Yamefundishwa na
Watu wengi, maarufu na wasio maarufu, Wanawake kwa wanaume. Kila mmoja akiwa na
Upekee wake kulingana na MUNGU alivyomwelewesha, au alivyogundia Binafsi.
Vitabu navyo vimeandikwa juu ya Sekta hii. Hii Sekta ni Nyeti sana, ndiyo maana
Imekuwa na Mkazo mkubwa sana. Hii Sekta inaweka Msingi mzuri wa MTU Kujitambua na
Kuweka Alama Chanya duniani.
●Hata Mimi Lackson
Tungaraza, hili Somo kwangu ni Pana sana. Nililiambatanisha kwenye KITABU
Changu KIPYA ambacho kitatoka muda sio mrefu, ila bado naona haliishi na MUNGU
anazidi Kunipatia vitu vipya Kila wakati.
●Leo nataka
Nikushirikishe kwa #Ufupi juu ya #MAONO na #KUSUDI, kama MUNGU alivyonifunulia
tena;
(Chukua KWA Sehemu
yako)
Maono kwa lugha nyingine NI NENO
LA MUNGU LINALOKUJA KWA MTU KWA NJIA YA PICHA.Wengine husema A CLEAR PICTURE OF THE END WHILE AT THE
BEGINNING.
Maono Yanakuwa ndani
ya KUSUDI.
》Ukiona Maono yako
hayaendani na KUSUDI LA Uwepo WAKO hapa duniani, basi hayo si Maono Halisi.
》Maono yanakusaidia
kukaa katika KUSUDI LA Uwepo WAKO hapa duniani.
♠KUSUDI LA YESU
kuwepo duniani lilikuwa ni Kuwaokoa Watu wake na DHAMBI zao (Mathayo
1:21).Hivyo Maono aliyokuwanayo yalikuwa yanaendana na KUSUDI HILO.
●Utaona ya kwamba
KUSUDI linakuwa ndani ya stetimenti moja ambayo ni Wazi (in a single clear statement).
》Na ndivyo ilivyokuwa
kwa Yohana mtoto wa Zakaria, kwa SAMSONI mtoto wa Manoah, kwa Yeremia, kwa
Yeremia na wengine Wengi.
Maono ni Kuona Ukamilifu wa
JAMBO hata kabla hujaanza. Bwana YESU KRISTO aliona amekwisha kufa na
kufufuka baada ya siku Tatu hata kabla
ya huduma yake kushamiri.
》》In other words
"WHERE DO YOU SEE YOURSELF AFTER 5, 10, 15 YEARS LATER?" (JIJIBU)
Kuna MWALIMU
wetu mmoja wa "Open Source Technology" aitwae Mr. Mutembei kule
CIVE-UDOM aliwahi Kuuliza hilo Swali darasani. NIKAONA VIJANA wengi Wakianza
KULALAMIKA ya mwaka hilo swali haliendani na Kipindi, vijana wenyewe walikuwa
na Mwaka wa Tatu na wa nne, wa Shahada. NIKATABASAMU na Kuanza kuwasikiliza kwa
makini, mmoja baada ya mwingine (KILA mtu alikuwa anajibu kwa SAUTI kubwa ili
darasa zima lisikie). Nami Nikasema kwa sehemu yangu na Kusangawa na wengi. NIKATAMBUA,
VIJANA WENGI WANATAFUTA UBORA WA MAISHA LAKINI HAWANA MAONO HALISI (Ndio maana
Kila Fursa wanaitaka ili mradi tu ina Pesa ya kutosha).
Mungu anapokupa #Maono, Maono
hayo yanakuja na IMANI. Hivyo ukiona Maono uliyonayo hayana imani ndani yake,
uwe na mashaka nayo.
》》Ndani ya
Maono, tunaenenda kwa IMANI WALA si kwa KUONA (2Kor 5:7). Kuona ni kazi ya
macho, na macho huwa hayaoni mbali, hayaoni KESHO. Na kama Maono yangekuwa
yanaambatana na MACHO, basi Vipofu wasingeweza Kufika mbali (wasingekuwa na
Maono).
Kuna #Vipofu ambao waliweza
Kugusa dunia na Kuacha Alama Chanya kwa sababu ya #MAONO (VISION). Mfano mzuri
ni dadangu HELEN KELLER.
HELEN_KELLER.
●Jina lake zima ni
HELEN Adams KELLER.
_Huyu dada alizaliwa
akiwa na Afya nzuri tu kama wengine wengi.
Wazazi wake walikuwa ni Kate Adams KELLER na Colonel Arthur Keller.
●Miezi 19 baada ya
Kuzaliwa, HELEN KELLER alipatwa na UGONJWA WA AJABU SANA ambao haukufahamika
VYEMA. Ghafla akawa KIZIWI (Deaf) na KIPOFU (Blind).
●Licha ya UPOFU
uliompata, HELEN KELLER bado alikuwa na #Maono, kwa sababu Maono hayabebwi au
hayaambatani na #Macho. Alianza kufundishwa na mwalimu wake ANNE SULLIVAN jinsi
ya Kuunda Silabi na Sentensi. Akafundishwa na Kutamka na MWALIMU wake SARA
FULLER.
#Maono yalimfanya
AFANYE MAMBO MAKUBWA SANA Dùniani ambayo hata wengi wetu hawajafanya hata sasa.
》Alianza KUWASAIDIA
Watu wenye Hali kama yake, kuwahamasisha na Kuwapa Tumaini Jipya.
》》Leo
anakumbukwa kwa Ushiriki wake katika Siasa, Mhadhiri (Lecturer), Mtu wa KWANZA aliyekipofu na
Kiziwi kupata Shahada ya Sanaa, na Mwandishi (Author). Alikuwa na Vitabu vingi
tu kama vile "The Story of my Life, The WORLD i live in, The song of the
Stone Wall, Light in my Darkness n.k"
Na hapo
alikuwa #KIPOFU na #KIZIWI. Kwanini wewe ushindwe?? UNAJITETEAJE SASA!!
》Aliwahi kusema ya
kwamba NI JAMBO LA KUSIKITISHA, LA HATARI SANA, KUONA NA USIWE NA MAONO).
"It's a TERRIBLE thing to SEE and have no VISION"
SOMA: NIMEAMUA_KUFUNGUKA
#Remember
"Our Greatest
Enemies are our own Doubts and Fears"
"Don't expect
SOMETHING different if you Keep to do the SAME things"_Brian Tracy.
"If you don't
Beat the RECORD of your Parents, you haven't SUCCEEDED"_ Dr. David Oyedepo
#MAONO yanaleta pia
#NIDHAMU kwenye maisha ya mtu; UWEZO WA KUJIZUIA(Kukataa KUFANYA MAMBO yaliyonje ya Maono hata kama yana
#PESA NYINGI na kuwa na Mvuto.)
》Ni vigumu mtu
KUJIZUIA kama hana #MAONO halisi KUTOKA
KWA MUNGU aliyehai(Mith 29:18).
Zaidi sana Jipatie Kitabu Changu kinachoitwa 'SITARUDI NYUMA TENA' kwa gharama ndogo tu ya Tsh.5000/- na Utapata Masomo haya na mengine mengi kwa Undani Zaidi. Hautajuta hata siku moja.WhatsApp! 0764793105
Facebook! fb.com/ltungaraza
0 comments:
Post a Comment