KWANINI SOKO LA AJIRA LIMEPUNGUA SANA KWA KASI KARNE HII?
Habari yako rafiki yangu mpendwa?
Napenda nikupe pongezi kwa kufuatilia masomo yetu
mbali mbali katika mitandao ya jamii na kuhudhuria semina zetu za Ujasiriamali
kwa njia ya Whatsapp na barua pepe. Leo tutajifunza mada uliyoisoma hapo juu
katika kichwa cha habari.
KILA SIKU WATU WANAKESHA MITANDAONI NA KATIKA BAO ZA MATANGAZO KUTAFUTA NAFASI ZA AJIRA |
NAFASI ZA AJIRA KILA SIKU ZINAPUNGUA KWA KASI YA AJABU NINI TATIZO? |
WANAVYUO WANA PRESHA YA INTERVIEW ILI WAWEZE KUPATA AJIRA JE, SULUHISHO NI SERIKALI? |
Kila mara utawasikia wagombea Ubunge, udiwani,
uraisi wakisema, “Mkituchagua sisi kwa hakika soko la ajira kwa vijana
litapanda kutoka asilimia fulani hadi asilimia fulani.” Pia vijana wa kike na wa
kiume masikioni mwao hupenda kusikia maneno kama hayo, lakini mambo hubadilika
kuwa ndivyo sivyo pindi viongozi hao wanapoingia madarakani na kumaliza vipindi
vyao vya uongozi bila kutimiza ahadi yao hiyo kwa vijana ambao ndiyo walio
wengi nchini. Nini tatizo?
Lackson Tungaraza, baada ya utafiti wake ameweza
kubaini kuwa tatizo siyo viongozi wala mfumo wa elimu nchini kama wengi
wanavyolalamika, wakiwemo watu mashuhuri na maarufu nchini.
Tatizo ni “Sayansi na teknolojia”. Unaweza shangaa au kukataa ni kwanini iwe Sayansi na
teknolojia na siyo Serikali!!?
Ukuaji wa Sayansi na teknolojia nchihi na duniani
kote unaathiri sana soko la ajira hata kwa wasomi kila siku, ndiyo maana wenye
vyeti ni wengi kuliko wenye ajira.
Jiulize mambo yafuatayo;
1. Wako
wapi waliokuwa wanavusha watu ziwani kwa mitumbwi na mashua?
2. Idadi
kubwa ya vijana waliokuwa wanaishi kwa kuwarushia watu nyimbo kwenye simu zao
kutoka kwenye Kompyuta,imeenda wapi?
3. Idadi
kubwa ya vijana waliokuwa wanasafisha mchanga migodini na kuchimba madini, imekimbilia
wapi?
4. Idadi
kubwa ya watu waliokuwa wanalima mashamba yaw engine kwa jembe la mkono,
imeenda wapi?
Utagundua kuwa
baada ya ugunduzi wa meli/boti, smartphones, bulldozers, tractors, robot
n.k. Idadi kubwa ya watu wameondolewa katika sehemu zao za ajira za mwanzo.
Mfano, kazi ambazo wangeliajiri watu 200 kiwandani kubeba vyuma na bidhaa
zingine, hufanywa na Roboti mmoja au idadi kubwa ya watu ambao wangeliajiriwa
na serikali kubeba moramu, mchanga, kuponda kokoto, hufanywa kwa mashine ambayo
inaendeshwa na watu wachache sana. Na mambo mengine mengi kama hayo.
Ni wakati wako dada, kaka, mjomba, shangazi, baba,
mama kufanya biashara inayoendana na ukuaji wa Sayansi na teknolojia. Wakati
unasumbuka kutafuta fremu/pango kwa ajili ya kufungua biashara, wateja wengine
wanafikishiwa bidhaa zilizo bora zaidi hadi milangoni mwao, atakuja saa ngapi
kwako?
NI WAKATI WA KUCHUKUA MAAMUZI YA KUTAFUTA SULUHISHO LA TATIZO LA AJIRA KATIKA MAISHA YAKO USITEGEMEE SERIKALI MUNGU KAWEKA KITU CHA THAMANI NDANI YAKO |
Biashara ya Mtandao au Network Marketing ni biashara
inayoweza kuleta mapinduzi ya kimtazamo na kiuchumi kwako kama ilivyofanya kwa
wengine, bila kujali kiwango cha elimu, uzoefu bali ni msukumo uliyomo ndani
yako kuyafikia malengo yako ya kifedha. Wasiliana nasi kupitia Whatsapp kwa
nambari 0764793105 kuifahamu biashara hii na uendeshwaji wake.
Kama tayari una biashara na unapenda kuifanya kuwa
ya tofauti na yenye mvuto mkubwa, kuna kitabu ambacho tunakitoa bure kabisa ili
uweze kukuza biashara yako. Kimeandikwa “JINSI YA KUFANYA BIASHARA YAKO KUWA YA
TOFAUTI NA YENYE MVUTO MKUBWA.” Ili
kupata Nakala ya kitabu hicho, tuma Jina lako na Anuani ya barua pepe (Email
address) kwenda namba 0764793105 au kwenye Email ya lacksontungaraza@gmail.com
Usisite kuuliza jambo lolote lile pale unapopata
utata, wewe ni mtu wa maana sana kwetu. Pia unaweza kuwatumia na wengine taarifa
hii au kutoa maoni yako hapa .Ahsante sana na ubarikiwe na Bwana.
Nini mtazamo wako juu ya hili?
ReplyDeleteUsisite kutoa maoni yako hapa