Sunday, November 26, 2017


"MAFANIKIO hayaji kwa Ukubwa au Udogo wa kile Ulichonacho, bali kwa namna Unavyotumia kile Ulichonacho" ~Lamax

Kila siku nikikumbuka Hatua nilizopitia Kufika hapa nilipo Leo Kimaisha, ninapata hamasa ya Kumshukuru Mungu kwa kunifundisha kwa Kila Hali. Nami sio wa Kwanza, kwani hata Mtume Paulo alifundishwa na Mungu KUSTAHIMILI Kila hali; kushiba na Kuona njaa, Kufanikiwa na kutofanikiwa, kuwa na Vingi na Kupungukiwa, na mwisho wa mafundisho hayo akasema kwa hakika Niliyaweza mambo yote katika yeye anitiaye Nguvu.


Muda Kadhaa Uliyopita Nilikuwa natumia Simu ya Tecno S3 (pichani) katika Kuandaa Masomo (Audio, Video, Nukuu, Makala) Mengi niliyokuwa nikiweka Mtandaoni. Screen yake ilikuwa ndogo, UBORA wa picha ulikuwa wa kawaida sana, RAM na Memory nazo zilikuwa ndogo. Lakini Licha ya hayo yote Nilikuwa nikiandika hata Makala yenye Maneno zaidi ya Mia tano  (500) na kuweka Facebook na katika Blog yangu, na Kuanza kusomwa na Watu waliokuwa wakitumia Simu za Gharama kubwa kama IPhone, IPad, Samsung, Nokia n.k. Watu  Wengi walikuwa Wanastaajabu wakiniona nayo hiyo Simu. Wengine wakawa wananiuliza "HIVI HUWA UNATUMIA NINI KUANDIKA YALE MASOMO YAKO YA WHATSAPP?" na nikawa nawajibu "NI HII SIMU NILIYONAYO." Wakawa hawaamini kama ni kweli, maana walitarajia ya kwamba Ningekuwa na Bonge la Simu.
SIMU YANGU-TECNO S3


Baada ya Wengine Kuona aina hiyo ya Simu niliyokuwa nikitumia, wakaanza kuniambia ya kwamba Ninajiaibisha, hiyo Simu sio ya Hadhi yangu; Screen yake ni ndogo sana na ninaandika kwa Shida Sana. Nikawa nikiwasikiliza tu na kisha kuendelea na Mipango yangu, kwa sababu kwangu Haikuwa Adhabu Bali Kipindi cha Mpito. 

Nikaendelea na UAMINIFU huo kwa Miaka mitatu (2014-2017). Nikawa nikifanya Kazi ya Uandishi kwa Ustadi na kuwasaidia Wengi.


Kilichokuwa kinanisaidia sana ni Neema ya MUNGU, #MAONO yaliyonipatia NIDHAMU na UVUMILIVU, Pamoja na Kutumia kwa UBORA kile kidogo nilichokuwanacho kwa Wakati huo. Na mwisho wa Siku nikazidi kuwa bora zaidi kwa sababu MATENDO yananguvu kuliko MANENO, ACTIONS Speak Louder than WORDS. Na kisha baadae nikapata Simu ya Kisasa ya Samsung Galaxy Grand Prime Plus. 

Maandiko matakatifu yanasema "Aliye Mwaminifu kwa Madogo/Machache huwa MWAMINIFU Pia kwa Makubwa/Mengi"


Hivyo Usisumbuke sana katika kutafuta Makubwa ama Mengi ili kupata Mafanikio katika yake Uyafanyayo, kikubwa ni Kufanya kwa UAMINIFU, UVUMILIVU na Ustadi kwa Madogo/Machache uliyonayo ili Kupata Makubwa/Mengi Uyatakayo.




"Uwe MWAMINIFU"

"I have Never Seen a Great Person with an Easy Past. Your Present Situation is not your Final Destination, the Best is yet to Come. Keep Moving Forward while fully believing in Christ Jesus"



Lackson Tungaraza

lacksontungaraza.blogspot.com

0764793105

0 comments:

Post a Comment

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI