Licha ya kwamba kwa sasa Umegubikwa na wimbi kubwa
la Majonzi kwa sababu ya kutokupokea simu na Kujibu Meseji zako, lakini naamini
ya kwamba bado unazo NGUVU Za Kuusoma UJUMBE huu kwa umakini kwa kuwa bado
unaujua Umuhimu wangu kwako.
Unakumbuka siku ile nilipokutwika maji pale
Kisimani? Ndio iliyokuwa siku yangu ya kwanza kufanya hivyo kwa jinsia ya Kike.
Sikuwa kabisa na msaada huo kwa wengine. Ilikuwa siku ya tofauti sana kwangu
kiasi cha Kulala na kuota tukiwa wote Kisimani kama Wamiliki wenye Furaha sana.
Asubuhi yake nikachukua pesa yangu ya Akiba na Kununua "Diary"
niliyoitumia hasa katika Kuandika hiyo NDOTO, nikiamini kabisa yaweza kuwa ni
kweli.
Unakumbuka asubuhi hiyo nilikuja nyumbani kwenu
Kuomba Mbolea? Yote ni kutaka kukutia machoni pangu tena ili nifarijike. Baadae
nikakuomba tuongee kidogo, nawe ukanikubalia bila kinyongo.
Nakumbuka siku hiyo niliamua Kuacha Ukimya na
kukwambia YA MOYONI Mwangu. Hukuamini, ukaniambia nikupe muda ili utafakari
vyema. Nikajipa moyo na kukukubalia kwa Shingo Upande. Baada ya siku tano za
Ukimya na kuadimika, hatimae ukaniambia UKO TAYARI kuwa nami katika MAHUSIANO.
Siku hiyo niliondoka nikiwa na Furaha sana kuliko hata ya wakati ule
nilipotangazwa kuwa "Mwanafunzi mwenye Ufaulu wa Kwanza" mkoani kwetu.
Baada ya wiki kadhaa nikakuomba tukutane pale
LAMAX HOTEL kwa mazungumzo na kupata Kuona Filamu mpya pamoja. Ukanikubalia kwa
moyo mkunjufu kwa kuwa uliamini kabisa ya kwamba Ninakupenda kwa Dhati.
Sikumbuki vizuri yaliyotokea wakati wa mazungumzo ila tulijikuta ndani ya Shuka
tukiwa pamoja katika Chumba cha Wageni. Wote hatukuwa na TABIA hiyo, ila ndivyo
ilivyotokea.
TAARIFA zikafika kwa wazazi wako, ukanitetea na
kusema ya kwamba ni UONGO. Nikafurahi sana kwa kumpata MSAIDIZI kama
nilivyosoma siku moja kwenye Kitabu cha Mwanzo cha kwenye Biblia ile ya Babu
yangu kizaa mama.
©Lackson Tungaraza
Fb.com/ltungaraza
|
Najua uliyafanya yote hayo ili nizidi kukupenda na
kuwa karibu zaidi nawe.
Ni mwaka wa Pili sasa tangu ile siku pale njiani
nilipokwambia ya kwamba Sitaki Kuona Meseji yako tena katika simu yangu ya
mkononi. Ulidhani ni Utani, ukaendelea kufanya kinyume na nilivyokwambia,
nikaamua nisikujibu lo lote.
Hata kama nimeandika Mengi yanayokaribia kujaza
Kurasa za Vitabu, ila Naomba niseme nawe kabla ya kupatwa na Umauti au Dunia
kuisha.
Ni mwaka mmoja sasa unaelekea kuisha tangu siku
ile nilipoamua kumrudia Mwumba wangu katika mkutano mkubwa uliofanywa na MOSES
KULOLA kabla ya kufariki. Ni kama vile huyo mzee alikuwepo kipindi nafanya
mambo mabaya kwa #SIRI.
Nimejifunza
mambo mapya na Mengi sana katika Biblia niliyopewa BURE pale mkutanoni.
Mojawapo ni haya ambayo ninataka uyajue leo;
❤Kipenzi nimegundua ya kwamba SIKUWA
NAKUPENDA KABISA, ila ILIKUWA NI TAMAA ZA MACHO NA MWILI. Hukuwa MSAIDIZI wangu
kama nilivyosoma kwenye Biblia ya babu yangu kizaa mama, kwa sababu bado
hatukuwa #Wanandoa.
❤Kipenzi, Mwanaume ye yote akikwambia
ya kwamba HAWEZI KUJIZUIA MBELE YAKO, au Kukwambia ya kwamba NI VYEMA AJUE
#UTAMU WAKO KABLA YA NDOA ILI ASIUZIWE MBUZI KWENYE GUNIA.. Huyo HANA UPENDO WA
KWELI Kwako, ila NI TAMAA ZA MACHO NA MWILI wake tu.
Nilipokuwa Nasoma hiyo Biblia, nilikutana na
habari za mtu ambaye alinipa Mtazamo mpya juu ya Kupenda katika MAHUSIANO.
Naomba ninakili ili ujisomee mwenyewe na kuamini.
#Mwanzo
29:18-20
[Yakobo
akampenda Raheli akasema, Nitakutumikia MIAKA SABA kwa kumpata Raheli, binti
yako mdogo.Labani akasema, Afadhali nikupe wewe kuliko mtu mwingine; kaa
kwangu.Yakobo akatumika miaka saba kwa kumpata Raheli. IKAWA MACHONI PAKE KAMA
SIKU CHACHE TU KWA VILE ALIVYOMPENDA.]
Umeona! UPENDO wa KWELI Unavumilia yote, HAUTAFUTI
mambo yake yenyewe na wala hauhesabu mabaya.
Asiyeweza
Kuvumilia hadi Umalize Masomo yako, huyo hana UPENDO wa KWELI kwako. Asiyeweza
Kuvumilia hadi Mfunge Ndoa, huyo hana UPENDO wa KWELI kwako.
"NGONO HAITUNZI PENZI KWA WATU AMBAO SIO
WANANDOA" Ingekuwa hivyo, hata Mimi ningekuwa pamoja nawe katika MAHUSIANO
hata sasa.
#WAOAJI
HAWANA PAPARA KABISA Kipenzi wangu. Mara zote wana UPENDO wa KWELI wa kutaka
Kuona mkifika katika #NDOA Salama, huku Kila mmoja akiwa anajua Majukumu yake
yote.
USIWE MSAIDIZI WA MWANAUME YE YOTE YULE KABLA YA
NDOA.
》Usikubali Kushikwa_shikwa MWILI wako. Mimi
nilifanya hivyo kwako na tukaishia kuwa pamoja ndani ya Shuka pale Lamax Hotel, tena kwa mfululizo. TUNZA HUO
MWILI KWA AJILI YA MUME WAKO AMBAYE UTAPEWA NA MUNGU.
AKILI
za Kuambiwa katika Semina ya Mahusiano, Changanya na zako bila Kusahau
kumwuliza Mungu ili AKUSAIDIE.
Naomba nisikuchoshe sana, sijamaliza Kuandika yote
ya moyoni, ila kuna KITABU KIPYA ambacho kitakusaidia Kujua zaidi ya hapo.
Kinaitwa "SITARUDI NYUMA TENA" na kitakuwepo hadharani muda sio
Mrefu. Mwandishi ni Yule Kijana wa pale karibu na Lamax Hotel, aitwae #Lackson
Tungaraza. JIANDAE KUKIPATA HIVI KARIBUNI.
👉Sehemu ya Nne ya Kitabu hicho
itakusaidia sana Kipenzi changu.
Mawasiliano yake;
0764793105 (#WhatsApp)
Uwe na Siku njema sana. Ikimpendeza Mungu nitakuja
nikuone japo kidogo.
KWA SASA KITABU HIKI KINAPATIKANA
PIGA 0764 793105
KITABU KINAPATIKANA KWA SASA
ReplyDeletePIGA/SMS: 0764 793105
TSH. 5000/= tu