Thursday, January 21, 2016


AMUA LEO NI NANI ATAKAYEKUWA MSHAURI WAKO

MSHAURI MZURI NI YULE ANAYEKUPA MAWAIDHA MEMA

Habari yako rafiki yangu mpendwa?
Karibu tena katika mfululizo wa masomo yetu kupitia mitandao ya kijamii, jipongeze kwa afya na uhai uliopewa na Mungu hadi siku hii ya leo kwa sababu ni wengi walitamani kuwepo katika nafasi kama hiyo yako lakini hawajawezi na pia wengine walishaaga dunia. Kumbe siyo jambo la kujivunia, ila ni la kushukuru na kusema Ahsante Mungu.

Napenda leo tuangalie hili suala la kuchagua Mshauri katika maisha. Mwanadamu yeyote yule timamu ni kawaida kupitia vipindi vya magonjwa, kushindwa, ajali, misiba,kufeli mitihani, kukoswa ajira n.k. Lakini katika hayo yote mtu anahitaji kuwa na Mshauri ili aweze kufanya maamuzi yaliyo sahihi kwa ajili ya hatima ya maisha yake ya sasa nay a baadaye. Je, Mshauri wako ni yupi?

CHAGUA MSHAURI ANAYEFAA. UTAKUGHARIMU UKIKOSEA.
Inawezeka ni kweli unaye mtu ambaye huwa ana kushauri katika mambo mbali mbali ya kimwili na kiroho, lakini, Je! Ushauri anaokupa ni sahihi au ni wa kukunufaisha kwa muda na kisha baadae kuumia zaidi? AKILI YA KUAMBIWA, JUMLISHA NA YA KWAKO, uone kama unafaa au la. Siyo kila ushauri ni wa kufanyia kazi papo hapo bila kufanya utafiti, natumaini utanielewa tu kidogo kidogo hadi tufike.

Ngoja nikupe mfano kutoka katika maandiko matakatifu. Kulikuwa na mfalme aitwae Herode, huyu mfalme alimwoa mke wa nduguye Filipo. Jambo hilo halikumpendeza Yohana na hivyo akamwambia Herode, siyo halali yeye kuwa na mke wa nduguye. Naye Herodia (mke wa Herode, aliyechukuliwa kutoka kwa Filipo) akawa akimvizia Yohana ili amwue kwa sababu ya kuongea ukweli.

Siku moja Herode akawa anafanya karamu kwa ajili ya siku yake ya kuzaliwa na aliwaalika majemadari na watu wenye vyeo wa Galilaya. Binti yake Herodia aliingia, akacheza kwa ufanisi mkubwa na kumfurahisha Herode sana. Herode akamwambia aombe lolote atakalo na atapewa, hata ikiwa ni nusu ya ufalme wake.
Binti akaenda kumuliza mamake, aombe nini? Akamwambia, aombe kichwa cha Yohana Mbatizaji. Kwa sababu ya kiapo cha Herode mbele ya wageni, Yohana akakatwa kichwa. Tunajifunza nini hapa?

YOHANA KUKATWA KICHWA KWA SABABU YA MSHAURI MBAYA


Herodia ndiye aliyekuwa mshauri wa binti yake, na ndiyo maana binti yake alimfuata baada ya kupata jambo jipya. Lakini, Je! Ushauri ulikuwa mzuri? La hasha. Kuna watu ambao wapo kwa ajili ya kuwapoteza wengine kwa manufaa yao binafsi. Inawezekana unataka kuoa na ukamwomba rafiki yako akushauri, naye akakushauri uachane na mchumba wako halafu baadaye unamkuta naye. Wengi wamelizwa sana kutokana na Washauri waliowachagua katika maisha yao. Jiulize, anayekushauri juu ya biashara, ndoa, elimu, afya ni Mshauri sahihi au ndiye anayekupoteza katika dira ya maisha?

Chukua hatua leo ya kufanya tathimini katika maisha yako na wale ambao unawaendea kupata Ushauri kutoka kwao, ikiwa hawafai tengana nao mapema.
Nakushukuru sana kwa kusoma makala hii hadi mwisho, ubarikiwe na Bwana na uwe na hekima ya kuchagua Mshauri mwema.

Ni mimi rafiki yako mpendwa,
Lackson Tungaraza.
0764793105, kwa jambo lolote nijulishe (whatsapp,call).
WHO IS YOUR BEST ADVISOR? IT NEEDS ENOUGH KNOWLEDGE TO CHOOSE 
Join Lackson Tungaraza 
Whatsapp: 0764793105
Facebook/instagram: Lackson Tungaraza. 
HAVE A NICE DAY.




0 comments:

Post a Comment

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI