Kati
ya maeneo ambayo huwa yanawatia watu Joto Kubwa ni eneo la Umalizaji. Umalizaji
huu huenda mbali zaidi katika mchezo wa Mpira, katika Utumishi, kwenye Chumba
cha Mitihani, kwenye Ndoa, Uchaguzi Mkuu n.k... Eneo hili huwafanya wengine
kupata Heshima na wengine Kudharauliwa.
Kuna
Wachezaji ambao huwa wanapiga sana Chenga katikati ya Uwanja na kisha kushindwa
Kuwa na Umaliziaji mzuri (Kufunga Goli), kisha kuanza Kusemwa vibaya na
Washangiliaji. Vivyo hivyo kwa Wanafunzi ambao huwa wanafaulu sana Mitihani ya
ndani ya shule na kushindwa Kumaliza vyema (kufaulu mitihani ya nje).
Pointi
yangu kubwa ipo katika UMALIZAJI. UNAMALIZAJE HUU MWAKA WA 2017??
Naamini
kabisa ya kwamba MAJIRA kama haya mwaka Jana, kuna mambo ambayo Ulighairi
kuyafanya na kusema ya kwamba utayafanyia kazi ndani ya mwaka huu wa 2017.
Lakini pia Uliupokea Mwaka huu kwa Shangwe na Ndelemo za "HAPPY NEW YEAR
(HERI YA MWAKA MPYA)" huku Ukiwa na MALENGO na Mipango mingi kwenye
'Diary' zako kubwa. Ulikuwa Moto sana, hukuacha Kuhudhuria Semina mbali mbali
na Kusoma Vitabu vingi.
Nakuuliza
tena "UNAMALIZAJE HUU MWAKA WA 2017??"
Mwaka
huu Unapokwisha, ni JAMBO gani Umelifanya au Utalifanya na kuweka Kumbukumbu
Chanya kwenye Maisha yako?
Inawezekana
ulikuwa na MALENGO na Mipango mingi sana na hujafanya kama Ulivyokuwa umepanga
mwanzoni mwa mwaka huu. Usife MOYO na Kughairi tena kwa kusema ya kwamba
Utafanya Mwakani. MUDA bado upo. Ni wewe tu Kubadili namna unavyoona, kufikiri
na kuamini Nafsini mwako. Huwezi ukafanikiwa zaidi ya Yale yanayofanyika
Nafsini mwako.
Amua
Leo kuchagua JAMBO moja na kuliwekea NGUVU kubwa hadi lifanikiwe (Focus). JAMBO
ambalo litakuachia Kumbukumbu Chanya ndani ya maisha yako utakapokuwa
ukiukumbuka huu mwaka wa 2017. Wazungu husema ya kwamba "half a Loaf is
better than nothing" na "Better Late than Never"
Ni BORA Uchelewe na Kufika kuliko Kukata tamaa na kuwa Sanamu.
Ni BORA Uchelewe na Kufika kuliko Kukata tamaa na kuwa Sanamu.
Mungu
anakuwazia MAWAZO Mema, Usimwangushe kabisa. Atakapokuja kuchukua hesabu ya
Yale uliyoyafanya mwaka huu, basi jitahidi akute hata jambo moja ambalo Umelifanya
kwa Ukamilifu na kwa Uaminifu. USIWE NA VIPORO VINGI, ZINGATIA UBORA.
Kwa
Upande wangu, Nilikuwa pia na Mipango na MALENGO, baadhi yamefika mbali na
mengine bado. Lakini moja kubwa lilikuwa ni Kumiliki KITABU changu KIPYA katika
mfumo wa hardcopy. Na sasa limefanikiwa kwa 90%. Nikiamini ya kwamba NITAONGEA
NA WATU WENGI SANA KUPITIA HICHO KITABU KIPYA kuliko ambavyo Ningefanya kwa
njia ya KUONGEA Ana kwa Ana na mtu mmoja mmoja huko Shuleni, kanisani au
Mitaani.
Dhamiria
kufanya JAMBO ambalo litapandisha Thamani yako. Dhamiria pia kupata hicho KITABU changu KIPYA katika mfumo wa
hardcopy. Ndani yake Utapata mambo ya kukusaidia Kumaliza huu mwaka vyema na
kuanza mwaka mpya Ukiwa na kiapo cha "SITARUDI NYUMA TENA"
Tafakari:
UNAMALIZAJE HUU MWAKA WA 2017!! Vizuri au Vibaya!! Amua sasa.
FUNGUA
( lacksontungaraza.blogspot.com )
Ninayomengi
sana ya Kuandika lakini hutabadilika Usipofanyia kazi hata hayo machache.
Mengine utayakuta Kitabuni.
0764793105
Lackson Tungaraza
|
Naitwa
Lackson Tungaraza.
Fb.com/ltungaraza
0764793105 (#WhatsApp)
Fb.com/ltungaraza
0764793105 (#WhatsApp)
SHARING
IS CARING.
0 comments:
Post a Comment