NGUVU YA MANENO YATOKAYO KATIKA VINYWA VYETU
Walisema manabii na
mitume, “Atakaye kupenda maisha na kuona siku njema auzuie ulimi wake usinene
mabaya, Na midomo yake isinene hila” (1 Petro 3:10). Wengine wakaongezea”Mtu atakula
mema kwa matunda ya kinywa chake” (Mith 13:2). Hayo yote yalitokea ili sisi
tupate kujifunza namna gani tunaweza kuwa sehemu salama kwa kuwa makini nay ale
tunayoyatamka kutoka katika vinywa vyetu.
Walisema, nimeamini na
mimi nakwambia leo “MANENO NI SILAA” tena silaa yenye nguvu zaidi ya bunduki,
mabomu au wanyama wakali wa mwituni. Wananchi wameingia katika balaa la kupigwa
na Askari ovyo kwa sababu ya maneno mabaya ambayo viongozi fulani waliyatamka.
Ndoa zimevunjika, zimetengana, yote sababu ya maneno waliyoyatamka wana ndoa
hao.
Wanafunzi shuleni
wanaendelea kufeli mitihani yao, afya za wagonjwa kuzidi kuwa mbaya kila siku
kisa maneno waliyojitamkia. Wanasema, “Mimi ni wa kufeli tu”, “hatuna historia
ya kudumu kwenye ndoa”, “umasikini tumeumbiwa”, “huu ugonjwa ni wa kwangu” n.k.
Tukibadili aina ya
maneno yanayotoka vinywani mwetu, tutakuwa na amani, umoja, furaha na maendeleo
katika jamii na kwetu pia kwa sababu hapatakuwepo na kauli mbaya za kuleta
misuguano
Tofauti iliyopo kati ya
waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa au tajiri na masikini, ni aina ya maneno
yanayotoka katika vinywa vyao. Matajiri wanatamka maneno ya ushindi hata kama
wako katika hali ngumu, wanajiamini hata kama mazingira waliyopo yanaleta hofu,
waamini katika kutimiza malengo hata kama wengine wanakata tamaa, na maneno yao
yanaashiria hivyo.
Baada ya kusoma juu ya
nguvu iliyopo katika maneno tunayoyatamka kutoka vinywani mwetu, mithiri ya kuleta umasikini,
magonjwa, vifo katika maisha yetu. Kuanzia leo chukua hatua ya kuchunguza yale
unayoyatamka juu ya maisha yako na juu ya watu wanaokuzunguka, kwa kufanya
hivyo utapata mabadiliko ambayo hukutegemea hata katika biashara yako.
Hili somo limewasaidia
wengi na kubadili aina ya maisha waliyokuwa nayo hapo awali, akiwemo Bwn.
Lackson Tungaraza, blogger wa makala za kuikimboa jamii na Motivator, pia
wanafunzi wa vyuo vikuu nchini. Wasiliana nae kujua zaidi, yale anayoyajua hadi
sasa..Elimu haina Mwisho.
Nakukumbusha juu ya
semina ya mwaka wa mafaniko wa 2016, itakayoanza tarehe 8 Januari kwenye makundi
ya wasap na Email(barua pepe). Hivyo ni vyema ukalipia mapema gharama za semina
kabla ya muda kufika ili kuleta mafanikio ya kiuchumi, kimtazamo na kiroho
mwaka 2016. Mada zilizopo ni;
1.
Jinsi ya kupata Wazo bora la Biashara
Kuna watu wengi ambao
wana Mitaji lakini hawajui wafanye biashara gani itakayowapa mafanikio
2. Siri itakayo badilisha maisha yako
mwaka 2016
Hii Siri itakupa
ushindi wa kiuchumi na katika mfumo wako wa maisha
3. Jinsi ya kuweka Malengo na njia za
kufanikisha Malengo yako mwaka 2016
Utapata
Mbinu zilizofupi na za Uhakika
4. Mambo ya kuepuka ili ufanikiwe
kiuchumi mwaka 2016
Kuna mambo mengi ambayo yamekuwa yakiwazuia watu kufanikiwa kiuchumi, yamechambuliwa
vizuri. Pia baada ya Semina utapata Bure copy ya kitabu kiitwacho “SIRI AMBAZO
MFANYA BIASHARA HUJAZIJUA” sehemu ya kwanza iliyopewa jina la “JINSI YA KUFANYA
BIASHARA YAKO KUWA YA TOFAUTI NA YENYE MVUTO MKUBWA.”
Gharama ni Tsh. 10,000/- tu na Semina itafanyika wiki
nzima kuanzia tarehe 8 Januari. Hivyo wahi mapema nafasi hii muhimu kwa kutuma
pesa yako kwenda namba 0764793105, utaona
jina limeandikwa Lackson Tungaraza .
Usisahau kutuma Jina lako kwa ajili ya uhakiki na barua pepe(Email Address) kwa
njia ya SMS. Ikiwa hauna Wasap au Barua pepe, nijulishe ili upate masomo kwa
njia ya Inbox yako ya Facebook. FANYA UWAMUZI SAHIHI. Usisite kuSHARE na
kuCOMMENT hapa.
JIFUNZE KUJIAJIRI NA KUJITENGENEZEA KIPATO CHA ZIADA Lackson Tungaraza Blogger & Motivator 0764793105 USIPITWE NA SEMINA HII MUHIMU 2016, MWAKA WA MABADILIKO |
unalipi la kusema juu ya hili?
ReplyDeletetoa maoni yako hapa