu katulia kama vile hana jambo la kufanya, kumbe anasubiri mtu fulani afanye na ndipo na yeye afanye. Inawezekana biashara unayoifanya  uliiga kutoka kwa jirani au rafiki yako, Masomo unayosoma shuleni uliiga sehemu baada ya kusikia kuna soko la ajira ukiyafaulu vizuri n.k.
Unapokuwa unamuiga mtu mwingine, unakuwa umedharau kipaji  au ujuzi wako ambao Mungu kakupatia. Biashara yako ingekuwa katika kiwango kikubwa sana kama ungetumia Ujuzi wako binafsi au mfumo wako wa maisha ungekuwa bora kwa kufuata yaliyo yako bila kuiga. ACHA KUIGA, FANYA AMBAYO MUNGU KAWEKA NDANI YAKO.

Ø MTU WA KUSHINDANA
Kuna watu ambao wapo hadi sasa duniani kwa ajili ya kushindana na ndoto za watu wengine. Kila mtu kaumbiwa jambo la kipekee ndani yake, linalomtofautisha na wengine na ndiyo maana ukitazama “finger print” au alama ya kidole chako ni ya kipekee duniani kote. Hata mapacha  wakifanana kwa kiwango gani lakini “finger print” zao ni tofauti.
Unapokuwa unashindana na Malengo na Ndoto za watu wengine, utaumia wewe mwenyewe. Muulize Farao ni yapi yalimtokea na majeshi yake ya Misri kwa kushindana na ndoto ya Musa ya  kuwatoa wana wa Israeli Misri na kuwapeleka Kaanani.
Wanasema, “Adhabu ya kaburi aijuaye ni maiti.” Mtu anapopanga malengo yake ya kutimiza, anakuwa ameshajitolea wakfu kwa changamoto yoyote ile itakayokuja mbele yake pasipo kukata tamaa. Wewe unaposhindana naye, utajihumiza na kukata tamaa. Usishindane na ndoto wa mtu mwingine, wala mfumo wake wa maisha.

Ø MTU WA UPEKEE
Ninaposema “Mtu wa Upekee” ni mtu ambaye anatenda yale ambayo yanatoka moyoni mwake na kuyaamini, yanaweza kuwa ni ya kiroho au ya kimwili.
Watu wa tabia hii huwa wanafika mbali kimafanikio kwa sababu wanatenda yale ambayo wanayaamini kutoka moyoni, maana akili hudanganya na pia kukatisha tama lakini moyo ndiyo umebeba uhalisia.
Ninakushauri sana ndugu yangu utoroke huko uliko, uje katika kundi hili la tabia la “Mtu wa Upekee.” Biashara yako na mfumo wako wa maisha ndani ya huu mwaka utabadilika na kuwa bora ukiwa “Mtu wa Upekee”. LIVE YOUR REALITY.

Napenda nikukumbushe juu ya Semina yetu kwa njia ya Mtandao (Online Seminar) itakayoanza tarehe 8 Januari kwenye makundi ya Wasap na kupitia barua pepe(Email). Masomo yatakayofundishwa ili kuleta mafanikio ya uhakika katika maisha yako mwaka 2016 ni;

1.      Jinsi ya kupata Wazo bora la Biashara
Kuna watu wengi ambao wana Mitaji lakini hawajui wafanye biashara gani itakayowapa mafanikio

2.     Siri itakayo badilisha maisha yako mwaka 2016
Hii Siri itakupa ushindi wa kiuchumi na katika mfumo wako wa maisha

3.     Jinsi ya kuweka Malengo na njia za kufanikisha Malengo yako mwaka 2016
Utapata Mbinu zilizofupi na za Uhakika

4.     Mambo ya kuepuka ili ufanikiwe kiuchumi mwaka 2016

Kuna mambo  mengi ambayo yamekuwa  yakiwazuia watu kufanikiwa kiuchumi, yamechambuliwa vizuri. Pia baada ya Semina utapata Bure copy ya kitabu kiitwacho “SIRI AMBAZO MFANYA BIASHARA HUJAZIJUA” sehemu ya kwanza iliyopewa jina la “JINSI YA KUFANYA BIASHARA YAKO KUWA YA TOFAUTI NA YENYE MVUTO MKUBWA.”
PATA KITABU HIKI BURE KABISA BAADA YA SEMINA
2016, MWAKA WA MABADILIKO
Usipange Kukosa Semina Hii


·        Gharama ni Tsh. 10,000/- tu na Semina itafanyika wiki nzima kuanzia tarehe 8 Januari. Hivyo wahi mapema nafasi hii muhimu kwa kutuma pesa yako kwenda namba 0764793105, utaona jina limeandikwa Lackson Tungaraza . Usisahau kutuma Jina lako kwa ajili ya uhakiki na barua pepe(Email Address) kwa njia ya SMS. Ikiwa hauna Wasap au Barua pepe, nijulishe ili upate masomo kwa njia ya Inbox yako ya Facebook. KAZI NI KWAKO.

SHARE(shirikisha) na ndugu,jirani na rafiki zako juu ya hii Semina . Kwa lolote , 0764793105 (SMS/Piga/Wasap) 


MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI