JITAMBUE KUANZIA LEO
Heshima na Shukrani za
dhati zikufikie wewe msomaji wa Makala zangu za Uelimishaji kupitia Mitandao ya
Kijamii ya Facebook, Twitter, Linkedln, Instagram pamoja na blog yangu
(lacksontungaraza.blogspot.com) kwani umekuwa msaada wangu kusonga mbele ndani
ya mwaka 2015 na sasa tena uko pamoja nami mwaka 2016. Nimejipanga huu mwaka kukupa Masomo na Semina mbali mbali
ambazo zitakuwezesha kujitambua na kufanikiwa ndani ya huu mwaka ili
itakapofika tarehe 31 Disemba ziwepo shuhuda nyingi za mafanikio kwa kila mmoja
wetu, hivyo usiache kufuatilia masomo yangu na pia kuwa rafiki yangu facebook (
www.facebook.com/ltungaraza
).
Leo nitazungumzia suala
la mtu kujitambua ana tabia ya aina gani maishani ili afanye mabadiliko na
kusonga mbele. Nimezitenga hizo tabia katika makundi matatu ambayo kwa uhakika
na wewe umo kama ukijitathimini baada ya kusoma. Makundi hayo ni;
Ø MTU WA KUIGA
Kama wewe ulikuwa
msomaji mzuri wa hadithi zaSungura na Fisi, utagundua ya kwaamba fisi alikuwa
anaiga mambo mengi kutoka kwa Sungura; njia alizokuwa akitumia Sungura kupata
chakula wakati wa njaa, Ujanja n.k. Na hivyo kupelekea Sungura kuonekana ni
Mjanja zaidi ya Fisi. Fisi alijikuta yuko matatani kwa kuwa na tabia ya kuiga.
Katika mfumo wa maisha
ya mwanadamu, kuna watu ambao wao wapo kwa ajili ya kuiga ya wengine, hawana ya
kwao. Inawezekana na wewe upo katika kundi hili lakini endelea kusoma,
utagundua cha kufanya.
Unamkuta mtu katulia
kama vile hana jambo la kufanya, kumbe anasubiri mtu fulani afanye na ndipo na
yeye afanye. Inawezekana biashara unayoifanya
uliiga kutoka kwa jirani au rafiki yako, Masomo unayosoma shuleni uliiga
sehemu baada ya kusikia kuna soko la ajira ukiyafaulu vizuri n.k.
Unapokuwa unamuiga mtu
mwingine, unakuwa umedharau kipaji au
ujuzi wako ambao Mungu kakupatia. Biashara yako ingekuwa katika kiwango kikubwa
sana kama ungetumia Ujuzi wako binafsi au mfumo wako wa maisha ungekuwa bora
kwa kufuata yaliyo yako bila kuiga. ACHA KUIGA, FANYA AMBAYO MUNGU KAWEKA NDANI
YAKO.
Ø MTU WA KUSHINDANA
Kuna watu ambao wapo
hadi sasa duniani kwa ajili ya kushindana na ndoto za watu wengine. Kila mtu
kaumbiwa jambo la kipekee ndani yake, linalomtofautisha na wengine na ndiyo
maana ukitazama “finger print” au alama ya kidole chako ni ya kipekee duniani
kote. Hata mapacha wakifanana kwa
kiwango gani lakini “finger print” zao ni tofauti.
Unapokuwa unashindana
na Malengo na Ndoto za watu wengine, utaumia wewe mwenyewe. Muulize Farao ni
yapi yalimtokea na majeshi yake ya Misri kwa kushindana na ndoto ya Musa
ya kuwatoa wana wa Israeli Misri na
kuwapeleka Kaanani.
Wanasema, “Adhabu ya
kaburi aijuaye ni maiti.” Mtu anapopanga malengo yake ya kutimiza, anakuwa
ameshajitolea wakfu kwa changamoto yoyote ile itakayokuja mbele yake pasipo
kukata tamaa. Wewe unaposhindana naye, utajihumiza na kukata tamaa. Usishindane
na ndoto wa mtu mwingine, wala mfumo wake wa maisha.
Ø MTU WA UPEKEE
Ninaposema “Mtu wa
Upekee” ni mtu ambaye anatenda yale ambayo yanatoka moyoni mwake na kuyaamini,
yanaweza kuwa ni ya kiroho au ya kimwili.
Watu wa tabia hii huwa
wanafika mbali kimafanikio kwa sababu wanatenda yale ambayo wanayaamini kutoka
moyoni, maana akili hudanganya na pia kukatisha tama lakini moyo ndiyo umebeba
uhalisia.
Ninakushauri sana ndugu
yangu utoroke huko uliko, uje katika kundi hili la tabia la “Mtu wa Upekee.”
Biashara yako na mfumo wako wa maisha ndani ya huu mwaka utabadilika na kuwa
bora ukiwa “Mtu wa Upekee”. LIVE YOUR REALITY.
Napenda nikukumbushe
juu ya Semina yetu kwa njia ya Mtandao (Online Seminar) itakayoanza tarehe 8
Januari kwenye makundi ya Wasap na kupitia barua pepe(Email). Masomo
yatakayofundishwa ili kuleta mafanikio ya uhakika katika maisha yako mwaka 2016
ni;
1. Jinsi
ya kupata Wazo bora la Biashara
Kuna watu wengi ambao wana Mitaji lakini hawajui
wafanye biashara gani itakayowapa mafanikio
2.
Siri
itakayo badilisha maisha yako mwaka 2016
Hii Siri itakupa ushindi wa kiuchumi na katika mfumo
wako wa maisha
3.
Jinsi
ya kuweka Malengo na njia za kufanikisha Malengo yako mwaka 2016
Utapata Mbinu zilizofupi na za
Uhakika
4.
Mambo
ya kuepuka ili ufanikiwe kiuchumi mwaka 2016
Kuna mambo mengi ambayo yamekuwa yakiwazuia watu kufanikiwa kiuchumi,
yamechambuliwa vizuri. Pia baada ya Semina utapata Bure copy ya kitabu kiitwacho “SIRI AMBAZO MFANYA BIASHARA
HUJAZIJUA” sehemu ya kwanza iliyopewa jina la “JINSI YA KUFANYA BIASHARA YAKO
KUWA YA TOFAUTI NA YENYE MVUTO MKUBWA.”
PATA KITABU HIKI BURE KABISA BAADA YA SEMINA 2016, MWAKA WA MABADILIKO Usipange Kukosa Semina Hii |
·
Gharama ni Tsh. 10,000/- tu na Semina itafanyika wiki nzima kuanzia tarehe 8
Januari. Hivyo wahi mapema nafasi hii muhimu kwa kutuma pesa yako kwenda namba 0764793105, utaona jina limeandikwa Lackson Tungaraza . Usisahau kutuma
Jina lako kwa ajili ya uhakiki na barua pepe(Email Address) kwa njia ya SMS.
Ikiwa hauna Wasap au Barua pepe, nijulishe ili upate masomo kwa njia ya Inbox
yako ya Facebook. KAZI NI KWAKO.
SHARE(shirikisha) na ndugu,jirani
na rafiki zako juu ya hii Semina . Kwa lolote , 0764793105 (SMS/Piga/Wasap)
Je unapenda kujiunga na hii semina lakini bado una mashaka?.. Unaweza ukaandika tatizo lako hapa au ukanitafuta kwenye namba yangu 0764793105
ReplyDeleteKuwa muwazi
helo mr Habar za kaz
ReplyDeletetunashukuru kwa semina za kujikwamua kimaisha hasa hasa kwa ss vijana
ndugu mwandishi, kwa sasa kuna tatizo kubwa la ajira hasa kwa vijana wanao tokaa ma vyuoni sasa tunafanyaje ili kujiajiri wenyewe??
Na hii ni kwa sababu ya wasomi wengi ofici kuwa chache
Ndugu mwandishi swal kwangu bado linanipa utataa ni kwa namna gan vijana wanaweza kujiajiri wenyewe ili tujikwamue kimaishaa?
John Fidelis Mbuya, ahsante sana kwa kutoa ya moyoni ili kuleta ukombozi kwa vijana wengi nchini. Nakushauri sana ujiunge na hii semina itakayoanza tarehe 8 Januari kama nilivyoelezea hapo juu. Mtu yeyote yule ambaye anataka kujikwamua kiuchumi akaribie kwenye hii semina, naamini baada ya semina maisha yako yatakuwa tofauti.
Deletekutakuwepo muda wa maswali na majibu pia.
kumbuka semina ni wiki nzima
Vijana wengi wanadanganyana vyuoni, kwamba wakimaliza tu masomo watapata ajira tena ya mishahara minono. Wanasahau ya kwamba kuna wenzao wa mwaka juzi, mwaka jana wapo bado mitaani wanazunguka na vyeti. Ni vyema kijana, mama, baba ukajiunga na semina hii ya kuleta ukombozi 2016....HUTOJUTA
ReplyDeleteVijana wengi wanadanganyana vyuoni, kwamba wakimaliza tu masomo watapata ajira tena ya mishahara minono. Wanasahau ya kwamba kuna wenzao wa mwaka juzi, mwaka jana wapo bado mitaani wanazunguka na vyeti. Ni vyema kijana, mama, baba ukajiunga na semina hii ya kuleta ukombozi 2016....HUTOJUTA
ReplyDelete