Tuesday, September 12, 2017

Hapa tunaongelea maisha ya mtu mmoja mmoja (mtu binafsi), sio ya Kikundi cha watu fulani, maana kuna watu wanaopenda Kujificha kwenye Vivuli vya wengine ili wao wasipatwe na Ukali wa Jua.



●Naitwa Lackson Tungaraza. Tuangalie sasa hizo tabia;

1: HAWANA UHAKIKA WA MAISHA YA KESHO

Maisha yao ni ya KUBAHATISHA, Maisha ya liwalo na liwe, Maisha ya nitajua muda ukifika.  

●Mara nyingi wanaishi maisha ya HOFU SANA; Wakisikia Ajali zimekuwa nyingi barabarani msimu huu, basi wanaacha Kusafiri kabisa kwa Hofu ya Kifo. Wakisikia Masomo fulani ni magumu chuoni na wengi wanafeli, basi wanaghairi Kusoma. Hofu zimewajaa kwa habari ya Maisha ya Kesho.


Mfano mzuri ni wana wa Israeli (Kut 14).


👉Walitoka Misri na vyombo vya Fedha na Dhahabu, pamoja na Mavazi, kama ambavyo wengi wetu wamepata PESA NA MALI. Cha AJABU, HAWAKUWA na Uhakika wa maisha ya Kesho.

👉Walipokuwa wamepanga pale karibu na bahari ya Shamu, wakawaona Wamisri wanakuja NYUMA yao, WAKAOGOPA SANA, Wakamlilia Mungu katika Mashaka na Kuanza KUMLALAMIKIA MUSA.

Kwa KUTOKUWA na Uhakika wa maisha yao ya kesho; waliona ni BORA wangebaki Misri na KUENDELEA kuwatumikia Wamisri, ni BORA wangefia Misri lakini sio Jangwani. Hawakuona lo lote Jema ila MABAYA, wakawaza tu juu ya KIFO.

MUSA ALIYEKUWA NA #MAONO HALISI KUTOKA KWA MUNGU alikuwa na Uhakika wa maisha ya Kesho. Hakuogopeshwa na vishindo vya farasi vya jeshi la Farao. Akawaambia watu, "MSIOGOPE, SIMAMENI TU, MKAUONE WOKOVU WA BWANA ATAKAOWAFANYIA LEO; Kwa maana hao Wamisri mliowaona Leo hamtawaona tena milele. BWANA ATAWAPIGANIA ninyi, nanyi Mtanyamaza Kimya"


Unadhani ni kwanini watu HUJIUA baada ya KUFELI mitihani, baada ya kuachwa kwenye Mapenzi, baada ya Kutumbuliwa (kufukuzwa kazi), baada ya biashara zao kufilisika na mipango kugoma? NI kwasababu ya KUTOKUWA na Uhakika wa maisha ya Kesho.
SOMA: "JIFUNZE KWA MWANAMKE MCHAPAKAZI MAZNAT"

 Uhakika huo unakuja kwa NJIA YA IMANI, Sio kwa njia ya maneno na Maandishi. Unadhani ni kwanini Mungu alisema ya kwamba "Mwenye haki wangu ataishi kwa IMANI pasipo kusita-sita?"

 Nelson Mandera unamfahamu? Unadhani ni kwanini alikubali KUENDELEA Kufungwa Gerezani kwa miaka 27 badala ya kuchagua njia ya Mkato kama wewe? Uhakika wa maisha ya Kesho.

Sinema ya "SARAFINA" Ushaiona au kusimuliwa? Sarafina anaimba "FREEDOM IS COMING TOMORROW " katikati yà Majanga makubwa ambayo hayashawishi kufanya hivyo kabisa.  WEWE JE??



2: WANALALAMIKA SANA 

Suluhisho kubwa la mambo wanayopitia ni Kulalamika tu, na hii inaambatana na Kipengele cha Kuacha Kujizuia (Mith 29:18).

👉Wana wa Israeli waliona ni BORA Kulalamika tu, KUMLALAMIKIA MUSA kuliko kutafuta Utatuzi.

Hata wewe pia unapenda sana Kulalamika unapokutana na Changamoto kwenye MAHUSIANO, waalimu wanapokufelisha kwa makusudi, ukipatwa na ugonjwa/UDHAIFU fulani Mwilini, ukiongezewa Majukumu kazini au Mshahara kuchelewa Kutoka n.k

"PASIPO #MAONO WATU HUACHA KUJIZUIA "

👉HABAKUKI Nabii alimlalamikia sana Mungu kwa Yale aliyoyaona yakiendelea kwenye Jamii; Haki kupotoshwa, Rushwa imekithiri, magonjwa na shida kibao.

》》MUNGU akamwambia AIANDIKE NJOZI (MAONO) Kwasababu Maono ni Suluhisho la Malalamiko.

●Wenye #MAONO hawalalamiki ovyo ovyo. Wanaamini Kuna Kesho yenye Ushindi na UTUKUFU. Ndio wale waimbao "MY TOMORROW MUST BE GREATER THAN TODAY"
Wakati wanafunzi wanahofia juu ya UGONJWA aliokuwa nao Lazaro, ya kwamba Atakufa, YESU aliona Uzima. YESU akawaambia, "UGONJWA HUU SIO WA MAUTI, BALI ni kwaajili ya UTUKUFU WA MUNGU..
wewe huwa UNAONA NINI Unapopita/unapopitishwa katika magumu? Mema au Mabaya!! Je huwa unaona kama DANIELI katika Tundu la Simba? Huwa unaona kama Daudi MBELE ya Goliathi? Huwa unaona kama MALKIA Esta MBELE ya Sheria ya Hamani na Mfalme Ahasuero? Huwa unaona kama akina Meshaki, Shadraka na Abednego katika Tanuru liwakalo moto? Huwa unaona kama Paulo na Sila Gerezani?

KABLA YA KUTAFUTA PESA NA MALI, TAFUTA KWANZA #MAONO HALISI KUTOKA KWA MUNGU

Wana wa Israeli walikuwa na vyombo vya Fedha na Dhahabu na bado hawakupata Uhakika wa maisha ya Kesho, na bado walilalamika sana.

MAONO yatakupa Ujasiri hata Ijapobadilika Nchi ya TANZANIA! Mungu atakuwa kwako Kimbilio na NGUVU, na Msaada uonekanao wakati wa mateso (Zab 46:1-2).

"FANYIA KAZI NAWE UTAFANIKIWA SANA "

"Hamna haja ya KUENDELEA kuwalalamikia VIJANA wa LEO kwa namna wanavyoishi ikiwa bado HATUJAWAJULISHA HABARI YA MAONO HALISI KUTOKA KWA MUNGU " Kila Kitu Kinatengenezwa.

Zaidi sana Jipatie Kitabu Changu kinachoitwa 'SITARUDI NYUMA TENA' kwa gharama ndogo tu ya Tsh.5000/- na Utapata Masomo haya na mengine mengi kwa Undani Zaidi. Hautajuta hata siku moja.

WhatsApp! 0764793105
Facebook! fb.com/ltungaraza




0 comments:

Post a Comment

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI