Leo ukimwuliza Mtoto wa Darasa la
Kwanza 1-5 (Moja kutoa Tano) ni Sawa sawa na ngapi, atakwambia haiwezekani, ni
Lazima pawepo mahali pa kukopa. Lakini ukimwuliza hilo hilo Swali aliye Darasa
la Tano atakwambia ni Sawa sawa na -4 (hasi Nne). Wanafunzi ni wale wale lakini
Majibu tofauti. Na Kila Mmoja yuko Sahihi kulingana na kiwango cha Maarifa
alichonacho kwa wakati huo.
Ni jambo gani ninalotaka ujifunze
kupitia huo mfamo wa hapo Juu? Sikiliza, kwenye maisha yako Yote ya hapa
Duniani, usitegemee ya kwamba kuna Siku Watu wote watakuwa na Mtazamo kama
wako, Akili kama zako, wala kiwango cha Maarifa kama ulichonacho. Never.
Unaweza Ukaandika, ukasema, au ukatenda
Jambo ambalo ni Sahihi lakini Ukapingwa sana kana kwamba hauko Sahihi, na
waliokupinga ndiyo wako Sahihi. Hiyo isikutishe sana. Inawezekana Wameamua
kupinga kwa Sababu ndiyo kazi inayowaweka Mjini (Siku zote wapo kwenye kambi ya
Upinzani kwa Kila Jambo), au hawajui walitendalo kwa Sababu ya Kiwango cha Maarifa
na aina ya Usahihi walionao, au hawataki Ukweli ujulikane (wanataka Watu Wengi waendelee kutembea
gizani katika upofu, na wao wanufaike zaidi).
Kumbuka ya kwamba, kupingwa kwa Jambo Sahihi hakuondoi
Usahihi wa hilo Jambo hata kama waliyolipinga watashinda.
Aiseeeh! Songa mbele, wasikutishie nyau. Unajua hata
waliyokuwa wanapinga ujio wa Simu Janja
(Smartphone) kwa kusema ya kwamba ni za Freemason na zinanyonya Damu za
Watu za Mikononi, ndiyo WANAOONGOZA Leo kwa kutumia hizo Simu. Kupingwa
Sio kuzuiliwa. Yesu alipingwa ya kwamba Sio Mwana Pekee wa Mungu
Ingawa Ishara zote zilionesha ndiye. Hata hivyo kupinga Kwao hakukuondoa Ukweli
kwamba Yeye ndiye Mwana wa Mungu aliye hai. John Magufuli alipingwa sana wakati
wa kampeni za Uchaguzi mwaka 2015 wakisema ya kwamba hawezi kuwa Rais wa Nchi
kwa Sababu alifanya Makosa ABC alipokuwa Waziri. Kwani kupinga kwao kulimfanya
asiwe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Hahahaha, Jibu unalo.
"Ukishindwa kusonga Mbele kwa Sababu
ya kupingwa, basi Ujue ya kwamba Ulikuwa Hujui ulitendalo hata kabla ya kuanza
kulitenda ulitendalo Leo." - LAMAX.
AMUA LEO KUWA WA TOFAUTI. Kuwa Yule unayetakiwa kuwa. Usiwe
Yule anayetakiwa Kuwa kwa Sababu ya matakwa ya Watu fulani fulani.
Tukutane baadae.
By Lackson Tungaraza (Mwandishi wa Vitabu Kadhaa ambavyo
Unaweza ukavipata Leo na ukaweza kunoa Uwezo uliyomo ndani Yako).
@LACKSONTUNGARAZA
#0764793105 WhatsApp.
https://lacksontungaraza.blogspot.com
#LamaxQuotes #LIVING4MANY #LamaxLibrary
0 comments:
Post a Comment