Friday, March 8, 2019


Furahia Kila Siku Mpya ambayo Unapewa na Mwenyezi Mungu. Usipofurahia Leo uliyopewa na Mungu, Unadhani Kesho na Kesho kutwa zina nini cha Ajabu sana ambacho Kitakupa Furaha.?

Hata Kama Unawaza sana Juu ya Kupata Pesa ya Kulipa Kodi ya Nyumba, Ada za Watoto Shuleni, Mahari, Mkopo wa Benki... Furaha Isikuondoke Kabisa, hasa Furaha ya BWANA - Kwa Sababu Furaha ya BWANA ndiyo NGUVU Yako.


Kuna Wakati Unaweza Ukadhani ya kwamba Ukipata Aina fulani ya Simu, Gari, Nyumba, Mavazi, Watu, au Kiwango fulani cha Pesa, ndipo Utapata Furaha Isiyokuwa Kifani. Lakini huo Uongo mkubwa sana. Nakuhakikishia ya kwamba Utabaki kuwa vile vile hata Kama Utavipata Kupita Ulivyotarajia. Kuwa na Furaha ni Kuamua kutokea Ndani Yako hata Kama huna pesa, Mali, Umaarufu, n.k.

Wengi Mlitamani Kufika Vyuo vikuu na Kupata Digrii kwa Kuamini ya Kwamba Ndipo Mtapata Heshima Kubwa Kwenye Jamii na Kuwa na Furaha Isiyokuwa Kifani, Lakini baada ya Kufika huko Vyuoni na Kisha Kuhitimu, Mmegundua ya Kwamba MAMBO NI YALE YALE Kama ya Shule ya Msingi, Sekondari, na Mtaani. Wengine Mlidhani Mkioa na Kuolewa ndipo Mtakuwa na Furaha, Mlidhani Mkiajiriwa Kwenye Kampuni Kubwa na Kupata Mishahara Minono ndipo Mtayafurahia Maisha... hahahaha! Yote Yamekuwa Ubatili Mtupu kwa Sasa! Mmegundua ya kwamba Mlikuwa Mnakimbiza Upepo Msiojua Utakako wala Uendako.

Lengo Sio Kumkebehi yeyote Yule, Bali Kukushauri Uwe na Furaha ya BWANA hata Kama huna Yale Unayodhani Unayahitaji kwa Sasa. Furaha ni ya Muhimu sana. WaPo Wenye pesa nyingi na Mali lakini Hawana Furaha kwa Sababu hawana Afya Njema. Wewe uliye na Afya Njema lakini huna pesa na Mali, Mshukuru Yehovah Yahweh kwa hilo. Maadam Uko hai na una Afya Njema, Unaweza Ukapata vingine Kama Kawaida.

USIKUBALI KUTOKUWA NA FURAHA KWA SABABU YA MATOKEO MABAYA YA SHULENI, KUKOSA AJIRA, MSHAHARA MDOGO, KUTOKUOLEWA, KUTOKUWA NA PESA YA KUFANYIA BIASHARA, KUTOKUWA NA WATU WA KUKUTIA MOYO, N.K.

MAISHA NDIYO HAYA HAYA, YAFURAHIE KATIKA BWANA. Imeandikwa, "MAISHA ni zaidi ya CHAKULA, na MWILI zaidi ya MAVAZI."

IFURAHIE LEO, KESHO ITAAKISI FURAHA YAKO YA LEO.

       ..Ahsante sana.
Mawasiliano: +255-764793105.
@lacksontungaraza
AMUA LEO KUWA WA TOFAUTI.

Related Posts:

  • HATUA ZA MAFANIKIO "MAFANIKIO hayaji kwa Ukubwa au Udogo wa kile Ulichonacho, bali kwa namna Unavyotumia kile Ulichonacho" ~Lamax Kila siku nikikumbuka Hatua nilizopitia Kufika hapa nilipo Leo Kimaisha, ninapata hamasa ya Kumshukuru Mungu k… Read More
  • FURAHA YA SIKU MPYA Furahia Kila Siku Mpya ambayo Unapewa na Mwenyezi Mungu. Usipofurahia Leo uliyopewa na Mungu, Unadhani Kesho na Kesho kutwa zina nini cha Ajabu sana ambacho Kitakupa Furaha.? Hata Kama Unawaza sana Juu ya Kupata Pesa ya K… Read More
  • JE UNAOGOPA KUPINGWA? Leo ukimwuliza Mtoto wa Darasa la Kwanza 1-5 (Moja kutoa Tano) ni Sawa sawa na ngapi, atakwambia haiwezekani, ni Lazima pawepo mahali pa kukopa. Lakini ukimwuliza hilo hilo Swali aliye Darasa la Tano atakwambia ni Sawa sawa… Read More
  • KWANINI WATU HAWAFANIKIWI KWENYE MAISHA YA KILA SIKU-Tungaraza (made with Spreaker) KWANINI WATU HAWAFANIKIWI KWENYE MAISHA YA KILA SIKU-Tungaraza (made with Spreaker) Source: http://ift.tt/2gbY85E kuna mambo kadha wa kadha ambayo huwa kwa namna moja ama nyingine huwafanya watu wasifanikiwe katika maisha ya… Read More

0 comments:

Post a Comment

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI